Kitabu cha ukweli - Mlango Wa pili "ENZI TUKUFU"



[ 1 ]

1. Hapo mwanzo kabla ya anga na ukiwa kupatikana, kulitangulia ‟enzi” tukufu. 

2. Enzi hiyo ni milki kamilifu ambae huweza yote na hujua yote.
3. Ilitangulia yenyewe ulimwenguni bila kufanyika ajili ya kukamilika kwayo. 

4. Ni mamlaka yenyi kuenea kiushindi, bila upungufu wowote.

5. Na utangulizi wa enzi kadiri ya ukamilifu ndio uzima ambae ni umungu.
6. Uzima huo, ambae ni umungu, ulikua enzini hali ya kua mwenyenzi Mungu.
7. Alitangulia mwenyewe mbele ya vyote hali ya kua yote katika yote, kadiri ya mwanzo wa vyote.

24

8. Hapakupatikana yeyote badala ya mwenyenzi Mungu, ajili ya upekee wa milki yake kamilifu.
9. Alikua ametawala peke yake kabla ya ulimwengu na walimwengu, katika mamlaka yake mwenyewe.
10. Mwenyi kukamilika namna ya kujieneza katika yote bila msaada wa yeyote.
11. Enzi ni taa ya ulimwengu, kadiri ya chemchem ya mwangaza wa aina yote.
12. Na itanguliapo taa, kifuatacho ni nuru yake.
13. Na ndio maana, baada ya utangulizi wa enzi tukufu, kilicho fuata ni nuru yake.
14. Nuru ni sehemu ya utukufu wa taa, kadiri ya uvuli wake.
15. Enzi ni taa kadiri ya ujuzi, ni fahamu kuu ambae humiliki kila kitu, isiyo zaufika wala kushindwa na chochote, ajili ya kuenea.
16. Na sehemu ya utukufu wake inayo mtoka kadiri ya nuru yake ni hewa (anga) kadiri ya fikara.
17. Neno lake ndio nuru yake ambae kutoka ndani mwake; imepatikana kadiri ya mapenzi yake na huzingatiwa kadiri ya nguvu yake namna ya utokezaji.
18. Ulimwengu na walimwengu vilifanyika kwa njia ya mapenzi yake.
19. Mungu akitaka kitu Fulani kipatikane hukiruhusu «kiwe» na mara «hupatikana».
20. Ni kwamba kwa kitu kupatikana inatakita kipangiliwe (mbele) katika mapenzi ya Mungu.
21. Umbiko hufanyika kwa njia ya neno lake kadiri ya mapenzi yake.
22. Na katika mapenzi yake ndio katika roho yake ; kwamba aliye katika mapenzi ya Mungu ni roho takatifu ya Mungu. 

23. Roho ya Mungu haipatikane katika uzima wake, lakini katika mapenzi yake.
24. Uzima wake ndio katangulia mapenzi yake ; kama vile taa itanguliavyo mwangaza.
25. Uzima ndio Enzi ambae ni dhati yake ; yaani ndio umungu.
26. Na mapenzi yake ndio nguvu yake kadiri ya roho yake ambae ni miongoni mwa nuru yake.
27. Roho yake sio dhati yake ; wala nguvu yake sio uwezo wake .
28. Uwezo wake ni mamlaka iliye dhatini mwake kadiri ya milki ya ushindi.
29. Mamlaka ya uwezo wake ndio katokeza nguvu yake kiutendaji.
30. Na nguvu yake ni miongoni mwa idhini yake kadiri ya tendo lake kiutokezaji.
31. Alipo kua akitawala peke yake kabla ya umbiko kufanyika, roho yake ilikua, mfano wa uvuli wake ; yenyi kufulumia katika neno lake hali ya kua mapenzi yake.
32. Roho na neno ni miongoni mwa nuru yake, na nuru yake sio Uzima wake.
33.
Na ndio maana hakuna roho – Mungu wala Mungu roho, na pia hakuna neno-Mungu wala Mungu – neno, kwani dhati yake haiwezi kuchangana na uvuli wake.
34. Umungu ni ukamilifu, ndani mwake hamuna utafauti wowote wala mipaka wala viungo, ispokua upekee kadiri ya uzima.
35.
Hakika Mungu mwenyenzi ni mumoja tu, mkamilifu katika sifa ya upekee, m’bora wa kutangulia.

[ 2 ]

1. Mwenyenzi Mungu alitangulia ulimweguni kabla ya vyote kupatikana.
2. Alikua amestawi katika utukufu wa dhati yake mwenyewe hali ya kua mwanzo wa vyote.
3. Lakini hakuona ya kama hali hiyo ya upekee pasipo vitu vingine ni kitu cha kushikamana nacho.
4. Ndipo alipo umba, kwa mapenzi yake, viumbe mbalimbali ili mamlaka yake itawale juu yao hali ya kua mufalme wa wote.
5. Akainua anga juu ya ukiwa, namna ya daraja katika umbiko.
6. Akaweka wanahewa-halisi juu ya wanahewa-haramu,na akaweka wanahewa-haramu juu ya wazilahewa, ili aitwe musimamizi wa wasimamizi, mtukufu wa daraja.
7. Uwingi wa viumbe vyake haukuunajisi kamwe utukufu wake huo wa ajabu, hakubadirika wala kutingizika, kupungua wala kuongezeka.
8. Ni yeye ndio hubadiri umbo zao kadiri apendavyo ; akiwafanyia mipaka katika umbo zao na katika maisha zao.
9. Na hudhihirisha uzaifu na upungufu wa kila umbo ili asalie peke yake katika ukamilifu.
10. Kadiri alivyo tangulia hali ya kua mwanzo wa vyote ndivyo atakavyo salia pekee hali ya kua mwisho wa vyote.
11. Wakati atakapo poza kila umbo, ili asalie mwenyi uzima hali ya kua yote katika yote kadiri ya mwanzo wa vyote. 12.
M’bora wa kutangulia ambae huanzisha na hukomesha vyote kwa mamlaka yake mwenyewe.
13. Mwenyi kutawala kabla ya viumbe, juu ya viumbe, na baada ya viumbe, mufalme wa milele.
14. Mtukufu anaye timiza kwa idhini, mshangiliwa wa viumbe ajaaye heshima, mjuzi aliye juu.
15. Hutoa neno lake kadiri ya mapenzi yake mfano wa nuru yake ku watu, ili kuwanusuru na shari ya giza.
16. Mara ya kwanza hutoweka katika utaratibu, mfano wa mwana Kondoo, kipindi cha ujengaji.
17. Na mara ya pili hutoweka katika ushujaa, mfano wa mwana simba, kipindi cha ubomoaji.
18. Siku hiyo neno la Mungu litasaga milima kuisawanisha ardhi, hakuta bakia bonde wala kisuguu:
19. Hakuta patikana mwengine mwenyi mamlaka ya kutenda badala ya Mungu mwenyenzi, ispokua yule atakaye

25

ruhusiwa, itakua kama ilivyo kua kabla ya uumbaji.
20. Na baadaye ndipo atakapo chamusha tena umbo atakayo idhinia, mola mtukufu, mfinyanzi wa maisha.
21. Hakika Mungu mwenyenzi hufanya vile apendavyo kwenyi viumbe vyake, wala hakuna aliye huru mfano wake.

[ 3 ]

1. Ujuzi haustahili kuanza kwa namna yoyote ile ajili ya ukamilifu wake.
2. Kinacho anzaka ni kile kipungufu kisisho kamilika ; kile kisicho jiweza na kisicho weza, kisicho jijua na kisicho jua lolote.
3. Ukamilifu ni utukufu, namna ya kuenea katika yote kimilki na kibusara bila upungufu wowote.
4. Ni hali tukufu sana pasipo doa wala kasoro, mipaka wala uzaifu wowote katika yeye.
5. Hakuna maanzio wala makomeo wala kasoro, mipaka wala utafauti ndani mwake.
6. Hakika kuanza na kukoma ni uvuguvugu utokao katika uzaifu na upungufu.
7. Mungu hukamilika pasipo upungufu wowote ajili ya kupatikana na milki ya ushindi,ambae ni uwezo wa kuenea kadiri ya mamlaka.
8. Mtukufu wa ajabu ambae uwezo wake ni muujiza wa maajabu, ambae kiumbe hakiweze kuukagua.
9. Fikara haikagui ujuzi, bali ujuzi ndio ukaguao fikara pasipo shuruli yoyote ajili ya ushindi wa milki yake.
10. Hakika tendo sio chochote mbele ya mtendaji, hawafanani wala kulingana katika hali zao.
11. Lau kama fikara ingeli fahamu siri ya utukufu wa ujuzi kama ingeli zidia ujuzi ama kulingana.
12. Na kama fikara ingeli zidia ujuzi isingeli fanyika bali kutangulia. Na ujuzi usingeli tagulia bali kuanza.
13. Mtoni haumezi kamwe bahari, bali bahari ndio imezayo mtoni.
14. Hakika umungu ni siri kubwa sana isiyo kaguliwa na yeyote ulimwenguni.
15. Kama kungeli kua wa kufichua siri hiyo ya utukufu wa umungu hasingeli fanyika huyo bali kutangulia; na siri hiyo isingeli tangulia bali kufanyika.
16. Lakini kuona kama hakuna azidiaye utukufu wa umungu, ndio maana hakuna ajuaye siri ya utukufu wa Mungu mwenyezi.
17. Kungeli kuwako ajuaye siri ya umungu, kama angeli kuwako ajuaye namna ya kutangulia kwake, ambae humfanana.
18. Na kama kungeli kuwako wa kumfanana, (wao wote) wasingeli tangulia hali ya kukamilika.
19. Maana ukamilifu haustahili kulingana wala kufanana na chochote, wala upungufu wa uwingi haumgusi kamwe.
20. Hakika kutangulia kwake ndio kukamilika kwake, hakuna mwegine aliye na hali tukufu kama hiyo.
21. Na baadhi miongoni mwa watu, baada ya kushindwa kukagua siri ya utangulizi, hulazimisha kila kitu kianze namna Fulani.
22. Na ilihali haiwezekane kiumbe kipatikane pasipo muumbaji kutangulia.
23. Ni kwamba ya faa kupatikane mmoja asiye kua zaifu ambae hutangulia bila msaasa wa yeyote atakaye weza kutokeza toka sifuru vitu mbali mbali
24. Milki yake hiyo iliyo muwezesha kutangulia bila kuanza ndiyo itakayo muwezesha kutokeza ambacho hakikua popote.
25. Hakika ni kawaida mtokezaji kutangulia bila kutokezwa, hasipo tangulia hawezi kutokeza toka sifuru, maana atakua mzaifu.
26. Maana uzaifu ule ulio mfanya ashindwe kutangulia mwenyewe bila kufanyika ndio utakao mfanya ashindwe kuumba.
27. Kama kweli kuna viumbe vilivyo fanyika, ni kwamba kweli kabisa kunapitakana mtangulizi asiye fanyika aliye wafanya.
28. Haiwezekane kiumbe, ambae ni zaifu na pungufu, kujitokeza chenyewe; kitajitokezaje na hali hakikua ila sifuru? 29. Hakutokee chochote bila utangulizi wa milki kibusara, milki yenyi ukamilifu ambae haifanyikake ajili ya kuenea. 30. Hufanyika ambae nizaifu na pungufu, ambae hukosewa milki ya kujieneza mwenyewe, ambae kabla ya kufanyika hakuwaka ila sifuru.
31. Uzaifu na upungufu huo wa kuwa sifuru muda Fulani haumgusi kamwe mwenyi uzima ambae pekee hutangulia.
32. Hakika utangulizi ndio mamlaka ya uumbaji; kwamba atanguliaye ndio aumbaye.

[ 4 ]

1. Ulimwenguni kumepatikana viumbe vingi sana: baadhi miongoni mwao ni wenyi maisha na wengine hawana maisha.
2. Ni umbiko ambaye kafanyika na mwenyi busara kamilifu, ambae hutokezwa bila yao yenyewe kufahamu wala kutaka, wala haikuwa na la kufanya ajili ya kutokuwa chochote.
3. Kiumbe ni zaifu sana mbele ya muumbaji wake, sio chochote wala lolote, wala kisingeli patikana bila idhini ya mfinyanzi wake.
4. Kuumba ni tendo la ajabu ,namna ya kugeuza sifuru kua kitu Fulani sambamba na idhini, maajabu ya kutokeza

26

ambae hakikua popote.
5. Ni mamlaka kubwa kadiri ya uwezo wa vyote ,ambae idhini yake hutenda.
6. Milki kuu isiyo patikana katika upungufu, ambae hupatikana katika ukamilifu peke yake.
7. Ni kwamba anaye stahili kuumba ni Yule aliye mkamilifu.
8. Na mkamilifu ni yule asiye na upungufu kimilki na kibusara, asiye zaufika kwa kuanza na kukoma, ambae hashindwake na chochote.
9. Na yule mkamilifu ambae hupatikana pasipo upungufu wa kuanza na kukoma ndio aliye tangulia, na atanguliae ndio mwenyi uzima.
10. Muujiza wa kutangulia ndio maajabu ya kuumba, yaani uwezo wa kupatikana bila kuanza ndio uwezo wa kutokeza ambae hakikua popote.
11. Kuona kama Mungu peke yake ndio aliye tangulia ulimwenguni ndiye peke yake aliye umba kila kitu.
12. Ni mwenyi milki kibusana izidiayo, yenyi uwezo wa kufanya kila kitu kadiri apendavyo, bila tatizo wala shuruli. 

13. Ni yeye aliye mkubwa wa vyote ku yote wala hakuna wa sawa yake, mtukufu wa daraja.
14.
M’bora wa kuumba aliye na milki ya ushindi, chemchem ya upatikanaji wa kila aina.
15. Kuumba sio kuunda ; kwani kuunda ni kubadiri umbo iliyo kutwa. Ni namna ya kutumia kitu ambae hakukianzisha. 16. Kwa kuunda chuma, hutumia jiwe ambae yeye hawezi kuifanya.
17. Hakika kuunda sio kutokeza toka sifuru, bali ni kubadiri umbo iliyo fanyika zamani.
18. Kuumba ni tendo la mwenyi ujuzi ; na kuunda ndio tendo la mwenyi fikara
19. Kilicho «umbwa» ndio umbo, na kilicho undwa ndio << chombo >>, ni tafauti kabisa umbo na chombo.
20. Umbo hutokezwa na mjuzi toka sifuru, lakini chombo hutokezwa na mwanahewa tokea umbiko.
21.
Hakika Mungu mwenyenzi ni m’bora wa kuumba, wapekee katika daraja hiyo, mshindi aliye juu.

[ 5 ]

1. Mwenyenzi Mungu ndio husababisha ulimwengu namna ya kuutokeza katika kuumba kwake.
2. Ni yeye awezaye ndio mwanzo wa yote, yaani ndiye mwanzishaji wa kila kitu.
3. Mwanzo wa vyote ndio chemchem ya upatikanaji wote na maisha yote katika ulimwengu.
4. Ni yeye mtangulizi ambae hutangulia awali peke yake namna ya kuenea kabla ya vyote, na baadaye hutokeza kila kitu ambae hupatikana ulimwenguni.
5. Ni hiyo milki yake ambae ni mamlaka kubwa sana na zaidi ndio kamfanya atangulie na pia atokeze kila kile kadiri ya mapenzi yake
6. Milki ya ushindi ni mamlaka juu ya kila kitu ambae huweza yote bila kushindwa na chochote
7. Haiwezekane Mungu kuanza sababu ya ushindi wa milki yake ambae hukamilika katika kuweza yote, maana kuanza ni alama ya uzaifu na upungufu wa kutopatikana hapo awali. Na ilihali uzaifu na upungufu haumgusi kamwe mwenyi ushindi kimilki.
8. Ni kwamba habari ya kuanza kwa kitu ni habari ya uzaifu na upungufu wake ambae hupatikana katika umbiko, haistahili kamwe kupatikana katika umungu.
9. Hakika tendo kuanza ndio alama kubwa sana ibainishayo uzaifu na upungufu wa kitu.
10. Na tendo kutangulia ndio alama kubwa iyakinishayo uwezo na ukamilifu wa kitu.
11. Maajabu kadiri ya muujiza wa kutangulia kwake huwasangaza sana watafiti ambae hujaribu kupapasa utukufu wa uzima, hata wakifikia kubisha sababu ya kushindwa, hata wakikubali umbiko peke yake.
12. Kama italazimika kila kitu kianze, ni kwamba hulazimika kila kitu kiumbwe
13. Na kama italazimika kupatikane viumbe peke yao, ebu tuambie ginsi vitakavyo umbwa pasipo muumbaji.
14. Ni muimu, lazima na kawaida muumbaji kutangulia mbele ya vyote, na baadaye ndipo hutokeza kila umbo kadiri apendavyo.
15. Maana kwa kiumbe kuumbwa, inatakika kutangulie milki kibusara itakayo weza na itakayo jua kutokeza umbo.
16. Viumbe haviwezi kamwe kutangulia ajili ya ukosefu wa milki kamilifu, na ndio maana hudai msaada kwa wao kupatikana.
17. Watatangulia je wenyewe na hali hapo awali hawakua ispokua sifuru?
18. Hakika umungu ni muujiza wa kutangulia ulimwenguni kwa walimwengu kupatikana.
19. Hakika umungu ni muujiza wa maajabu, milki isiyo fananishwa, fahamu isiyo na kipimo, mamlaka ya maajabu ulimwenguni.
20. Utangulizi wake ni muujiza una staajabisha viumbe ajili ya udogo wa fahamu yao ; na ilihali hii ndiyo hakika ya kawaida ya umungu.
21. Ni haki na kawaida kusangaa kuenea kwake ambae ni utukufu wa ajabu sana, mamlaka ya kutangulia hali ya kua yote katika yote, milele na melele
22.
Mola wa anga na ukiwa, M’bora wa kuenea ambae hakosekane kamwe muda wowote ule, wa pekee aliye huru, mtukufu aliye na uzima

27

[ 6 ]

1. Mwenyenzi Mungu aliumba kila umbo kwa haki, katika usawa wa kawaida ya umbiko.
2. Huwafanya katika utafauti, ajili ya uwingi wao, kufatana na upungufu wao.
3. Haiwezekane viumbe kua namna moja ajili ya kua na upungufu.
4. Na upekee ndio utukufu ambae hupatikana kwake mwenyi ukamilifu.
5. Kadiri ya umbile fulani ndio kadiri ya upungufu fulani ajili ya ukosefu wa milki kamilifu.
6. Jumuiya la upungufu mbalimbali hutimiza umbiko.
7. Ujuzi wa muumba ambae ni fahamu ya ajabu ndio humfanya atokeze viumbe vya kila aina, bila kurudishia ; maana busara yake ni kubwa sana, haitafute sura ya kutokeza wala kushindwa na utokezaji upya.
8. Ndio maana kumepatikana sura nyingi sana, ijapokua ni katika umbile moja lakini tafauti.
9. Utafauti wa hali zao hutokana na uzaifu pamoja na upungufu ambae ni asili ya umbiko.
10. Hakika hakiumbwe ispokua kipungufu ambae hakina ukamilifu.
11. Ijapokua viumbe huzidiana, sio kwamba muumbaji alipendelea baadhi miongoni mwao, bali kawaida ya umbiko
12. Maana pasipo uzidiano, utafauti usingeli patikana kati yao ; na kama utafauti usingeli patikana kwao bila shaka uwingi usingeli kua kwao.
13. Na kama uwingi usingeli kua kwao, kama wangeli kua katika upekee.
14. Na ilihali upekee haugusike kamwe na upungufu, wala haufanyikake, bali ndio utukufu wa muumbaji kadiri ya ukamilifu.
15. Eti itawezekana viumbe kua muumbaji? Ama ni kweli wote wawili wakuwe wakamilifu katika upekee?
16. Kumbe ya faa kukiri upungufu wa kila umbo kwamba ni kawaida kabisa, wala sio kosa wala upendelevu wa muumbaji.
17. Ni kweli kabisa mutu ni mwenyi makosa ajili ya kutengeneza kiato na kofia?
18. Lau kuma kiato kingeli zingatia kazi yake na kuilinganisha na kazi ya kofia kingelisema: hakika mutu hupendelea kofia sababu huiheshimu kwa kuibeba na hunizarau mimi kwa kunitesa na uzito wake kuni kanyaka.
19. Ebu tuambie ni kweli kabisa uyu mutu alifanya kosa kuunda kiato ? ama ni kweli kabisa alipendelea kofia?
20. Ndivyo pia kuhusu muumba na viumbe vyake. Hakika Mungu mwenyenzi hana hatia yoyote ajili ya kuumba umbo fulani na upungufu Fulani
21. Hakika kila umbo ilifanyika katika kawaida ya umbiko, ikifaa kadiri ya kipaji chake ulimwenguni.
22. Thamani ya umalaika ni katika utetezi wa uzuri katika kupinga ubaya.
23. Na thamani ya ushetani ni katika utetezi wa ubaya katika kupinga uzuri.
24. Haiwezekane kutetea uzuri katika kupinga ubaya wakati hakuna ubaya ulimwenguni.
25. Na pia haiwezekani kutetea ubaya katika kupinga uzuri wakati hakuna uzuri ulimwenguni.
26. Umbile zao zisingeli timilika pasipo wote wawili kuumbwa, wala maisha yao isingeli timilika katika kawaida yake. 27. Ni kwamba maisha ya malaika isingeli patikana bila ubaya kuumbwa.
28. Na pia maisha ya shetani isingeli patikana bila uzuri kuumbwa.
29. Maana utetezi baina yao ndio maisha yao walio pewa mfano wa kazi yao maalumu.
30. Na kama mmoja kati yao asingeli umbwa, bila shaka maisha ya mutu isingeli patikana, kwani maisha ya mutu ni utetezi baina ya uzuri na ubaya.
31. Uhai hupatikana katika uzuri ajili ya kuimarika katika kupinga ubaya.
32. Na pia mauti hupatikana katika ubaya ajili ya kuimarika katika kupinga uzuri.
33.
Hakika mwenyezi Mungu ni M’bora wa kuumba, mwenyi busara kamilifu; ni haki kumsifu na kumshukuru kuliko kumlaumu; ni upumbafu ulio-je kumlaumu ajuaye?
34.
Ametakasika mwenyezi Mungu bingwa wa kufahamu, atendaye katika kawaida ya kutenda, M’bora wa kukadiria.

[ 7 ]

1. Tukuzeni mwenyenzi kila siku maishani mwako, wala usipitiwe hata siku moja bila kumsifu na kumshukuru, maana ndiye pekee anaye stahili kuhimidiwa.
2. Mola mshindi wa walimwengu, mtukufu apangaye na apanguaye kadiri ya idhini yake, wala hakuna kilicho njee ya mipangilio yake, yaani hakuna kilicho kinyume na idhini yake.

3. Hupangilia katika kujua kila umbo; akifahamu bila kusahau yote yatakayo tenda kila umbo kabla ya kuziumba.
4. Na ndio maana huwaagiza yale watakayo tenda, na ilihali huyafahamu kabla ya kuwatokeza; ili kutimiliza kawaida ya umbile zao.
5. Ni maagizo yake ndio hutimiliza maisha ya kiumbe, maana kuagiza kwake ndio kuumba kwake, ni kuyaruhusu yapatikane kadiri ya idhini yake.
6. Hapana kulaumu amri ya Mungu, kwamba ni namna gani huwa agiza watu kuwawekeeni sheria;
7. Hayo ni kwa sababu alipenda kupatikane watakatifu miongoni mwao, ambae wata wa fuata wakaaji wa mbingu, ndio maana aliweka maamrisho yake.

28

8. Na pia kupatikane wachafu miongoni mwao ambae watafuata wakaaji wa hadeze; ndio maana aliweka makatazo yake.
9. Maana kauli yake tukufu hutenda kwa ajabu ya kutimiza idhini yake, yaani kutokeza kwa rafla kama apendavyo.
10. Na maagizo yake hayabadiri kamwe mapenzi yake wala kutafautiana, maana agizo lake hutokea mapenzini mwake.

 11. Mapenzi yake hupangiliwa naye kabla ya kutukiza, na hutimilizwa na kauli yake kadiri ya agizo lake.

12. Nayo mapenzi yake haikadiriwake, lakini hukadiriana katika usawa bila hatia yoyote.
13. Wala hadondokake katika kupenda kwake, na ndio maana haifai kushakia kawaida ya idhini yake tukufu wala kulaumu lolote katika tendo lake.
14. Maana yeye hujua na viumbe hawajui lolote, na huweza vyote na ilihali viumbe hawawezi lolote.
15. Je! Utamkosoa ambae hukuzidia? Ama ni kweli jembe itamuongoza mlimaji?
16. Ni lazima na kawaida kupatikane utafauti mkubwa katika umbiko sababu ya upungufu uliye asili ya umbo zao.
17. Huinuka juu ya viumbe maisha urakibuni, na pia hushuka chini ya viumbe, maisha uatiduni.
18. Kila kiumbe kinayo neema ya namna yake, lakini kuna daraja mbali mbali katika neema yao.
19. Hakika hupokea ujira mkubwa tokea mbinguni, katika urakibu.
20. Ni njia ya kwendea mbinguni, bustanini mwake mola karima.
21. Njia yenyi Baraka, ambae husalimisha umbo, ujira na faraja maishani.
22. Pendeni Mwenyenzi Mungu aliye tangulia kukupendeni kabla yako na kukutokezeni toka sifuru, na kukujaalieni maisha na vifaa vyake na nuru ili upate kushukuru.

[ 8 ]

1. Shuudieni utukufu wa mapenzi ya mwenyenzi ambae hujaza tabaka la anga na tabaka la ukiwa.
2. Hakutukie chochote wala lolote ulimwenguni ila ni ndani ya mapenzi ya Mungu mwenyenzi.
3. Na ambae hupatikana njee ya mapenzi yake Mungu, hukosekana ulimwenguni.
4. Ni timilifu sana mapenzi yake, ajili ya kutokea katika ukamilifu mfano wa uvuli wake.
5. Kuona kama upumbafu haupatikani katika mapenzi yake tukufu ndio maana hupatikana katika usawa kila atendalo. 6. Ni yeye mtendaji mkuu, wa kweli na haki, aliye na shani kamilifu mumiliki wa ulimwengu.
7. Hakika mambo yote hutendeka kwa niaba ya mjuzi, ni ajabu ilioje utimilifu wa tendo lake.
8. Kuona kama hakuna aliye na fahamu kama yeye ambae angeli fahamu siri ya uwezo wake huo wa ajabu, ndio maana hakuna awezaye kutefua ajabu ya kutenda kwake.
9. Mwenyezi huchipua toka sifuru shuruli ya kila namna kadiri ya kawaida ya umbiko.
10. Na huifadhika katika mwongozo wake, ndani ya kanuni tokea ukamilifu ambae ni nuru takatifu.
11. Nuru ya Mwenyenzi ni katika mapenzi yake, kadiri ya sehemu ya utukufu wake.
12. Kuona kama nuru ya Mungu ni uvuli wa utukufu wake yeye aliyeko milele, ndio maana nuru yake pia ni milele.
13. Tumieni maishani mwenu nuru ya enzi takatifu ili mupate karama ya uhai, maana ni nuru ya taa isiyo zimika.
14. Nuru yenyi ladha umboni kadiri ya usalama, zawadi ya utimilifu wa maisha
15. Na katika maisha, nuru hupatikana katika ibada ya Mwenyenzi.
16. Matumizi ya ibada ndio matumizi ya nuru takatifu ambae ni uadilifu kitendo kadiri ya usilimu.
17. Heri mutu aliye silimu maishani mwake, maana huchagua uhai ambae ni neema kubwa ya kuishi salama milele.
18. Ni neema na rehema kutoka kwa Mungu Mwenyenzi, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.
19. Usilimu ni mwenendo wa wakaaji wa sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani, ambae ni uadilifu na ustaarabu katika unyenyekevu.
20. Ni mila ya wakaaji wa mbinguni wenyi hidaya kadiri ya nuru maishani, ambae hutimiliza umutu.
21. Katika mpango ulio imarishwa na idhini tukufu, huko juu ya maala pa juu, ambae hujaa fahamu yote.
22. Kutenda adili na zamiri safi, katika unyenyekevu, ndio matumizi ya nuru katika njia iliyo nyooka.
23. Na aliye katika njia iliyo nyooka amekwisha faulu katika utetezi wake, na mambo yake yote ni katika usalama.
24. Maana ni katika mapenzi ya Mungu, na aliye katika mapenzi ya Mungu ni roho takatifu ya Mungu mwenyenzi.
25. Hakuna lisilo wezekana enzini ajili ya milki ya ushindi iliyemo na ndio maana hutawala yote milele.
26. Milki hiyo ni mamlaka ya ajabu katika kutaka, ambae utasi wake ni huru katika kutenda, ambae tendo lake ni utokezaji upya sambamba na idhni yake tukufu, mola hodari aliye na utukufu wa ajabu.
27.
Mkamilifu aliye na ushindi, msamehevu na mrehemevu, m’bora wa kuenea ulimwenguni.

[ 9 ]

1. Hii ni habari ya uzima wa Mungu Mwenyenzi.
2.
Mola wa anga na ukiwa, m’bora wa kuenea, aliye na shani kuliko vyote ulimwenguni.
3. Mtukufu aonaye yote pasipo kutazama; asikiaye yote pasipo shuruli ya kutekeleza, m’hodari aliye na ujuzi.
4. Ni yeye pekee aliye na uhuru, atendaye yote bila sharti wala shuruli  yoyote, ambae uzaifu na upungufu wa kufikiri haumgusi kamwe
5. Msaafu aumbae katika usawa, akiongoza peke yake vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani; taa tukufu ya

29

ulimwengu
6. Nuru humfumuka kwa wingi, hidaya ya anga na ukiwa ambae humulika kadiri ya kuzagaa juu ya ulimwengu
7. Mtakatifu wa ajabu, aliye stawi arshini peke yake, akijaa utukufu na heshima.
8. Ameinuka kuliko vyote, wala hakuna mwengine mfano wake katika daraja; mufalme wa wafalme wote
9. Mwenyi milki ya ajabu isiyo tokea wala kuendea, kupungua wala kuongezeka, wa pekee anaye enea kabisa.
10. Mamlaka juu ya kila kitu, utukufu wa milele, thamani ya ulimwengu
11. Hakuna mfano wake angani na ukiwani, mteza nguvu, afanyaye apendavyo
12. Mwenyi kujaa hali ya kua yote katika yote akienea pote, katika milki na katika busara
13. Ni yeye aliyeko daima na imara pasipo kufanyika wala kufanyiwa mtukufu atanguliaye
14. Akienea peke yake awali hali ya kua mwanzo wa vyote ulimwenguni
15. Mshindi asiye tanguliwa na yeyote ku vyovyote, ambae ukamilifu wake hukosekanisha kabla na baada dhatini mwake.
16. Muhimidiwa aliye na sifa kamilifu, ambae utukufu wake huienea mbingu na dunia.
17. Mkuu aliye juu, mola wa nyakati zote, aliye tayari muda wote kumiliki ulimwengu.
18. Niyeye peke yake asiye fikiwa na yale asiyo ya taka, ambae huhukumu yanayo tendeka ulimwenguni.
19. Hakika Mungu ndio mzima, ajaaye utukufu wakuenea, wala hakuna mfano wake wala wakutaniana naye, mkuu aliye na uwezo wote.

[ 10 ]

1. Ametakasika mtukufu aliye na ushindi, mola mshangiliwa, bingwa wa mabingwa ulimwenguni.
2. Mwenyi ufalme wa ajabu, ambae hukamilika pekee, juu ya maala pa juu, hali ya kujaa fahamu yote, enzini.
3. Aliye kwa siri bila mfanano, mtegemewa wa haki.
4. Ndiye mjengaji wa umbiko, atendaye kwa kasi la idhini yake .
5. Msifiwa wa ajabu aliye na mamlaka ya kumiliki, ambae viumbe humtaja kwa majina mengi kadiri ya kutenda kwake. 6.
Wakali anapo jenga umbiko humuita; M’bora wa kuumba, m’neemeshaji mwingi wa rehema, baba wa salama...
7. Na wakati wa ubamoaji humuita: M’kali wa kuadhibu, mdhikishaji na mkomeshaji, bingwa wa banashari...
8. Na kujenga kwake na kubomoa kwake ni katika baadhi la juu angani
9. Maala ambae muumbaji kawa kadirieni maisha na mauti, katika mpango ulio imarishwa na idhini tukufu.
10. Akaweka uhai juu ya maki ya mbingu, na mauti chini ya mbingu
11. Na hulinda siri ya umbiko la wanahewa haramu katika maunganio ya mbingu na hadeze.
12. Ni maala mfano wa baraza la kambi, hujumuika humo kabla na baada ya kuishi duniani, kwa muda muchache tu
13. Na badaye hujumuika kila yule kambini mwake ambae zamiri yake hutegemea.
14. Mwenyenzi huwaneemesheni kuwatayarishieni kambi iliyo bora sana kwao wafanyao ibada duniani. Na pia iliyo mbovu sana kwao wafanyao uovu duniani.
15. Akikupambieni bustani na nuru kubwa; nuru yenyi ladha umboni, pumzi yenyi manukato.
16. Huninginia ndani mwake, mfano wa nyota katika kumeremeta, wajumuikao.
17. Hakika shukrani ni zake mwennyenzi Mungu, mola wa majeshi yote, aliye na mamlaka yote.
18.
M’bora wa wapodoaji ambae rangi yake huokoa umbo ijipakaayo, mpanaji wa daraja.
19. Mzima aliye muujiza katika kutangulia, na maajabu katika kuumba mtukufu asiye linganishwa.
20. Hufanya apendavyo ajili ya kujaa milki kamilifu ambae huweza yote.
21. Ni mkubwa saana mwenyenzi mungu, mwingi wa baraka ambae hujaa heshima na sifa kamilifu.
22. Na humtukuza vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani, mola wa kila umbo, mkamilifu katika yote.

[ 11 ]

1. Sifa na heshima humustahili mwenyenzi Mungu aliye kikweli ambae hualikwa na walimwengu kuhitaji msaada wake, mlezi wa viumbe.
2. Mjuzi asiye sahau wala kusinzia, muonaji na msikiaji wa jumla ya viumbe
3. Ameona yote ulimwenguni na ilihali hana kiungo chochote kiitwacho jicho ndani mwake.
4. Na husikia yote ulimwenguni na hakuna kiungo kiitwacho sikio ndani mwake.
5. Na pia husema na ilihali hana kinywa dhatini mwake.
6. Ujuzi wake huzidia macho kwa kuona, na huzidia masikio kwa kusikia, na pia ujuzi wake huzidia kinywa kwa kusema.
7. Hakika kujua ni kuweza yote, hakuna kisicho fanyika na mjuzi.
8. Ni mwenyi utukufu sana ambae macho ya viumbe hayawezi kumzingantia, ispokua kwa njia ya vitimbi vyake, machoni kiroho.
9. Maana kinacho onaka umboni mwa mutu ni huo mjengo kihewa ambae ni pumzi.

30

10. Pumzi ni mjengo kihewa, kuona kama hewa ndio fikara, ni kwamba mjengo kihewa ndio mjengo kifikara.
11. Kuona ni kufahamu, na kusikia pia ni kufahamu
12. Maana pumzi ni fikara, na fikara ni fahamu ; kumbi kinacho onaka katika umutu ni hiyo fikara ambae hufahamu, ni yao ndio macho ionayo.
13. Na pia kinacho fanya mutu asikie ni fikara, ni yao ndio masikio isikiayo.
14. Jicho na sikio kimwili ni viungo mfano wa njia ambae fikara hupitia kwa kuona na kusikia, yaani kwa kufahamu. 15. Katika umbo la mwanahewa-haramu, kuna aina tano ya mapito ya fikara yake kwa kufahamu jambo.
16. Ni katika viungo vitano vya utambuzi, na vyao ni ; jicho, sikio, ulimi, pua, na mwilini mwake.
17. Mapito ya fikara katika jicho ndio utazamaji ; na katika pua ndio unusaji ; na katika ngozi ama mwilini mwake ndio ugusaji ; na katika ulimi ndio uonjaji.Na katika sikio ndio utekelezaji.
18. Mutu huzingatia kimwili kwa njia ya utazamaji, utekelezazi, unusaji, ugusaji na uonjaji.
19. Uzingatiaji kimwili hutambua umbiko peke yake, wala hauwezi kuzingatia enzi tukufu ambae ni tafauti sana na umbiko.
20. Huzoroteka uzingatiaji kimwili ajili ya ujinga upatikanao mwilini.
21. Na ndio maana kwa kumuona Mungu Mwenyenzi sio kawaida kumtazama kimwili, lakini ni kawaida kabisa kutumia utaalamu kifikara ambae ni akili, kadiri ya utazamaji kiroho kwa ku zingatia uzima wa Mungu.
22. Hushukiwa na nuru akili urakibuni, na pia hufunikwa na giza akili uatiduni.
23. Akili hutimilika katika matumizi ya ibada, hakika huzingatia bayana utukufu wa Mwenyenzi, yule afanyaye ibada katika mustari wa neno la Mungu.
24. Akipata kuzingatia utukufu wa enzi kwa njia ya mbingu takatifu, akionana na watakatifu, wa mbinguni ambae humnukulu mola wa walimwengu.
25. Hakika fikara huzingatia kidogo tu katika kupapasa, ispokua ujuzi ndio uonao kikweli.
26. Na ndio maana muonaji wa kweli ulimwenguni ni Mungu peke yake, mshindi ajuaye.

[ 12 ]


1. Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu, ambae peke yake katangulia ulimwenguni kadiri ya kuenea.
2. Mwenyi kuwako kikamilifu kwa ushindi wa milki yake, akitawala juu ya yote ulimwenguni kwa mamlaka yake mwenyewe
3.
Mtukufu zaidi ya vyote hodari aliye na sifa na heshima, mkuu na m’bora wa mashujaa katika kutenda, chemchem ya baraka ulimwenguni.
4. Aliye mwanzo wa vyote ajili ya kutangulia, mamlaka ya ajabu itokezayo, wa pekee aliye na ujuzi, mshindi aliye juu. 5. Hakuna aliye mtangulia yeye ajili ya kutokuanza, maana hutangulia kabla ya matukio yake.
6. Hakuna «kabla» yake ajili ya kutokuanza ; angeli kua na mwanzo wake kama kungeli patikana kabla yake, maana kungeli kua muda wa mbele ya tarehe ya kuanza kwake.
7. Na pia hakuna «baada» yake ajili ya kutokua na mwisho wake, angeli kua na ukomo wake, kama kungeli patikana baada yake ; maana kungelipatikana muda wa nyuma ya upatikanaji wake kiisha tarehe ya ukomo wake.
8. Mwenyenzi hushinda maanzio na hushinda makomeo, mtukufu aliye na shani ya ajabu, ambae hupatikanisha vyote ulimwenguni
9. Hutangulia namna ya kuenea, kadiri ya ukamilifu akihepukana na upungufu wote.
10. Hakika ni bahati na furaha kwetu enzi tukufu kutangulia, kama sivyo sifuru ingeli tawala milele, maana hakungeli patikana watu wala kufanyika lolote.
11. Ni muujiza ulio-je kutangulia kwake? hakika hali kama hiyo ndio utukufu wake huo wa ajabu ya kuenea katika yote.
12. Na utukufu wake huo wa ajabu ya kuenea katika yote ndio ukamilifu ambae ni uzima
13. Na ukamilifu ni katika upekee ajili ya ushindi wa milki yake
14. Ndio maana kuna Mungu mmoja tu bila mshirika ambae hutawala ulimwenguni, milele na milele.
15. Kama kungeli kua mwengine wa namna yake hasingeli kua na ukamilifu, maana uwezo wake ungeli kua na mipaka, kwani hasingeli kua na utasi juu ya mwenzake.
16. Na hali kama hiyo ya uzaifu wa kushindwa na fulani ndio upungufu ambae haumgusi kamwe mkamilifu.
17. Na kama angeli kua na mipaka kimilki na kibusara hasingeli kua na uwezo wa kuumba, bali angeli kua na ginsi ya kubadiri kimatumizi umbo aliyo ikuta tayari imekwisha umbika, wala hasingeli tangulia bali angeli anza .
18. Ni kwamba ukosefu wa milki kamilifu hufanya kitu kiwe na mwanzo wacho hali ya kua kiumbe sambamba na makadirio ya mshindi aliye kamilika .
19. Hasingeli enea mshindi lau kama kungeli kua mwengine, maana katika ukamilifu hakuna utafauti wala mipaka, kufanana wala kulingana na chochote

[ 13 ]

31

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu-m’bora wa kukadiria, mola mtukufu, mkuu wa wapanaji
2. Ni yeye aliye enea ulimwenguni, ambae peke yake huepukana kabisa na asili.
3. Asili hupatikana kwao viumbe, ambae hukosewa milki kamilifu.
4. Viumbe wenyi fikara timamu hutafuta ufahamu wa asili yao, wakijifunza hakika ya matokeo yao na maendeleo yao katika ulimwengu

5. Umbo zao na maisha zao ni karama kutoka kwa Mwenyenzi Mungu, mola wa walimwengu.
6. Hutokezwa toka sifuru, viumbe vyote, pasipo matakwa yao, wakikadiriwa umbo bila kuichangua wala kuhelewa mradi wake.
7. Wakitayarishiwa vifaa vya maisha yao kabla ya umbo zao kufanyika, hata wakitokezwa sambamba na idhini yake.
8. Hakika viumbe ni zaifu sana, umbiko kiusaidizi, ambae hudai msaada kwa wao kuishi.
9. Kuona kama wamepatikana ulimwenguni pasipo manuizi yao, ndio maana maisha yao hupangiliwa na yule aliye watokeza toka sifuru.
10. Kwani wao wenyewe na maisha yao ni mpango ulio pangwa na muumba aliye kwa siri.
11. Na pasipo mpango wake mwenyenzi, maisha yao ni bure hali ya kukosekana .
12. Wote kwa jumla huishi kwa idhini tukufu ya muumba wao wala hakuna maisha njee ya idhini yake tukufu.
13. Kuona walifanyika pasipo wao wenyewe kutambua wala kutaka ,mamlaka ni kwake Mwenyenzi kuwakadiria ginsi apendavyo.
14. Huwakadiria umbo, maisha na sheria kadiri ya mapenzi yake, kwa njia ya neno lake.
15. Hupatikana wote kwa njia ya neno lake na pia huishi kadiri ya neno lake.
16. Ndio maana kila mutu hulazimishwa kutumia neno la Mungu ili apate uhai, maana maisha kinyume na nuru ya Mungu hukoma namna ya kupotea.
17. Mwenyenzi Mungu aliwatokeza wote namna moja, katika idhini yake tukufu, lakini ka fanya utafauti katika umbile zao ili uwingi upatikane kwao.
18. Huandalia katika kawaida ya umbiko, shuruli fulani kadiri ya kipaji fulani, utimilifu wa karama.
19. Haimjuzu Mungu kutokeza umbo moja peke yake maana upekee haustahili kwake yule asiye na uwezo wa vyote, maana ni mzaifu ambae hudai msaada, bali hustahili yeye aliye mkamilifu, ambae huweza vyote bila shuruli wala tatizo lolote.
20.
Na hii ndio kawaida : ‟upekee katika umungu, na uwingi katika umbiko”
21. Uwezo wa vyote husababisha upekee katika ukamilifu kadiri ya uzima ambae ni umungu.
22. Na upungufu ndio husababisha utafauti, na utafauti ndio husabisha uwingi, katika umbiko.
23. Ni kawaida kila umbo kupatikana na upungufu fulani, maana upungufu ndio asili yake, yaani alitokea katika upungufu.
24. Hakiumbwe ulimwenguni ispokua kipungufu, ambae ni zaifu kinyume na uwezo.
25. Ni hiyo hali pungufu kadiri ya sifuru ndio uzaifu ambae hugeuzwa na milki kamilifu kua kitu fulani.
26. Kimegeuzwa ajili ya kua zaifu, maana kisingeli kua pungufu na zaifu kama kisingeli umbwa, kwani kingeli kua kamilifu kadiri ya kuenea kimilki na kibusara.
27. Kilicho umbwa ni kitu pungufu na zaifu, hakika umbo fulani ni upungufu fulani.
28. Kilicho kamilika hakiumbwake ajili ya kuenea pasipo maanzio wala makomeo.
29. Ni kwamba haifai kumlaumu muumbaji ajili ya kuumba umbo fulani na upungufu fulani.
30. Kama italazimika umbo fulani isiwe na upungufu wowote, ni kwamba hulazimika umbo ile kua kamilifu.
31. Na kama umbo fulani italazimika kua na ukamilifu, ni kwamba umbo iyo hulazimika kua muumbaji, maana ukamilifu haupatikani ispokua katika umungu.
32. Eti viumbe havistahili kujumuika ulimwenguni ispokua muumba peke yake?
33. Wapumbafu humlaumu Mola wa walimwengu ajili ya utafauti wao usababishwao na upungufu wao, wakitarajia ukamilifu hali tukufu ya upekee kadiri ya umungu.
34. Bila kutambua ya kama ukamilifu haufanyikake wala kufanana na yeyote munamna yoyote ile ajili ya kuenea.
35. Hakika aliye na anaye stahili ukamilifu ni Mungu peke yake, lakini viumbe vyote ni katika upungufu.

[ 14 ]

1. Utakatifu ni wake Mwenyenzi Mungu, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe; Mola wa wanahewa na wazila hewa, mshindi aliye juu.
2.
Huongoza kwa kauli yake tukufu, m’bora wa kutenda ambae hutokeza kila upatikanaji ulimwenguni.
3. Ni yeye mkadiriaji wa kila umbo, aongozaye umbo baada ya kuipatikanisha .
4. Ameinuka sana zaidi ya yote, mwenyi mamlaka ya kuenea katika ulimwengu.
5. Akihukumu kihakika vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani pasipo msaada wala shauri la yeyote
6. Ni kwa sababu hakuna mwengine aliye kamilika kama yeye ndio maana husalia peke yake katika utukufu wa ajabu 7. Mjuzi wa siri, ambae hutefua ndani ya kila zamiri, tajiri wa habari ulimwenguni

[ 15 ]

32

1. Ni nani anaye mkanusha Mwenyenzi Mungu?
2. Ni nani yule anaye shakia uzima wa muumba wake?
3. Je! Amejidai mwenyewe kwa dalili gani?
4. Eti ni yeye ndio katangulia bila kuanza ambae hustaili kuumba walimwengu?
5. Ama ni yeye ndio muweza wa vyote na Mjuzi wa vyote vilivyomo ulimwenguni? 6. Ama ni kweli yeye ndio mkamilifu asiye gusika na upungufu wowote?
7. Ama huzani kama ulimwengu na walimwengu hujitokeza vyenyewe katika sifuru?


[  16 ]


1. Humkanusha Mwenyenzi, kwamba hakuna utukufu wa namna hiyo, ajili ya uchache wa elimu.
2. Fikara yao hukomea katika mwili, kwamba kilicho na mwili ambae njia tano ya fikara kupitia hudhatiti ndio kipatikanacho.
3. Huo ndio upumbafu wa kweli, hawazingatie ila kidogo tu.
4. Tazama! kunapatikana sehemu zingine kubwa saana kuliko dunia, namna ingine ya upatikanaji kinyume na hali ya dunia, ambae utazamaji kimwili hauzingatie hata kidogo.
5.
Katika sehemu hizo hupatikana baadhi tukufu kabisa la ‟Enzi”, ambae hujaa milki kibusara.
6. Ni milki hiyo ndio huweza kufanya yote, ambae haigusike na uzaifu wala upungufu wowote ajili ya ushindi.
7. Na milki hiyo ya ajabu, yenyi kujua na kuweza yote ndio enzi yake Mungu.


[ 17 ]


1. Shuudieni uzima wa mwenyenzi ulimwenguni.
2. Hakika viumbe vyote ni hunusu na vipande, ambae kafanyika muda falani.
3. Hawakuwa muda fulani na hawata kuwa muda fulani.
4. Ni wavuguvugu katika upatikanaji wao ajili ya kukosewa milki kamilifu.
5. Ni milki hiyo ndio hustiri upatikanaji pasipo kutingizika wala kubadirika.
6. Ni hali tukufu sana kadiri ya utangulizi ambae huenea katika yote, pekee.
7. Utangulizi ni namna ya kupatikana bila mwanzo wala mwisho ni hali tukufu sana kadiri ya ukamilifu, na ukamilifu ndio uzima; na uzima ndio umungu.


[ 18 ]

1. Mutu hukosewa milki ya ushindi, ni umbo zaifu kabisa, yenyi kuzoroteka kimilki na kibusara, ajili ya kuvaa mwili. 2. Maana mwili ni ujinga, hushirikishwa fikara na ujinga ndani mwake.
3. Ndio maana mutu hufikiri na husahau, namna ya kuzingatia na kulala.
4. Kupitiwa namna ya kulala ndio tunda la mwili, na pia kufikiri namna ya kuzingatia ndio tunda la pumzi.
5. Hakika mutu ni umbo pungufu sana, ambae haina uwezo wowote wa kupatikana bila msaada.
6. Ni umbo zaifu sana isiyo weza lolote.
7. Umbo yenyi kufuata kanuni ya mshindi, ambae peke yake bila msaada isingeli patikana ulimwenguni.


[ 19  ]


1. Ulimwenguni kuna utangulizi wa milki kibusara ambae ni mamlaka ya kuweza na kujua yote, ambae uzaifu haupatikani ndani mwake.
2. Mamlaka yake huenea katika yote kimuujiza bila kuanza wala kukoma. Mola mshindi, uwezo wa milele.
3. Ni kwa sababu huenea (katika yote) ndio maana hakuna maanzio yake, maana huanza kile kisicho enea ambae ni kipungufu.
4. Milki hiyo ya kuenea pasipo mipaka ndio daraka kubwa sana na zaidi kadiri ya uwezo wa vyote.
5. Na uwezo wa vyote ndio mamlaka ya uumbaji ; haumbe ispokua yule aliye na uwezo wa kutenda yote.
6. Muujiza wa kuenea ndio maajabu ya kutokeza ambae hakikua popote ulimwenguni ; ni uwezo wa ajabu ambae hakuna kiumbe kiwezacho kuukagua ajili ya udogo wa fikara mbele ya ujuzi.
7. Hakika mjuzi ndio hutangulia, kadiri ya kuenea ; na pia pekee hutokeza, kwa mamlaka yake, ambae hakikua popote ulimwenguni.

[ 20 ]


1. Ujuzi ni busara kamilifu, fahamu ya ajabu sana ambae haishindwe wala kusahau kitu.
2. Na fahamu ya vyote ndio milki kibusara, ambae ni ushindi juu ya kila kitu.
3. Na ushindi juu ya kila kitu ndio uwezo wa vyote, mamlaka ya kumiliki kila jambo.
4. Hakuna mwengine aliye na mamlaka mfano wake, wa pekee aliye stawi arshini.
5. Viumbe vyote ulimwenguni hulindwa naye, wala hakipatikani chochote kinyume na idhini yake.

33

6. M’bora wa kutenda, aliye na kasi ya ajabu mapenzini mwake.
7. Mungu mwenyi uzima, ajaaye utukufu mkuu asiye zembea wala kuchoka, mtakatifu wa kweli, aliye juu.

[ 21 ]

1. Mwenyenzi huenea maala pote katika yote, mwenyi utukufu usiye pungukiwa kitu, mshindi ulimwenguni.
2. Ni mwenyi uhuru kiupatikanaji, ambae hujaa katika kua, akistirika milele na milele.
3. Hupatikana pasipo mipaka namna ya kutawala pasipo ukomo ulimwenguni.
4. Ni mwenyi kuwako daima, ambae hakukosekana wala hata kosekana muda wowote ulimwenguni.
5. Ni kwa sababu Mungu pekee ndio mkamilifu mwenyi kuenea katika uwezo na katika busara.
6. Milki yenyi ushindi kibusara aliyo nayo ndio humkamilisha namna ya kuhepukana na upungufu wote.
7. Hakika mkamilifu ni mbalimbali kabisa na mpungufu, maana yule ni muweza yote, na uyu ni zaifu sana ambae hawezi chochote.

[ 22 ]

1. Haiwezekane kamwe sifuru kutenda, na ndio maana inatakika, kwa hakika, utangulizi wa milki yenyi ushindi ili tendo ipatikane.
2. Ni kwa sababu sifuru ni ujinga ndio maana haina ginsi ya kutenda.
3. Ujinga hauwezi kutenda lolote sababu ya kujaa uzaifu na upungufu ndani mwake, ispokua ujuzi ambae hujaa uwezo na ukamilifu ndio uwezao kutenda, ajili ya kuenea.
4. Kuenea ndio kukamilika, namna ya kutokua na upungufu wowote
5. Na ambae huenea ulimwenguni ndio yule ajaaye ujuzi, mwenyi mamlaka yote ku vyote, mtukufu wa ajabu.
6. Ni yeye atanguliaye na aumbaye, aliye shinda ; ambae utukufu wake na mamlaka yake humtenganisha na sifuru milele.
7. Ni lazima milki ya ushindi itokeze vitu mbali mbali toka sifuru, kwa umbiko kupatikana, kama sivyo hakungeli tukia chochote wala lolote katika sifuru.


[ 23 ]


1. Kuona ni kufahamu, na kuonekana ni kufahamika.
2. Sio kwamba kuzingatia na kiungo cha mwili kiitwacho jicho peke yake ndio kuona.
3. Fahamu hupatikana kwa njia nyingi, maana fikara ni shuruli kubwa sana
4. Ni utaalamu ndio huleta ufahamu wa aina nyingi ambae mwili hauwezi kuzingatia.
5. Ni kwamba anaye zingatia utukufu wa mwenyenzi amemuona Mungu, maana amefahamu ya kwamba kuna Mungu. 6. Na yule asiye zingatia utukufu wa Mwenyenzi ndio kipofu asiye muona Mungu wala hawezi kufahamu ya kwamba kuna Mungu ajili ya uchache wa fikara yake.
7. Mutu hawezi kuonana na Mungu uso kwa uso sababu hawalingane kibusara; maana kuonana uso kwa uso ni kufahamiana sawa sawa; na kufahamiana sawa sawa ni kua katika daraja moja ya busara, kwamba kadiri ya fahamu ya uyu ndio pia kadiri ya fahamu ya yule, hata wakifahamiana namna moja
8. Mungu hujua lakini mutu hajui ; ndio maana mutu huzingatia tu utukufu wa mwenyenzi bila kuonana naye, maana kuonana ni kufahamiana
9. Haiwezekane kufahamiana na yule asiye kua na daraja moja nawe katika busara.
10. Mungu kutoonekania viumbe ni hasa ajili ya ukubwa wa daraja ya busara yake mbele ya viumbe.
11. Daraja ya busara yake ni kubwa sana na zaidi ambae viumbe hawaoni hata pa kuanzia wala pa kukomea katika utafiti wao ; na ndio maana uzima wa Mwenyenzi ni muujiza mkubwa sana mbele ya viumbe .
12. Viumbe hustaajabu sana hali hiyo tukufu ya mwenyenzi Mungu, ambae, haikurubiane kamwe na hali zao zaifu.


[ 24 ]


1. Ulimwengu ni jumla ya tabaka tatu : la enzi, la anga na la ukiwa.
2. Katika enzi hupatikana utukufu wa ajabu sana ; maana ndio shina kadiri ya chemchem ya vilivyomo angani na ukiwani.
3. Enzini hujaa ujuzi pekee, milki kuu ajabu ambae haifanane na chochote.
4. Na angani hupatikana fikara ya kila aina, na utukufu haupatikane humo ispokua chembeya huko juu katika sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani.
5. Na ukiwani hupatikana ujinga, hamna utukufu wowote ajili ya giza, ni maala pa zaifu sana ambae hapafanyike lolote. 6. Na anaye patikana enzini ndio Mungu pekee mtukufu na mbora wa kuenea ambae hustawi katika uhuru. Hakuna maikalio yake kwani hana kiungo chochote ndani mwake wala kimo. Hakae wima wala chini sababu ya kuto fanana na kiumbe.
7. Ni mkamilifu wa ajabu ambae hafanane na maikalio ya yeyote miongoni mwa viumbe; maana maikalio fulani ni namna ya upungufu fulani.

34

8. Mungu muweza atafananishwaje na umbo alizo ziumba ? kila umbo ni pungufu na zaifu tafauti kabisa naye mkamilifu aliye na uwezo wa vyote.
9. Hakika uzima wa Mungu ni jambo kubwa sana na zaidi kadiri ya muujiza usio fananishwa wala kulinganishwa na upungufu wowote.

10. Ndio maana haifae kulinganisha uzima na maisha maana maisha ni upungufu na uzima ni ukamilifu. 11. Wala Mungu hakae angani wala ukiwani; maana yeye sio mwanaanga wala muzilahewa.
12. Lakini kuona kama Mungu hustawi enzini pekee ndio maana huitwa kwa jina la Mwenyenzi.

[ 25 ]

1. Aliye na uwezo wa vyote hataabikake wala hashurulikake ajili ya chochote, mola mshindi apatikanaye enzini. 2. Atakavyo hutukia bila kazi yoyote; ni mwenyi mamlaka ya kutenda bila shuruli.
3. Kazi hufanyika na wazaifu wasio kua na milki ya ushindi.
4. Hushurulikia utimilifu wa umbo zao ajili ya kusongwa na upungufu.

5. Ndio maana hutetea muda wote maishani ajili ya kutokamilika.
6. Na utetezi wao ndio maisha yao kadiri ya kazi maalumu walio pewa, namna ya shuruli kubwa ya kutafuta ginsi ya kutimiliza umbo zao ambae hutatizwa namna ya kuzoroteka na upungufu.
7. Na upungufu huo ambae huzikumba umbo zao ndio asili yao.
8. Na asili yao hiyo ya upungufu ndio msingi wa umbiko lao, maana wasingeli umbwa bila kua upungufu.
9. Hakiumbwe ispokua kipungufu; maana kilicho kamilifu hakifanyikake kwa namna yoyote ile.
10. Ni asili ya umbo, ambae ni upungufu, ndio humtatiza kiumbe namna ya kutetea, akifanya kazi mbalimbali ili apate utimilifu.
11. Lakini kwake aliye kamilifu hakuna tatizo lolote wala shuruli, wala hafikiwake na asiyo ya taka, wala hatumikake kwa kutenda jambo.
12. Mwenyenzi mtukufu hutenda kwa idhini yake, atakavyo hutukia kwa rafla, mumiliki aliye na shani ya ajabu.
13. Na ndio maana Mungu peke yake ndio aliye stawi hali ya kuwa huru kabisa, ambae hataabikake kwa kufanya kazi yoyote ile.
14. Huko mwenyenzi huongoza umbiko baada ya kuitokeza toka sifuru.
15. Na uongozi wake huo sio kazi mfano wa uongozi wao viumbe, bali kwake hufanyika kila jambo kwa idhini, bila shuruli yoyote.
16. Ni ajili ya kua na milki ya ushindi ndio maana Mungu hagusike na shuruli yoyote ile.

[ 26 ]

1. Ni upumbafu sana kulinganisha uzima na maisha.
2. Maisha ni uzaifu mkubwa, ni upungufu usio na thamani pasipo msaada.
3. Na uzima ndio milki ya ajabu sana, namna ya kuenea katika yote, thamani ya ulimwengu ambae pasipo yeye kusingeli fanyika chochote ; ni ukamilifu kimilki ambae hutenda kwa idhini bila shuruli.
4. Kumfananisha mzima na yule anaye ishi ni upumbafu kabisa.
5. Ni uchache wa akili ndio hufanya watu wamfananishe Mola wao na hali zao zaifu, maana wamezani ya kwamba hufanana na wao.
6. Mungu muumba hana maisha ya aina yoyote ile ajili ya kuenea, ni mwenyi uwezo wa yote ambae hagusike kamwe na uzaifu huo wa kuishi, kwani kuishi ni kutetea kadiri ya shuruli kifikara.
7. Mtukufu asiye gusika na shuruli yoyote, ambae mapenzi yake hutimiza bila kazi, mshindi aliye na mamlaka ya ajabu. 8. Mwenyenzi ni mwenyi uzima tafauti na maisha ; ni mwenyi kuenea, katika kuwako, ambae hutangulia ulimwenguni. 9. Wanahewa ndio wenyi maisha, ambae hutaabika na shuruli ya kutetea, ambae hutumika kazi ili kudumisha umbo zao.
10. Hutaabika ajili ya uzaifu na upungufu katika busara, hawana milki kibusara.
11. Hakika kutamka tu «maisha ya Mungu» ni kukufuru kabisa ni kama kumtusi kadiri ya kuunajisi utukufu wake wa ajabu.
12. Hakuna mwengine aliye kamilifu ulimwenguni kama vile Mungu ; ni yeye pekee aliye na uzima, ambae uzaifu na upungufu wa kuishi haumgusi kamwe.

[ 27 ]

1. Enzini kuna heshima kubwa sana ; hakuna ila utukufu mtupu kadiri ya upekee.
2. Naye mwenyenzi hustawi katika heshima kubwa sana, msifiwa aliye inuka zaidi, mkuu.

35

3. Hakupatikane utafauti, shuruli wala uwingi wala upungufu ndani mwake.
4. Ni kwa sababu humo ni eneo la milki kibusara ambae haina kasoro wala doa, hakuna palipo wazi ambae pangeli jazwa.
5. Uwingi hupatikana angani na ukiwani, maala penyi uzaifu na upungufu, ambae hujazwa na mumilki aliye yatokeza toka sifuru
6. Mungu mwenyenzi ni mkamilifu ambae uwingi hauna fasi kwake, ni mwenyi upekee ajili ya kuenea
7. Na ndio maana hukamilika peke yake enzini bila wa kuchangia naye fasi.
8. Kama huitwa Mwenyenzi ni kwa sababu ya kupatikana peke yake humo enzini, hakuna wenyenzi, bali kuna mwenyenzi ajili ya upekee.
9. Enzi ni kambi la ajabu, humo hujaa uwezo wote wenyi ushindi namna ya muujiza wa maajabu.
10. Ni upumbafu sana kulinganisha enzi na vitu vipungufu ambae hupatikana angani na ukiwani.
11. Ni viumbe ndio hutumia namna ya kula anga na ukiwa ili vipate kusikimiza umbo zao za kihewa na za kimwili, kimaisha.
12. Asiye kula miongoni mwa wanahewa hawezi kuishi, maana chakula ndio hujenga umbo za kihewa na za kiukiwa. 13. Aliye wa hewa hutumia hewa namna ya kula kadiri ya kupumua, na aliye wa mwili hutumia mwili namna ya chakula.
14. Hayo ni kwa sababu ni wapungufu na wazaifu ambae hutafuta vifaa ili kusaidia umbile zao.
15. Lakini mkamilifu hatumiake kifaa chochote ili kusaidia uzima (wake), bali yeye ni mwenyi kuenea katika yote, bila kiu wala njaa, shida wala tatizo lolote.
16. wala uweji wake haudai kifaa chochote wala msaada wowote ajili ya kukamilika namna ya kuenea kiushindi.
17. Wala yeye mtukufu hatumiake enzi kama vile wanahewa hutumia hewa namna ya kupumua.
18. Hakika mwenyenzi ni mwenyi ukamilifu wa ajabu, ni yeye mwenyewe katika upekee namna ya utupu wa enzi.
19. Hakuna sehemu mbili kwamba uyu ndio mwenyenzi na hii ndio enzi, lakini utupu wa ajabu;
20. Enzi ndio dhati yake mwenyewe, hakuna utafauti wa maki ndani mwake.
21. Kungeli kua utafauti kati yake na enzi kama vile wanahewa na hewa yenyewe walivyo bila shaka asingeli itwa mwenyenzi bali mwanaenzi, na upekee usingeli kua kwake.
22. Lakini kuona kama yeye ni utupu wa enzi, ndio maana hakuna Wanaenzi ispokua mwenyenzi peke yake.


[ 28 ]

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, M’bora wa kuumba, Mola wa pahali pote, mufalme aliye juu.
2. Hakuna mwengine ila yeye, mshindi aliye tangulia kadiri ya kuenea kabla ya ulimwengu.
3. Ni yeye aliye kua, aliyeko na atakaye kua, namna ya muujiza ambae mipaka haipatikani ndani mwake
4. Hakuna kabla yake wala baada yake, maanzio wala makomeo ; kuzaa wala kuzaliwa, kuchoka wala kushindwa.
5. Mwenyi milki ya ajabu ambae hushinda maanzio na makomeo mtukufu asiye badirika
6. Haimjuzu muweza kuzaufika kwa kuanzishwa na kukomeshwa.
7. Ni yeye ndio muanzishaji wa kila umbo, la wazi na siri.
8. Mtangulizi wa vyote ulimwenguni, ambae peke yake hutokeza kwa idhini yake vilivyomo angani na ukiwani, mkuu asiye kua na wa zaidi yake.
9. Milki yake humfanya atangulie pekee bila mfanano, na aumbe kila kiumbe bila msaidizi, na atawale juu ya yote bila mshirika.
10. Bingwa mkuu, aliye na kasi la uwezo wa kutenda, mkamilifu wa ajabu
11. Kuumbwa na kuzaliwa ni uzaifu mkubwa sana, ambae haumgusi wala kumkurubia mwenyenzi aliye jaa milki ya ushindi.
12. Kila kilicho zaliwa ni kiumbe zaifu kabisa, ambae ni tafauti kabisa na Muumbaji (wake).


[ 29  ]


1. Ushindi ni wake mwenyenzi Mungu ; mudiriki wa ulimwengu.
2. Mungu wa wanahewa na wazilahewa, mtegemewa, aliye inuka kuliko yote, ambae hutawala kwa ushindi wa milki yake.
3. Ni yeye mkuu wa masiku, mkongwe, ambae huzidia wote ajili ya kutangulia.
4. Ni mkubwa sana na zaidi ajili ya kuenea kiupatikanaji pasipo kabla wala baada yake.
5. Ni hali tukufu sana hiyo ya kukamilika katika kuwako ndio jambo ambae humfanya ainuke juu ya yote bila wa kulingana naye
6. Ni mwenyi mamlaka kubwa ajabu, ambae hupindukia walimwengu wote kwa jumla.
7. Hakuna mwengine akurubiaye utukufu huo wa ajabu wenyi kupatikana kadiri ya muujiza, ambae fikara haiwezi kamwe kukagua hakika ya kadiri yake
8. Milki katika busara ijaayo utukufu na ushindi kadiri ya kuzidia, juu ya maala pa juu ulimwenguni.

36

9. Hujieneza mwenyewe kadiri ya kujienelea kiutangulizi namna ya mamlaka ya milele kadiri ya ukamilifu.
10. Na ukamilifu ndio uzima, na uzima ndio umungu, na umungu ndio ufalme wa milele.
11. Hakika Mwenyenzi Mungu ni mkubwa kabisa, mtukufu anaye stahili kusifiwa, ambae peke yake hujaa mamlaka ya milele.
12. Ametakisika Mwenyenzi Mungu, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe, ambae hustawi katika uhuru, mkadiriaji wa karama, aliye pasipo yeyote, milele na milele.

[  30 ]

1. Ulimwengu sio chochote pasipo enzi ; isingeli kua ukamilifu wake kama ulimwengu usingeli patikana.
2. Ukamilifu wake humueneza pasipo maanzio wala makomeo, hali ya kua yote katika yote.
3. Ni lazima kabisa kumshukuru Mwenyenzi, maana bila yeye kusingeli patikana yeyote wala chochote miongoni mwa viumbe.
4. Na watu hujiuliza, ni wapi enzi hupatikana katika ulimwengu?
5. Na ni namna gani hustawi enzi ulilmwenguni?
6. Ni gani rangi ya enzi tukufu?
7. Hakika kila ulizo iko na jibu yake.

[ 31 ]


1. Ametakasika Mwenyenzi aliye inuka juu ya maala pa juu ulimwenguni, Mungu mwenyi ushindi, mtukufu wa daraja. 

2. Hupatikana juu ya ulimwengu na walimwengu sababu ya kua na mamlaka kubwa ajabu, ambae hutokana na ujuzi uliye busara kamilifu.
3. Kama husemekana enzi ipo juu, sio kwamba ni juu duniani ama juu mbinguni, wala kuhusikana na kuketi kwa kiumbe chochote.
4. Enzi tukufu hupatikana juu sana ajili ya busara yake kubwa, ni daraja ya busara yake ndio huzidia yote na kuzidiya yote ndio kuinukia yote kadiri ya kua juu ya yote.
5. Kuona kama ameshinda vyote vilivyomo ulimwenguni ndio maana huinuka juu kabisa, na viumbe vyote hupatikana chini yake.
6. Milki kamilifu ambae humjaa ndio utukufu na mamlaka kubwa yenyi kumfanya atukuzike zaidi ya vyote ulimwenguni.
7. Kwa kutambua juu na chini ulimwenguni ni lazima kutambua kwanza ginsi enzi ilivyo katika ulimwengu.
8. Enzi tukufu ni taa ya ulimwengu isiyo zimika ; na taa huzingatiwa katika mwangaza wake ; upande wa taa hupatikana mwanga mkubwa, na mbali na taa upande wa giza hupatikana mwanga mdogo sana wenyi kufifia.
9. Kuona kama enzi ndio iliye juu, upande wa enzi ndio juu na upande wa giza, mbali na enzi, ndio chini.
10. Ndio maana mbingu ipo juu na dunia ipo chini, ulimwenguni.
11. Viumbe waliyemo mbinguni ndio waliye juu kuliko viumbe vingine vyote.
12. Hakika daraja ulimwenguni hutokana na busara ; aliye na busara kubwa hupatikana juu na aliye na busara ndogo hupatikana chini.
13. Na aliye juu katika watu ni nabii na walii wa Mungu, ambae hujazwa na nuru tokea mbinguni, ajili ya hayo huinuka juu sana mfano wa wakaaji wa mbinguni.
14. Wala sio kwamba masulutani na matajiri ndio waliye juu, ispokua miongoni mwao atakaye amini Mungu mwenyenzi na kuishika kimakini dini yake
15. Kweli kabisa ukubwa wa imani ndio ukubwa wa daraja ya mutu.

[ 32 ]
1. Enzi tukufu, huko juu, hustawi katika utukufu wa mamlaka yake mwenyewe.
2. Hairuke kama yenyi mabawa, wala kuketi kama yenyi miguu, wala kusegamia katika chochote kile.
3. Je! Umesangaa kustawi kwa enzi bila kugusa chochote wala kutokea popote kadiri ya utukufu wa upekee?
4. Eti hauone ginsi alivyo weka mbingu bila nguzo! ebu niambie yeye mwenyewe!!!
5. Milki yake ya ajabu humstawisha katika ukamilifu namna ya kua shina la vilivyomo ulimwenguni.
6. Wala uzaifu wa kujumuika na kuitaji haumkurubie kamwe.
7. Ni yule aliye zaifu ndio hujumuika, namna ya kufaa na kufaidika kimatumizi, katika umbiko.
8. Anacho kiruhusu kuketi bila kusegamia wala kuninginia hutii amri yake sababu ya ushindi wa mamlaka yake, kefule yeye mwenyewe!
9. Mamlaka yake ni ya ajabu sana ambae ni utasi juu ya kila jambo ; imemfanya astawi kikamilifu katika upekee utangulizini kadiri ya mwanzo wa vyote.
10. Mtukufu wa ajabu ambae hakae ndani ya chochote cha utafauti naye mwenyewe, lakini hustawi enzini hali ya kua utupu wa enzi tukufu.

37

11. Maana enzi ndio yeye mwenyewe, na ndio maana hustawi katika utukufu wake huo wa ajabu.
12. Ni yeye aliye msingi wa ulimwengu, ambae katokeza vyote vilivyomo, atanguliaye pasipo msaada wa mwengine.

[ 33 ]
1. Utakatifu ni wake Mwenyenzi Mungu, mshindi wa yote, ambae humiliki kila jambo.
2. Utukufu wa enzi ni muujiza usio fananishwa na chochote, mamlaka yenyi kuenea.
3. Kila kilicho umbwa kilipewa umbile yacho fulani ili kidhihirike kwayo : kama vile hulka, kimo na rangi, kadiri ya sura fulani.
4. Usizani ya kama enzi ipo na rangi mfano wa hiyo rangi ya umbiko ; haiwezekane muumba kufanana na kiumbe.
5. Kama husemekana «rangi ya Mwenyenzi», sio mfano wa rangi yenu, bali utajo wa nuru yake takatifu, namna ya kungaa kwake.
6. Hakika Mola wako ni tafauti kabisa na kila jambo ; hafanane wala kulingana na chochote ku vyovyote.
7. Ametakasika Mwenyenzi mtukufu aliye muujiza kiutangulizi na maajabu kiutokezaji, Mola mshindi, mufalme aliye kamilika.

[ 34 ]
1. Utakatifu ni wake Mungu Mwenyenzi, Muumbaji wa ulimwengu.
2. Mkuu anaye tawala maala pote, akijaa hekima ya ajabu.
3. Hana shida ya msaidizi, wala hachokake kusimamia viumbe vyake.
4. Ni mwenyi uwezo wa kufanya kila jambo, wala tatizo la kutetea halimkurubie kamwe. 

5. Ujuzi wake umemfanya amiliki aina yote ya fahamu, bila shuruli yoyote.
6. Hasahau wala hadondoke, mtakatifu aliye na busara kamilifu.
7. Mola wa jumla ya viumbe, mtukufu aliye juu.
 

[ 35 ]

1. Mungu alitangulia mwenyewe kabla ya viumbe kupatikana, hakukua kitu kingine kinyume na dhati yake tukufu.
2. Amekua yote katika yote mwenyi kukamilika
3. Alitangulia peke yake bila kuanza, kadiri ya kuenea ulimwenguni, katika mamlaka yake mwenyewe.
4. Maana uwezo wake ni mwingi ajabu ambae humfaya akamilike bila upungufu wowote.
5. Ni upungufu ndio unao sababisha uzaifu wa kushindwa
6. Lakini kwake yeye mkamilifu asiye gusika na upungufu, huweza yote bila uzaifu wa kushindwa.
7. Amejaa uwezo wa ajabu, mamlaka ya utendaji ambae hukadiriana pasipo kukadiriwa na yeyote, mola mtukufu, mfalme wa ajabu.

[  36 ]

1. ukamilifu na pia kuna upungufu, katika ulimwengu.
2. Ukamilifu ni hali tukufu sana, kadiri ya uzima, upatikanaji wenyi kuenea.
3. Ameenea katika uwezo hali ya kua muweza wa vyote, na ameenea katika fahamu hali ya kua mujuzi wa vyote
4. kuenea kiupatikanaji ndio kua na uzima, yaani (kupatikana) bila ku anza na bila kukoma, katika upatikanaji, na katika uwezo na katika fahamu.
5. Upungufu ndio hali dhalili sana, namna ya kutoeneana katika yote.
6. Haeneane katika upatikanaji wala katika uwezo wala katika fahamu.
7. Na hali ya kutoeneana ndio kupungukiwa kadiri ya hunusu na kipande, jambo lisilo endelea mbele na nyuma kiupatikanaji na kiufahamu


[ 37 ]


1. Ukamilifu umepatikana katika tabaka la Enzi
2. Ni utukufu wa ajabu usio jumuika wala kunajisika, na ndio maana hauko angani wala ukiwani.
3. Ispokua upungufu ndio upatikanao angani na ukiwani
4. Na kuona kama ukamilifu umepatikana enzini peke yake, ndio maana aliye enzini ndio mkamilifu, wala hakukua na hakuna na akutakua mwengine mfano wake popote ulimwenguni.
5. Kuona kama ukamilifu umepatikana kwake aliye enzini na aliye enzini ndio Yule anaye itwa mwenyenzi Mungu, ni kwamba aliye mkamilifu katika ulimwengu ni Mungu mwenyenzi peke yake.
6. Ni yeye anaye jaa utukufu, namna ya kupatikana kadiri ya kuenea, mtangulizi aliye na uzima.
7. Mwenyi kujaa kadiri ya kuenea katika kua, katika kuweza na katika kujua, mola wa siku yote katika yote, mshindi aliye juu.

[ 38 ]

38

1. Upungufu umepatikana katika tabaka la Anga na pia katika tabaka la ukiwa.
2. Ni hali zaifu sana isiyo kua na milki ya ushindi, imekosewa mamlaka ya kujieneza bila msaada.
3. Kuona kama upungufu umepatikana angani na ukiwani ambae mumejaa wakaaji wengi.
4. Ni kwamba wanaanga na wakiwa ndio wapungufu katika ulimwengu.
5. Ni wao ndio wadhalili, wenyi kupatikana bila kueneana, ambae hutaabika na shuruli ya utetezi.
6. Wamepatikanishwa na kupangiliwa kimaisha, wala hawakua ispokua sifuru.
7. Hali yao hutokana na sifuru ambae ni uzaifu mkubwa, wamekua mfano wa makadirio yake yeye aliye kamilifu.

[ 39 ]

1. Utukufu wa ukamilifu ni mamlaka ya ajabu ambae huzidia kila kitu.
2. Ni muujiza wa maajabu upatikanishao kila kitu ulimwenguni.
3. Haukuanza mu namuna yoyote ile lakini ulitangulia wenyewe kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho 

4. Ni utukufu wa ajabu usio linganishwa na chochote ajili ya ushindi wake, hakuna mfano wake ulimwenguni. 

5. Hali kama hii ndio uzima, mamlaka ya kuenea kadiri ya utangulizi.
6. Na uwezo wa kutangulia ndio mamlaka ya uumbaji
7. Haumbe ispokua aliye tangulia, na hatangulie ispokua aliye mkamilifu.

[ 40 ]
1. Upungufu ni dhati ya umbiko, maana kinacho fanya aumbwe ni ajili ya kupungukiwa kimilki na kiufahamu.
2. Hakuwaka chochote kabla ya kuumbwa kwake sababu ya kupungukiwa, angeli kua kamilifu kama angeli tangulia kuwako kadiri ya kuenea bila kuanza mu namuna yoyote ile.
3. Ndio maana yule anaye umbwa, ametokezwa tokea upungufu na kufanyika umbile fulani.
4. Kama hasingeli tokezwa bila shaka asingeli patikana ulimwenguni.
5. Maana hakuwa na uwezo wowote ila sifuru tu, humu hamna ila ujinga mtupu.
6. Hakika katika ulimwengu huu umbiko imetokana na upungufu na uumbaji ndio unao tokana na ukamilifu.
7. Ni kwamba muumbaji ndio mwenyi ukamilifu na kiumbe ndio mwenyi upungufu.


[ 41 ]

1. Ukamilifu ndio uzima, ni hali tukufu ya upekee inayo tokana na milki ya ushindi, hakuna cha zaidi yake.
2. Amekua yote katika yote, hasinzie wala halali, na hachoke wala kushindwa, na hakosekane wala kubadirika
3. Amekua yote katika kupatikana, hakuna aliko tokea wala aliko endea, mtangulizi wa mbele na nyuma
4.
Mwenyi sifa kamilifu ajuaye yote zaidi ya woote ulimwenguni ,m’bora wa kuenea
5. Hii ndio hali tukufu ya yule aliye enzini ambae hujaa mamlaka ya ajabu
6. Sifa yake imeachana sana na sifa ya viumbe maana kiumbe ni chenyi upungufu ambae ni uzaifu
7. Hakika hali ya mwenyenzi ni muujiza wa maajabu, na ndio maana viumbe wamestaajabu sana ukubwa wake hata wengine wenyi uzaifu kifikara wamefikia kubisha.


[ 42 ]


1. Hakungeli patikana chochote bila mwenyenzi kutangulia ulimwenguni.
2. Maana yeye ndio mwanzo wa vyote, ambae hutokeza toka sifuru.
3. Milki yake ya ajabu humfanya aenee maali pote katika kuweza na katika kujua, kadiri ya ushindi katika yote.
4. Kwa kuweza kutokeza kitu ambae hakikua inabidi kua mkamilifu, yaani kutokua na upungufu ao uzaifu wowote. 5. Kwani yeyote aliye na upungufu ni mzaifu, na aliye zaifu hana uwezo wowote, hajiweze na hawezi kitu.
6. Ni kwamba atakaye kanusha utukufu wa ukamilifu na kukubali tu uzaifu wa upungufu ni pumbafu kabisa.
7. Hakungeli patikana chochote bila mkamilifu kutangulia, na mkamilifu ndio yule aliye enzini anaye itwa Mungu.

[ 43 ]


1. Ulimwengu, ambae ni jumla ya tabaka tatu, umefanyika na yule aliye kamilifu atanguliaye katika mamlaka yake mwenyewe.
2. Mbingu, hadeze na dunia vilifanyika kwa idhini yake wala hakuna kilicho njee ya mapenzi yake.
3. Kinacho fanya kitu kijumuike ulimwenguni ni ruhusa yake inayo tokana na mapenzi yake.
4. Maadamu umbo Fulani imepatikana ni kwamba huruhusiwa naye.
5. Na ambacho hukataliwa naye hakiwezi kujumuika.
6. Na kama umbo Fulani hujumuika lakini imetumia makatazo ya Mungu, hufupisha maisha yacho namna ya kipande, na baadaye kitafutwa katika hesabu ya walimwengu.
7. Hakuta bakia ispokua dhati yake Mtangulizi aliye juu.


 [ 44 ]

1. Kila kiumbe asili yake ni upungufu, hakuna umbo iliyo kamilika kamwe.

39

2. Kilicho kamilifu hakiumbwake, maana ni chenyi kuenea, hakina shida ya msaada wa yeyote.
3. Kama unaona kitu ao umbo angani ao ukiwani, ijapokua kikue kya kustaajabisha, katika uwezo ao katika fahamu ama dalili yoyote ile, tambua ya kama ni kiumbe kilicho umbwa na mwenyenzi.
4. Kitu kile kingeli kua kamilifu kama macho yako haingeli weza kukizingatia ana kwa ana, wala hakingeli jumuika angani wala ukiwani, bali kingeli stawi katika enzi tukufu.
5. Enzi haigawanyikake wala kujumuika, mfano wa hewa; hakuna kitu kitakacho jazwa enzi ndani mwacho angani wala ukiwani.
6. Musidanganyike na mwanahewa yeyote yule atakaye jidai ujuzi, hakuna kujumuika kwa mjuzi ; angeli kua mjuzi asingeli pumua hewa wala kupatikana duniani ama mbinguni ama hadezeni, lakini angeli patikana enzini maala penyi kuhifadhika ambae macho ya kiumbe haizingatie bayana.
7. Hakika mwenyenzi Mungu hafanane na umbo yoyote ile wala haamake kutoka enzini kusafiri angani Mufalme wa ajabu anaye stawi kiushindi, wa pekee aliye juu.


 [ 45 ]

1. Enzi ni tabaka kuu zaidi ya yote, eneo tukufu ijaayo mamlaka imepatikana kadiri ya kutangulia bila mwanzo wala mwisho.
2. Ni yenyi upekee ajili kutogusika na kitu, na ndio maana haiwezi kujumuika wala kuingia ndani ya chochote cha umbalimbali na dhati yake
3. Inabidi vitu vyote viliokutwa huko viondoshwe namna ya kupotezwa, ili dhati yake isalie huko peke yake
4. Kama ni angani inatakika hewa na wakaaji wake wote wapotee namna ya kutopatikana kwa enzi kuketi maala hiyo
5. Taa haiwezi kuingia ndani ya mwangaza wake ama kutokea humo
6. Na kama ni ukiwani inatakika ukiwa na wakaaji wake wote wapotee namna ya kufutwa kwa enzi kuketi maali hapo 7. Hakika enzi tukufu ya Mungu haijumuikake katika umbiko, lakini yao ni katika upekee, na ndio maana hakuna kitu cha kumfanana wala cha kumkurubia katika milki.

 [ 46 ]

1. Utakatifu wa mbingu umetokana na nuru ya enzi inayo mjaa, ambae huangazia bila kufifia wala kuzimika
2. Nuru hiyo ni kifaa kikuu cha maisha ambae hutimiliza umbo
3. Ni neema kubwa kupatikana karibu na chemchem ya nuru
4. Ole kwao waliyeko njee mbali sana na kisima cha nuru, maana huko ni hatari ya giza yenyi kufunika wala hawazingatie lolote katika utukufu wa taa ya ulimwengu
5. Hufanikiwa sana na mwangaza huo aliye wa roho, akimeremeta kama tungi kandokando mwa taa ya ulimwengu
6. Nuru yenyi ladha ya ajabu nafsini, zaidi ya yote ambae hunusuru na hustiri umbo.
7. Elekeeni kwenyi enzi tukufu ili mupate kukurubishwa, hakika bustani ni fasi bora ya kujumuika.

[ 47 ]
1. Nini kinacho kufanya ukanushe uzima wa Mungu?
2. Bila kutangulia kwake kama ulimwengu na walimwengu visingeli patikana kamwe.
3. Upatikanaji wa umbiko humaanisha utagulizi wa mjuzi awezaye kufanya mambo yote kwa mamlaka yake mwenyewe.
4. Kutangulia kwake ni muujiza, na kutenda kwake ni maajabu.
5. Ameenea katika upatikanaji na pia huenea katika utendaji, mzima aumbaye.
6. Milki yake ni yenyi ushindi katika yote bila mfano wake ulimwenguni.
7. Hakika Mungu ndio mwenyi uzima ambae hukamilika peke yake ulimwenguni.


[ 48 ]

1. Mungu ni mwenyi haki ambae hutenda haki, hakuna atakaye mkosoa.
2. Yeye ni chemchem ya kweli na haki ajili ya ukamilifu wake, maana uzaifu wa kudondoka haumkurubie kamwe
3. Na kama ametokeza umbo mbalimbali yenyi uzidiano katika neema yake sio upendelevu wala makosa
4. Hayo hutokana na upungufu ambae ndio asili ya kila umbo
5. Kule kutokamilika kwao ndio jambo liletayo utafauti kati yao, na utafauti huo ndio kisa cha uwingi kupatikana kwao ili kila yule ajazikishe maala pake, kupatikane kawaida ya umbiko
6. Angeli umba wote namna moja bila utafauti wala uzidiano kama maisha isingeli timilika kwao na haistahili upekee katika uzaifu wala upekee haufanyikake, maana ndio alama ya ukamilifu.
7. Ndio maana umbali mbali umepatikana kwao wapungufu ajili ya kutojieneza, wamefanyika kadiri ya mapenzi ya muumba ; kila yule na hali yake na kazi yake ijapokua ni aina moja kiumbile.


[ 49 ]

1. katika ukamilifu ambae ni uzima, hakuna utafauti wala uwingi bali ni upekee ajili ya kuenea.

 2. Utafauti usababishao uwingi hupatikana katika upungufu ajili ya uzaifu wa kutoeneana
3. Uwingi ndio jambo linalo timiliza maisha yao, ni kifaa kikuu katika utetezi wao.
4. Mutu asingeli ishi bila maji kuumbwa, na hewa, udongo, mimea, wenziwe...

40

5. Hakuna maisha wala thamani ya upatikanaji wa kiumbe peke yacho bila aina zingine, maana ni katika uzaifu.
6. Na utafauti fulani ni uzaifu fulani. Ndio maana haifae kulazimisha kuwa sawasawa katika upungufu ambae ni jambo lisilo sawa, ispokua ukamilifu ambae ni uzima ndio jambo lenyi usawa.
7. Kumbi ni vema kukubali uzidiano baina yenu maana asili yenu ni upungufu ambae ni uzaifu.

[ 50 ]
1. Mzima aliye juu alipangilia vema ajili ya kuwapelekeni katika utimilifu.
2. Amewawekeeni neno lake kuwa nusura ya tatizo la upungufu asilia.
3. Atakaye amini kweli atapata bahati ya kuingia katika utimilifu wa umbo.
4. Nafsi yake itatulizwa kutokana na tatizo yote kwa jumla.
5. Shida yake yote itatimilizwa bila yeye kutaabika na shuruli yoyote ile, wala mauti haita mufikia kamwe

 6. Hali hii ndio utimilifu wa umbo, sio ukamilifu, lakini neema kubwa yenyi kustiri umbo
7. Basi tumieni neno la Mungu kama inavyo stahili ili mupate kutimilika nafsini.

 [ 51 ]
1. Atakaye amini Mungu, na malaika zake, na mitume yake, na vitabu vyake, bila shaka umbo lake litatimilizwa

 2. Atapewa uhai kadiri ya hunusu, zaidi ya kipande, kama kistari cha usawa kilicho na mwanzo bila mwisho
3. Aliumbwa lakini hata kufa tena, ameondolewa mipaka katika upatikanaji wake
4. Amekuwa mfano wa nuru ya taa isiyo zimika ambae huangaza milele na milele
5. Hii ndio neema kadiri ya mshahara wa wale watakao pokea neno la Mungu na kulitumia kama kawaida
6.
Hakika mwenyenzi ni mwema, mkweli, mwenyi haki, m’bora wa kukadiria, atakasikaye na ajuaye
7. Ni muimu kwenu kuamini kweli hii ambae kafunuliwa na mola wenu aliye juu.

 [ 52 ]
1. Mungu alijua ya kwamba hali yake ni muujiza mbele ya watu, ndio akafanya muusiano kati ya mbingu na dunia, ili wapate kuzingatia utukufu wake.
2. Akaagiza malaika na roho ili wawaonye watu, wakiwaletea habari nzuri kutoka kwake.
3. Ndio maana kumuamini mjumbe wa Mungu inakua ni jambo muimu kwa mutu .
4. Hata tumwa bayana malaika wala roho kutoka mbinguni kua mtume wenu, ispokua watu wenzenu tu ndio watakao inuliwa na kupewa neema hiyo .
5. Ni amri kwenu kuwaamini wote, wala musibague baina yao .
6. Na yule anaye muamini yesu masiya kiisha akamkataa nabii mtukufu muhamadi, imani yake ni ya bure kabisa ; na pia yule anaye muamini Muhamadi na kiisha akamkataa Nabii mutukufu yesu masiya, bila shaka imani yake ni ya bure kabisa
7. Mungu ni mumoja na ujumbe wake ni mmoja na dini yake ni moja ya usilimu

[53]


1. Nuru ya Mungu ni jambo kubwa sana katika maisha ya mutu .
2. Ni rehema ya Mungu inayo timiliza umbo iliyo jazwa
3. Hakuna umati pasipo nabii, wala nabii pasipo umati .
4. Nuru imewaka na kungara sana katika rangi mweusi, maana huzagaa katika kifaa maalumu.
5. Huu ni ukweli kutoka kwa mola wenu mzima aliye juu .
6. Basi itumieni na hekima wala musiichafue kwa kuichanganya na upuuzi wa shetani, ni rehema ya muumba kwa wakaaji wa Dunia.
7. Roho ni tayari kuwashukia wale watakao amini ujumbe huu.

 [ 54 ]
1. Hapana kubisha uzima wa Mungu muumba anaye stawi katika enzi tukufu
2. Ni upumbafu kupinga uzima na kukubali tu maisha .
3. Hakungeli patikana maisha yoyote bila utangulizi wa uzima ulimwenguni .
4. Lau kama ni upungufu ndio ulio kutwa hapo awali, bila shaka viumbe vyote visingeli umbwa ; sifuru ingeli bakia milele.
5. Utangulizi wake ndio Muujiza mkubwa unao staajabisha, na ili hali ndivyo anavyo stahili kwa maana yeye ni uzima tafauti kabisa na kila umbo.

41

6. Ili bidi kutangulie ujuzi mbele ya vyote, fahamu ya ajabu isiyo shindwa na lolote, ambae hutokeza toka sifuru.
7. Hakika Mungu ni mwenyi mamlaka ya ajabu kuliko walimwengu wote, ni muweza wa vyote na mjuzi wa vyote, ambae hastahili kufanana na kitu kipungufu.


 [ 55 ]

1. Ujumbe wa Mungu haukuteremushwa ispokua kwa wenyi akili.
2. Ni raisi watu kuzingatia uzima wa Mungu kwa njia ya neno lake.
3. Lakini neno lake ni ngumu sababu hutumiwa katika lugha ya watu isio kua yake, maana kutenda kwa Mungu ni mbalimbali sana na kutenda kwa watu.
4. Kwa kusikilizisha watu ilibidi kuyalinganisha na kusema kwao ili wapate kufahamu.
5. Na ndio maana hutumia lugha ya watu katika ujumbe wake namna ya mifano.
6. Lugha yote ni yake Mungu ni yeye ndio kawafunza watu lugha mbalimbali, na ndio maana imeruhusiwa kuomba ao kusali katika lugha unayo fahamu.
7. Mungu hana kabila wala lugha, hana upungufu huo wa kiumbile sababu yeye sio kiumbe ; atakuaje na lugha na ilihali hakuna mwengine wa namna yake ambae wangeli kua na zungumza katika lugha hiyo?


[ 56 ]

1. Mungu ni mwenyi uwezo wa kufanya kila kitu, mtukufu aneemeshaye kila kabila na kila umati.
2. Na ndio maana kila lugha ipo na jina la Mungu ndani mwake.
3. Ni alama ya neema yake ku watu wote kwa jumla, kwani kila kabila imepatikana na vipenzi vyake.
4. Wala sio lazima aitwe tu katika jina yake ya mulugha fulani.
5. Ni bora kumtaja katika lugha unayo tumia ao unayo penda miongoni mwa lugha zake.
6. Ameyapenda ma lugha yote na majina yake yote aliyo iweka ndani mwayo, mjuzi wa ya siri na ya wazi. 

7. Hakika Mungu mwenyenzi ni m’bora wa kukadiria na ni mwenyi hekima kamili.


[ 57 ]

1. Mungu ni uzima kadiri ya ukamilifu, amepatikana katika utangulizi bila mwanzo wala mwisho
2. Ni milki kiujuzi yenyi ushindi ndio inayo mfanya awe na utukufu huu wa ajabu.
3. Milki hiyo, ndio dhati yake mwenyewe, mamlaka kuu yenyi kumiliki shuruli na wakati.
4. Na ndio maana hana shida wala umri maalumu, mtukufu anaye tangulia kuenea ulimwenguni.
5. Alikua, yuko na atakua, mwenyi uzima ulimwenguni.
6. Maisha na muda hukadiriwa naye, amempa umri mrefu amtakaye na pia humpa umri mfupi kadiri ya idhini yake, na vivihivyo kuhusu maisha yao.
7.
Hakuna mola mwengine mfano wa Mungu mwenyenzi, m’bora wa kuumba anaye jaa mamlaka, mtakatifu aliye juu.


[ 58 ]

1. Umungu ni mamlaka ya ajabu, milki kamilifu isiyo badirika, ushindi katika yote milele na milele. 

2. Ni mwenyi uwezo wa vyote ambae idhini yake hutimiza, hakuna upatikanaji njee ya mapenzi yake . 

3. Kama mutu anapatikana duniani ni kwa ruhusa yake mumiliki aliye juu.
4. Basi shangilieni uzima wa mola wenu aliye enzini, mtangulizi wa vyote anaye jaa utukufu.
5. Msifiwa wa ajabu anaye miliki ulimwengu, bingwa wa mabingwa, muheshimiwa aliye juu.
6. Ametangulia kadiri ya kuenea, mwenyi uwezo na ushindi, mtakatifu aliye enzini.
7. Hakuna mola mwengine sawa na Mungu mwenyenzi, wa pekee aliye na uzima.


 [ 59 ]

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, m’bora wa kuumba aliye umba shetani kwa ulimi wa moto, kadiri ya kapi iliyo anguka .
2. Akashirikisha pumzi na mwili mwepesi wa moto ambae hupatikana ndani mwake kama uchafu unao fanya afifie kadiri ya pumzi chafu angani
3. Utazani kwamba ni mwanahewa-Halisi aliye najisika ajili ya ukubwa wa pumzi yake, na ilihali yeye ni mwanahewa- haramu.
4. Mwili wake hauzingatiwe ila mfano wa giza, kadiri ya uchafu ndani ya anga
5. Amepatikana mbali na chemchem ya nuru ndio maana hufifia pumzi yake pasipo nuru.
6. Hayo ni kwa maana amepatikana na mwili asilia ijapokua huogelea angani.
7. Hakika shetani ni mwanahewa-haramu anaye ishi njee ya dunia, katika hadeze.


 [  60 ]

1. Utakatifu ni wake mwenyenzi Mungu, mubora wa kuumba, aliye umba malaika kwa anga tupu, kadiri ya idhini yake.

42

2. Akamfanya kua pumzi tupu isiyo shirikishwa na chochote.
3. Na ndio maana yeye ni mwanahewa-halisi, asiye changanya hewa na mwili wowote,
4. Ni pumzi timilifu na takatifu kadiri ya nuru, ndio maana humeremeta.
5. Ni umbo kubwa isiyo fikiwa na kifo maana hakuna mtengano wa pumzi na mwili wowote ndani mwake.
6. Amepatikana karibu na chemchem ya nuru, ndio maana humeremeta, mwangaza wa taa isio fifia wala kuzimika.

 7. Hakika malaika ni umbo hai, kadiri ya uvuli wa enzi, ambae huishi njee ya dunia, katika mbingu takatifu.


[ 61 ]


1. Mwenyenzi Mungu ni m’bora wa kuumba, ambae katokeza uzuri na ubaya angani. 

2. Amefanya mila mbili ambae hutenganisha wanahewa, humo angani.
3. Moja ni alama ya uvuli wake na ingine kinyume cha huo.
4. Uvuli wa ukamilifu ndio utimilifu, na utimilifu ndio chemchem ya uzuri.
5. Na kinyume cha utimilifu ndio uaribifu, na uaribifu ndio chemchem ya ubaya.
6. Anaye timiliza mambo hufanya uzuri ; na anaye haribu mambo hufanya ubaya.
7. Hii ndio njia mbili ambae umbiko hupitia angani.


[ 62 ]

1. Mwenyenzi Mungu hana mila yoyote ile, maana yeye ni tafauti kabisa na umbo.
2. Maana mila ni umbo, ambae kafanyika kwa wakaaji wa anga.
3. Na ndio maana utakuta katika wanaanga mila hii mbili.
4. Uzuri kwao wahelekeaye taa, na ubaya kwao wahelekeaye giza.
5. Ni mila ya watetezi, ambae hupatikana na pumzi nafsini mwao.
6. Haipatikane kwao wasio na pumzi kamwe.
7. Hakika mila ndio umbo la wanaanga, haipatikane kwa mwenyenzi wala kwa wakiwa.


[ 63 ]

1. Mwenyenzi Mungu sio muzuri wala yeye sio mubaya.
2. Hafanane na umbo yoyote maana yeye ni wa pekee anaye zidia kila kitu.
3. Uzuri ni adui wa ubaya, na ubaya pia ni adui wa uzuri ; uyu huangamiza yule, na yule pia huangamiza uyu.

 4. Mungu angeli kua na mila fulani, bila shaka angeli angamizwa na ile ingine.
5. Upekee wake wa kuto jumuika wala kulingana unamfanya awe huru kabisa mbali na kuangamia.
6. Ni mwenyi mamlaka ya ajabu sana ambae huepukana na uzaifu wa aina yote.
7. Sifa yake huzidia vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani, maana yeye ndio mwanzo wa vyote.


[ 64 ]

1. Mungu muumba sio muzuri wala sio mubaya, bali yeye ni mkamilifu.
2. Amezidia uzuri maana, uzuri ni utimilifu wa jambo.
3. Na utimilifu ni uvuli wa ukamilifu, yaani ni miongoni mwa nuru yake takatifu .
4. Hawezi kulingana na uvuli wake, lakini yeye huzidia.
5. Ndio maana Mungu amezidia uzuri, maana uzuri ni katika umbiko ambae haina ukamilifu.
6. Ukamilifu ndio hali tukufu sana isiyo na doa, utakatifu wa ajabu, kadiri ya usawa wenyi kuenea. 

7. Hakika umungu ni utukufu wa ajabu sana, muujiza wa maajabu ulimwenguni.


[ 65 ]

1. Uzuri ni mfano wa rangi ya enzi, humeremeta wote wajipakao.
2. Malaika na roho ndio umbo timilifu, kadiri ya nuru ya Enzi tukufu.
3. Na ndio maana ni wenyi mila nzuri kabisa, utimilifu wa pumzi katika eneo la anga.

 4. Na mutu yeyote atakaye fuata malaika na roho atafanyika nuru ya Enzi tukufu.
5. Nuru isiyo zimika wala isiyo fifia, mwangaza wa mbinguni.
6. Matumizi ya mila hii ni matumizi ya nuru ya Mungu, namna ya kujipakaa rangi yake. 

7. Ametakasika mwenyenzi Mungu, mkamilifu tena wa pekee m’bora wa kuumba.


 [ 66 ]

1. Uzuri umetokana na nuru, na ubaya umetokana na giza.
2. Aliye katika nuru hutumia silaha za nuru, na aliye katika giza hutumia silaha za giza. 

3. Nuru ni ufahamu na giza ni upumbafu.
4. Nuru ni sehemu ya utukufu wa taa ya ulimwengu.
5. Na taa ya ulimwengu ndio ujuzi ambae ni enzi kadiri ya uzima.

43

6. Hupungukiwa sana yeyote aliye mbali na chemchem ya nuru, ambae huelekea giza. 

7. Hakika neno la mjuzi huangazia kila nafsi inayo litumia.


[ 67 ]


1. Mungu hafanane na umbo yoyote ile lakini amezidia sana kila kitu.
2. Kile kilicho kitukufu katika umbiko ni kitu dhalili sana mbele ya mwenyenzi aliye «uzima».
3. Na ndio maana lugha zenu hazitakase kweli yake ispokua katika mifano.
4. Kutenda kwenu sio sawa na kutenda kwake muumba, na ilihali hamsemi ila kadiri ya utendaji wenu.
5. Fikara ya watu wa dunia ni chache sana, haizingatie ila kidogo tu.
6. Na ndio maana «umungu» huwastaajabisha sana na wengi miongoni mwao hawauzingatie wala kuukubali.
7. Hakika kulitangulia milki kamilifu yenyi ujuzi ambae hujaa mamlaka ya ajabu yenyi kutokeza kitu ambae hakikua popote, na ambae hujieneza bila msaada ajili ya kukamilika ambae imeitwa «mwenyenzi Mungu».


[ 68 ]

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu muumbaji wa kila umbo, mkuu anaye tawala milele na milele.
2. Vyote huanzia kwake na vyote kukomea kwake.
3. Hakuna cha utafauti na idhini yake wala upatikanaji njee ya uumbaji wake.
4. Mbingu na dunia hufuata kanuni yake, wala hakuna cha kumpinga wala cha kumuhukumu.
5. Na kama hajumuike duniani na pia mbinguni, sio kwamba hukosekana, bali yeye hustawi katika enzi tukufu, katika upekee.
6. Utukufu wake wa ajabu umemfanya atengane na vitu visio kua na ukamilifu, maana kugusana na upungufu ao kuchangikana na huo ni kupungukiwa ao kuzaufika.
7. Ameketi mbali sana na viumbe, lakini ameona na ameweza kutenda vya huko kwenyi viumbe zaidi ya wenyi kambi hilo ; hakika Mungu ndio muweza wa vyote tena mjuzi wa vyote.


[ 69 ]

1. Nuru ya Mungu ni sehemu ya utukufu wake, kama vile mwanga ulivyo sehemu ya utukufu wa taa.
2. Kuona kama mwenyenzi ni mkamilifu, nuru yake ni utimilifu.
3. Na pia kwa maana mwenyenzi ni mjuzi, nuru yake ni fikara.
4. Na kuona kama Mungu ni enzi tukufu, nuru yake ni anga(hewa).
5. Kwa maana mwenyenzi ni uzima, nuru yake ni maisha.
6. Na kuona kama Mungu ni muumba, nuru yake ni umbiko.
7. Hakika nuru ya Mungu huzingatiwa kwa namna mbali mbali, kadiri ya matazamio, bila shaka mwenyenzi ni Muujiza wa maajabu ulimwenguni


[ 70 ]

1. Enyi watu wa dunia, aminini Mungu mwenyenzi aliye wa umbeni kwa udongo.
2. Ni yeye aliye tangulia kupatikana ulimwenguni bila msaada wa yeyote.
3. Mtukufu wa ajabu ajaaye mamlaka yote, ambae hutenda kwa idhini bila kutumika kazi.
4. Yeye ndio mwenyi kuwako daima muda wote, hana mwanzo wala mwisho, mkamilifu aliye juu.
5. Hapana kushakia uzima wake, maana amepatikana juu sana hatua na viumbe.
6. Na ndio maana haifae kulazimisha kumgusa ao kumtazama kama munavyo gusana na kutazamana (ana kwa ana) nyinyi kwa nyinyi, kwani yeye ni tafauti sana nanyi tena kuna hatua kubwa ajabu baina ya dunia na enzi.
7. Mimi ni shaidi wa uzima wake, maana nimeagizwa maneno naye tukizungumza sauti kwa sauti.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kitabu cha ukweli - Mlango wa saba : "KAULI TUKUFU"

MWANDISHI WA KITABU: