Kitabu cha ukweli - Mlango wa saba : "KAULI TUKUFU"

( 1 )  SIMAMIZI LA SHAADA

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mkarimu ,anaye nifanya kua simamizi la shaada yake.
2. Amenipatia ushaidi wa uzima wake ili  (watakaye amini) wapate kua yakini na uzima wa mola wao.

3.wengi miongoni mwa wasilimu walikua na toa shaada gizani pasipo kuzingatia bayana.
4. Na ndio maana wamemfananisha Mwenyenzi na kiumbe ,na wengine wametumia uwingi katika umungu.
5. Nimetumwa ili  kusilimusha makafiri na wanafiki, ambae humkanusha Mungu kwa wazi na kwa siri.

100

6.  Anaye jidai kumuamini Mungu bila kutambua (kama) umungu ni nini ,ni miongoni mwa wanafiki .
7. Ujumbe huu ni nuru  ambae hufumbua macho kuwaonesha waziwazi uzima wa Mola wao. 

8. Atakaye amini ujumbe huu  atakua yakini  kwamba Mungu iko mzima.

9.  Hata kua tena miongoni mwa makafiri wala hâta kua tena miongoni mwa wanafiki.
10. Kuamini Mungu katika yakini kuna mfanya mutu ajitenge na shirki ya aina yote.
11. Elimu ndogo inamfanya mutu amufananishe Muumba na kiumbe.
12 .Na pia inamfanya mutu akose woga wa Mungu moyoni mwake.
13. Nabii anaye mpachika mwana kondoo wa Mungu daraja ya umungu ni Nabii wa uwongo.
14Watu hawana woga tena kwa kujipatia daraja ya utume,wala hawana tena woga kwa kumupatia kiumbe 
daraja ya umungu.

15. Mwana kondoo wa Mungu hakujilinganisha na Mungu wake kamwe.
16. Hakufanya ispokua mapenzi ya Mola wake ,ya kuwapatia walio silimu maisha ya milele kwa kuwafundisha

Kutoa shaada ya Mungu.
17. Na ndio maana Mungu alimpenda sana na kumpandisha katika cheo mbinguni.
18. Kiumbe hakiwezi kugeuka kua Mungu wala kumfanana mu namuna yoyote ile.
19. Mungu ni wa pekee aliye pasipo yeyote ,juu ya maala pa juu ,mwenyi kuenea.
20. Mola wenu haumbiwake wala habadirikake wala hafananake na yeyote wala chochote.
21. Kuamini ya kama kiumbe chenzako ndio Mungu wako ni upumbafu wa namba ya juu.
22. Na ijapokua kiumbe hicho kikufanyie nini ,usikiweke pa nafasi ya muumba wako kamwe.
23. Aliye kuumba wewe ndio aliye muumba na yeye pia,na kumtukuza namna hiyo.wala hasingeli kua chochote bila mapenzi ya Muumba.

.24 Mungu peke yake ndio anaye umba,mtukufu aliye tangulia kabla ya ulimwengu na walimwengu kupatikana

25. Mungu hakuzaa wala hakuzaliwa ,hasinziake wala halalake ,hagonjwake wala hafake.
26. Jina la Mungu hali stahili kupewa yeyote wala chochote ,hakuna mwengine aliye na uzima kama yeye .
27. Heri mutu anaye shaidilia umoja wa Mungu Mwenyenzi peke yake bila kumchanganya na yeyote wala 
chochote.

28. Umungu ndio uzima ,yaani ukamilifu .
29. Kua Mungu ni kua mkamilifu ,mwenyi uzima bila hata chembe ya upungufu.
30. Na kwa kua mkamilifu ni lazima kua na uwezo wa kufanya kila kitu, pia na ujuzi wa kujua kila kitu.
31. Muweza wa yote alitangulia kadiri ya kuenea bila upungufu wowote ,na pia hutokeza toka sifuru vilivyomo

angani na vilivyomo ukiwani .
32. Hapana kumpatia yeyote daraja ya umungu.
33. Hakuna umbo ya kumfanana sababu umbo zote ni katika upungufu tafauti sana naye aliye katika ukamilifu. 34 .Umungu ambae ni uzima ni tafauti sana na maisha,yeyote anaye ishi hastahili kuitwa Mungu.
35.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu, mjuzi aliye juu ya maala pa juu ,arshini.
36. Ni yeye peke yake aliye na milki kamilifu, anaye patikanisha na anaye kosekanisha ulimwenguni.
37. Hakuna Mola mwengine kama yeye ,mshindi anaye tawala pahali pote ulimwenguni.
38 . Bila yeye kutangulia kama ulimwengu ni sifuru.
39. Mungu ndio chemchem ya upatikanaji wote na maisha yote.
40. Upatikanaji peke yake ni kwao wazilahewa ,maana wamejumuika bila kuishi.
41. Kujumuika sio kuishi lakini kupatikana.
42. Kuishi ni kupumua hewa namna ya kulinda pumzi umboni.
43. Na kulinda pumzi umboni ndio kua na fikara,
44. Na kua na fikara ndio kua na maisha.
45 .Sio kwamba kila yule anaye jumuika ulimwenguni ndio anaye ishi, ispokua yule anaye fikiri ndio anaye

ishi.

46. Na hafikiri yeyote ispokua yule anaye pumua hewa, ambae hulinda pumzi ndani mwake,
47. Kiumbe ambae hewa huingia ndani mwake pasipo kulinda pumzi, yaani pasipo kupumua ,hakiwezi kufikiri. 48. Ni mfano wa majani ,miti ,mimea ...hawawezi kufikiri sababu ya kuto Linda pumzi ndani mwao.
49 .Hewa inayo katiliza ndani mwake haimsaidie ispokua kwa kugua.
50 .Mungu ndio m'bora wa wafundi ,mjuzi asiye iga kwa yeyote ambae wote huiga kwake.
51. Amejitambulisha kwa watu kwa njia ya ufunuo, akiwaagiza mitume wake kauli tukufu yenyi wokovu.
52. Anajua ya kama umbo ya watu ni zaifu ajili ya mwili, ndio maana huwatumia mitume.
53. Hakuna lawama yoyote kwake maana amewawekeeni wazi mambo ya kiroho ambae mwili hauwezi

101

kuzingatia.

54 Usilazimishe kumzingatia kimwili yeye asiye kua na mwili.
55. Kauli yake tukufu ndio nuru ambae hufumbua macho .
56. Uzima wa Mola wenu ni bayana katika vitabu vyake vitukufu,someni wote nakala ya ufunuo wake.
57. Mungu ndio bwana wa mabwana anaye simamia wanahewa wote pia na wazilahewa wote .
58. Utawala wake ni katika kweli na haki maana yeye ndio mjuzi, hakuna wa kumkosoa.
59 .Kama umbo fulani ni buguza maishani mwako na umbo lako pia ni buguza katika maisha ya wengine.
60. Kadiri Shetani anavyo furahi anapo wanasa watu, ndivyo pia watu wanavyo furahi wanapo wanasa

wanyama katika mitego yao.
61.Kumlaumu yule anaye kuzidia fahamu ni upumbafu wa kweli,hakuna lawama kwa mjuzi. 62. Shukrani ni kwake mwenyenzi aliye umba nuru na giza.

63. Aliye nipatia kauli tukufu katika sehemu saba kadiri ya funguo saba.
64. Anaye fundisha wanahewa wote katika hekima ya ajabu.
65. Maneno ya kitabu cha ukweli ndio mwongozo kwa walimwengu wote.
66. Atakaye tumia kauli tukufu hii kama chakula ya kiroho ya kila siku ,Mungu atamjaza malaika na roho

takatifu nafsini mwake.
67. Pumzi yake itafanyika roho takatifu ,na atakua mkaaji wa bustani atakapo ihama dunia .
68. Heri mutu anaye amini kitabu hiki ,ambae huisoma aya zake kwa wingi kila siku na kuitangaza ku watu . 69. Mola wake atamtukuza kuanzia duniani mpaka mbinguni.
70. Hakika ni mwenyi heshima kubwa mbinguniyule anaye amini ujumbe huu.

( 2 ). KABATI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,mwenyeji wa ulimwengu.
2. Mtukufu aliye umba mbingu aina saba ,na akaumba ardhi aina saba,ile katika anga na hii katika ukiwa .
3. Mola mjuzi aliye fanya anga kadiri ya fikara ,na akafanya ukiwa kadiriya ujinga.
4. M'bora katika kuumba aliye tokeza ulimwengu na walimwengu bila kutumika kazi.

5.Akitaka kitu fulani kipatikane husema:kiwe na palepale kinakua.

9 .Ni yeye anaye tokeza kila umbo kulijaalia upatikanaji pia maisha.
10 Mwanzo wa vyote ,mwenyi mamlaka ya vyote ,kiongozi wa viumbe vyote.
11. Aliye na tumaini ya mwengine badala yake ni pumbafu wa kweli.
12. Kiumbe chenzako hakiweze kukuokoa bila idhni ya Mola wako.
13 Shari na mema vyote vimetoka kwake ,muumba wa nuru na giza .
14. Ambae ni shari kimwili huenda ni heri nyingi kiroho.
15. Usimlaumu mola wako kwa lolote ,ndiye mjuzi wa siri anaye miliki fahamu yote .
16. Magumu ya maisha ya dunia isikupoteze njia,ukavumilia na kuzidisha ibada ,utapewa daraja mbinguni.
17 .Hakuna yeyote aliye amini asiye jaribiwa,heri mutu anaye shinda jaribu
18. Musilimu anaweza kujaribiwa kwa namna ya kuachana ,mara magonjwa ,ufakiri ,mazingizio...
19. Hapana kukufuru ajili ya kujaribiwa,hakika baada ya dhiki ,urakibuni,ni faraja.
20. Umtukuze Mola wakowakati wote na umsujudie yeye peke yake ,wala usitegemee mwengine badala yake.,

21.Ni yeye anaye ona yote na ni yeye anaye sikia yote,mujibu wa dua.
22. Mtendaji wa jumla yamatendo ,anaye miliki kila kitu ulimwenguni.
23.Hakuna Mola mwengine kama yeye,wa pekee aliye juu.
24. Enzi ndio kibla cha walimwengu wote ,tegemeo na kimbilio la wote wenyi akili. 25. Tumieni wote ujumbe huu ,enyi wanaadamu,hakika hii ndio nuru ya maisha yenu. 26. Imani zaifu ya unafiki ,haina tena fasi ndani mwake anaye amini ujumbe huu.

27. Tukuzeni jina la Mola wenu popote mulipo ,hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu mwenyenzi peke yake

28. Mungu ndio kiongozi mwema ,anaye chagua mwalimu wa kila umati .
29. Hakuja kua mtume wa mwisho Mola wenu ataendelea kuwaleteeni wajumbe wake mpaka mwisho wa dunia

30. Atakapo rudia tena mwana kondoo wa Mungu ili apate kumuondoa masih dajali na kuisawanisha ardhi namna yakuinyoosha sawasawa,ndio ukomo wa utume, yaani kufikia kiyama.

 31. Yule atakaye jidai utume na ili hali Mungu hakumtuma ,ni kama mwenda wazimu anaye jitumbukiza shimoni.

32. Ogopeni Mungu ukweli wa kuogopa,wala usipime kumzingizia Mola wakokwa lolote.

33. Mungu anasemaka na watumishi wake katika njia mbalimbali.

102

34. Mara kwa kusema naye sauti kwa sauti ,mara kuwatumia malaika na roho ,marakwa kuwafungua macho,mara kwa kuwafungua masikio,na zaidi sana kwa njia ya ndoto.
 35 . Ndoto ya mtumishi wa Mungu ni miongoni mwa ufunuo ,lakini ufunuo wote sio unabii wala wote sio utume.

36. Kumuona malaika ao roho, bayana ao katika ndoto ,pia nabii ao mtume ,ni neema kubwa .

 37. Ni alama ya uchamungu inayo maanisha daraja ya mutu kiroho .
38. Wakaaji wa mbinguni ndio nuru ya Mungu inayo angazia dunia.
39. Kuwapokea maishani mwako ni kupatikana katika nuru, namna ya kujazwa.

40. Na anaye jazwa nuru ya Mungu ndani mwake ni miongoni mwa roho ,mkaaji wa bustani.
41. Ataingizwa mbinguni katika bustani ya neema hali ya kua roho takatifu.
42. Anaye amini Mungu na mitume yake yote pia na vitabu vyake vyote, ndio anaye jazwa roho takatifu wa

Mola wa ulimwengu.
43.Mitume wa Mungu ni wengi sio yesu peke yake wala sio Muhamadi peke yake wala sio Mussa peke yake... 44. Na vitabu vya Mungu ni vingi sio taurati peke yake ,wala sio zaburi peke yake ,wala sio Injili peke yake,

wala sio qur'ani peke yake ,wala sio kitabu cha ukweli peke yake...
45. Kila mjumbe alipewa maneno na Mungu, na île maneno aliyo pewa na Mungu ndio kitabu cha Mungu.
46. Kumbuka alipo ni chugua roho takatifu, akisema : kuja twende ni kuoneshe.
47. Nikaenda naye tukafika kwenyi nyumba, nikaona malaika anatokea humo ,na akanikaribisha ndani yake.
48. Tukaingia ndani ,mulikua na meremeta mfano wa kilauri .
49. Tukaingia ndani ya chumba upande wa kulia ,tukakuta humo Roho mfano wal'mutu, Aliye kua ameketi

katika kiti mbele ya meza ya muviringo .
50. Akanipokea kwa shangwe,akisema : karibu sana ,ili upate kua yakini na ( utume wa ) Ahmadi .
51. Akaniambia akisema : tazama hii kabati !vile vitabu vyote ndio vitabu vya Ahmadi
52. Kabati ile ilikua ya bilauri yenyi kujaa vitabu.
53Katika nyumba nzuri sana, yenyi kumeremeta na nuru.
54. Roho akasema : Ahmad aliubiri maneno mengi ambae hupatikana ndani ya vitabu hivi unavyo viona ndani

ya kabati hii.
55. Nenda kuwaambia watu kwamba Ahmadi alitumwa na Mungu mwenyenzi.
56. Usilimu ndio dini ya haki mbele ya yule aliye umba mbingu na ardhi.
57. Kua yakini na upekee wa Mungu kwamba hakuna mwengine kama yeye na kuamini mitume wote pia na

vitabu vyake vyote ,ndio kua katika dini ya haki.
58. Kilicho kigumu kwao ni kuamini mitume wote kwa jumla ,yaani kutumikisha mafundisho ya mitume wote

kadiri inavyo stahili.
59.Uwingi wa madini umetokana na uchache wa imani pia na uchache wa elimu.
60. Uchache wa imani unawafanya wakose woga wa Mungu na hata wafikie kujiundia vikundi mbalimbali vya

kidini ,ajili ya hanasa ya dunia.
61. Na uchache wa elimu unafanya watu watumie maandiko matakatifu kwa uziwi na upofu.
62. Hakuna dini ingine kinyume na usilimu,dini ya mitume wa Mungu wote kwa jumla.
63. Wala jumuiya (madhehebu)la kidini sio dini ,wala uwingi wa mitume sio uwingi wa ma dini.Kuna Mungu mumoja na dini yake moja,

Mitume wake ndio wengi.
64. Enyi walio silimu! unganeni katika kamba moja ,na mupendane musigombane wala musiachane musije

mukaanguka katika mutego wa Shetani.
65. Wala usifanye jumuiya la kidini ajili ya siasa ya dunia, wala ajili sifa na utajiri wa kidunia

66. Mola wa ulimwengu ni mumoja na dini yake ni moja
67. Hakuna dini ya watu wa rangi fulani wala hakuna dini ya watu wa kabila fulani.Bali moja tu kwa watu wote.

68.Shangilieni uzima wa Mola wenu ,mtukufu anaye jaa mamlaka isio kua na Kipimo, mshindi.
69. Shukrani zote zina mustahili mungu mwenyenzi wa pekee anaye tosheleza walimwengu wote kwa jumla. 

70. hakuna mola mwengine kama yeye , Muumba wa mbingu saba na ardhi saba,wa miujiza Aliye juu.

( 3 ). ONDOA SHAKA

1. Enyi walio silimu, jiepusheni na ushirikina mû namna yote, wala usimsujudie yeyote ila Mungu peke yake.
2. Ushambulizi wa wachawi na wanafiki usikutoe katika njia iliyo nyooka .
.3 .Sio zambi kumuendea mutumishi wa Mungu ili akuombee ao mganga ili akutunze.
4. Kilicho muimu kwako ni kumtumainia Mungu, hakuna mutu atakaye kunusuru bila idhni ya Mola wako.
5. Maombi yako kwa Mungu ndio bora zaidi, hapana kukata tamaa.
6. Ni bora zaidi kuanza na toba ,kujisihi kwa Mungu akusamehe zambi zote ,tangu kupata akili mpaka sasa ,na baada ya toba

103

utafanya ibada mbali mbali.
7. Hakika zambi ndio kiziwizi cha maombi ya mutu kwa Mola wake, pia na kukosa uyakini na uzima wa Mungu.
8. Wala usizarau zambi yoyote,utazani ni ndogo kumbi ni kubwa mbele ya Mola wako.
9.Wala usizarau wema wowote, kila tendo huesabika na Mola wako.
10.kumtegemea mutu ni kwenyi hasara kubwa, utazani ni tunda la nuru kumbi ni tunda la giza.
11 Na pia ni miongoni mwa ushirikina, utazani hauna shirki kumbi wewe ni miongoni mwa washirikina .
12. Na atakaye abudu ili kujionesha ku watu ao ajili ya hanasa ya dunia, ni miongoni mwa washirikina ambae huabudu kinyume na Mungu.
13. Kumtumainia Mungu zaidi ya wote ndio imani ya kweli.
14. Ondoa shaka ajili ya uzima wa Mola wako, Hakuna mwengine aliye na utukufu kama yeye .
15 . Mungu ndio muweza wa yote mwenyi mamlaka y'a milele, Hakuna asiye milikiwa naye.
16. Kama hauzingatie utendaji wa Mola wako maishani mwako ,ni kwamba hauja takasika bado.
17. Kua mguu njiani mguu porini kuna mfanya mutu afunikwe na giza mbali sana na nuru ya Mungu.
18.Heri mutu anaye jifanya kua mzalili mbele ya Mola wake, kama vile mtoto mchanga mbele ya mzazi wake.
19. Ambae humtumainia Mola wake katika mambo yote na kumtii sana na zaidi.
20 .Mola wenu amewapenda sana wanyenyekevu wenyi upole moyoni.
21. Na jitengeni na wakaaji wa hadeze maisha yako yote ili usije kuingia zimuni baada ya kufa kwako.
22. Zimu ni kambi mbaya sana, kurafikiana na wakaaji wa humo ni kujifanya kua mkaaji wa zimuni.
23. Mshirikina hawezi kukupatia nguvu wala ushindi kwani yeye ndio muzaifu wa kweli kiroho.
24. Nguvu inatoka mbinguni,na uzaifu unatoka hadezeni.
25. Kafara ya shetani ni udanganyifu mtupu, utazani ni nguvu kumbi ni uzaifu.
26. Urafiki na wakaaji wa mbinguni ndio unao leta nguvu ya ushindi nafsini mwenu.
27. Na pia unamfanya mutu kua mkaaji wa mbinguni, pamoja na malaika na roho, atakapo ihama dunia.
28. Mamlaka ni yake Mwenyenzi Mungu, muweza wa yote, mutukufu asiye kurubiwa na uzaifu wowote.
29. Nguvu yote imetoka kwake, mumilki anaye patikanisha na anaye kosekanisha ulimwenguni.
30. Vitu vyote hupatikana kwa idhni yake, mtendaji wa jumla ya matendo,aliye pasipo yeyote.
31. Sema : akitaka Mwenyenzi Mungu itafanyika. Hakika pasipo idhni yake hakufanyike lolote.
32. Upatikanaji wako na maisha yako hutokana na idhni yake.
33. Umshukuru Mola wako kwa neema aliyo kupatia:kila ulicho nacho ni neema kutoka kwa Mungu.
35. Shukrani zote zinamustaili Mwenyenzi Mungu Mola wa ulimwengu.
36. Kauli tukufu ni ukweli ambae hutokea enzini. na ndio maana hakuna shaka ndani mwake.
37. Mungu ndio anaye fundisha wanahewa wote ili wapate kutumia njia iliyo nyooka.
38. Maisha haitimilike pasipo neno la Mungu.
39. Atakaye tumia neno la Mungu ndio atakaye ishi milele.
40. Ma nabii na mitume ndio wanao pokea neno la Mungu na kuwafundisha watu.
41. Ni amri kwa kila mutu kuwaamini wote pasipo kumpinga yeyote, lakini usifananishe aliye na mizimu na yule aliye na roho takatifu.
42. Kwa kutambua mtume wa kweli sio miujiza peke yake lakini hasa ukweli wa maneno aliyo kuja nayo .
42. Zama hizi wengi ndio wadanganyifu wanao jidai utume kwa ugumu wa nyoyo zao.Na ilihali hawakutumwa na Mungu.
43. Ramli sio unabii, wala kuubiri maandiko ma takatifu sio kua mtume wa Mungu.
44. Mjumbe wa Mungu ni mwenyi elimu, hekima na maarifa ya kiroho,mwenyi nuru ya Mola wa Ulimwengu.
45. Amejaa wanahewa_halisi nafsini mwake, mwenyi imani timamu.
46. Hakika mutamutambua kwa matendo yake, mnyenyekevu wa kweli mwenyi upole moyoni.
47. Anaye jidai utume pasipo ujumbe ni mdanganyifu ,sio mjumbe asiye na ujumbe.
48. Ukweli umejitenga na uwongo, pia uzuri umejitenga na ubaya.
49. Mtume wa Mungu hawezi kununua wala kuuzisha neno la Mungu.wala hawezi kumlinganisha Nabii yeyote na Muumba wake.
50. Mtume wa Mungu hawezi kununua wala kuuzisha nguvu ya Mungu.wala hawezi kuomba mwengine kinyume na Muumba. 51. Mtume wa Mungu hawezi kutumika kazi ya Mungu ajili ya hanasa ya dunia.
52. Mtume wa Mungu hawezi kufanya kazi ya Mungu kama viashara :alipewa kwa bure na anatoa kwa bure.
53. Mtume wa Mungu hawezi kulazimisha watu kutenda mema na ilihali mwenyewe hatendake mema.
54. Mtume wa Mungu ni mwalimu ambae kauli yake na matendo yake hufundisha watu.
55. Imani yake ni kubwa, mpaka itadhihirika,ijapokua ushambulizi wa watu wa dunia.
56. Mtume wa Mungu hawezi kuhubiria watu ispokua Yale anayo funuliwa na Mungu.
57. Mtume wa Mungu hawezi kushindwa kusali : wala hawezi kusali pasipo kusoma sura ya ufunguzi, wala hawezi kusali pasipo kutoa shaada, wala hawezi kusali pasipo kumsujudia Mungu.
58. Mtume wa Mungu hawezi kua muovu wala mnafiki;wala kufanya (siasa ya) upelelezi.

59. Ogopeni Mungu ukweli wa kuogopa, hapana kujidai utume na ilihali Mungu hakukutuma.
60. Amini Mungu aliye tangulia ulimwenguni, mkamilifu asiye gusika na upungufu.
61. Na aminini wa malaika wake pia na roho, na aminini pia mitume wake pia na vitabu vyao vyote.

 62. Usiamini Nabii ao mtume wa uwongo ambae ndani mwake hamna hâta chembe ya nuru ya Mungu.

104

63. Nabii wa kweli ao mtume wa kweli hawezi kumpinga Nabii wa kweli wala mtume wa kweli. Wala hawezi kuja na ushuuda wa mjumbe wa zamani bila kufunuliwa chochote kuhusu mjumbe wa umma wake.
64. Zama hizi mjumbe yeyote atakaye kuja na ushuuda wa taurati na zaburi hali ya kua amekanusha injili ni mjumbe wa uwongo.

65. Na mjumbe yeyote atakaye kuja na ushuuda wa injili hali ya kua amekanusha qur'ani bila shaka ni mjumbe wa uwongo.
66. Na mjumbe yeyote atakaye kuja na ushuuda wa qur'ani hali ya kua amekanusha kitabu cha Ukweli bila shaka ni mjumbe wa uwongo.
67. Ni bora zaidi kumtaja mtume wa zama zako katika sehemu ya pili ya shaada yako.
68. Na pia ni kawaida kuwataja mitume wa kubwa katika sehemu ya pili ya shaada yako.
69. Mitume wa Mola wako wenyi daraja kubwa zaidi ni Yesu masiya, Mussa,Muhamadi na Eliya.
70. Ametakasika mwenyenzi Mungu,m'bora wa kuumba, anaye podoa vipenzi vyake kwa namna ya ajabu.

( 4 ) DINI BORA


1. Ewe mpenzi wa Mungu! Tumieni Usilimu kama dinimaishani mwako ,wala usiritadi baada ya kusilimu .
2. Anaye silimu sio mbaguzi wa mitume ,ni bora zaidi kutumia umoja wa Mungu pia na uwinmgi wa mitume yake.
3. Katika ma nabii na mitume kunapatikana wakubwa na wadogo,na pia kuko wa zama zako na wa zamani.
4. Hakuna asiye kua wako ,wala asiye stahili kushahidiliwa nawe.

5. Mola wa ulimwengu amewapenda sana wanao toa shaada katika uyakini ,ambae hutumia vilivyo maneno ya mitume wote . 6. Umealikwa kutumia dhati tukufu yaYesu Masiya,mkuu wa ma nabii,anaye jaa nuru kubwa,utazani jua ya asubui.
. 7. Amekupenda sana na tayari amekwisha kutengenezea njia ,upate kuingia mbinguni.
8. Na umealikwa kutumia dhati tukufu ya Muhamadi ,bwana wa mitume ,anaye jaa nuru kubwa ,utazani maandamo ya mwezi. 9. Amekutengenezea njia ,kwa idhni ya Mola wake,ili upate kuingia salama mbinguni.

10. Makundi ni mengi katika wafuasi wa Bwana Yesu lakini sio yote itakayo pokelewa mbinguni.
11. Na pia kunapatikana makundi mengi katika wafuasi wa Muhamadi lakini sio yote itakayo pokelewa mbinguni.
12. Hupokelewa mbinguni wale wanao amini Mungu mwenyenzi,na mitume yake yote na vitabu vyakevyote.
13. Wale ambao hawana ubaguzi wa Mitume, ambae hawakukata undugu wa kimwili wala hawakukata undugu wa kiroho.
14. Wale ambae kadiri wanavyo mpenda Bwana Yesu ndivyo wanavyo mpenda pia mtume Muhamadi pia na mitume wengine wote
15. Roho akaniambia akisema : hakika Nina kuambia Mola wa ulimwengu ni mwingi wa huruma ,alisamehe baadhi miongoni mwao wakati wao.
16. Hakuwaacha wote kupotea,maana ni mwenyi rehema za kuenea , ni mpole sana tena msamehevu .
17. Katika walio mfuata Yesu masiya, lilikubalika mbinguni jumuiya la kidini katolika,kwa huruma wake.
18. Na katika walio silimu kwa kumfuata Muhamadi lilikubalika mbinguni jumuiya la kidini Ahmadiya.
19. Sio kwamba yote walio kua nafanya ni bora kabisa ispokua kwa huruma wake Mwenyenzi.
20. Kusujudia sanamu ya nabii wa Mola wao ni zambi,lakini waliifanya kwa ujinga.Kuona kama waliitumia kama kumbukumbu pasipo kuiyakinisha moyoni ndio maana walisamehewa.wakati huu atakaye endelesha ibada kama hii ataangamia.
21. Na sala yao ni pungufu ,walitumia kisomo cha sura ya ufunguzi ,lakini hawakusujudu wala kutoa shaada.
22. Kumkataa mtume wa Mungu ndio jambo ambae kawaangamiza wengi miongoni mwa watu.
23. Atakaye kataa kutubu na kuacha imani hiyo pungufu,ameangamiza nafsi yake mwenyewe.
24. Makundi haya sio dini ,lakini jumuiya za kidini ,katika dhati tukufu ya Yesu masiya pia na katika dhati tukufu ya Muhamadi
:”dini bora kabisa ni Usilimu”.
25. Kutumikisha yaliyo kuja kabla ya Yesu masiya, bila kutumia injili ,ni kumpinga bwana Yesu.
26. Na kutumikisha ujumbe ulio kuja kabla ya Nabii Muhamadi ,bila kutumia qur'ani,ni kumpinga Nabii Muhamadi.
27. Na kutumikisha yale yalio kuja kabla ya Kalonda bila kutumia kitabu kitukufu cha ukweli,ni kumpinga shahidi wa Mungu Kalonda.
28. Kuamini sehemu na kupinga sehemu ya neno la Mungu ni ukafiri mtupu.
29. Maneno ya Mungu haipinganake bali hujazikishana , maana ni kweli moja.
30. Makafiri wamedanganyia kuamini ma nabii na mitume wa zamani hali ya kua wamempinga kabisa mtume wa umati wao.
31. Heri walimu wanao hubiri maandiko ma takatifu ya vitabu vya Mungu vyote .
32. Mungu ni mumoja ,na kweli yake ni moja ,na dini yake ni moja.
33. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu peke yake, na hakika Mussa, na Yesu ,na Muhamadi,... walitumwa na Mungu.
34. Someni sura za ufunguzi katika sala,ambae hupatikana katika kitabu cha ukweli na katika kitabu cha qurani, na pia inayo patikana katika kitabu cha Injili.

35. .Hakika sura ya ufunguzi,na sijida na shaada ni mambo muimu katika sala.
36. Laiti mungeli muamini nabii mtukufu Muhamadi,mnara wa nuru ya Mungu,
37. Dini ya Yesu masiya ndio dini ya Muhamadi na ndio dini ya Mussa...
38. Atakaye mpinga Muhamadi amekwisha mpinga Yesu masiya na Mussa na Ibrahimu...na mitume wengine wote.
39. Kujifanyia yale ambae Bwana Yesu hakuwafunza ,ndio jambo ambae huwatoa katika dini aliyo kuja nayo ya usilimu. 

40. Sema : bwana Yesu hakufundisha yote wanao ya fanya, mengi wamejifanyia wenyewe.

41. Hakuwafundisha kusali kadiri wanavyo sali,wala hakuwafundisha kufunga saumu kama wanavyo funga. 42. Kwa kusali, mwana kondoo wa Mungu aliwapanga wanafunzi wake, nyuma yake ,katika sahafa.
43. Na akamuimidi Mola wake na kushaidilia uzima wa Mola wake na kusoma sura ya ufunguzi na kusujudu. 44. Alikua akifanya hivyo kila siku asubui na mangaribi,

45. Katika kipindi cha asubui alikua na fanya hivyo mara mbili,

46. Na katika kipindi cha mangaribi alikua na fanya hivyo mara tatu.
47. Anaye muamini Yesu masiya ni yule anaye fuata mafundisho ya Yesu masiya.
48. Mungu ni mkamilifu tafauti sana na viumbe vyote,ametangulia kadiri ya kuenea bila upungufu wowote.
49. Yeye ndio mwanzo wa vyote,aliye tokeza vitu vyote kwa jumla.
50. Kila yule ni kiumbe alicho kiumba ,mtukufu zaidi ya wote,anaye miliki walimwengu wote kwa mamlaka yake mwenyewe.

 51. Amezidia wote mwenyenzi Mungu,mumilki anaye patikanisha kwa idhni yake na anaye kosekanisha pia kwa idhni yake.
52. Maisha yako imetokana na idhni yake, mpanaji wa pumzi ,anaye jengea kiumbe makao.
53. . Roho ni tunda la neno lake, chombo halisi cha mchoraji,ambae hulindwa vizuri nyumbani mwake.
54. . Mbinguni hakuna mabadiriko ya usiku na mchana,wala mabadiriko ya kipwa na mashika.
55. . Kambi lenyi starehe kadiri ya bustani ya neema,hakuna usingizi wala shuruli ya kazi .
56. . Maisha ni yenyi kutimilika humo kadiri ya starehe ya milele,ni tayari kwake kila kile atakacho hitaji .
57. Hakuna huzuni wala kilio ispokua furaha na shangwe kila wakati.
58. Heri mutu anaye muamini Yesu masiya kama Nabii na mtume wa Mola wa ulimwengu, mwenyi daraja kubwa sana mbinguni
59. Yeye ni nabii na mtume wa Mungu mwenyi cheo kubwa mbinguni, zaidi ya wa malaika.
60. Mola wa ulimwengu alimupatia utukufu wa namba ya juu,maana alimkurubisha sana naye.
61. Mungu ndio aliye mupatia utukufu kama huo,hapana kumpimanisha naye.
62. Yeye ni kiumbe ambae hakiwezi kufanya lolote bila ya idhni ya muumba wake.
63. Hakuna kiumbe cha kumlinganisha nacho yeye aliye kiumba pamoja na wengine wote wanao jumuika ulimwenguni.
64. Kama mtukufu uyu ( Yesu masiya )anapatikana ni kwa idhni ya Mola wake.
65. Mola wake angeli penda kumuondoa ,bila shaka angeli futika kwa rafla, hange kua miongoni mwa wanao ishi wala hangeli kua miongoni mwa wafu ,bali angeli kosekana ulimwenguni,ingeli kua kwake kama ilivyo kua kabla ya kuumbwa kwake. 66. Uwezo wa Mola wake ni wa ajabu sana ,maana ni milki kamilifu, halingane na yeyote kwani wengine wote ni viumbe alivyo viumba.
67. Mola wako halingane na yeyote wala chochote,mamlaka yake ni yenyi kuenea, wa milele aliye juu.

68. Humtukuza vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, Mola wa karne na karne,tumaini la walimwengu.

69. Mungu ndio anaye fanya yote,m'finyanzi wa vyote vilivyomo angani na vyote vilivyomo ukiwani.

70. Hakuna Mola mwengine kama yeye, wa maajabu aliye juu.

5). UMBO TIMAMU

9. Na ndio maana sio matamanivu ya mwili bali matamanivu ya roho.
10. Kusema kama Mungu hana shida na ibada kimwili ni kusema kama Mungu hana shida na matendo mazuri yanayo fanyika na mwili wa mutu.
11. Na kusema kama Mungu hana shida na matendo mema ni kukufuru Mungu, yaani ni kupinga neno la Mungu.
12. Mutu hawezi kutenda mema bila viungo vya mwili wake kuyatenda.
13. Na pia mutu hawezi kutenda mabaya bila viungo vya mwili wake kuyatenda.
14. Hali ya roho ya mutu huzingatiwa kupitia matendo ya mwili wake.
15. Kujidai kutenda mema kiroho peke yake bila kuyadhihirisha kimwili ni unafiki mtupu.
17. Wanafiki wamefikia hâta kuvunja amri ya Mola wao kwa kuzingizia matumizi ya ibada kiroho peke yake.

106

18. Wanafikia kuzini,kuuwa,kula haramu,kuacha sala...kimwili ,wakisema:tumeyafanya kiroho.
19. Hakika watu wanao fanya hivyo ni makafiri tena wanafiki wakubwa.
20. Mwili hutumikishwa kama inavyo stahili kimwili,na pia roho hutumikishwa kama inavyo stahili kiroho; mwili na roho ndio hujenga umbo la mwanaadamu.
21. Kama tafsiri kimwili ni lugha Inginena pia tafsiri kiroho ni lugha ingine tafauti,sio kwamba kunakua upinzani.
22. Lugha haipinganake,kila ile hutaja na husikilizisha mu namna yake.
23. Hakuna lugha ambae matumizi yake huvunja matumizi ya lugha ingine.
24. Kuacha sheria ya Mungu kimwili ni ukafiri wa bayana.
25. Na pia kuacha sheria ya Mungu kiroho ni ukafiri wa kisiri siri.
26. Mnafiki ni yule asiye timiliza mapenzi ya Mungu katika kawaida yake:Yule ambae huitupilia mbali kimwili ao Yule ambae huitupilia mbali kiroho.
27. Muaminifu wa kweli kabisa ni yule anaye tumia sheria ya Mungu katika kawaida yake, kimwili na kiroho.
28. Mwili wako pamoja na roho yako ndio umbo lako timamu.
29. Mwanahewa_haramu ambae hana roho ndani mwake ndio anaye tenda kimwili peke yake.
30. Na mwanahewa_halisi ambae hana mwili ndani mwake ndio anaye tenda kiroho peke yake.
31. Kwa kua na roho ndani mwako inabidi kua na imani ndani mwako.
32. Kua na pumzi mwilini mwako sio kua na roho ndani mwako.
33. Mutu anaweza kutenda kimwili peke yake, lakini hawezi kamwe kutenda kiroho peke yake pasipo viungo vya mwili wake kuyadhihirisha kitendo.
34. Kutenda kimwili peke yake ni kutenda na viungo vya mwili wake kadiri ya tamaa ya mwili wake pasipo mwongozo wa roho takatifu.
35. Hakika ibada ya Mungu sio matamanivu ya mwili lakini matamanivu ya roho takatifu.
36. Na ibada haidhihirike pasipo viungo vya mwili kuyatenda.Ndio maana haifanyikake kamwe kiroho peke yake.
37. Nabii ao mtume anaye amuru kuvunja alama ya dini ya Mungu ni nabii ao mtume wa uwongo.
38. Masih Dajali ni muovu mkuu atakaye kuja na maubiri ya mafumbo,akigeuza maana ya andiko kwa kuzingizia tafsiri ya kiroho.
39. Fanyeni ibada ya Mungu katika kawaida yake kama inavyo andikwa,ili mupate kuokolewa.
40. Mungu ndio anaye stahili kuabudiwa kwa haki ,muumba wa mbingu na ardhi aliye na mamlaka ya ajabu.
41. Alitangulia kabla ya ulimwengu na walimwengu bila msaada wa yeyote.
42. Mkamilifu aliye na mamlaka isiyo na kipimo,mfalme wa ajabu.
43. Alikua ,yuko na atakua,wa milele aliye juu.
44. Enzi ndio dhati yake, muweza wa vyote anaye pangilia kila upatikanaji na kila maisha.
45. Ndiye mjuzi anaye ona yote na anaye sikia yote.
46. Aliye muujiza wa maajabu,aliye pasipo yeyote,aliye juu ya maala pa juu.
47. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,m'ponyaji wa kila magonjwa ,anaye rehemu na anaye kirimu.
48. Ndiye muumba wa uhai na kifo ,anaye miliki vyote bila hitaji ya msaidizi .
49. Neno lake analo teremshia wachaguliwa wake ndio nuru yake inayo angazia wanaadamu.
50. Matumizi yake huleta nguvu ya kuishi milele,na kukosa kuitumia ndio huzaufisha kwa kupatwa na mauti ya milele.
51. Duniani maisha na mauti ni alama;maisha ya kweli hupatikana mbinguni ,na kifo cha kweli hupatikana hadezeni .
52. Mungu ameangazia watu na kuwajaalia daraja na kazi ya kiroho mbalimbali.
53. Mutu anaweza kua nabii na hali yeye sio mtume.
54. Na pia mutu anaweza kua mtume na hali yeye sio nabii.
55. Na pia mutu anaweza kua nabii na mtume .
56. Kila Mjumbe iko na ujumbe wake alio kuja nawo ,na ujumbe wake ndio kitabu chake alicho pewa na Mungu.
57. Kunapatikana wajumbe wakuu na wajumbe wadogo,na pia kunapatikana vitabu vikubwa na vitabu vidogo.
58. Wajumbe wote ni kwa watu wote ,na vitabu vyao vyote ni kwa watu wote pia.
59. Hakuna mtume wa dini fulani, na pia hakuna kitabu cha dini fulani.
60. Katika mwanzo wa upokezi wa ujumbe ,kama malaika ndio aliye fungua mbingu mbele ya roho ,mjumbe uyu ni nabii wa Mungu.
61 Na katika mwanzo wa upokezi wa ujumbe wake, kama roho ndio aliye fungua mbingu mbele ya malaika,mjumbe uyu ni mtume wa Mungu.
62. Na kama malaika na roho walifungua mbingu wote pamoja na kumshukia,mutu uyu ni nabii na ni mtume.
63.Unabii ni katika nuru ya zamana ,na uwalii ni katika nuru ya bustani.
64. Mitume wote sio manabii ,na manabii wote sio mitume.
65. Na tena ma walii wa Mungu wote sio mitume,ispokua miongoni mwao yule anaye pewa kazi ya utume.
66. Kunapatikana aina tatu ya uwalii :kuna usidiki,na ushahidi ,na usalihi.
67. Utume haupatikane ispokua katika usidiki na ushahidi .

107

68. Ma walii ambae hawa tambulikanake na watu wa dunia ni miongoni mwa masalihi.
69. Mola wenu ni mkadiriaji wa karama anaye patiana zawadi ya kiroho kwa amtakaye.
70Hakuna mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua mwenyenzi Mungu peke yake, na hakika Kalonda ni shahidi wake.

( 6 ) UTUKUFU WA KISOMO

1. Neno la Mungu ni dawa:ukingo na ponyo,hunusurika kila mutu anaye itumia kama kawaida.
2. Kisomo cha ukweli ni matibabu ya nafsi pia ya maisha ya yule anayeirudilia aya zake.
3. Malaika na roho humkurubia na kumjaza nguvu ya ushindi na nuru .
4. Na ndio maana amekua na uhuru pasipo kumilikiwa na falme za giza.
5 Amefunguliwa aliye kua amefungwa,na tena ni katika ulinzi wa namba ya juu ambaye bado kuvamiwa,ajili ya kisomo cha ukweli.
6 Mungu amempenda sana anaye soma kauli yake kila siku,amemutia katika kundi ya watumishi wake .
7 Hakuna atakaye weza kumunyanyasa aliye mikononi mwa Mola wa viumbe.
8. Wachawi wamejiandaa vita naye,wanataka kumuondoa ao kumunajisi ajili ya chuki..
9. Hawataki kuona mutu anaye meremeta na nuru kakika jamaa lao .
10. Ibada ya Mungu ndio jambo muimu katika jihadi hiyo.
11. Kisomo hufuta doa za uchawi, kadiri nuru inavyo futa giza.
12.
Someeni ukweli katika vyote utakavyo vitumia ,kimwili na kiroho,ili maisha yako ipatikane katika ulinzi wa Mungu mwenyenzi.
13. Mola wa ulimwengu peke yake ndio tumaini na nguvu ya wasilimu,anaye tosheleza haja zote.
14. Yeye ndio kibla cha ulimwengu ,mshindi ,aliye na uwezo wa kufanya kila kitu.
15. Utakapo nuwiya kumsujudia,ni bora zaidi kuhelekea kibla.
16. Ukinyenyekea moyoni mwako Mola wa nyumba hii takatifu, mumoja Aliye enzini, hakuna mwengine ila yeye tu.
17. Atakaye nyenyekea kitu kinyume na Mola wa nyumba hiyo takatifu,bila shaka atakua miongoni mwa washirikina.
18. Mjuzi ni Mungu peke yake,anaye stahili kuamua wanahewa wote.
19 Hapana kuhukumu kiroho usije kuhukumiwa.
20. Wala usijipandishe katika daraja isiyo kua yako usije ukashushwa.
21. Wala usikose kufanya kazi ambae Mola wako alikupatia ajili ya kuogopa watu wa dunia,usije ukalaaniwa na Mola wako.
22. Ni kawaida kwa mwanaadamu kumuogopa Mungu zaidi ya wote.
23. Wala usitende lolote kadiri ya mapenzi ya watu ,lakini tendeni yote kadiri ya mapenzi ya Mungu.
24.Sema: Mungu ndio muumba wa ulimwengu na walimwengu.
25. Aliye tangulia kadiri ya kuenea,bila mwanzo wala mwisho.

26. Mkamilifu awezaye yote na ajuaye yote, mwenyi uzima.
27 Mwenyi mamlaka juu ya kila kitu, anaye hitajiwa na wote bila yeye kumuitaji yeyote.
28. Kiongozi pekee wa viumbe vyote kwa jumla,anaye jumuisha wote bila yeye kujumuika, wa pekee anaye stawi arshini.
29. Vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani ni mazao ya idhni yake,mfinyanzi wa upatikanaji na maisha.
30 . Mufalme wa wafalme wote anaye tawala milele, pasipo kutetea wala kukombolana wala kuchaguliwa.
31. Mola wa karne na karne ,mshindi anaye zidia wote, wa miujiza aliye juu.
32. Aliye huru kufanya kila apendalo ,hakuna wa kumkosoa wala wa kumuhukumu ,mtukufu aliye juu ya maala pa juu,mufalme.
33. Hana mwili wala pumzi ,mwenyi Enzi tukufu dhatini mwake.
34. Na ndio maana hayupo angani wala ukiwani,mwenyi hatua kabisa na viumbe vyote.
35. Anaye ona vyote na anaye sikia vyote,mjuzi aliye tangulia.
36. Ni vyake vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini,mwenyeji wa ulimwengu.
37. Alikua, yuko, na atakua ; Mwenyi ukamilifu tafauti kabisa na upungufu wote.
38. Mungu ndio mwalimu wa wote ,aliye mfundisha Kalonda ukweli wake na kumtuma nawo kwa watu wote.
39. Kitabu chake ni Ukweli usio na shaka,ujumbe wa ajuaye yote na awezaye yote.
40. Hakuna mwengine kama yeye ,mwenyi kupatikana kadiri ya kuenea.
41. Mola wenu ndio msaidizi wa wote katika shida zote,mwenyi rehema za kuenea.
42. Mjuzi wa kuumba anaye patiana ujira kulingana na majira ya imani yao.

43.Nuru yake Mwenyenzi imeangazia mbingu na ardhi,na vilivyomo hufuraikia matumizi yake.
44. Mola wa wanahewa wote na wazila_hewa wote ,anaye tawala juu na chini,na pia ndani na inje.
45. Hakuna pale alipo anzia wala pale alipo komea ,wa milele anaye patikana juu ya maala pa juu ulimwenguni.

 46. Heri Mutu anaye tumia maamrisho ya Mola wa ulimwengu na akaitupilia mbali makatazo yake.
47. Roho ametua nafsini mwake na kuongoza maisha yake.
48. Amebahatika kupata maisha ya milele, kadiri ya utimilifu ambae ni nuru ya ukamilifu.
49. Njooni wote tuingie katika usilimu ,dini ya haki.

50.Matayarisho ya Mola wenu mbinguni ni makubwa ajili yao watakao silimu.

51. Usidanganyike na mishirikina wanao jidai utume kwa ugumu wa nyoyo zao.
52. Wao ni warozi wakuu ambae hujitaidi kuroga wachamungu na lengo ya kuiba nyota zao.
53. Hawata weza kumpoteza yule ambae Mola wenu amekwisha muongoza.
54. Ombeni kwa Mungu akujaalie mwisho mwema ,na akuongoze ili upate kuingia mbinguni.
55. Kuongoka kwa mwanaadamu ni kusilimu na kumuabudu Mungu peke yake.
56. Mola wenu atawapiga kwa laana kubwa wale wanao piganisha nuru itokayo mbinguni.
57. Wale ambae hawataki kuamini ujumbe wa Mola wao.
58. Wale ambae wanashambulia haki na kweli na hali wanazingatia.
59. Mungu atamnusuru mchaguliwa wake kwa namna ya ajabu,makafiri watabakia vinywa wazi kwa kusangaa wokovu wake.

 60. Ni mwenyi uwezo wa kuokoa ijapokua mu dakika ya mwisho.
61.Mufalme wa wafalme anaye miliki vyote vilivyomo angani na vyote vilivyomo ukiwani.
62. Shaada na sijida humustahili yeye peke yake, Mola wa mambo yote kwa watu wote,mkamilifu aliye juu.
63.Mshindi anaye stiri maisha ya kila kiumbe,mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu.

64.Mola wa maajabu anaye sikia ambae bado kusemewa ,na huona ambae bado kupatikana.
65.Baba wa Salama Aliye Salama,chemchem ya upatikanaji na maisha,wa popote na milele.
66. Aliye tangulia ulimwenguni mwenyi kuenea katika tendo kua kadiri ya uzima tafauti kabisa na maisha. 

67. Bingwa anaye zidia kila kitu, wa pekee aliye huru ulimwenguni.
68. Mlinzi wa viumbe ambae idhni yake hutosheleza ,
69. Anaye fanya viumbe vyote vipatikane katika ulimwengu,m'bora wa kuumba.
70. Hakuna wokovu njee ya sheria yake,neno lake hutimiliza nafsi zao kadiri ya roho takatifu.

{ 7 } UTAJIRI

1. Ewe uliye amini ! Utakapo omba mali ni lazima uombe Mungu akujaalie pia busara ya Kutumia Mali hiyo.
2. Kuomba mali mingi pasipo busara ni kuomba shari kubwa, maana ni kujiweka katika mtihani.
3. Hakuna tajiri atakaye okolewa bila Kutumia Mali yake kadiri ya mapenzi ya Mungu.

4. Ni muimu kwa tajiri kutumikisha kazi ya Mungu na Mali yake,na kutoa zaka pia na sadaka.

 5. Mali yako ilete usalama katika jamii la Watu :usimzarau maskini wala usijivune.
6. Na Mola wako akubalike,na aabudiwe,na asifiwe kupitia mali yako.
7. Heri tajiri anaye Saidia watu wasio jiweza, anaye silimu na anaye amini.

8. Ole wao wajinga, wanao uzisha maisha yao ajili ya tamaa ya dunia. 

9. Wamefikia kufanya mapatano na Shetani,ili watajirike.
10. Wamezani kupata kumbi kupatikana( kupatwa).
11. Ushirikina ndio upotevu wa bayana.

12. Ni mfano wa kujitumbukiza mwenyewe motoni.
13. Utajiri wa kweli ni uaminifu,matendo nzuri ndio hudumu milele,mali isiyo punguka kwa kuchomba. 14. Anaye penda utajiri wa milele, afanye matendo mazuri,


{ 8 } MWALIMU MNAFIKI

1. Enyi walio silimu ! aminini Mungu katika yakini, wala usiabudu kiumbe chenzako kamwe.

2. Yeyote aliye zaliwa ni kiumbe kilicho umbwa kama wewe.

3. Ni amri kwa watu wote kuamini ma nabii wote na mitume wote.

4. Kuamini sio kuabudu,na yeyote atakaye abudu mtume ni sawa na yule anaye abudu sanamu.

5. Ni bora kuwafuata katika kazi ya Mungu.

6. Kumuendea mtumishi wa Mungu ili akuombee sio zambi,lakini bora zaidi ni kuwa yakini na Mola wako.

7.Ndio maana usiache kumuomba Mungu, ijapokua wengine wanakuombea.

8.Ni vema kumchunguza sana muombaji wako utakaye muitaji,kama ni wa kweli ao mnafiki.

9 . Mwalimu mnafiki anasemaka maneno mazuri sana lakini matendo yake mabaya sana.

10. Anaimiza watu watoe zaka na sadaka lakini Mwenyewe hatoake.

109

11. Amejidai kua na roho na ilihali ni mwenyi kua na mizimu (majini). 

12. Amesali sana na kuomba sana ili Watu wamusifu,na ilihali hana imani.

13. Kunapatikana sala nzuri na mbaya,na pia kunapatikana maombi nzuri na mbaya. 

14. Sala nzuri na maombi nzuri ni ile ambae kafunzwa na malaika ao na

roho.

15. Sala mbaya na maombi mbaya ni ile ambae kafunzwa na shetani ao na mizimu (majini).

16. Mungu peke yake ndio mpanaji wa karama.

17. Mutu atakaye jidai mamlaka ya kupatiana zawadi ya kiroho, ni mdanganyifu.

18. Shetani leo amejitukuza katika maombi mbaya na sala mbaya . 19. Kundi ya maombi ambae hupuuza sala, ni mtego wa shetani.
20. Nguvu ya Mungu hupatikana,zaidi sana, kwa njia ya sala, kisomo,saumu na dhikri...

21. Waombaji wa kweli ni wa nyenyekevu tena wapole wa moyo;

22. Wanasali sana,na humsifu Mungu Sana, wala hawaombake chochote kwa mgonjwa.

23. Tegemea kwa Mungu peke yake, wala usikate tumaini, Mola wako ni tayari wakati wote.


{ 9 }. MAKARI NGAMBO NA NGAMBO


1. Kauli ya Mungu ni silaha ya makari ngambo na ngambo ,inajenga na inabomoa.

2. Atakaye itumia katika kawaida yake hujenga nafsi yake pamoja na maisha yake.

3. Na atakaye kataa kuitumia katika kawaida yake,amebomoa nafsi yake pia na maisha yake.

4. Anaye tumia kauli tukufu ya Mungu mwenyenzi,amepatikana

nuruni.

5. Na asiye tumia kauli tukufu,amepatikana gizani.

6. Aliye nuruni hujumuika mbinguni, katika bustani, hali ya kua roho.

7. Na aliye gizani hujumuika hadezeni, katika zimu, hali ya kua muzimu.

8. Uzingatiaji kimwili ni tafauti kabisa na uzingatiaji kiroho.
9. Kimwili na kiroho ni katika upungufu, ispokua ujuzi wa Muumba ndio fahamu kamilifu.
10. Fahamu ya vyote ambae hutokeza vyote, Mamlaka ya milele yenyi kumiliki ulimwengu wote.


{ 10 }. UTUKUFU WA KAULI

1 Kauli ya Mungu mwenyenzi ndio tukufu,ni ukweli usio kua na doa.
2 Ni tukufu sababu hutamkwa na mjuzi asiye dondoka na asiye kumbuka. 

3 .Kauli ya kiumbe sio tukufu ispokua nakala ya ujumbe wake mwenyenzi.

 4 .Ndio maana kauli tukufu hupatikana kwa Nabii na kwa Mtume, ambae humnukulu mwenyenzi.

5 .Kutumia neno la Mungu ni kutumia kweli na haki.
6 .Wala haongoke yeyote ispokua anaye tumia kauli tukufu maishani mwake.
7 .Basi ishikeni kimakini kauli ya kitabu hiki ili upate kutimilika.
8 . Kisomo cha kitabu hiki humjaza mutu nguvu ya kiroho.

11. Heri mutu mwema aliye na zoezi ya kuamka usiku kwa kusali na kuirudilia aya zake kwa wingi katika kisomo. 

12. Amekurubiwa na malaika na Roho takatifu, nafsi yake humeremeta na nuru ya Mungu mwenyenzi.
13. Kauli tukufu ndio hutenganisha kafiri na muaminifu :
14. Anaye tumikisha Kauli tukufu ndio muaminifu,

15. Na asiye tumikisha Kauli tukufu ndio kafiri.

110


( 11 ). UJUMBE NI KITABU

1 .Mwenyenzi Mungu amekwisha tuma ma Nabii wengi na Mitume wengi duniani.

2.Kila mjumbe alipewa kauli tukufu ili apate kuongoza watu katika njia iliyo nyooka.

3.Kauli tukufu hiyo ikaandikwa ndio kitabu cha Mungu.
4.Ndio maana kila mjumbe alipewa kitabu.
5.kunapatikana vitabu vya Mungu vikubwa na vidogo.
6.Ukubwa wa kitabu unatokana na uwingi wa maneno.
7.Kupewa maneno mengi sio kupewa daraja kubwa, Bali ni kupewa 
kazi kubwa.

8.Unabii unatokana na ukubwa wa daraja,na utume unatokana na ukubwa wa kazi.

10.Ni lazima kwa musilimu kuamini vitabu vyote :
11.Uchache wa maneno sio uzaifu wa maneno, wala uwingi wa 
maneno sio utukufu wa maneno.

12.Mungu amekwisha tuma wajumbe wengi na maneno mengi,lakini sehemu ndogo ndio iliyo fika wakati wetu.

13.wakati wetu huu vitabu vikubwa ni : Ukweli,qur’ani ,injili,zaburi ,na taurati.

14 Hakika vitabu vyote ni Sawa, vikubwa kama vile vidogo, maana hujenga kweli moja.

16.Ndio maana ni amri kwenu kuamini Mitume yote,usiamini uyu na kumpinga yule.

17.Vitabu vya manabii na Mitume wote ni muimu kwa watu wote
19. Heri mutu anaye amini Mungu mwenyenzi na malaika zake, na Mitume yake yote,na Vitabu vyake vyote.

20. Usimpinge Yesu masiya ajili ya kumuamini Muhamadi.

21. Na usimpinge Muhamadi ajili ya kumuamini Bwana Yesu.

22. Na usimpinge Kalonda ajili ya kumuamini Bwana Yesu,na usimpinge mtukufu wa daraja Yesu Masiya ajili ya kumuamini Kalonda.

23. Na usimpinge Muhamadi ajili ya kumuamini Kalonda, wala usimpinge Kalonda ajili ya kumuamini mtume mtukufu Muhamadi.

24. Na usipinge kitabu cha ukweli ajili ya kuamini qurani na Injili,na Zaburi na Taurati.

25. Wala usipinge Qurani na Injili na Zaburi na Taurati, ajili ya kuamini kitabu cha Ukweli.

26. Muaminifu wa kweli ni yule anaye muamini Mungu Mwenyenzi peke yake,na akaamini Malaika wake wote ,na akaamini mitume yake yote ,na akaamini vitabu vyake vyote.

27.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote !

{ 12 }. KIZIWIZI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,m'bora wa kutenda,aliye tokeza, toka sifuru,fikara na ujinga

2. Vilivyomo angani na Vilivyomo ukiwani ni mazao ya idhni yake.

3. Amepatikana kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho, uzima ushindaye.

4. Alikua ,iko ,na atakua, mkamilifu asiye kurubiwa na uzaifu kamwe, mwenyeji wa ulimwengu.

5. Juu yake hakuna mwengine,na pahali pake hakuna mwengine,na chini yake hakuna mwengine ,wa pekee aliye juu.

6. Ni mfalme wa wafalme wote, anaye miliki upatikanaji wote na maisha yote.

7. Mtukufu asiye kurubiwa wala kumilikiwa, uwezo wa kuenea.

 8. Kama unataka kuzingatia utendaji wake, amini na tubu.

111

9. Kiisha ujitolee kutimiza mapenzi ya Mola wako.
10. Bila shaka utazingatia utendaji wake maishani mwako.
11. Maana utajazwa Roho takatifu.
12. Kinacho ziwilia mutu kujazwa nguvu ya Mungu ni uovu.
13. Wala hajibiwake kadiri ya maitaji aliye na mashaka,pia Aliye na ujinga.
14. Kua na mashaka ni kukosa yakini.
15. Na kukosa yakini ndio kukosa Imani.
16. Anaye amini Mungu mwenyenzi huamini pia kadara ya Mungu
17. Ametumikisha yale ambae Mola wake aliamrisha,na amekatazika na yale ambae Mola wake alimkataza.
18. Katika furaha humshukuru Mola wake kwa wingi, yakini kwamba ni msaada wake.
19. Na katika Magumu husubiri na humuomba Mungu na humshukuru, yakini kwamba ni mapenzi ya Mola wake. 

20. Hamlaumu Mola wake kamwe, yakini kwamba Mungu anajua ambae yeye hafahamu, anatenda yote bila kasoro. 

21. Amempenda Mola wake kwa moyo wake wote na kumtumainia katika yote.


{ 13 }. UTAFAUTI

1. Sema :kumlazimisha Mungu atende kama unavyo tenda wewe,ni kumlazimisha aishi kama unavyo ishi wewe.

4. Kiumbe hakina enzi wala ujuzi ndani mwake, Bali hupatikana na hewa pia na fikara kadiri ya uvuli wake,na kiumbe kingine hakina hewa(pumzi) wala fikara.

5. Hakiwezi chochote bila idhni ya Mola wake.

6. Kiumbe amejifunza kwa sababu hana ujuzi.
7.Mwenyi ujuzi hajifunzake kwa yeye kufahamu,anajua yote bila shuruli yoyote.

8. Fasi yenye iko hakuna mwengine;
9. Amezidia walimwengu wote sababu ni ameweza yote.
10. Ni upumbafu sana kushakia uzima wake na ilihali umezingatia viumbe alivyo viumba.
11. Uzaifu na ujinga wenyi kua na viumbe usingeli patikanisha chochote angani na ukiwani pasipo kuumbwa. 12. Utangulizi kadiri ya Kuenea bila mwanzo wala mwisho haupatikane ispokua kwa mjuzi ,awezaye yote.


{ 14 }. KITU NA UVULI WAKE

1. Mwenyenzi ni mwenyi milki kamilifu,anaweza yote na anajua yote. 2. Uzaifu wa kuishi haumukurubie kamwe,wa miujiza aliye juu.
3. Kua na uzima ndio kukamilika,na kukosa uzima ndio kua mpungufu.

 4. Uzima ndio kitu chenyewe,na maisha ndio uvuli wake.
5. Anaye ishi hawezi kua mzima,na pia mzima hawezi kuishi, uzaifu na 
uwezo ni tafauti kabisa.

6. Watu wanafananisha uzima na maisha,na ilihali maisha ni upungufu na uzima ndio ukamilifu.

7. Uzima ndio ulio tokeza maisha toka sifuru, ni mamlaka inayo miliki kila kitu, uwezo wa kuenea.

 8. Ni amri kwa watu wote, Kusilimu na kutubu.
9. Kua yakini na uzima wa Mungu na kuacha kutenda zambi, ndio kuamini.
10. Heri mutu mwema anaye abudu Mungu katika yakini.
11. Na ole kwao wanao changanya ibada na shirki, maana wamepenywa na nuru ya Mungu.
12. Nuru na giza havichangane kamwe.

{ 15 }. SAUTI YA MUNGU

1.Ametakasika mwenyenzi Mungu,mtangulizi asiye jumuika njee yakambi lake.

2 .Wa pekee anaye stawi arshini bila jerani wala hitaji ya msaidizi. 

3.Mtukufu anaye miliki vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani,

m’bora wa kuenea.
4.Sauti yake hutokeza na hupoteza, mwenyi utasi juu ya kila kitu.

5.Karibu naye hungaa na nuru,na mbali naye hufifia na giza,taa ya ulimwengu.

6.Umaskini na utajiri hutokea kwake, mwenyeji wa vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani.

7.Ameachana na vitu vyote katika yote, hafanane na yeyote wala
chochote, wa miujiza aliye juu.
8.Enzi yake ni kama Muujiza wa maajabu, hakuna kilicho mfanana, wa pekee anaye kamilika.

{ 16 }. MWENYI KUJAA

1. Mwenyenzi Mungu ni bingwa wa mabingwa, mwenyi ushindi juu ya yote.

2.Kupatikana kwake ni muujiza ,na kutenda kwake ni maajabu. 

3.Mwenyi kujaa kadiri ya kuenea, hakuna penyi kua wazi ndani mwake.

4. Ndio maana hakua sifuru kabla yake,wala hatakua sifuru baada yake

5. Hakuna kabla wala baada,katika uzima.

6. Mungu peke yake ndio mwenyi uzima, mkamilifu aliye tangulia ulimwenguni.

. 7. Hakuna wa kumuanzisha wala wa kumkomesha, wa milele aliye juu.

112

8. Yeye ndiye Aliye wa tangulia wote hakuna wa kumtangulia yeye maana ndiye mwanzo wa vyote.

9. Na ndio maana Hakuna mkubwa kwake.

 

{ 17 } MTUME WA MWISHO


1. Mwenyenzi Mungu ndio aliye ni funulia ukweli huu ninaye watangazieni.

2.Mimi Mwenyewe pasipo mwongozo wake singeli fahamu lolote.

3. Makafiri hawaamini ujumbe huu sababu umeletwa na mutu mweusi. Pia sababu hawataki mutu kutumwa na Mungu tena.

4. Maana wamekwisha muwekea Mungu mwenyenzi mipaka kwamba hapashwe kutuma Mtume mwengine tena.wakisema kama wale alio watuma zamani wametosha.

5. Mola wenu hawezi kukomesha kazi ya malaika na roho,kiisha aendeleshe kazi ya shetani na mizimu.

6. Kazi ya malaika na roho ni kuwaimiza Watu kutenda mema.

7. Na kazi ya shetani na mizimu ni kuwaimiza Watu kutenda mabaya.

8. Hakuja kua Mtume wa mwisho, ispokua wakati Yesu Masiya atakapo rudi Yeye ndio atakaye kua Mtume wa mwisho.

9. Aliye na masikio ya kusikia asikie !


(18).    UBISHI

1. Mwenyenzi Mungu amewapenda wale wanao amini ujumbe huu na kuutangaza.

2. Kua yakini na Mungu na kutii sheria yake, ndio kuamini Mungu. 

3. Hapana kusoma kitabu cha Mungu na lengo ya kumkosoa Mtume wake.

4. Kumubisha aliye tumwa ni kumubisha aliye mtuma.

5. Heri mutu anaye soma maandiko matakatifu ajili ya kujenga Imani yake na ya wengine pia.

6. Kitabu cha "UKWELI" ni mwongozo kwa watu wote, unao leta yakini moyoni.

7. Atakaye amini ujumbe huu ameokoa nafsi yake,na atakaye ukataa ameangamiza nafsi yake.


{ 19 }. TABLIGH

1 Mwenyenzi ni Mwenyi uwezo popote ,ametenda yote pahali pote, hakuna kisicho milikiwa naye.
2. Kaumu zote ni zake,amewaagiza watumishi wake na kuwaongoza Katika Njia.
3 Atakaye mpinga aliye tumwa ndio maskini,atanyimwa fadhila zote. 4.Kumbuka alipo kujia katika ndoto, akisema : mimi ndio yule aliye Anzisha kundi la tabligh.
5. Nimekuja kukuambia ya kwamba watu hawafuate tena mafundisho Yangu,wanakua na jifanyia matamanivu ya nafsi Zao.
6 Akivaa kanzu mweupe na suruhali mweupe na mtama weupe 
vikanyako wazi.

7 .Hakika Mola wako ndio Mjuzi wa siri, Hakuna ajuaye kama yeye, mfalme wa wafalme.


{ 20 }HIJA

1.Sema : kukataa kuhelekea, katika sala, ni kuvunja alama ya dini.

113

2 .Kuhelekeza uso kwenyi muskiti mtakatifu ao mlima mtakatifu sio kuabudu muskiti huo wala mlima huo.
3 .Ni kama anaye jumuika maala hiyo katika sala.

4.Kujumuika maala takatifu katika ibada hutakasa uchafu wote wa nafsi.
5.Kuhelekeza akili yako kwa Mungu ni kujiweka katika ulinzi wa Mungu, ndani ya nuru yake.
6.Maala takatifu ni fasi yenyi nuru kubwa, ambae huzunguukwa na wakaaji wa mbinguni.
7.Kuswalia humo na kuuzunguuka muskiti mtakatifu,na kupanda mlima mtakatifu ( karombwe ).
8.Ukitumia kisomo kitukufu cha «Ukweli »,na dua na sadaka ya kuchinja: ni kuondoa uovu namna ya kujitakasa, kwa Kutumia "UKWELI" ambae husilimusha ;
9.Ni mfano wa maisha ya wakaaji wa mbinguni,miongoni mwa alama za dini duniani.

10. Kwenda hija ni kama kutoka fasi ya giza na kwenda fasi ya nuru, yaani kuacha matendo ya giza na kushika silaha za nuru.

  1. Kuvaa mavazi takatifu ni kama kubeba bendera ya Usilimu ;

  2. Ni kuhifazi utupu , heshima ya musilimu, tafauti na kafiri aliye uchi kama mnyama.

  3. Baada ya kuoga maji ya chemchem ya maala takatifu,ndipo utakapo vaa;

  4. Ukifunika bega lako la kushoto na mkono wote ;na kufunua bega lako la kuume na mkono wote.

  5. Hali ya utakatifu, ndani mwako hamuzingatiwe ispokua mema.

  6. Hayo hufanyika katika ibada ya hija, katika maala takatifu :Muskiti mtakatifu wa benye karingila na mlima mtakatifu wa karombwe.

  1. Maala takatifu ni nyingi : kama vile muskiti mtakatifu wa makka,na mlima mtakatifu wa Arafa.

  2. Na muskiti mtakatifu wa Yeruzalemu pia na mlima mtakatifu wa Golgota...na mlima sinai,na mlima karmeli...na muji Seule..

19. Na atakaye zingizia matumizi kiroho peke yake, kiisha akavunja alama ya dini ya Mungu,bila shaka yeye ni mnafiki.

20. Na mwisho wa mnafiki ni mubaya,hufikia uharibifu hadezeni.

21.Mungu mwenyenzi ndio anaye ruzuku viumbe vyake, msamehevu na mrehemevu.
22.Ee Mola wetu ! Utujaalie mwisho mwema.
23.Ukaribishe Roho zetu mbinguni, katika bustani ya neema !
24. Hatuwezi kufanya lolote bila msaada wako,basi utusaidie na utuhelekeze kwako.
25. Mamlaka yako itawale maishani mwetu ,tukitawanyika duniani sambamba na idhni yako.
26. Na mapenzi yako itimilike duniani na  mbinguni.
27. Hakuna Mola mwengine kama Mwenyenzi,wa pekee anaye shahidiliwa na anaye sujudiwa.


{ 21 }. KUINGIA

1. Mola wenu amewaleteeni ujumbe huu mupate yakini.
2. Amejifunua katika kitabu hiki ili mupate kusilimu na kuamini.

114

3. Kusilimu ndio kuingia katika dini ya Mungu,yaani kutoa shaada kimwili.
4. Na kuamini ndio kuingia katika neno la Mungu, yaani kutoa shaada kiroho.
5. Kusilimu kuna mfanya Mutu atimize mapashwa ya dini ya Mungu.
6. Na kuamini ndio kunamfanya mutu atimize mapashwa ya neno la Mungu, yaani afanye mapenzi ya Mungu. 

7. Heri mutu anaye amini kweli hii, maana ni Mwenyi yakini na Mola wake.


{ 22 }. TAHARIFA NA MAFUNDISHO

1. Ujumbe ndio zawadi kubwa itokayo kwa Mungu mwenyenzi.
2. Kupata ujumbe kutoka mbinguni ndio kupokea zawadi ya nuru kubwa zaidi.
3. Zawadi hii inayo aina mbili : ya kimalaika na ya kiroho.
4. Kujazwa wa malaika mbele katika ufunuo ndio kupatikana katika unabii.
5. Na kujazwa roho takatifu mbele katika ufunuo ndio kupatikana katika utume.
6. Unabii ni taharifa ya Mungu kwa watu wote ili wazingatie mbele ya safari,penyi kua jiwe wasijikwale na penyi kua shimo wasitumbukie,bali wapate kufika salama mbinguni.
7. Na kazi ya utume ni mafundisho ya Mungu kwa watu wote ili watumie njia ya uzuri safarini( yaani mila nzuri maishani) wapate kufika Salama mbinguni.
8. Taharifa ya mambo yatakayo tokea ,huletewa sana na Nabii, zaidi ya mafundisho ya mila nzuri.
9. Na mafundisho ya mila nzuri huletewa sana na Mtume, zaidi ya taharifa ya mambo yatakayo tokea.
10. Kukomeshwa kwa unabii humaanisha kukurubia kiyama.
11. Na kukomeshwa kwa utume humaanisha kufikia kiyama.
12. Na ndio maana Hakuna Mtume wa mwisho ispokua atakapo rudi Yesu masiya.

{ 23 }SHUKRANI

1. Sema : nimemshukuru Muumba wa mbingu na ardhi anaye ni kinga na hatari ya kila namna ; 

2. Mlinzi wa viumbe anaye nusuru kimuujiza,na kuvruga mipango ya Shetani na watu wake.
3. Amemuokoa kila anaye kumbuka na kutubu,na kumfanyia wepesi mambo yake yote.
4. Warozi wana panga,na Mola wako anapangua yote.

5. Mungu mshindi, Mamlaka ya kuzidia ,mtendaji wa mambo makubwa yasiyo zingatiwa na macho yao.

 6. Heri mutu anaye msifu sana Mola wake na kumshukuru kwa wingi na kumuhimidi kila wakati.
7. Hakuna mwengine kama Mungu, bingwa anaye kamilika, mlezi wa viumbe. 


24.   KUSHINDA TAMAA


1. Kinacho haribu maisha ya dunia ni kujipendelea mwenyewe.

2. Kila yule hujitetea mwenyewe bila kujali maisha ya mwengine.

3. Hayo hutokana na uzaifu wa mwili, ambae hulazimisha matumizi ya mwili wenzake kwa kuishi.

4. Utetezi wa mwanahewa-haramu ni tafauti kabisa na utetezi wa mwanahewa-halisi.

5. Yule hutetea mwili na roho,na uyu hutetea roho peke yake.

6. Mapashwa ya mwili ndio inayo zaufisha,na hata afikie kutenda kinyume.

7. Na ndio maana inabidi kushinda tamaa ya mwili kwa kufaulu mbinguni.



25.    KUHAMA DUNIA


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, Muumba wa mbingu saba na ardhi saba.

2. Kutoka mu hii mbingu na kwenda mu mbingu ingine sio kuhama mbingu.

3. Na kutoka mu hii ardhi na kuingia mu ardhi ingine sio kuhama ardhi (dunia).

4. Kwa kuhamishwa mbinguni inabidi kutenda zambi,kama vile Anzanzilu alivyo hamishwa kwa kutenda zambi.

5. Na kwa mutu kuhama ardhi, inabidi afe, yaani mpaka pumzi yake itengane na mwili wake.

6. Wanasayansi wanao safiri humo duniani,wakafika maala iliye tafauti,wanazani wamehama ardhi.

7.  Mutu hawezi kuhama dunia, mpaka pumzi yake itengane na mwili wake.


26.  KAZI


1. Enyi walio amini ! helekezeni akili yenu kwa Mola wenu kila mara popote mutakapo kua.

2. Musimuasi Mola wenu ajili ya shuruli ya dunia.

3 . Kazi ni muimu kwa watu wote,wanaume na wanawake, maana inaleta riziki na usalama.

4.Kukataa kutafuta ni kujizulumu mwenyewe,ni kama anaye kataa kuishi.

5. Maana maisha ni utetezi baina ya mema na mabaya: utafiti wa usalama wa nafsi.

6. Kazi yoyote inayo fanyika sawa na kauli ya Mungu ni halali kwenu, ispokua ile inayo fanyika kinyume na kauli tukufu ndio haramu.

7.Kinacho haramisha kazi ni matumikio, kutenda kinyume ndio huharamisha kazi.

8. Katumika ku serikali  sio zambi,lau kama hautende kinyume na sheria.

9. Kazi mbaya ni upelelezi wa uku na kule kadiri ya ushartahabari .


27.  MAFUMBO


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kauli, anaye toa neno lake kimwili na kiroho.

2. Sehemu ya kauli yake hutolewa wazi wazi na sehemu ingine hutolewa katika ma fumbo.

3. Neno la Mungu lote sio wazi, wala neno la Mungu lote sio fumbo.

4. Atakaye tumikisha iliye wazi kadiri ya fumbo amepotea ,na atakaye tumikisha iliye fumbo kadiri ya iliye wazi amepotea.

5. Ubora wa matumizi ya kauli tukufu ni kati kwa kati :usiongeze wala usipunguze.

6. Usivunje amri ya Mungu kwa kuzingizia tafsiri ya kiroho.

7. Ibada ya Mungu Mwenyenzi kimwili ni kumbukumbu la ibada ya Mungu Mwenyenzi kiroho.


28.  KIBLA CHA WALIMWENGU


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba, aliye umba mashariki mbili na mangaribi mbili.

2. Enzi yake ni kubwa kuzidia mbingu saba na ardhi saba.

3. Pande zote ni zake : popote utakapo kua upo mbele yake,hakuna kwa kumfichamia.

4. Mola ni m'shindi anaye tawala katika yote, fasi yote, wakati wote.

5. Amesikia na ameona:kila kitu na kila fasi na kila wakati;wa popote na milele.

6. Enzi yake ndio kibla cha walimwengu wote,wa pekee anaye stahili kuabudiwa.

7. Mjuzi anaye badirisha maala takatifu kwa kila umati ,ili watu wa dunia wasifananishe maala takatifu na Enzi yake tukufu.


29.  KUA NA DINI


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu M'bora wa kauli.

2. Mtukufu anaye fundisha watu dini kwa njia ya mitume wake.

3. Baba wa salama aliye salama, anaye salamisha nafsi kadiri ya mapenzi yake.

4. Hana dini mutu asiye kua katika mapenzi ya Mungu.

5. Na sio katika mapenzi ya Mungu mutu asiye kua na mila nzuri.

6. Kua na dini humfanya mutu awe na mila nzuri.

7. Na kukosa dini kunamfanya mutu awe na mila mbaya.


30.  KUKOSA DINI


1.  Atakaye kataa usilimu kua dini yake na akajidai uaminifu kua dini yake,hana dini.

2. Haiwezekane mutu kuamini Mungu bila kukubali ya kwamba Mungu Mwenyenzi yupo.

3. Lakini inawezekana Mutu kusilimu bila kufikia imani ya kweli.

4.Mutu anaweza kukubali ya kwamba Mungu Mwenyenzi yupo bila kuacha kufanya uovu.

5. Kufanya uaminifu kama dini pahali pa usilimu ni kufanya zambi.

6. Na kuitana waaminifu pahali pa kuitana wasilimu ni zambi, maana ni kushuudia uwongo.

7. Kwa kuamini kikweli inakubidi usilimu,na kwa kusilimu kikweli inakubidi uamini.

8. Kupakaliwa mafuta na Mungu ni kupodolewa na Mungu, yaani kujazwa nuru ya Mungu.

9. Na hajazwe roho takatifu ispokua muaminifu wa kweli;

10. Kujidai kua mpakaliwa mafuta hali ya  kua njee ya usilimu, ni kujidai kua muaminifu bila kua yakini na uzima wa Mungu.

11. Na hali kama hii ndio kukosa dini,na kuto kua na dini ndio upotevu wa bayana.



Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kitabu cha ukweli - Mlango Wa pili "ENZI TUKUFU"

MWANDISHI WA KITABU: