Kitabu cha ukweli - Mlango wa kwanza "USILIMU"

1. UFUNGUZI

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba.
2. Mlezi wa viumbe aliye na uzima, wa pekee anaye stawi arshini.

3. Mola mshindi awezaye yote na ajuaye yote.

4. Ni wewe mkamilifu tunaye kuomba msamaha wa zambi zetu .

5. Na ni wewe Mkarimu unaye tosheleza maitaji ya waja wako.

6. Utupatie zawadi ya kiroho, na utubarikie na utuokoe.

7. Utukaribize mbinguni baada ya kufa kwetu (Amin!!!).

2. KIYAMA

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, Mufalme aletaye ujumbe ku watu ili kusadikisha uzima wake.
2. Atakaye amini kwamba Mungu peke yake ndiye mwenye uzima,na kuamini ujumbe wake wote ndio musilimu.
3. Watu wengi hawakubali ya kama ukamilifu upo, bali wamekubali tu upungufu ambae ndio hali yao pia, wameshindwa kuzingatia njee ya kambi lao.

4. Mwenyenzi Mungu ndio muumbaji wa Anga na ukiwa, aliye tangulia kabla ya ulimwengu na walimwengu.
5. Bwana wa mabwana aliye na utasi juu ya kila falme, anaye rehemu na anaye kirimu.
6. Hakuna aliye huru kama yeye, mustaarabu wa milele, asiye fikiwa na asicho kitaka, hajaanake na hasira wala hajaanake na cheko.
7. Mkamilifu asiye najisika na upungufu wowote, hakuna upatikanaji njee ya idhini yake, na ndio maana hakuna cha kum'buguzi.
8. Ni muweza wa kila jambo, mtendaji wa jumla ya matendo, anaye umba na anaye uwa.
9. Kiumbe hakiwezi kumuongezea wala kumupunguzia chochote, Enzi yake humiliki Mbingu, Hadeze na Dunia, uwezo wa kuenea.
10. Arshi yake sio chombo wala umbo, lakini ni utukufu usiyo kurubiwa.
11. Uwezo wa Mungu hauna mipaka, lakini wenye kuenea namna ya kukamilika pasipo upungufu wowote.
12. Haifae kumuwekea Mungu mipaka katika utendaji wake. Yeye ndio Mfalme Mkamilifu, Muweza yote, anaye hukumu vyote bila kuhukumiwa na yeyote.
13. Wamekufuru wanao sema : << uumbaji umekomea hapa,Mungu hata umbaka tena chochote >>.
14. Na wamekufuru wanao sema : << uyu ndio mtume wa mwisho,Mungu hata tumaka tena (mtume) mwengine >>
15. Ogopeni Mungu kikweli, wala usipokee andiko takatifu kwa uziwi na upofu, usifikie kukufuru bila kufahamu.
16. Kauli tukufu hutoweka katika lugha za watu, amemfunulia kila Mtume katika lugha yake ili apate kusikia.
17. Mungu hana lugha maalumu bali lugha zote ni zake, ndiye aliye tokeza yote kwa jumla.
18. Kutenda kwake ni tafauti na utendaji wa viumbe, ndio maana kweli yake hukadiriwa katika mifano.
19. Mungu sio mfano wa kiumbe wala uzaifu wa kuishi (ao kufikiri) haumkurubie kamwe.
20. Mwenyenzi Mungu ni muujiza, hakuna kilicho mfanana, ukamilifu wake ni hali ya upekee, mamlaka ya milele.
21. Muumba wako hayuko mbinguni wala hadezeni wala duniani, lakini yeye hustawi Enzini.
22. Enzi imepatikana juu sana kupita mbingu.
23. Amestawi katika dhati yake mwenyewe hali ya kua yote katika yote, mwenyi kuenea.
24. Sema : Usilimu ni usalama wa nafsi katika mapenzi ya Mungu,yaani ndio dini ya Mungu Mwenyenzi.
25. Kusilimu ndio kuingia katika dini ya Mungu, na anaye silimu ndio musilimu.
26. Kuamini kwamba Mungu Mwenyenzi yupo mzima, na ndiye Muumbaji,na ndiye muabudiwa,hakuna mwengine kama yeye.
27. Na pia kuamini Mitume yake yote, yaani kutumikisha maneno ya mitume yake yote kwa jumla.
28. Ndio kuingia katika dini, yaani kusilimu, kadiri ya kusalamisha nafsi katika mapenzi ya Mungu.
29. Mitume huamrishana mema na kukatazana mabaya na huwabashirieni habari ya kiyama,wala hawahitilafiane kwa lolote
30. Ni amri kwa wasilimu wote kufanya ibada, hakika imani pasipo ibada ni bure kabisa.
31. Kila tendo njema linalo fanyika sababu ya kupata radhi ya Mungu ni miongoni mwa ibada.
32. Na usifanye ibada yoyote ispokua ajili ya kupata radhi ya Mungu.
33. Tendo njema lolote linalo fanyika kinyume na tumaini ya kupata thawabu kwa Mungu sio miongoni mwa ibada ya Mungu.
34. Sala na dua (ombi) ni mambo mbili tafauti kabisa,laiti mungeli musikiya Nabii mtukufu Muhamadi.

4

35. Ibada kubwa zaidi ya yote ni Sala.
36. Kumuimidi Mungu na kufunga sala, kusujudu na kutoa shaada na kutakiana amani,katika kipindi maalumu ndio kusali.

 37. Utakapo funga sala, soma sura za ufunguzi zote ili sala yako ikubalike
38. Na utakapo sujudu, umtukuze Mola wako na kumuomba, hakika yeye ndie anaye jibu maombi ya watu.
39. kufanya safari ya kwenda maala pa takatifu ajili ya kutimiza ibada mbalimbali kwa yule aliye na uwezo ni miongoni mwa ibada kubwa ya hija
40. maala pa takatifu duniani ni miskiti takatifu na milima takatifu na miji takatifu.
41. Ni kawaida kusali na unyenyekevu, hali ya kuogopa Mungu:muskitini ao mlimani ao nyumbani ama popote utakapo kua.
42. Hapana kufanya upuuzi wowote katika sala: usipige mziki wala usicheze katika sala.
43. Sala ndio ibada kubwa sana yenyi kuleta nguvu ya ushindi na nuru ndani ya musilimu, pia na saumu na dhikiri.
44. Umsujudie Mola wako asubui na jioni na usiku, na umtukuze mchana.
45. Hakika maneno mazuri ambae humtukuza Mungu huzidisha umri wa mutu anaye ya tamka.
46. Na atakaye jidai kua roho tupu na ili hali iko na mwili, yaani angali na ishi duniani, kiisha akavunja alama ya dini, atanyimwa fadhila ya mbinguni.
47. Ni bora kutumikisha mwili katika kuijenga roho, kuliko kutumikisha roho katika kuujenga mwili.
48. Maadamu mutu angali na ishi duniani, inamubidi kutumikisha mwili na roho, maana ndiyo umbo lake timamu
49. Matendo ya mwili wake ya ongozwe na roho takatifu katika kuitimiliza ibada.
50. Mungu ni Mfalme wa ajabu anaye stahili kuhimidiwa usiku na mchana.
51. Ni yeye anaye tawala peke yake ulimwenguni pote bila wa kumkombola, Mfalme wa milele.
52. Mkuu aliye huru kufanya anayo penda bila kiziwizi, ambae huukumu yanayo tendeka ulimwenguni.
53. Amejaa mamlaka yote, Mtukufu kuliko wote anaye miliki walimwengu wote.
54. Msikiaji na mpokeaji wa maombi ya viumbe, Mjuzi wa hesabu ya walimwengu.
55. Watu hawafahamu daraja yake, ndio maana wame mlinganisha na viumbe, wakimuwekea wapinzani kwa midomo yao.

56. Hakuna kiumbe cha kumgombeza Mwenyenzi Mungu, vyote kwa jumla ni chini ya uwezo wake.
57. Vyote hufuata kanuni yake mshindi, maana hutokana na idhni yake tukufu.
58. Shetani sio mpinzani wa Mungu, lakini mpinzani wa Malaïka.
59. Yule ni simamizi la ubaya na uyu ni simamizi la uzuri, Mfano wa kinyume chake, na ndio maana hupingana.
60. Mungu aliye tafauti na umbo hizi, hagusike na lolote katika shuruli zao.
61. Mola Mkarimu ni m'bora wa mahakimu, humlipa kila mmoja wao sawasawa na matendo yake.
62. Mungu angelipenda Shetani asijumuike kama asingeli muumba.
63. Na kama ali muumba sio makosa, upungufu asilia ulibidi upatikanaji wa namna hiyo kufanyika.
64. Ni mfano wa kapi iliyo anguka wakati wa uchoraji.
65. Kadiri mchoraji anavyo kusanya makapi yote baada ya kazi na kuyatupa, ndivyo Muumba atakavyo kusanya (ma) Shetani na wote waliomfuata na kuwatupa Hadezeni (motoni).
66. Hawata kuwa miongoni mwa wanao ishi, wala hawatakua miongoni mwa wafu ,bali watakosekana ulimwenguni,itakua kwao kama ilivyo kua kabla ya kuumbwa kwao.
67. Ndipo wale watakao rithi watakua salama ndani ya bustani, maana mustaki wao amekwisha ondolewa
68. Shetani hana maisha ya milele, bali yeye ni mwenyi umri mfupi sana, hasira imewaka ndani mwake sababu anafahamu kwamba kiyama ni karibu.
69. Mungu ni m'bora wa kukadiria, anaye miliki wakati, ambae kawawekea wakaaji wa dunia siku ya mwisho.
70. Siku hiyo Mungu atamtuma Yesu Masiya ili asawanishe ardhi sawasawa, hakuta bakia bonde wala kisuguu.
71. Waovu wata angaika na kulia na kujilaumu, na waaminifu ndio watashangilia neema ya Mola wao.
72. Hakika ahadi ya Mungu itatimia, hakuta chelewa hata nukta moja.
73. Jitayarisheni vizuri, Enyi wasilimu,ili mupate kurithi bustani ya neema siku ya mwisho.
74. Makafiri wanauliza wakisema : itatimia lini ahadi hii? si leo,tangu kuumbwa kwa Adamu mpaka ujio wa Yesu Masiya manabii walitabiri neno hili lakini hakikutokea.

75. Yesu Masiya pia alitabiri neno hili akisema: Kiyama ni karibu, hakikutokea mpaka ujio wa Muhamadi.
76. Na Nabii Muhamadi pia alitabiri neno hili akisema:<< Hakika kiyama ni karibu >> ,hakikutokea mpaka ujio wa Ahmadi.
77. Naye Ahmadi pia alitabiri kuhusu kiyama, hakikutokea mpaka leo, kitatokea wakati gani?
78. Sema: "Hakika kiyama ni karibu sana", ma nabii na mitume walio pita mbele yangu walisema kweli kabisa.
79. Dunia ni umbo dhalili, haiwezi kudumu milele ajili ya uzaifu wa mwili.
80. Wakaaji wake ambae huvaa miili huzoroteka na ujinga pamoja na wakaaji wa Hadeze.
81. Siku moja mbinguni ni muda wa miaka elfu duniani.
82. Tangu Yesu Masia kwenda mbinguni mpaka ujio wa Muhamadi,haikuenea hata siku moja mbinguni.
83. Na tangu Muhamadi kwenda mbinguni mpaka ujio wa Kalonda ni muda wa siku moja na nusu mbinguni.

5

84. Na tangu mwanzo wa Dunia mpaka leo hii ni muda wa masiku chache mbinguni.
85. Mutu mwenyi akili asijali muda ulio pita kabla yake, wala muda utakao kuja baada yake, lakini ni vema kwake kutumia vizuri umri wake katika njia ya Mungu ili apate kurithi bustani ya neema hiyo siku ya mwisho.
86. Watu wa Dunia wamezani kama wamedumu na ili hali hawajadumu, hayo husababishwa na uzaifu wa mwili.
87. Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.

3. PAPU KWA PAPU.

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'juzi wa kuumba,aliye na uwezo kamili,ambae hutegemewa na kila kitu.
2. Upatikanaji wote umetoka kwake,ni yeye anaye weza yasiyo wezekana kwao viumbe,anaye tenda maajabu bila mfano wake.
3. Anapo fanya miujiza ndipo watu hutetemeka hali ya kuogopa punde kidogo wanasahau.
4. Mungu ni Mshindi anaye jaa mamlaka ambae hupatikana kimuujiza bila msaada wa yeyote.
5. Alitangulia kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho, wa pekee aliye kamilifu.
6. Ni yeye anaye helekeza waja wake kwenyi kheri ya kila namna,na kuwahepusha na shari ya kila namna.
7. Muhimidiwa aliye na sifa kamilifu, wa milele juu ya mambo yote.
8. Lakini walio kufuru hawajali utukufu wake, wamemtolea maovu ya kila namna.
9. Wamejigamba ajili ya kupewa muda duniani, hawafahamu kwamba kutafikia muda ulio wekwa ambae haki itainuliwa. 10. Hayo ni kwa sababu hawa hazibiwe papu kwa papu pindi wanapo kosa, hukumu itafanyika siku ya mwisho baada ya maonyo yote.
11. Matukio yote hutoka kwake, hakuwezi kufanyika jambo kigeni katika ujuzi wake.
12. Hakuna kitakacho badiri mpango wake,maana vyote ni chini ya uwezo wake
13. Kauli tukufu ndio mpango wake usio badirika, haita pita bure mpaka itimie.
14. Heri mutu anaye tekeleza kwa makini kauli ya Mwenyenzi Mungu.
15. Mungu ndio mkweli wa ahadi ambae kauli yake hutimiliza idhni yake.
16. Ametangulia katika fahamu ya vyote isiyo badirika, haiongezeke wala kupunguka ajili ya kuenea.
17. Vipi itaongezeka ambae imekwisha jaa kabisa! hakuna kuongezeka wala kupunguka katika jambo lenye kukamilika.
18. Ni bora zaidi kutii amri ya Mungu kuliko kugeuzageuza maneno kwa kiburi, hakika Mola wenu anajua sana mradi wa kila jambo.
19. Usijilinganishe na Mola wako kwa lolote wala usishakie anayo ya sema, kwani hauna fahamu ya kumkosoa yeye ajuaye yote.
20. Ogopeni sana Mungu, mamlaka isiyo na kipimo, Mlezi wa viumbe aliye pasipo yeyote.
21. Mumiliki wa anga na ukiwa atawalaye katika ulimwengu bila mfano wake.
22. Mbingu, hadeze na Dunia hufuata hukumu yake,wala hakuna umbo njee ya kawaida yake.
23. Muumbaji, atokezaye kwa rafla bila kutumika kazi na bila shauri na yeyote,Mjuzi aliye juu.
24. Atakaye toa shaada na kuishi katika woga wa Mungu, Ataingizwa mbinguni na kuishi milele.
25. Amegundua baba wa siri aliye kwa siri, anaye fanya siri kwa siri.
26. Mola Mshindi atanguliaye namna ya kuenea katika tendo kua, kwake hakuna kuanza wala kukoma Mfalme mwenyi kukamilika.
27. Mkongwe zaidi ya wote, wa maajabu anaye patikana juu ya wakati,ambae humiliki muda wote bila kipimo.
28. Yeye ni tafauti na viumbe vipatikanavyo ndani ya wakati na chini ya wakati, kadiri ya umri fulani.
29. Enzi yake ndiyo inayo mkamilisha bila upungufu wowote,milki ya ushindi ambae huzidia kila kitu
30. Anakua yote katika yote, Mkuu wa majeshi, ambaye ukubwa wa milki yake humfanya awe huru kuliko wote,
31. hupatikana kile anacho idhinia,Bingwa asiye buguziwa.
32. Msifiwa wa ajabu, Mola wa karne na karne, tumaini la walimwengu.
33. Baba wa salama aliye salama, Mtangulizi na Mtakatifu, anaye rehemu viumbe vyote kwa jumla.
34. Enyi walio silimu! Tumieni urakibuni matendo yenu na ogopeni Mungu ukweli wa kuogopa ili mupate kuokolewa.
35. Afazali watu wa kuzingizie bila wewe kuwamo, ijapokua wakuzarau usibabaike, hakika wao ndio wenye hasara.
36. Mungu alikupatia akili kua kifaa cha maisha, jinsi ya ukaguzi baina ya mema na mabaya.
37. Kama haufahamu mradi wa hukumu yake fulani, helewa kwamba Mola wako anajua zaidi.
38. Hakika sheria ya Mungu haikuja ila kwa wenyi akili, ambae hujichagulia njia wenyewe.
39. Watu wengi wamesilimu ajili ya hanasa ya dunia, wala hawana tumaini ya wokovu.
40. Na wakisali masiku chache tu wanachoka na kuacha na kugeuka, wanapupia kumshirikisha Mola wa walimwengu.
41. Hawa ndio wenyi hasara hiyo siku ya maamuzi, mambo yao yote ni ya kidunia, hawana akiba yoyote mbinguni.
42. Ni bora kusilimu ajili ya kupata radhi ya Mola wako, ukitarajia wokovu siku ya mwisho, na pia kuonesha shukrani kwa yule aliye kuumba.
43. Wasiwasi ni ya Shetani, heri kua na subira, usiache sala na maombi na wema,hakika Mola wenu hutosheleza kila nafsi

6

inayo muhitaji.
44. Kadiri unavyo kula kila siku ili kuujenga mwili wako, ndivyo unavyo pashwa kusali kila siku ili kuijenga roho yako.
45. Usiharakishe jambo ambae Mungu ameikawisha, wala usikawishe jambo ambae Mungu ameisha harakisha.
46. Na usifunue kile Mungu amekifunika, wala usifunike kile Mungu amekifunua.
47. Tulia baada ya kuomba, usitafute kujibiwa pale pale, wasiwasi ni alama ya tamaa ya maisha ya dunia, pia ni alama ya imani haba.
48. Lau kama Mungu angelikua na jibu dua ya watu papu kwa papu, bila shaka taratibu hii ya maisha isingeli kuwako, wala dunia aingeli patikana.
49. Mutu angeli omba utimilifu wa nafsi yake, kama ingeli takika ageuzwe roho takatifu papu kwa papu.
50. Na kama angeli omba uharibifu wa nafsi, ingeli takika ageuzwe muzimu palepale.
51. Umutu ungeli futika mbele ya wakati na pia mipango iliyo pangiliwa muda mbalimbali isingeli timilizwa.
52. Maombi ya mwanadamu haipatikane katika ukamilifu, lakini katika upungufu.
53. Dua nyingi za watu huruka mipaka, hazistahili kujibiwa papu kwa papu, isije kuleta muvrugo katika kawaida la umbiko. 54. Kama watu elfu moja wangeli omba ufalme wa dunia yote kila mutu, ingeli takika kufanyike ma dunia elfu, ili kila yule ajibiwe papu kwa papu, kadiri ya hitaji yake.
55. Watu wote hawakuzaliwa siku moja bali siku mbalimbali, makarne na makarne, inabidi kaumu zote zipite mpaka siku ya mwisho.
56. Hakika Mwenyenzi Mungu ni M'bora wa kukadiria, mwenye ujuzi.
57. Kila analo lifanya ni haki, hakuna kosa hata kidogo.
58. Je! utamkosoa Mjuzi aliye kuumba? ama ni kweli jembe itamuongoza mlimaji?
59. Ni vema kumsifu na kumshukuru Mungu kuliko kumlahumu, anajua msiyo ya fahamu.
60. Matendo ya watu yamelindwa huko juu,hiyo siku ya kiyama itakua ndio wakati wa mavuno,kila yule atavuna aliyo ya panda.
61. Mungu amewakadirishieni malipo kwa kuwapa sehemu duniani na sehemu kubwa kuwalindia mbinguni, ili muda ulio kadiriwa utimie.
62. Mungu peke yake ndio mzima, anaye stahili kuabudiwa, mwenyi kuenea katika tendo kua, wa milele aliye juu.
63. Viumbe hawana uzima, bali hunusu na vipande,wamepatikana bila kuenea katika tendo kua.
64. Yule anaye kosekana kiisha anapatikana, kiisha tena anakosekana, hayuko kabisa.
65. Ni mwenyi kuwako kikweli, yule asiye kosekana muda wowote, anaye enea katika tendo kua.
66. Hakika uzima ni utukufu wa ajabu, mamlaka yenyi ushindi kadiri ya kuenea.
67. Mungu ni Mkubwa sana, Mtukufu mwenyi uwezo zaidi ya kila kitu,Bingwa mkuu asiye shindwa na chochote,Mumilki aliye juu.
68. Tenda adili popote ulipo, ukitarajia kuleta amani duniani.
69. Siasa yako isiwe uchimbi wala uvamizi, lakini amani kwa watu wote.
70. Wala usifuraikie aibu ya mwenzako,wala usimnyanyase yeyote,lakini tizama wenziwe kwa upendo na furaha.
71. Wala usimtegee aliye amini usije ukamfanana Shetani.
72. Mungu ni mumoja na dini yake ni moja,hakuna dini ya Mussa wala ya Yesu,wala ya Muhamadi.
73. Ma nabii na mitume wote walipewa kazi ya kusilimusha watu,yaani kuwaingiza watu katika dini ya Mungu.
74. Lau kama watu wangeli fuata maubiri ya manabii na mitume wote vilivyo, hakungelikua mgawanyiko wowote kati yao. 75. Haya ni kwa sababu wamebagua miongoni mwa mitume.
76. Hakika yule asiye amini mitume wote hawezi kuingia mbinguni,kumpinga Mmoja tu ni kama kuwakanusha wote kwa jumla.
77. Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.


4. MUAMINIFU

1. Mungu ni jina lake yeye aliye umba viumbe vyote kwa jumla,Mshindi anaye jaa utukufu,ambae huthamanisha ulimwengu.
2. Hakuna mwengine anaye stahili kuitwa jina hili isipokuwa yeye peke yake, imemaanisha upekee wa ukamilifu.

3.Ni Muweza na Mjuzi wa mambo yote,anaye miliki ulimwengu.

4.Na atakaye mpachika mwanahewa ama muzilahewa jina hili,amebuni zambi kubwa,maana amenajisi utukufu wa Mfalme wa wafalme.

5.Hana umbo sababu hakuumbwa,sio mume wala muke,hutangulia mwenyewe tafauti na kila kitu .

6.Mungu ni Baba wa salama aliye Salama,mkuu ajaaye mamlaka,ambae tamko lake hutokeza ambacho hakikua,mfinyanzi wa umbo za walimwengu.

7.Hatendake kama watendavyo viumbe,mtukufu aliye na uwezo wa kuenea.
8.Kiumbe hutaabika na shuruli ya kila namna na hali yeye hashurulikie chochote,M'bora wa kuenea.
9.Na ndio maana Mola wa viumbe hana maisha lakini yeye ni Mzima,mwenyi uhuru.
10.Hana shida yoyote ajili ya kuenea,hakuna palipo wazi katika yeye ambae pangeli dai kujazwa,Mkamilifu aliye juu.

11.Milki kamilifu inayo hukumu yote yanayo tendeka,wapekee kadiri ya muujiza wa maajabu.

12.Mufalme wa wafalme na bwana wa mabwana, anaye jua yote bila kusahau na kuweza yote bila kushindwa, mtukufu aliye juu.

13.Yeye ndio tumaini la walimwengu na kimbilio la wasilimu.

14.Ombeni yote unayo hitaji,utapewa ,msaada wake ukufikie kadiri ya unyenyekevu wako.
15.Yeyote anaye ishi pasipo kuzingatia uzima wa Mungu ni kipofu,hana akili ambae ndio macho ionayo. 16.Uwezo wote ni wake Mwenyezi aliye na mamlaka ,mtukufu atendaye kwa idhni bila kazi yoyote.
17.Hakuna aliye na sifa mfano wake maana pekee huzidia kila kitu.
18.Milki yake ni kubwa zaidi,ambae husababisha miujiza pindi anapo tenda,m'bora wa kuumba.
19.Mtukuzeni Mungu aliye na ushindi,Mola wa jumla ya viumbe,atakasikaye na azidiaye.
20.Mila nzuri katika imani,inaleta usalama wa nafsi yako milele na milele.
21.Matendo ya muaminifu ni tafauti na(matendo) ya makafiri,maana wameachana njia katika safari zao.
22.Na ndio maana watafika maala mbalimbali;aliye amini ataingia mbinguni na aliye kufuru ataingizwa hadezeni 

23.Muaminifu ametenda adili popote,ni m'nyenyekevu tena mpole wa moyo.
24.Ni mtenda salama,mfano muzuri wa kuiga ,tafauti na muovu anaye leta wasiwasi katika jamii la watu.

7

25.Muaminifu ni mwenyi yakini kwamba Mungu anamuona popote alipo na amehifadhi yote anayo ya tenda kwa siri ao kwa wazi.

26.Mwenyi utaalamu,anaye pokea watukufu wambinguni maishani mwake. 

27.Ametambua haki yake na ya wengine pia,mwenyi kumiliki tamaa ya nafsi yake.

28.Yeye sio mkali wala hana kiburi,ametumia uadilifu hali ya kua moyo wake umejaa woga wa Mungu.
29.Ametenda urakibuni daima;akawa mwanamuke humtii mume wake,na akawa mwanaume humpenda muke wake,kila yule hutosheka na mwenzake.

30. Husaidia wasio jiweza na hufikiria maendoleo ya jamii la watu.

31. Moyoni mwake hana kiburi wala fitina,chuki wala tamaa mbaya.

32. Humsujudia mola wake asubui,jioni na usiku,pia humtukuza mchana.Heri mutu anaye soma kitabu hiki usiku na mchana.

33. Nongo haina fasi moyoni mwake,amesema kweli wakati wote ijapokua katika hatari.

34. Kwake ni afazali kujishusha kuliko kujipandisha,hana hila wala majivuno.

35. Yeye sio muuwaji wala mzinifu,sio mwizi wala mvamizi,hadanganyake wala hasengenyake.

36. Ni mwepesi wa kusamehe pindi wanapo mkosea,na pia huomba masamaha pindi anapo kosea,hana mima wala naziri na yeyote.

37. Hazingiziake yeyote ijapokua yeye huzingiziwa kila mara na watu wa dunia.

38. Hana chonganisho wala wasiwasi moyoni mwake,mpole anaye tenda haki.

39. Amewapenda sana walio amini na amewasikitikia sana walio kufuru, wala hazarau yeyote.

40.Anapo tazama wenzake hufuraika moyoni,mutu mwema anaye patanisha walio gombana,wala hafuraikiake magumu ya mwenzake.

41.Wala yeye sio mshirikina wala 

mnafiki,sio mwongo wala mwivu.
42.Muvumilivu tena mpenda cheko,anaye tumika kadiri ya nguvu yake ili apate kuishi,hana uvivu wala kangami.
43.Hakika hii ndio mila ya musilimu mwenyi imani anaye tumainia Mungu maishani mwake.
44.Kusilimu na nia safi ni neema,wala hakiri uzima wa Mungu isipokua kwa ukarimu wake mwenyenzi.
45.Shika ulicho pewa ewe uliye amini, hakika zawadi ya kiroho ndio pato na ngao.
46.Utakatifu ni wake Mungu,M'shindi aliye huru, mtawala anaye zidia,m'bora wa kuenea.
47.Kwa nini hustarehe duniani walio kufuru na ili hali huwafanyia hila waaminifu?
48.Sema: makafiri wamepewa muda mchache duniani kufatana na kawaida la umbiko ili dunia isiondolewe kabla ya wakati. 

49.Kuifanya dunia isipatikane na uovu wowote isingelikua ila mbingu takatifu.
50.Na kuifanya dunia isipatikane na wema wowote isingelikua ila Hadeze.
51.Kwa dunia kupatikana ilibidi umbiko ya namna hii kupatikana,maana dunia ni changachanga ya uzuri na ubaya.
52.Ni maunganio ya anga na ukiwa,maisha ya humo ni kwa wanahelewa haramu wote .
53.Utafauti wa maisha yao utatokea siku ya malipo,kila yule atavuna aliyo ya panda.
54.Aliye kufuru duniani ataangamia na aliye amini duniani ataokolewa.

55.Starehe ya makafiri ni ya muda,umbo dhalili kuliko umbo zingine zote .
56.Matamshi yao haina buguza yoyote huko juu,na vivihivyo matendo yao,bali hubuguzi nafsi zao wenyewe.

57.Wao ni mfano wa makapi,hujumuika sababu mchoraji angali na chora,wataogotwa na kutupwa motoni.
58.Ujumbe wake ndio ufundi wake ambae huchora nafsi ya wanaadamu:wanao upokea ndio vyombo halisi na wanao ukataa

ndio makapi inayo anguka.
59.Uchoraji wa pumzi unaendelea mpaka siku ya kiyama,ndipo Mungu atakapo tenganisha adili na batili.

60.Mungu ni muweza wa vyote na mjuzi wa vyote atanguliaye mwenyewe bila msaada wa yeyote,mtukufu asiye fanana na yeyote ajili ya kuenea.

8

61.Atakavyo hufanyika kwa rafla,mlezi wa viumbe anaye miliki ufalme wote,mshindi aliye juu.
62.Mungu ni taa ya ulimwengu,ameangazia viumbe kwa utukufu wa dhati yake.
63.Nuru yake hutokea ndani mwake,imetua mbinguni na kuzagaa kama mwangaza wa taa kwenyi kilauri.
64.Heri mutu anaye fikiwa na nuru,pumzi yake imetakasika,amefanana mwangaza usio fifia wala kuzimika utokao Enzini.

65.Amepata maisha ya milele sababu ya kuamini ujumbe utokao kwa Mungukiongozi pekee wa jumla ya viumbe. 66.Watu wengi hawaamini ajili ya kiburi na chuki,wame chukia neema aliyo pewa mchaguliwa wake.
67.Na yule ambae Mola wake amemtukuza, hakuna atakaye weza humzalalisha.
68.Na yule ambae Mola wake amemzalalisha ,hakuna atakaye mtukuza.

69.Anaye jazwa na nuru hupata uhai na anaye fikiwa na giza hupatwa na mauti.
70.Fanyeni ibada kwa wingi,wala usitoshe tumaini ya kutoshelezwa na Mungu peke yake.
71.Mola wako atakujaza roho kadiri ya msaidizi,hakuna kitakacho angamiza nafsi yako.
72.Mungu ni muweza yote,mwokozi, wa miujiza,anaye jumuisha pasipo kujumuika,shina la vilivyomo ulimwenguni. 

73.Ni bora kumtukuza usiku na mchana,mtatuzi wa shida zote,akadiriaye na asaidiaye.
74.Mwenyezi ametosheleza kua mlinzi,tegemeo na kimbilio la watu.
75.Anaye penda kuishi salama milele ashike maagizo ya Mola wake Mlezi wa viumbe.
76.Amani imetawala mbingumi ajili ya uzuri, na mateso imetawala hadezeni ajili ya ubaya .
77.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.


5 . MATIBABU

1.Ametakasika Mwenyezi Mungu,M'bora wa kuumba,mamlaka itokezayo kuujaza ulimwengu
2.Mola wa ulimwengu wote,Mumiliki anaye patikanisha na anaye kosekanisha
3.Walio kufuru wamesema hakuna maisha ingine kinyume na hii ya duniani!
4.Sema: Maisha ya dunia sio ila alama mfano wa kifebe,maisha ya kweli ni hiyo ya mbinguni
5.Kinacho fanya mwili udumu ni pumzi,vikatengana tu,mwili huaribika kwa haraka
6.Na pumzi inakua na nguvu zaidi ilipo pekeyake bila kuchangikana na mwili.
7.Aliye wa dunia hazingatie isipokua mwili peke yake,mfano wa kipofu,hawezi kuzingatia roho.
8.Mtenda mema ni pumzi timilifu ambae hukomazwa na jaza la mbinguni,ndio maana huishi milele.
9.Tafauti na makafiri wanao kufa mara ya pili ,kuharibika kwa mwili duniani ,napia kuharibika kwa pumzi hadezeni. 10.Na yule ambae hukosewa mwili na hukosewa pia pumzi hayuko bali hukosekana ulimwenguni.

11.Waovu watakufa mara ya pili baada ya kutaabika muda mrefu na maumivu ya wakati wa kubomoka kwa pumzi zao hadezeni.

12.Hawata kua hai wala hawata kua mauti,humo sio ila maala pakubomolea umbo,ndio maana hawata ishi milele humo bali watakosekana baadaye.

13.Mola wenu ni mwenyi uwezo wa kubomoa mjengo kihewa kama alivyo na uwezo wa kuujenga,hakuna kigumu kwake,mumiliki aliye juu.

14.Hadeze ni kambi mbaya sana na ndio maana haidumu kama mbingu.
15.Ma nabii na mitume ambae wamekwisha ihama dunia,wamekwisha ionja raha ya bustani.
16.Kwao hakuna maamzi ni watakatifu walio chagua urakibu kama njia.
17.Wamegeuzwa nuru ya taa isiyo zimika,neno na nguvu yake kadiri ya roho takatifu.
18.Ujuzi ni wake Mwenyezi Mungu,mwalimu wa walimwengu,anaye funulia watu mambo ya siri.
19.Ndiye anaye fundisha watu kugundua,wala hakuna anaye unda pasipo msaada wake,m'bora wa wanao ruzuku. 

20.Kupatikana kwenu na kutenda kwenu ni katika makadirio yake,mtukufu aliye huru kutenda yote anayo ridhia.

 21.Makafiri hujigamba kwa maovu wanayo ifanya, hawafahamu ya kwamba muda wao ni mufupi.
22.Hakika waovu watalia muda wote mpaka mwisho,wala cheko haitapatikane kwao humo hadezeni .
23.Hadeze hupoteza umbo kama vile moto upotezavyo kuni.
24.Maisha ya humo ni fupi sana,ni muda wa kubomoka kwa umbo lote na ndio maana hupatwa na maumivu kali. 25.Afazali kurefusha umri wako kwa kutenda adili,ukitembea urakibuni kwa imani na amani.
26.Nini kitakacho kudanganyeni katika maisha ya dunia na hata mufikie kupotea?
27.Vyote ni vya bure kabisa hakuna cha kudumu, starehe ya milele hupatikana mbinguni.
28.Tetea namna ya kustiri umbo lako milele,ukipata kufuzu kwa mazao ya zamiri yako.

29.Hakika matumizi ya neno la Mungu ni matibabu ya nafsi.
30.Mungu ametosheleza kua mlinzi,mfariji na m'bora wa wanao rithi.
31. Mwenyi ukamilifu,anaye miliki na anaye kadiria,tegemeo la walimwengu.
32.Mola wa miujiza anaye fanya maajabu,wa pekee asiye lingana wala kufanyika,Mjuzi aliye juu. 

33.Mfalme wa vyote anaye jaa uwezo wa vyote,mtukufu atanguliaye kadiri ya kuenea.

 34.Mwingi wa rehema na mlinzi mwema,anae letea watu usalama kuwalinda na shari ya Shetani. 

35.Kila hatua ya mutu huviziwa na Shetani,amemtegea ili amuangushe katika imani.

9

36.Atakae fuata maubiri na akazoea kusoma kitabu kitukufu hiki kila siku kiasi cha nguvu yake,Mungu atamjaza nguvu ya ushindi.

37.Anae soma aya zake katika mpango maalumu na kuitumia maishani mwake kadiri ya silaha na ngao,ndio shujaa katika mapambano.

38.Mwenyenzi amelea wote kwa usawa,akiwagawia neema mbali mbali kwa ukarimu wa jaza lake.
39.Usimlaumu Mola wako ijapokua umefikiwa na madhara ya aina yote,lakini zidisha ibada,ukisoma aya zake kwa wingi,na kuomba masamaha na wokovu.

40.Mungu pekee ndio aliye huru,afikiwake na asicho kitaka,anaye zidia walimwengu wote.
41.Ni zambi kubwa kabisa kuchanganya nuru na giza,mara hutumia uchawi na mara hutumia ibada.
42.Na wanao tumia vitabu vya ushirikina,ambae hualika majeshi ya zimuni,na kuwafananishia mizimu na roho,wakisema:kuna mizimu nzuri na mbaya wamepotea.

43. Hakuna mizimu  (majini) nzuri,umbo hizi zingeli kua na mila nzuri zisingeli jumuika hadezeni bali mbinguni.

44. Sala ambae hupangiliwa na mizimu,ikisaliwa na mutu,hukurubiwa na jeshi la zimuni,na fadhila yake hukomea zimuni.

45. Mizimu inayo majina mengine katika lugha zingine,usidanganyike ajili ya lugha.

46. Atakaye unga urafiki na mizimu,ameangamiza nafsi yake.

47. Ni vema kuunga urafiki na watakatifu wa mbinguni,ukiwasiliana (kukurubiana)nao kwa njia ya ibada.

48. Hakika kuwasiliana na Malaika na roho kunaleta furaha ya milele.

49.Umbo za kihewa zinazo mteremukia mutu bila kualikwa,na kumuelekeza kwenye dini ya Mungu ni miongoni mwa roho ndogo ndogo ya barazani mwa mbingu.

50.Mushirikina hujivuna anapo tumia jeshi lake,anazani kupata kumbi kupatikana,na amezani kajaa nguvu kumbi kazoroteka. 

51.Mungu amemkirimu muaminifu kwa namna ya ajabu,kumruzuku na kumkinga na hatari ya kila namna.
52.Tosheka na ulinzi wa Mola wako,usitafute walinzi wengine kinyume naye,hakuna mwengine kama yeye.
53.Kama dunia ili kunyanyasa,lakini mbingu imekutukuza,umepewa kila unacho hitaji na kufanyiwa wema wa kila namna ajili 
ya uadilifu wako.

54.Mungu ni mkubwa anaye fanya makubwa,akiinuka katika daraja isiyo fananishwa,mwenyi ushindi. 55.Atakaye mpenda sana hunusuru nafsi yake na atakaye mkataa huangamiza nafsi yake.

56.Ni upumbafu kumkataa Mola wako aliye kuumba na ili hali ndio hifadhio ya nafsi yako,hakuna chemchem ingine ya maisha badala yake.

57.Hakika aliye silimu hatendi ila kwa hekima,anaogopa kuruka mipaka aliyo wekewa na Mola wake. 58.Ametakasika Mwenyezi Mungu,mlezi wa viumbe,anaye tarajiwa na wote katika mambo yote,M'bora wa kukadiria.

 59.Usiku ni wake na mchana ni wake,mpanaji mkuu anaye zawadia kila umbo,mkuu na mshindi anaye tawala milele. 60.Hapana kuzembea katika imani,Shetani na jeshi lake wanayo desturi ya kiviziana katika uzembe.
61.Na yule aliye dondoka,atakapo tubu,atazingatia wakati roho atakapo mrudilia

62.Roho na Malaika hawarogewake wala kuuwawa, bali huchuguwa hatua na nafsi iliyo dondoka,na humrudilia tena atakapo tubu.

63.Muaminifu anaye sali sana na kutumia aya za kitabu hiki kama dhikri,atahepushwa na uchawi wa aina yote.
64.Tegemea kwa Mungu aliye uzima,muweza yote aliye chemchem ya maisha,hakuna mwengine kama yeye ambae 
angaliweza kusimamia jumla ya viumbe.

65.Ametukuzika Mwenyenzi aliye juu,bila yeye kusingeli patikana chochote,m'bora wa kuumba.

66.Mshangiliwa aliye na sifa kamilifu, wa ajabu anaye enea namna ya kujaa katika tendo kua tafauti na uzaifu wa kuishi,mzima.

67.Hana baba wala mama,bibi wala bwana,wala uzaifu wa kujumuika haumkurubie kamwe,wa pekee anaye stawi arshini,hakuna msaada njee ya mapenzi yake,mlinzi mwema anaye fariji viumbe.

68.M'bora wa kuumba anaye umba ginsi ya kuendelesha umbiko,mtukufu anaye helekeza fikara yao kwenyi ugunduzi wapate kutumia faida ya umbiko.

69.Mungu hakuumba chochote kwa bure hapana,bali matayarisho makubwa ajili ya maisha yao.
70.Watafiti wangeli amini vilivyo,kama wangeli funuliwa zaidi,lakini mwingi wa rehema huwafahamisha bila kujali upuuzi 
wao.

71.Mwenyenzi Mungu ni mwema sana na zaidi,amezawadia watu neema ya kila namna.

 72.Mchoraji wa pumzi ya wanaadamu,Mjuzi anaye geuza mutu kua roho,M'bora wa kuumba.

73.Kusilimu kwa mutu ndio mwanzo wa uchoraji wa pumzi yake,ndio maana waovu huanguka kadiri ya makapi kandokando yake.

74.Kuona kama nuru na giza haviambatane,ndio maana waovu humshambulia aliye amini wa kianzia na masingizio na kumalizia na ushambulizi mkali.

75.Hakika wao ndio makapi inayo anguka wakati pumzi yake inapo fanyika roho takatifu.
76.Muaminifu atakapo jaribiwa,ajiandae kuvumilia na kusamehe,apate kukomaza umbo lake la sasa la kiroho.

77.Yeye ni mfano wa mboleo ya uzuri,nafsi ya mbinguni inayo pamba matunda mazuri.

78.Basi jihazarini,Enyi wanaadamu,musije kuanguka kadiri ya makapi pembeni ya wachamungu.

79.Utakatifu ni wake Mwenyezi Mungu,mlinzi mwema,anaye okoa kutokana na vitimbi vya Shetani. 80.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.


10

6.MAKAO

1.Ametakasika Mwenyezi Mungu aliye uzima ,milki kamilifu itanguliayo kadiri ya kuenea, fahamu ya vyote itokezayo ambacho hakikua, kiongozi wa jumla ya viumbe.

2. Amepana maisha ya milele kwenyi viumbe halisi ambae hutii sheria yake.

3. Kila maisha iko na kawaida yake,iliye muimu kutimilizwa na umbo lake.

4. Ole kwao makafiri ambae hukataa mwongozo utokao kwa Mola wao,wametumikisha matamanivu ya nafsi zao.

5. Neno la Mungu ndio kawaida ya maisha ya mutu,atakaye ishi kinyume na kawaida yake hupoteza umbo lake.

6. Tukuzeni jina la Mola wenu mshindi awezaye yote, Mola wa mashariki na magharibi,chemchem ya nuru ulimwenguni.

7.Mlinzi wa viumbe anaye ziwilia watu shari ya kila namna,na kuwafungulia Heri kwa wingi,na kuwafutia giza kwa nuru yake,na kuwafanyia mapito ardhini na angani,Mola wa nyakati zote,mfariji wa milele.

8.Hakuna Mola mwengine kama yeye,wa pekee anaye ruhusu kipatikane ao kikosekane ulimwenguni. 9.Muanzishaji wa vilivyomo angani, na vilivyomo ukiwani,m'bora wa kuumba.

10.Tatizo huzingira maisha ya watu ajili ya kupinga sheria ya Mungu,hakika Mwenyenzi ndio mtatuzi wa mashida,Mkarimu aliye juu.

11.Teteeni namna ya kufika mbinguni mupate utimilifu,mutaishi bila kufikiwa na kifo,wala hamtafikiwa na msiyo ya taka,bali furaha ya milele.

12.Kuweni na upendo na fanyeni dhikri kwa wingi ,mukirudilia aya zake kwa kuisoma kiasi cha nguvu yenu,na kumtapa hakika ya kadiri yake.

13.Namna ya kuonesha shukrani kwa Mola wako kufatana na uwingi wa rehema zake.
14.Na ndio namna ya kupakiza nguvu ya ushindi ndani ya nafsi yako.
15.Dhikri ni ibada kubwa,mfano wa funguo ya kheri,maana anapo tukuzwa Mungu ndipo Shetani hulia.
16.Na kulia kwa Shetani ndio alama ya mafanikio ya mutu,kwani inapofanyika dhikri hushuka rehema ya Mungu kwa wingi. 17.Na wakati Mutu anapo kataa kumtukuza Mungu ndipo Shetani hucheka.
18.Na kucheka kwa Shetani ndio alama ya hasara kwa mutu,kwani laana humfikia anaye kataa kumtukuza Mwenyenzi. 19.Kesheni katika ibada mujichugulie jaza la nuru litokalo mbinguni.
20.Malaïka na roho huporomoka taratibu,kufuata sifa ya Mwenyenzi,wakileta fadhila nyingi kwa waja wake.
21.Mlinzi ni Mungu, muhifadhi wa milele,anaye nusuru shaidi wake na shari ya kila namna.
22.Makafiri wameimizwa na Shetani ili washambulie haki,hawata weza kumuangamiza ambae Mungu kamuokoa.
23.Nuru ya wachamungu huangamiza giza iliyemo ndani mwao makafiri.
24.Hakika nuru na giza haviambatane kamwe ,maana uyu ni kinyume cha yule.
25.Bila shaka waaminifu hufikiwa na vitimbi vya kila namna ambae hujaribu kuangusha haki.
26.Yule atakaye vumilia na kubakia imara bila kugeuka,pumzi yake itageuzwa roho takatifu na kupata neema ya kuishi milele. 27.Mola wenu ni mwepesi wa kuhisabu katika kheri kuliko shari,mpenzi wa watu.
28.Watu wengi wamepotea ajili ya ushirikina,wamejaana na jeshi la zimuni bila woga ajili ya kuipenda sana dunia.

29.Na wanao silimu pasipo kutubu wamepotea,maana wao ni wanafiki,wanazidi kutumikisha jeshi la zimuni,wamejiwekea kiziwizi baina yao na nuru ya Muumbaji wao.

30.Magumu ya dunia isiwapotezeni,enyi wanaadamu,hiyo ni mtihani, kuweni yakini kwamba itakwisha na baadaye furaha ya milele.

31.Katika wema wake mshindi,hubadiri machungu kua furaha ,maana yeye ni Baba wa salama aliye Salama 32.Hakuna mfano wake popote,maana kilicho njee ya dhati yake ni tafauti naye,ijapokua neno lake sio yeye.

33.Mwenyenzi hagusanake na chochote,maana yeye ni Mkamilifu ,kugusana ao kuchangikana na kitu zaifu ao pungufu ni kuzaufika ao kupungukiwa.

34.Na ijapokuwa umbo fulani hufanya miujiza,haina uzima,maana uzima ndio ukamilifu. Ingeli kua na uzima isingeli jumuika duniani wala hadezeni wala mbinguni,bali ingeli stawi enzini.

35.Mungu hawezi kujumuika katika umbiko bila hiyo kufutika,maana Enzi yake hufuta upungufu wote kando kando yake,hakuna ginsi ya kukurubia dhati yake.

36.Kama unaona yeyote ama chochote duniani ao hadezeni ao mbinguni,tambua ya kama ni mwana hewa ao muzila hewa. 37.Hapana kumfananisha yeyote na Mwenyenzi,hakika Mola wenu ni tafauti kabisa na viumbe.
38.Kuonekana na umbo fulani ni kua kiumbe fulani.
39.Na kulazimisha Mungu aonekane na umbo fulani ni kulazimisha Mungu awe kiumbe fulani.

40.Eti hakustahili kupatikana muumbaji isipokua viumbe pekee yake?
41.Kama ndivyo kitajitokezaje kiumbe ambae ni zaifu pasipo muumbaji?
42.Haiwezekane kuonana uso kwa uso na Mwenyenzi aliye muuijiza wa maajabu,ambae hana uso wala umbo.
43.Enzi iko mbali sana na dunia;vilivyomo duniani tu hauvizingatie vyote,wala vilivyomo hadezeni na pia vilivyomo mbinguni

na ili hali ndio vilivyo pamoja nawe angani na ukiwani.
44.Hakuna kujumuika wala kufanana katika umungu na ndio maana katika viumbe vyote hakuna mfano wake.

45.Ni wapekee anaye tawala ulimwenguni bila mshirika,angeli fanana na fulani hasingeli kamilika;bali angeli kosewa uwezo wa kutangulia kadiri ya kuenea.

46.Mungu ni Mfalme anae inukia kila kitu,viumbe vyote ni chini ya uwezo wake katika mambo yote. 

47.Kila mutu ashike imani hii ya kumpwekesha Mwenyenzi peke yake,hakuna anaye fanana naye.
48.Kila kilicho njee ya dhati yake ni miongoni mwa viumbe,ijapokua nuru yake sio sawa naye
49.Vitu vyote ni katika upungufu,hakuna anaye fanana naye,maana ukamilifu uliye umungu ni katika upekee. 

50.Shuudieni umoja wa Mungu,enyi watu,hakika Mola wenu amewapenda sana wanaotoa shaada.

51.Na anaye shaidilia umoja wa Mungu,akakubali ujumbe wake wote,yeye ndie anaye silimu.
52.Mungu alitangulia katika mamlaka yake mwenyewe,anaye miliki kila kitu, Bwana wa ma bwana.
53.Ni kheri kumtegemea peke yake,katika magumu na(katika) furaha,vyote ni vyake yeye muweza wa vyote.
54.Sio zambi kutunzwa utakapo gonjwa,lakini usifanye shirki.
55.Sio zambi kuuliza usicho fahamu,ni vema kuchuma elimu katika neno la Mungu,upate kuridhika usiwe mnafiki.
56.Sio zambi kulipisha kisasi kwa yule anaye chupa mipaka,lakini ni bora zaidi kuvumilia na kusamehe.
57.Sio zambi kuowa,lakini uowe mwanamuke ao wanawake,njee ya undugu wa damu.
58. Sio zambi kuolewa,lakini uolewe na mume njee ya undugu wako wa damu.
59.Alaaniwe yule anaye owa mwanaume mwenzake,na alaaniwe yule anaye olewa na mwanaume mwenzake.
60.Na alaaniwe yule anaye owa mwanamuke mwenzake,na alaaniwe yule anae olewa na mwanamuke mwenzake.
61.Na walaaniwe muke na mume wanao zini njee ya ndoa zao.
62.Watoto ndani ya ndoa ni wa bwana na bibi na hupewa haki ya kuwarithi.
63.Muzinifu hastahili kupewa isipokuwa azabu ya kifo,hakika madhalimu hunyimwa fadhila zote.
64. Maisha haiendelee pasipo sheria ya Mungu,tumieni uadilifu popote mtakapo kua,na ogopeni Mungu,wala msiruke mipaka. 65.Mupendane wote kwa jumla,hakika upendo ndio jambo kubwa katika imani,imehepusha mutu kutenda zambi mingi. 66.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu,anaye chipua maisha ya kila aina,Mwalimu wa jumla ya wapumuao.
67.Mola mwenyi uwezo wa ajabu,mamlaka ya kudiriki vyote kwa jumla,M'bora wa kuumba.
68.Mufalme anaye tawala vitu vyote bila mshirika,wa pekee anaye angazia kila umati,taa ya ulimwengu.
69.Ma Nabii na Mitume ndio vipenzi vyake ambae hutangaza kweli yake kwa kauli na matendo.
70.Maneno wanao kuja nayo sio yao,lakini ya Mola wao aliye watuma
71.Na yule atakaye fitinisha baina ya Mjumbe na watu wake ili wasimuamini aliye tumwa,ni mfano wa pumbafu anaye jiandaa

73.Mungu ametukuzika namna yote,amehepukana na upungufu sababu ya kukamilika kwake,hapungue wala haongezeke,mwenyi kuenea bila kasoro.

74.Yeye ni yote katika yote zaidi ya yote,Bingwa mshindi anaye tenda bila kufanya kazi.
75.Mungu wa miujiza anaye miliki ulimwengu,muabudiwa anaye sikia na anaye jibu maombi ya watu.
76.Ametangulia katika uwezo na katika ujuzi hali ya kua muweza wa vyote na mjuzi wa yote.
77.Mjuzi anaye tabiri kuzaliwa kwa mujumbe wake kabla ya ndoa ya mababu wa huyo.
78.Anajua yalio pita yote,ya sasa na yote yatakayo kuja baadaye.
79.Yeye ndio mwanzo wa vyote,chemchem ya upatikaji na maisha .
80.Kila kilicho na mwanzo kipo na mwisho,kilicho muanzisha kinaweza kumukomesha.
81.Sema:Mwenyenzi habadirishake makao kama vile kiumbe,kwake hakuna kuhama,wala kushurulika maana yeye ni mwenyi

kukamilika.
82.Yule asiye kua na mwanzo ndie asiye kua na mwisho sababu ya kutangulia kadiri ya kuenea,maana yeye ni mkamilifu. 83.Amestawi milele katika Enzi tukufu,Milki isiyo gusana na chochote cha umbalimbali naye.
84.Mamlaka yake ni kubwa zaidi,hupoteza kwa rafla upungufu wote kandokando yake.
85.Mtukufu aliye pasipo yeyote,wa pekee kadiri ya mwanzo wa vyote,Mjengaji wa makao ya wote anaye pangiza viumbe. 86.Fasi yenye Mungu iko ndipo alipokua na ndipo atakapo kua milele na milele.
87.Amani ya Mungu iwe juu ya wasilimu wote.


7. DAWA

1.Utakatifu ni wake Mwenyenzi Mungu,muhifafhi wa milele anaye meremeta zaidi ya mwangaza.
2.Mumiliki wa falme zote,asiye kurubiwa na yeyote ku vyovyote ulimwenguni.
3.Anga na ukiwa hutii amri yake,wala hakuna umbo njee ya kawaida yake.
4.Mtukufu wa kauli ajaaye mamlaka kadiri ya uwezo wa vyote.
5.Hutokeza ambacho hakikua popote,amekua yote katika kutenda ,na yote katika kufahamu,Bwana wa ulimwengu. 6.Mtakatifu wa ajabu anaye jaa huruma,ambae husamehe zambi zao wanao tubu.
7.Mungu mkubwa anaye tenda kwa haki,ambae ajabu ya tendo lake hufanyika kadiri ya fumbo mbele ya viumbe.

8.Nuru juu ya nuru,tumaini na kimbilio,mwenyi kujieneza kadiri ya ukamilifu.
9.Mola wa pekee anaye jumuisha walimwengu kwa idhni yake.
10.Mamlaka yote imetoka kwake,ni yeye anaye podoa wasilimu na rangi yake takatifu.
11.Mlezi wa viumbe aliye na upendo,ambae kawawekeeni wasaidizi katika maisha yenu.
12. Ameumba mbingu angani na dunia katika maunganio ya anga na ukiwa,kadiri ya mpango maalumu. 13.Mungu mjuzi aliye Enzini,muujiza wa maajabu ulimwenguni.

14.Watu wamenajisi utukufu wake katika masemi yao,maana lugha zao hazitimize hakika ya hali yake.
15.Hakika ujuzi ni tafauti kabisa na fikara,kila atendalo mwenyi ujuzi huzidia sana kutenda kwao wenyi fikara 16.Ni mshindi juu ya kila kitu,Mola wa ulimwengu wote,Mfalme anaye stahili kuhimidiwa.
17.Amejaa uwezo usio na kipimo,ambae humiliki vyote ulimwenguni
18.Mushinda-kushinda anaye tawala viumbe vyote kwa jumla,uwezo wa kuenea.
19.Hakika,ushindi ni wake Mwenyenzi,M'bora wa mahakimu afanyaye mambo yote kwa haki.
20.Hazulumiwe yeyote miongoni mwa viumbe vyake,kila yule amefanikiwa na rehema zake kadiri ya kipaji chake.

21.Umbo zote hutoshelezwa naye,kwake hakuna upendelevu,ujuzi wake umetimiliza umbiko katika kawaida yake. 

22.Usilaumu lolote,lakini kuwezi yakini kwamba mfinyanzi wenu amejua sana na zaidi.
23.Umbiko ni mfano wa fumbo ambae hufumbilika na yule anaye funuliwa na Mungu.
24.Ugunduzi wote wa mutu kuhusu vifaa vya nafsi yake,katika maisha yake,unatoka kwa Mungu.

25.Maisha njee ya nuru haiendelee,lakini hukoma kadiri ya kupotea.

26.Komboa nafsi yako kwa kutumia neno la Mungu,maana hutatua shida zote maishani.

 27.Hakika neno la Mungu ni dawa ya kila magonjwa.

28 Watu wangeli fahamu faida ya kisomo kitukufu namna ya dhikri,kama wangeli kua nasoma kauli tukufu ya kitabu hiki mara na mara kila siku.

29.Kauli tukufu ni mamlaka ,kutokezwa kwayo ni ajabu ya kupatikana kwa rafla ambacho hakikuwa.
30.Mungu hujitukuza sana katika neno lake: atakaye itumia atajazwa nguvu ya ushindi,wala nafsi yake haita vamiwa,lakini

31.Atakaye itumia katika kawaida yake,atafanyika umbo mpya ya mbinguni.
32.Laiti mungeli musikia Yesu Masia,mtukufu wa daraja aliye mfano wa kauli tukufu. 

33.Nuru kubwa yenyi nguvu mbinguni kadiri ya roho takatifu,wokovu wa watu. 34.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mneemeshaji anaye tukuza nafsi ya musilimu. 

35.Mola wa majeshi yote,anaye simamisha imara ufalme wa kipenzi chake.
36.Na kuvunja jeuri ya makafiri,na kulainisha kilicho kigumu.
37.Ni wewe unaye nusuru mutu aliye katika hatari,ukimsimamisha aliye anguka. 

38.Vikwazo vya maisha yake,hutoweka kama vile giza hufukuzwa na nuru. 39.Mumgu ni ponyo ya kila nafsi,msaada na wokovu wa watu.

40.Amemupa ushindi mutumishi wake,na kuwazalalisha watesi wake. 41.Utulinde kutokana na zulma,fitna pia na masingizio ya watu wa Dunia. 42.Sisi hatuna tegemeo ingine kinyume nawe.

12

43.Na kweli umetutosheleza katika maitaji yetu.
44.Mungu mkuu anaye lipisha kisasi,ambae humpiga aliye kusudia kutupiga, na humnyanyasa aliye kusudia kutu nyanyasa. 

45.Mtukufu aliye na ushindi juu ya kila kitu,anaye rehemu na anaye kirimu.
46.Uzima wake hauzingatiwe isipokua na wenyi akili.
47.Ni muujiza mkubwa sana usio lingana na chochote,jambo ambae hizidia fikara ya viumbe,iletayo msangao,ajabu ya utukufu

wake.
48.Mtangulizi pasipo msaada wa yeyote, atawalaye katika ulimwengu, uwezo wa kuenea. 49.Bingwa aliye na milki kuu,anaye fanya jambo bila shuruli yoyote,ambae idhini yake hutenda. 

50.Bwana wa mabwana aliye chemchem ya uwezo na fahamu,atakasikaye na ashindaye.


8. MUMILKI

1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mumilki,anaye pindua mipango ya maadui.

2.Mlinzi mwema anaye semelea walio onelewa na kuwapanguza machozi wanao lia.
3.Mumilki anaye jazikisha palipo wazi,na kunyoosha kilicho kunjama,na kuunganisha kilicho vunjika . 4.Hakuna kufaulu inje ya msaada wake,mtefuzi wa kila zamiri,anaye ona yote na anaye sikia yote.
5.Mola wa manabii na mitume wote,chemchem ya upatikanaji na maisha,kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.

6.Hakuna bwanaasiye muita Mungu bwana ,wala asiye tetemeka mbele yake,mufalme wa wafalme wote anaye jaa milki kamilifu,mwenyeji wa ulimwengu.

7.Alikua,yuko na atakua,mwenyi kuenea;hakuna mwengine kama yeye, wa milele aliye juu. 

9. IMANI TIMAMU

1.Usalama wa nafsi katika mapenzi ya Mungu ndio usilimu,dini ya Mungu kwa watu wote. 

2.Mtume anaye fundisha dini kinyume na hii,ni wa uwongo.

13

3.Kama unamtaja mtume uyu katika shaada yako na yule anamtaja mtume mwengine katika shaada yake,nyinyi wote ndio wasilimu.

4.Ispokuwa yule atakaye shaidilia Mungu mwengine kinyume na Mwenyenzi ,ndio aliye njee ya usilimu.
5.Usilimu sio kwa yule anaye mtaka nabii ao mtume fulani,lakini kwa yule anaye muamini Mungu na mitume wake wote.

 6.Sio kwamba usilimu ni kwa yule anaye muamini Muhamadi peke yake,walasio kwa yule anaye muamini Yesu Masiya peke

yake.
7.Kama mutu anasali kwa kumuhimidi Mungu na kufunga sala na kusoma sura ya ufunguzi kulingana na shaada yake,na

kusujudu pia na kutoa shaada katika kipindi maalumu,bila shaka mutu uyu ni musilimu.
8.Atakaye mtaja Muhamadi katika shaada yake,itakubaliwa na Mwenyenzi lau kama moyoni mwake ame waamini pia ma

Nabii na Mitume wengine wote.
9.Na atakaye mtaja Yesu Masia katika shaada yake,itapokelewa na Mungu lau kama moyoni mwake amewaamini ma Nabii na

Mitume wengine wote.
10.Na anaye amini mitume wote,ameamini pia vitabu vyao vyote,haiwezekane kuamini mtume ambae haukubali maneno yake. 11.Kitabu cha Mtume wa Mungu ni kile kinacho andikwa kwa njia ya ufunuo,sio kinacho andikwa kwa njia ya utafiti. 12.Katika utafiti munamo hitilafu,maana ni Kazi ya kibinaadamu" yenyi upungufu.
13.Anaye amini kitabu hiki kitukufu cha "ukweli",ni lazima kwake aamini pia Qur'ani na Injili na Zaburi na Taurati.
14.Na anaye amini Qur'ani ni lazima kwake kuamini kitabu hiki cha "Ukweli" na Injili,Zaburi na Taurati
15.Na vivihivyo kwa yule anaye amini Injili,Zaburi na Taurati,ni amri kwake kuamini kitabu hiki cha "Ukweli" na pia Qur'ani. 16.Sio muaminifu yule anaye amini sehemu na kukataa sehemu ya kauli tukufu.
17.Na ndio maana haifai kuchanganya utafiti na ufunuo.
18.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.


10. AL-KARIM


1.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu anaye funulia watu ili wapate kusadiki uzima wake

2.Watu hawawezi kumzingatia bila kufunuliwa,maana fikara yao ni yenyi kuzaufishwa na mwili
3.Utukufu wa mutu unatokana na nuru ya Mungu: anaye funuliwa ndio mtukufu na asiye funuliwa ndie mdhalili 4.Mungu alimutukuza Muhamadi kwa kumjaza nuru ya zamana ambae humulika duniani na mbinguni
5.Popote alipo kua duniani palionekana pamejaa nuru kubwa kadiri ya umbo ya zamanani.
6.Alipewa kazi kubwa ya kufundisha usilimu,
7.Hakika asiye amini kwamba Qur'ani ni Al-Karim,hataingia mbinguni;asema roho wa Mungu


11. UTAALAMU


1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu atanguliaye kadiri ya kuenea,juu ya maala pa juu

2.Uzima wake ni mbalimbali na kila kitu, ukafikiria kuhusu umungu,usizani kama kuna mfano wake,hakuna kitu cha kilinganisha na ukamilifu.

3.Usilazimishe kumuona Mungu na hiyo macho ya mwili wako isiyozingatia ila miili peke yake 4.Hauta muona kimwili yeye asiye kua na mwili,tena asiye jumuika angani wala ukiwani

5.Ukalazimisha Muumba akuonekanie ama ajumuike pamoja nawe,ni kwamba umelazimisha ageuke kiumbe,jambo lisilo wezekana

6.Umutu na mambo yake yote ni katika upungufu, hali kama hii haichuguane hata kidogo na mwenyi uzima 

7.Kumbi usimtazame Mola wako kimwili,lakini umtazame kiroho ili upate kuzingatia uzima wake


12. ALAMA YA DINI


1.Enyi walio silimu! fanyeni ibada katika usawa,usifanye upuuzi katika kazi ya Mungu,wala usijifanyie lolote pasipo

mwongozo wa Mungu wala usifute kitambulisho cha Dini
2.Na anaye jidai kusali kiroho pasipo kudhihirisha Sala yake kimwili ni miongoni mwao wafutao alama za dini ya Mungu.

3.Umbo la mutu ni timilifu katika changachanga ya mwili na pumzi
4.Mutu angelikua pumzi peke yake,asingelijumuika duniani,lakini mbinguni (ao hadezeni).
5.Nyenyekea uzima wa Mungu kimwili na kiroho,ili upate kutimilika
6.Kutumikisha mwili wako katika sheria ya Mungu ndio kuamini Mungu
7.Mwili wako ukatenda zambi,roho yako pia huchafuka,usijidai kua roho tupu na ili hali upo na mwili,yaani ukingali duniani


13.. SAUMU


1.Enyi walio amini! Mumelazimishwa kufunga saumu kwa kufuata jukumu lake. 

2.Saumu inayo sehemu mbili,kulingana na umbo lako:sehemu ya kimwili na ya kiroho.

3.Kutokula wala kunywa tangu asubui mpaka mangaribi,ndio kufunga kimwili.Na kutotumia kiungo chako hata kimoja kwa kutenda zambi,ndio kufunga kiroho.

4.Kimwili utafunga muda fulani na kufungula muda fulani,lakini kiroho utafunga bila kufungula mpaka mwisho wa umri wako.

5.Yule atakaye funga kimwili-tu bila kiroho ni miongoni mwa wanafiki;na vivihivyo kwa yule atakaye jidai kufunga kiroho-tu bila kimwili ni mnafiki.

6.Na kama hali yako haistahili:kama vile afya,safari,jela,umri... basi usifunge kimwili.
7.Usitumikishe roho ajili ya kuujenga mwili peke yake,ni bora zaidi kutumikisha mwili wako katika kuijenga roho yako,ili
 upate kurithi bustani ya neema mbinguni. 

8.kujishusha mbele ya Mungu kwa utiifu na heshima.
9. Asiye msujudia Mungu sio mnyenyekevu wala hana sala.

14. SIJIDA

1.Ametakasika Mwenyezi Mungu,wa pekee anaye stahili kusujudiwa.
2. Lengo ya kuumbwa kwa mwanaadamu ni kumuabudu Mungu.
3. Na kilicho muimu katika tendo kuabudu ni sijida.
4. Hakuna sala pasipo sijida na haistahili kwa mwengine ispokua kwa muumba peke yake.
5. Sijida ndio tendo kubwa la unyenyekevu,linalo leta utafauti kati ya sala na dua(maombi),ambae humaanisha kuabudu.
6. Kuona kama sala ndio ibada kubwa zaidi,ndio maana matendo haya makubwa, sijida na shaada, hupatikana ndani mwake. 

7 .Kuinama kadiri ya kupeleka uso mpaka chini,katika unyenyekevu,ndio kufanya sijida ,


15. UPEKEE


.1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu Mjuzi atendaye makuu ambae milki yake hustaajabisha

2.Upekee wa dhati yake humfanya azingatiwe na wenyi akili peke yake
3.Wasio kua na akili hawawezi kugundua uzima wake ajili ya uzaifu wa fikara yao.
4.Mwenyenzi ni Mkamilifu,amepatikana kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho.
5.Uwezo wake wa ajabu unamfanya kua katika upekee,hachuguane na yeyote wala hachangie fasi na yeyote. 6.Amestawi kikamilifu kadiri ya mwanzo wa vyote,chemchem ya upatikanaji na maisha.

7.Alikua,yuko na atakua,Mufalme wa milele. 

16.UFUNUO

1.Mwenyezi Mungu amefunulia waaminifu katika njia mbalimbali,zaidi sana katika ndoto. 2.Nuru imezidiana kufatana na daraja ya watumishi.
3.Ma Nabii na Mitume ni wenyi nuru kubwa,ndio maana ufunuo wao ni bayana.
4.Ufunuo wote sio unabii wala utume,unaweza kufunuliwa na ili hali wewe sio nabii wala mtume. 5.Usijidai utume ajili ya kufunuliwa,mpaka Mungu akutume ku watu na ujumbe wake.

6.Hakuna mjumbe pasipo ujumbe.
7.Na usiwe kama aliye gizani:kutofunuliwa hata kidogo ni alama ya imani haba.

14


17. UCHUPAJI

1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,kiongozi mkamilifu,anaye endelesha ulimwengu kadiri ya idhni yake

2.Mwenyi sifa kamilifu,anaye fanya yote tafauti na wote 3.Sifa ya viumbe ni pungufu ajili ya kutokamilika

4.Usimtukuze yeyote kwa sifa isiyo kua yake,ijapokua Nabii,usije ukaangamia ajili ya kuchupa mipaka. 

5.Uzuri wa jambo ni kati kwa kati,usizidishe wala usipunguze

6.Wengi wamefikia kuabudu Nabii ajili ya kumsifu kwa kuchupa mipaka
7.Mungu peke yake ndie anaye stahili kusifiwa sifa ya aina yote,kwani yeye ni mkamilifu,mwenyi uwezo wa vyote.


18. SHAADA


1.Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa ila Mwenyenzi Mungu peke yake,na hakika Yesu Masiya ni Mtume aliye

tumwa naye.
2.Hii ndio Shaada ya musilimu anaye tumia nuru ya Mungu katika dhati tukufu ya Yesu Masiya.
3.Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa ila Mwenyenzi Mungu peke yake,na hakika Muhamadi ni Mtume aliye tumwa

naye.
4.Hii ndio shaada ya musilimu anaye tumia nuru ya Mungu katika dhati tukufu ya muhamadi.

5. Kukiri kwa yakini kwamba Mungu peke yake ndio mwenyi uzima,na kushaidilia ya kwamba hakuna mwengine kama yeye ,na pia kuamini mitume wote,ndio kutoa shaada.
6. Anaye mtaja Yesu Masiya katika shaada yake pamoja na yule anaye mtaja Muhamadi katika shaada yake wao wote ndio wasilimu.

7. Atakaye bagua miongoni mwa mitume ndie kafiri asiye amini kauli ya Mungu; hakika shaada ndio tendo la msingi wa imani.

8. Kumtaja Nabii ao Mtume fulani katika sehemu ya pili ya shaada yako sio kuwakanusha wengine,hakika kuamini mitume wote ndio imani ya kweli.
9. Ni bora sana kumtaja mtume wa zama zako ao mitume wakuu ,katika sehemu ya pili ya shaada yako.


10. Hakika shaada ndio msingi wa imani,ambae huleta utafauti baina ya musilimu na kafiri.

 11. Hakuna imani pasipo shaada ya Mungu.
12. Yeyote asiye toa shaada sio muaminifu lakini kafiri.


19 . HALI


1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,Mzima,anaye stawi katika utukufu usio kurubiwa na yeyote
2.Hali yake ni tafauti na viumbe vyote,na ndio maana makao yake ni tafauti na kambi za wengine wote 3.Yeye hana pumzi wala mwili,ndio maana hapatikane angani wala ukiwani
4.Lau kama angelikua na hali ya viumbe,bilashaka angeli jumuika pamoja na viumbe
5.Kutojumuika pamoja na viumbe sio kukosekana ulimwenguni,kambi lenu sio ulimwengu wote
6.Hali yake ni tukufu ajabu inamfanya atengane na vitu vidhalili milele na milele
7.Amepatikana Enzini maala pa upekee,ukamilifu hauchangane na upungufu kamwe.


20. UCHIMBI


1.Ametakasika kabisa yule aliye Enzini,Mfalme anaye hukumu vilivyomo angani na ukiwani 2.Mamlaka itokezayo kuujaza ulimwengu,mtendaji wa jumla ya matendo
3.Mbingu na dunia hufuata hukumu yake,kiongozi wa mwili na roho,anaye miliki falme zote 4.Mamlaka yote imetoka kwake ;amempandisha amtakaye na amemshusha amtakaye

5.Uchimbi ni haramu kwa musilimu:usimgombanishe kiongozi wako wala jerani yako bila sababu,lakini umuombee ili Mwenyenzi amfanye kua muadilifu

6.Wala usipiganishe dini ya Mungu ajili ya kuimarisha mila ya ukafiri

7.Mwenyenzi ndie wa kutegemea katika yote,maana vyote hutokea kwake,ni yeye peke yake aliye na uwezo juu ya kila kitu 

21. USWAHABA

1.Neno la Mungu ndio nuru inayo angazia watu duniani
2.Mungu amemteremshia nuru amtakaye na kumupa kazi ya kiroho
3.Kuona kama amemupatia mutu kama wao,wengi huchukia na humzarau aliye tumwa

 4.Ni aibu kwao kumfuata mutu kama wao,ambae wamemzidia utukufu wa kidunia

5.Kumuamini mtume na kumfuata katika uhai wake ni neema,na ndio maana ni wenyi daraja mbinguni maswahaba wa mitume

6.Watu hujiunga upesi kwao watetezi wa Mambo ya kidunia ajili ya hanasa ya dunia.

7. Hawana yakini na uzima wa Mola wao ajili ya upofu,hawazingatie inje ya dunia.

22. USINGIZI


1.Uzima ni.wake Mwenyenzi Mungu,wa pekee anaye kamilika ulimwenguni
2.Asiye kubali uzima wa Mungu ni kwamba bado kuamuka katika usingizi
3.Watu wengi wameamini kwa midomo-tu,lakini moyoni hawana yakini na ukamilifu wake
4.Ni kwa sababu hawatumie njia yake ndio maana hawazingatie utendaji wake
5.Mungu ndio msimamizi wa maisha,mwenyi mamlaka ya ajabu ambae idhni yake hutenda bila kutumika kazi
6.Mola wa miujiza afanyaye maajabu,Mjuzi anaye hifadhi yote yanayo tendeka kila fasi na kila wakati, M'bora wa kuenea 

7.Hakuna Mola mwengine kama yeye,mumiliki,aliye tayari kutokeza mapya kila wakati pahali pote,wa pekee aliye na ushindi.


23. DINI MOJA


1.Usilimu ni usalama wa nafsi katika mapenzi ya Mungu .
2.Na ndio dini ya Mungu tangu mwanzo mpaka mwisho wa dunia.

3.Hata mababu zenu (wazee wenu) walikua wasilimu miongoni mwao kulikua wachaguliwa ambae Mungu kawafunulia na kawajaza roho kwa namna mbalimbali.

4.Maneno walio pokea haikuandikwa yote,lakini kayahifadhi vifuani kadiri ya kanuni yao.
5.Shetani akawa shawishi ili waingize shirki katika ibada yao,kama ilivyo desturi yake kwa kila umati.
6.Mwenyenzi alionesha mapenzi yake kwa kila kabila na kila umati,akiwajaalia nuru kulingana na fikara yao wakati wao. 

7.Walio silimu miongoni mwa mababu zenu walikuwa na mila nzuri sana,ya upendo kati yao na unyenyekevu kwa MwenyeziMungu.


24. TUNDA LA SHETANI


1.Ole wao wanafiki wanao jiundia wenyewe ma kundi ya kidini ajili ya anasa ya dunia
2.Hawana dini ispokua hufichamia katika neno la Mungu na ilihali hawana imani.
3.Wengi ni wanasiasa wanao tumia jina dini,ili wafaulu katika mambo yao
4.Na wengine ni wachawi ambae hutumia jina dini katika vikundi vyao ili wawadanganye watu
5.Na wengine hutumia neno la Mungu kama viashara ili watajirike kwa pesa na vifaa vya kimwili
6.Wanafiki kama hawa ndio wanao kataa kabisa kusilimu katika kweli na haki,maana wao ni « Tunda la Shetani« 7.Ispokuwa wanao tafuta kweli njia ya Mungu ndio wanao silimu na kutubu.


25. KIPINDI


1.Na utakapo nuwiya kusali ni lazima huelekeza akili yako yote kwa Mungu,kumuhimidi na kufunga Sala

2.Katika kisomo chako anzia na sura ya ufunguzi kulingana na shaada yako
3.Atakaye tumia dhati tukufu ya Muhamadi ,ni lazima kurukuu na kusujudu,(kulingana na kipindi anacho sali).
4.Na atakaye tumia dhati tukufu ya Yesu Masiya ni lazima kusujudu bila kurukuu,(kulingana nakipindi anacho sali). 5.Imamu mbele na wengine wote nyuma yake katika masahafa ,juu ya misala ao mfano wa hayo ;

16

6.Hakika mnao mfano bora kwake Muhamadi,na Yesu Masiya pamoja na mitume wengine wote

7.Watu wasio fahamu kusali ni wale wasio amini mitume wote,wanampinga mwalimu wa sala,ndio maana wanabakilia -tu katika maombi peke yake

26. KIVULI CHA MTUME

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, anaye fadhilisha mutu kwa kumkutanisha na neema.

2. Mutu anaye jazwa roho takatifu ni nuruni na matendo yake ni yenyi kubarikiwa.

3. Ameongozwa katika yote,mwenyi hekima timamu ambae huujenga sawa sawa umutu wake.

4. Hafikiriake mabaya wala kuyakurubia,miguu yake urakibuni maisha yote.

5.Amewanukulu ma Nabii na Mitume katika hoja na tendo,wala hatumikishe matamanivu ya nafsi yake bila kuyalinganisha na kauli tukufu

6.Mutu atakaye iga mila ya Mitume atakua kama kivuli cha Mtume,mwenyi kujazwa roho takatifu
7.Mungu peke yake ndio anaye stahili kupelekewa shukrani,Msamehevu na Mrehemevu,hakuna mwengine kama yeye.

27.UTANGULIZI
1.Wengine hawa muamini Mola wao katika yakini sababu hawaonane naye kama wanavyo onana wao kwa wao
2.Na ili hali wao ni katika upungufu mfano wa vifebe,hawastahili hata kidogo kukurubiana na ukamilifu
3.Enzi yake ni milki kamilifu inayo waka bila mfano wake ambae hufuta kwa rafla upungufu wa aina yote kando kando yake 4.Na ndio maana hakuna umbo yenyi kukurubiana na Mwenyenzi katika makao wala katika fahamu wala katika uwezo 5.Tendo kutangulia ni jambo ndogo sana kwa yule aliye kamilika,ndio kawaida yake sababu ni muweza yote,anaye enea kadiri

ya uzima
6.Kutangulia ni tendo lisilo wezekana kamwe kwa yule mpungufu sababu hukosewa milki kamilifu,ndio maana yeye huanza

maana ni hunusu na kipande.
7.Shangilieni uzima wa Mola wenu aliye Enzini,Mshindi,awezaye yote na ajuaye yote

28. TASWIRA
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,m'bora wa kuumba aliye umba mbingu saba na ardhi saba. 2.Na baina ya mbingu na ardhi akaumba Hadeze na dunia,kadiri ya maunganio.

3. Dunia juu ya ardhi na hadezeni chini ya mbingu.
4. Aliye na mwili mzito unao changikana na pumzi mwepesi,hudhihirika duniani.
5. Na aliye na pumzi nzito inayo changikana na mwili mwepesi ,hudhihirika hadezeni.
6. Ndio maana husemekana hadeze hupatikana angani na dunia hupatikana ukiwani.
7. Huzingatiwa na watu viumbe vinao husika na maisha yao,na havizingatiwe na watu viumbe visio husika na maisha yao.

29. MASHAKA
1.Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu,anaye tokeza anga na ukiwa pamoja na vilivyomo
2.Hakuna mwengine aliye na ujuzi kama yeye na ndio maana haifae kushakia lolote katika ujumbe wake
3.Kushakia neno litokalo kwa Mungu ni alama ya uchache wa imani na alama ya kiburi
4.Kama kweli upo yakini na ujuzi wake,haustahili kushakia utendaji wake,hauna budi ya kumkosoa Mjuzi
5.heri yule aliye amini maneno ya Mtume bila kushakia lolote analo sema wala analo tenda,maana ni mwenyi yakini kwamba

ameongozwa na roho wa Mungu
6.Kushakia asemalo Mtume ni kushakia kauli ya yule aliye mtuma,jambo ambalo humaanisha uchache wa imani 7.Mutu sio chochote katika fahamu wala lolote katika uwezo mbele ya yule aliye muumba

30. ALIKO LA JESHI
1.Roho takatifu ndio zawadi wanao pewa walio amini,inateremuka tokea juu mbinguni kwa amri ya Mungu Mwenyenzi
2.Kwa kupokea zawadi hii kwanza ni kusilimu na kutubu na kujitolea sana katika ibada
3.Kusali kila siku asubuhi na jioni,na usiku;hakika kumtukuza Mungu kwa wingi usiku humkurubisha mutu na watakatifu wa

mbinguni
4.Ni bora zaidi kupangilia mwenyewe kisomo na dhikri ya kila siku,pia na sala ya suna
5.Utakapo zoea kuifanya ibada uliopangilia kila mara,itakua kama anaye alika jeshi la mbinguni.
6.Roho ya Mungu itakukurubia na mwenyewe utazingatia upatikanaji wake ndani mwako bayana ama katika ndoto 

7.Malaïka na roho huporomoka kwa wingi maala inapo somewa kauli ya kitabu hiki kitukufu.

31. ASIYE FANANA

1.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu,Muhifadhi wa milele,anaye mililki vyote pahali pote muda wote 2.Mjuzi anaye elimisha wanahewa,na kuhukumu yote yanayo tendeka angani na ukiwani bila msaidizi 

3.Busara chache ya kibinaadamu hufanya mutu ajilinganishe na Mola wake
4.Mara hulazimisha kujumuika naye na mara hutaka kuhojiona naye kama kiumbe chenzake

5.Mola wako ni Mtukufu wa hali ya juu sana,na wewe ni kitu dhalili sana,hamlingane ku vyovyote kamwe 6.Kumlazimisha atende kadiri mtendavyo nyinyi ni kumlazimisha aishi kama nyinyi,na ili hali uzima sio maisha 

7.Mungu ni mwenyi kuenea,anapo tenda sio ila katika yote,kila yule ameishi kwa msaada wake Mwenyenzi.

33. UMUNGU
1.Ametakasika kabisa yeye anaye stawi arshini kadiri ya kuenea
2.Umungu ni utukufu wa ajabu,Milki kamilifu isiyo punguka wala kuongezeka ajili ya kuenea
3.Yeye ni yote katika kajua na yote katika kutenda, wa miujiza aliye na ushindi
4.Ufalme wake ni wa milele ajili ya kutangulia,Mola wa masharikina magharibi,kiongozi wa jumla ya viumbe. 5.Mungu wetu aliye Mungu wenu na Mungu wao,wala hakuna asiye milikiwa naye
6.Muhimidiwa na wote,anaye inukia wote ,aliye huru katika yote juu ya maala pa juu ulimwenguni
7.Mola wa pekee aliye na Enzi tukufu dhatini mwake kadiri ya uzima,M'bora wa kuenea.

34. KUKOSA SHUKRANI

1.Mungu ndio tumaini ya watu wenyi akili,wametambua mamlaka yake ambae humiliki kila kitu
2.Imani ndio humaanisha akili ya mutu,kukiri uzima wa Mungu ni neema
3.Kafiri hana akili wala shukrani,amepuuza neema ya Mola wake na kusema:sioni anacho nifanyia
4.Kila ulicho nacho ni neema kutoka kwa Mungu,wala haungeli patikana bila yeye kutangulia
5.Kafiri amempelekea adui yake shukrani na sifa ,akisema:shirki yangu ndio inayo ni saidia
6.Amekosa shukrani ajili ya uziwi na upofu,hana macho ya kuona wala masikio ya kusikia
7.Hakika mishirikina hawana amani katika maisha ya leo wala ya kesho,wamejitwiga mizigo ambae hawata weza kuibeba.

17

32. HATUA
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,Mfalme mkamilifu,anaye simamia viumbe vyote kwa hekima ya ajabu
2.Mwalimu wa walimwengu,anaye angazia watu kwa njia mbalimbali,M'bora wa viongozi
3.Hatua kubwa ya tafsiri ya kweli yake ni katika unabii na utume,yaani hupatikana kwa njia ya Malaïka na roho.
4.Na hatua ndogo ya ulabudishaji ni katika uhasidu na urozi maana hupatikana kwa njia ya Shetani na muzimu
5.Aliye katika njia ya Shetani na muzimu ni gizani na ndio maana hazingatie kweli ya Mungu
6.Na yule aliye katika njia ya Malaïka na roho ndio aliye nuruni,na ndio maana ameamini kweli ya Mungu ajili ya kuzingatia 7.Mungu Mwenyenzi ndio mwenyi uzima,ni amri kwa kila mutu kumuamini na kumuabudu.

35. NGUVU YA MAOMBI
1.Mungu ni mwenyi fahamu ya yote,Mjuzi,anaye jua ambae kiumbe hakihelewe;lakini kama yeye anajua ya mbele ya wakati ,ni kweli na wewe umejua kama yeye?

2. Na kama hauna ujuzi kama yeye,kwa nini kupinga amri ya Mola wako ajuaye yote?

3. Kama aliamrisha watu kumuomba,anajua faida ya maombi katika maisha ya wanaadamu.

4. Maombi ya waaminifu inayo nguvu ya kubadiri ili ambae ilikua imeandaliwa kwa watu.

5.Aliye kua wa kuangamia,ajili ya maombi anaweza kuokolewa;na pia aliye kua wa kuokolewa,anaweza kuangamia sababu ya kutofanya maombi.

6.Ibada ndio funguo ya kila la kheri na uovu ndio funguo ya kila la shari

7.Wala usijingikiwe kwa sababu Mungu anajua yote na ili hali wewe haujui kama yeye wala usijiamulie mwenyewe mbele ya wakati na ili hali haufahamu ya mbele ya wakati.

36. ARSHI
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,m'bora wa kuumba anaye stawi arshini
2.Amezidia vyote wala hakuna mfano wake popote ulimwennguni
3.Amewaleteeni ujumbe wake kwa namna ya mifano ili wapate kuzingatia
4.Kiti cha Enzi ambae ndio arshi yake Mwenyenzi ,sio mfano wa viti vyenu vya kuikalia,lakini utukufu ao ufalme wa milele 

5.Hakika sifa ya Mungu ni miongoni mwa tafsiri ya umungu
6.Ufalme wa milele ao utukufu wa ajabu usio najisika ndio hali yake Mwenyenzi
7.Kuona kama hakuna mwengine ajumuikaye Enzini,ndio maana hakuna wanaenzi isipokua Mwenyenzi peke yake.

37. NABII WA UWONGO
1.Dini inayo anzishwa na Nabii ao mtume wa uwongo ni ya uwongo pia na wanao shiriki pamoja naye wamepotea

2.Na maubiri yake sio ila udanganyifu mtupu,maana mwalimu wake ni Shetani
3.Kupiga ramli ama kuaguza sio kutabiri maono ,wala miujiza yake isi kudanganye hata Shetani pia huyafanya
4.Kilicho muimu ni maneno,kwani ndio ujumbe:kauli tukufu ni ukweli usio na shaka
5.Chunguzeni kauli yake na matendo yake na pia kumuomba Mungu akuoneshe undani wake
6.Nabii asiye kua na ujumbe wala haamini Mitume wote wala haamini vitabu vyote ni wa uwongo
7.Na pia nabii ao mtume anaye muita Nabii wa Mungu Yesu Masiya kua ndio mungu wake ni nabii ao mtumewa uwongo.

38. KIBLA
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu aliye umba kila kitu,wala hakuna kisicho kua chake.
2.Amestawi Enzini kadiri ya kuenea,pande zote ni zake,hakuna kwa kumfichamia.
3.Ni lazima kuhelekea kibla wakati wa Sala; ambae ni katika sehemu mbili: ya kimwili na ya kiroho.

 4.Kimwili ni kuhelekeza uso wako maala patakatifu,kwenyi muskiti mtakatifu ao mlima mtakatifu. 5.Atakaye tumia dhati tukufu ya Muhamadi,hujihelekeza kwenyi muskiti mtakatifu wa Maka.
6.Na atakaye tumia dhati tukufu ya Yesu Masiya hujihelekeza kwenyi muskiti mtukufu wa Yeruzalema.

 7.Na atakaye tumia dhati tukufu ya Mussa,hujihelekeza kwenyi mlima Sinaï.

8.Na atakaye tumia dhati tukufu ya ( Shahidi wa Mungu ) Kalonda,hukihelekeza kwenyi Muskiti mtakatifu wa Kadingila ao mlima (mtakatifu)Karombwe.

9.Ki roho,kuhelekeza akili yako yote kwa Mungu namna ya kumtegemea yeye peke yake,ndio kuhelekea kibla. 10.Kama haufahamu upande wa kibla ,usikose kusali kimwili,Mola wako ni tayari popote.

11. Na kama muskiti huhelekea kibla kingine na ilihali wewe hutumia dhati tukufu ya mwengine,usikose kusalia humo, pande zote ni zake.

12. Amani ya Mungu kwa wasilimu wote !

39. UTUKUFU

1. Enzi ni utukufu wa ajabu usio najisika, milki kamilifu kadiri ya uwezo wa vyote na ujuzi wa vyote.

2. Ilitangulia kimuujiza kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho namna ya kukamilika.

3. Utukufu wake huu ni wenyi kustaajabisha ajili ya kuzidia, ushindi katika yote, milele na milele.

4. Ni mwenyi uhuru ajili ya kuenea, mfalme anaye tawala ulimwenguni.

5. Pahali alipo hakuna mwengine,wa pekee aliye juu.

6. Kila kilicho njee ya dhati yake ni kipungufu, maana hutengana na ukamilifu.

7. Na ndio maana vyote vilivyomo angani na vyote vilivyomo ukiwani ni vitu dhalili sana mbele yake,hakuna mfano wake.

40.KITABU KITUKUFU
1.Kauli ya Mungu ni kweli na haki ambae ndani mwake hamna shaka
2.Kama kauli yake imeandikwa katika kitabu,bila shaka kitabu kile ni kitukufu,maana ni nakala ya ufunuo
3 Na ndio maana ni amri kwa watu wote kuamini vitabu vyake ambae kawa teremshia Mitume wake
4.Hapana kuamini sehemu na kukataa sehemu ya maandiko matakatifu: kama si kimwili kumbi ni kiroho
5.Ugumu ni kwamba neno lake huletewa kadiri ya kusema kwao viumbe ili wapate kufahamu
6.Ndio maana kunapatikana neno iliye waziwazi na ambae ni katika mifano
7.Kauli tukufu yote sio mifano wala kauli tukufu yote sio waziwazi,na ndio maana haiwahusu isipokua wenyi akili.

41. KWELI MOJA
1.Dini iliyo kuja na manabii wote ni Usilimu,hakuna Nabii aliye tumwa na dini ingine kinyume na hii 2.Usitafautishe dini ajili ya lugha zenu wala ajili ya uwingi wa mitume yake

18

8.Na atakaye tumia dhati tukufu ya (Shaidi wa Mungu) Kalonda,hujihelekeza kwenyi Muskiti mtakatifu wa kadingila ao mlima karombwe.

11.Na kama muskiti huelekea kibla na ili hali wewe hutumia dhati tukufu ya mwengine,usikose kusali humo,pande zote ni

zake.
12.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote.

39. UTUKUFU
1.Enzi ni utukufu wa ajabu usio najisika,milki kamilifu kadiri ya uwezo wa vyote na ujuzi wa vyote
2.Ilitangulia kimuujiza kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho namna ya kukamilika
3.Utukufu wake huu ni wenyi kustaajabisha ajili ya kuzidia,ushindi katika yote,milele na milele
4.Ni mwenyi uhuru ajili ya kuenea,Mufalme anaye tawala ulimwenguni.
5.Pahala alipo hakuna mwengine,wa pekee aliye juu.
6.Kila kilicho njee ya dhati yake ni kipungufu,maana hutengana na ukamilifu
7.Na ndio maana vyote vilivyomo angani na vyote vilivyomo ukiwani ni vitu dhalili sana mbele yake,hakuna mfano wake.

3.Usilimu ndio dini aliye kuja nayo nabii Mussa,Yesu Masiya na nabii Muhamadi,na pia mitume wengine wote
4.Wote walipewa kazi ya kusilimusha watu wa dunia ambae walikua bado kujisalimisha katika mapenzi ya Mungu

Mwenyenzi
5.Kuona kama mafundisho yao ni kweli moja isiyo pingana ambae huambatana sawasawa,ndio maana wote ni katika kundi

moja yenyi kushuudia kweli moja
6.Ukweli ni mmoja,utafauti wa madini unatokana na uchache wa imani pia na uchache wa elimu,na pia vishawishi 7.Basi ondokeni gizani na ingieni wote nuruni,mukijaana na imani ya Mungu Mwenyenzi

42. MACHO
1.Uzima wa Mungu ni utukufu wa ajabu,fikara ya viumbe haizingatie ajili ya uzaifu wake
2.Hali yake hustaajabisha kadiri ya muujiza,wa pekee bila mfanano
3. Fikara ya kiumbe ndio macho inayo zingatiaka ndani yake,kisicho kua na fikara hakiwezi kuzingatia chochote 4.Na utimilifu kifikara ndio utaalamu ambae ni akili,macho izingatiaye kimwili na kiroho
5.Akili huzingatia kile ambae kiungo cha mwili kiitwacho jicho hakiwezi kuzingatia
6.Ndio maana akili humzingatia Mwenyenzi Mungu ambae macho ya kimwili haiwezi kumzingatia
7.Mutu asiye amini Mungu ni mfano wa kipofu,amekosewa akili ambae ndio macho ionaye kiroho

43. KIWE NA KINAKUWA
1.Mungu asingelikuwako kama vyote visingeli kuwako,lakini kuona kama Mungu Mwenyenzi yupo,ndio maana ulimwengu na

walimwengu hupatikana
2.Mwenyenzi ni mwenyi milki kamilifu yenyi uwezo wa kuumba
3.Mamlaka kubwa ajabu ambae huweza kufanya kila kitu bila kutumika kazi.
4.Akapenda kutokeza jambo hawezi kutumika,lakini hutoa amri: <<kiwe na mara kina kuwa kadiri ya idhini yake>> 5.Ni kwa sababu alitangulia katika mamlaka yake mwenyewe, namna ya kuenea bila upungufu wowote

6. Hali kama hiyo ndio uzima kadiri ya ukamilifu, ndani mwake hamuna upungufu wowote,Muweza na mjuzi wa yote.

7. Ukamilifu wake ndio ulio fanya atangulie kadiri ya kuenea na ndio maana amepatikana na mamlaka kubwa kadiri ya uwezo wa vyote,chemchem ya upatikanaji na maisha.

46. SAUTI YA MUNGU
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba, aliye umba tabaka la anga na tabaka la ukiwa
2.Mamlaka yote imetoka kwake,ni yeye atanguliaye kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho
3.Hasemake kama wasemavyo viumbe, kwani hana kiungo chochote dhatini mwake
4.Sauti yake hutukia kwa rafla kadiri ya idhini yake, katika jina lake,mwenyi uhuru na ushindi
5.Kauli yake ni yenyi mamlaka ya utendaji wa vyote, kusikia sauti yake ni kufanyika upya kiroho
6.Mjuzi wa kusema anaye agiza yanayo tokea,sauti ya maajabu inayo tokeza,toka sifuru, umbo za kila aina
7.Hakuna Mola mwengine anaye stahili kuabudiwa ispokua Mwenyenzi peke yake, Mjuzi na muweza aliye na uzima.

47. UDHU
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu Mtukufu asiye na doa,anaye kosoa bila kasoro.
2.Ni yeye anaye amuru kuchuma udhu kwa kila aliye silimu, wala asisali yeyote katika najisi. 3.Udhu ni yenyi sehemu mbili,kadiri ya umbile ya mwanaadamu: kimwili na kiroho. 4.Kadiri maji inavyo safisha mwili,ndivyo neno linavyo safisha roho.
5.Ndio maana hutumia maji kama mfano ili kusafisha viungo vitano vya utambuzi,kimwili.

19

44. HAKIMU

2.Ni amri kuheshimu sheria ya Mfalme wa ulimwengu ambae atahukumu vyote wala hakuna atakaye weza kuhepuka hukumu yake.

3.Haifae kwenda kinyume na kauli yake sababu hakuna wa kukusemelea utakapo hukumiwa naye.
4.Mungu ndio muweza wa vyote anaye fanya yote kadiri apendavyo, mwenyi uhuru na ushindi.
5.Kauli yake imejaa nguvu ya ushindi,atakaye itumia duniani atageuzwa roho takatifu atakapo ihama dunia. 6.Ujuzi wa Mola wenu umemfanya ainuke sana zaidi ya wote, wala hakuna mwengine mfano wake.
7.Yeye ndio chemchem ya utukufu,jihelekezeni kwake,mupate kijitekulia utukufu wa kila namna.

45. BWANA WA ULIMWENGU
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu, anaye jua yote wakati wote pasipo kisinzia wala kulala
2.Ukamilifu wake umemfanya astirike katika yote, mbali na vitenguzi vyote,milele na milele.
3.Amejua yote na ameweza kufanya yote,namna ya kuenea katika yote kinyume na upungufu wote.
4.Mwenyi mamlaka na uhuru,mtawala wa vyote katika yote,wakati wote pahali pote ulimwenguni. 5.Ameumba,amekadiria na amelea,mkamilifu anaye jitosheleza na anaye tosheleza viumbe vyote,mshindi aliye na uzima. 6.Mungu ndio Bwana wa ulimwengu,Mufalme wa milele, anaye pindukia,anaye tangulia.
7.Hakuna mwengine kama yeye ,wa miujiza aliye juu.

6.Na pia hutumia neno la Mungu ili kusafisha roho ndani ya mutu .
7. Heri mutu anaye takasa mwili na roho,maana ametakasa nafsi yake yote.
8. Atakaye kataa kuchuma udhu kimwili na akazingizia kuchuma udhu kiroho ,ni miongoni mwa wanafiki.
9. Na atakaye kataa kuchuma udhu kiroho na akazingizia kuchuma kimwili ni miongoni mwa wanafiki.
10. Ni amri kwa wasilimu wote kuchuma udhu kimwili na kiroho,maana ndio utimilifu wa umbo lao.
11. Kitenguzi cha udhu kimwili ni najisi,na kitenguzi cha udhu kiroho ni zambi.
12. Chakula halali inayo ingia ndani ya mutu haiweze kumchafua,lakini Choo ambae hutoka ndani yake ndio humchafua.
13. Iliingia ndani mwake kadiri ya utimilifu,lakini imetoka ndani mwake kadiri ya uaribifu.
14. Roho yako isifanane na mwili wako,ambae huingiza halali kwa njia ya juu,lakini baada ya kazi ndani mwake , huitoshea katika njia ya chini kadiri ya kinyume chake hali ya kua haramu.
15. Neno la Mungu ambae ndio nuru,liingie ndani mwako kupitia akili yako,baada ya kazi yake ambae ni kufuta giza,itokezwe na akili yako kadiri ilivyo ingizwa,hali ya kua utimilifu.

48. NGAO
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu, muhifadhi wa milele, anaye jengea waja wake ngao
2.Muja wa Mwenyenzi ni yule anaye tumainia Mungu zaidi ya yote na pia huogopa kutenda zambi

3.Ametoshelezwa na roho takatifu ambae humsaidia kwa idhni ya Mungu; wala hatumiake kafara ya wakaaji wa Hadeze kua ukingo

4.Shetani amewaimiza sana wafuasi wake ili wa washambulie wachamungu,kuwategea mitego mbalimbali 5.Ulinzi wa Mungu ndio wenyi nguvu na ushindi,”ngao” ya miujiza,ambae huwakinga na mizinga ya maadui 6.Kauli tukufu ya kitabu hiki inapo tamkwa kila mara huleta nguvu ya ushindi ndani mwake anaye ya tamka 7.Hakika Sala na dhikri ,saumu na wema, hujengea mutu Ngao,hawezi kuangamizwa na chochote


50. MILKI KAMILIFU

1.Milki kamilifu ndio Enzi ambae ni uzima kadiri ya umungu
2.Mwenyi kua na milki kamilifu dhatini mwake ndio Mungu Mwenyenzi
3.Yeye ndio mwenyi uwezo wa kuumba,namna ya kutokeza ambae hakikua
4.Hayo ni kwa sababu ukamilifu ni ndani mwake,ndio maana huweza yote
5.Hali yake ni muujiza na matendo yake ni maajabu,wa pekee aliye juu
6.Hakosekanake muda wowote wala hatanguliwake na yeyote ku vyovyote,mwenyi kuenea 

7.Hakika Mwenyenzi ndio mwenyi uhuru peke yake, hakuna mwengine kama yeye.

51. CHAKULA YA ROHO
1.Mungu amempenda sana anaye pupia kutubu pindi anapo dondoka
2.Mwanaadamu ni mpungufu ,anaweza kudanganyika ajili ya uzaifu asilia
3.Maisha ya dunia ni jambo dhalili, haina utimilifu ajili ya uzaifu wa mwili
4.Utimilifu kimaisha hupatikana mbinguni, kambi tukufu yenyi kujaa nuru ya taa isiyo zimika

 5.Anaye tumia urakibu ndio mzaliwa wa sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani

6.Na atumiaye uatidu ndio maskini tena mnyonge, anaye viringita gizani ,umbo la hadezeni. 

7.Tumieni neno la Mungu kadiri ya chakula ya roho, ili mupate kuishi salama milele na milele

20

49.BIDII

Mungu Mwenyenzi alimuumba mwanadamu ajili ya kumuabudu,na ndio maana ibada ni muimu maishani mwake.

2.Hapana kuacha wala kupumzika masiku kadhaa bila kumsujudia Mola wako
3.Ni amri kumuabudu kila siku, maishani mwako, mpaka mwisho wa umri wako
4.Wala usijingikiwe moyoni mwako ajili ya ibada yako ya zamani kwamba imetosha; wala usivunjike moyo ajili ya kutojibiwa 
papu kwa papu

5.Mwenyenzi hawezi kukuzulumu, kuweni yakini kwamba kila utendalo huhesabika na atakulipa kwalo 6.Usitafute sana malipo duniani ,lakini tetea kwa bidii malipo ya mbinguni ambae hudumu milele

 7.Imani ni katika tumaini ya maisha ya mbinguni,asiyekua na tumaini hana imani

52. MKAMILIFU
1.Enyi watu wa dunia! ni lazima kwenu kumuabudu Mungu Mwenyenzi aliye umba mbingu ,hadeze na dunia bila kutaabika na

kazi yoyote
2.Viumbe havikujitokeza vyenyewe sababu hukosewa uwezo wa vyote; ilibidi kupatikane mwenyi milki kamilifu ambae peke

yake huweza yote ili awatokeze wote toka sifuru.
3.Vyote ambae mumeviona na ambae hamuvione vimetoka kwake , pasipo uzima wake hakungeliumbwa chochote. 4.Mungu hafanane na viumbe kwani yeye ni Mkamilifu na viumbe vyote ni vipungufu.
5.Mkamilifu hastahili kuanza wala kukoma,hawezi kuchoka wala kushindwa,kusahau wala kujifunza...
6.Yeye ni muweza wa yote tena Mjuzi wa yote,na ndio maana ame kamilika hali ya kua na uzima .
7.Hakuna mwengine aliye nauzima ispokua Mwenyenzi peke yake

53. SALA
1.Enyi walio silimu! mumelazimishwa kusali kila siku ,asubui na mangaribi ,na pia kumtukuza mola wenu usiku na mchana.

2. Sala imeleta nguvu ya Mungu na pia humkurubisha mutu na mola wake .
3. Ni tendo bora kabisa mbele ya muumba,alama ya unyenyekevu na shukrani,ambae humpandisha mutu daraja ya kiroho.
4. Kufuta mabaya kwa mema ndio mradi wa kufunga sala.
5. Kisomo cha sura ya ufunguzi ni miongoni mwa funguo ya milango ya mbingu.
6. Kuitika uito wake na kunyenyekea dhati yake,na kukiri uzima wake kwa yakini ,ndio humaanisha kurukuu,kusujudu na kutoa shaada.
7. Kuchuma udhu na kuhelekea kibla na kusali ni kielelezo cha uchamungu,kadiri ya nakala ya maisha ya mbinguni.
8. Atakaye kataa kusali kimwili na akazingizia kusali kiroho tu ,ni miongoni mwa wanafiki.
9. Na atakaye kataa kusali kiroho na akazingizia kusali kimwili tu,ni miongoni mwa wanafiki.
10. Ni muswalina wa kweli yule anaye sali kama kawaida kimwili na kiroho na ndio mpenzi wa Mungu.
11.Usijidai kua roho tupu na ilihali uko na mwili,wala usijidai kua mwili mtupu na ilihali uko na pumzi.
12. Jihadharini na elimu kiakilia musije mukafuta alama za dini ya Mungu.

54. SHUJAA
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mtangulizi aliye kamilika tafauti na wote,mwenyi mamlaka ya milele 2.Mbingu,hadeze na dunia hupatikana kadiri ya mapenzi yake,wala hakuna upatikanaji njee ya idhni yake. 3.Shujaa mkamilifu anaye zidia kila kitu,mufalme anaye hukumu bila mipaka
4.Anaye stawi maala penyi utukufu wa ajabu,ambae kiumbe hakiwezi kukurubia
5.Wa miujiza anaye badiri majira ulimwenguni na ili hali mwenyewe habadirikake.
6.Musifuni yeye aliye mzima,chemchem ya fahamu ulimwenguni,anaye tumainiwa na wote katika mambo yote. 7.Mtukufu anaye miliki ufalme wa ulimwengu bila msaidizi wala muchoko,muweza wa kila jambo.

55. JAMBO MUIMU
1.Mwenyenzi Mungu ni baba wa wote,amelea viumbe vyote katika usawa,kiongozi mwema.

3.Tembea urakibuni namna ya kuingia nuruni,wala usitumie uatidu kamwe usije ukaingia gizani
4.Nuruni munamo kheri nyingi ajili ya kupatikana katika mapenzi ya Mungu,wala maisha haina ukomo 5.Ibada ndio <<Jambo muimu>> ku watu wote wenyi akili, wala usitumie uchawi kamwe maishani mwako. 6.Inaleta bahati ya kufikia wokovu wa roho yako.
7.Na uchawi ndio unaleta mikoshi maishani,namna ya kuangamiza nafsi kuingia hadezeni

5.Jina la kitabu hiki kitukufu ni <<UKWELI>>
6.Na inatakika kujenga Muskiti wetu maala petu, ambae watu watakua na salia wale watakao kuja kwetu. 7.Hii ni kauli tukufu kutoka kwa Mola wenu aliye Enzini,hakuna shaka ndani yake.

21

2.Ukapenda kupata msaada wake,utaupata bila shaka,lau kama utaamini na kutenda salama kama inavyo andikwa katika vitabu vyake

56. JINA YA KITABU
1. Ewe.Kalonda! ni mimi Mungu wako,nimekupasha ya kama hawata kukamata wala hawata kusuluhu kadiri wanavyo kusudia 2.Amka, na uvuke ngambo ya mtoni,nenda zako; maana makafiri(wanao taka kukusulubisha) wanakaribia;
3 .Kuona kama wao wamekutizama kwenyi T.V. sisi tumekupatia redio: yote watakao zungumuza juu yako utakua na sikia. 4.Inafaa kupata buku kabambi ya kuandikia maneno yote pamoja

57. FAIDA
1.Utakatifu ni wake Mwenyenzi aliye huru juu na chini, wa pekee asiye lingana na yeyote
2.M'bora wa kukadiria anaye tokeza kila umbo na faida yake kubwa,wala hakuna umbo isiyo kua na mafaa
3.Kile kisicho kua na faida katika maisha ya uyu kinayo faida kubwa katika maisha ya yule.
4.Ni kwa sababu kila kile kilifanyika na Mjuzi aliye na busara kamilifu
5.Haifai kulaumu chochote wala lolote ambae Mwenyenzi kalifanya,hafanyi ispokua yanayo stahili kabisa, lakini wanaadamu

hawafahamu
6.Lau kama wangeli fahamu faida ya kuumbwa kwa kila umbo, bila shaka wangelimuogopa Mungu na kumsifu na

kumshukuru
7.Na ijapokua uchafu ambae hutokea ndani ya kiumbe, na ijapokua kuumbwa kwa Shetani ambae ni simamizi la ubaya; maana

dunia isingelipatikana pasipo ubaya na uzuri kupatikana 58. KAWAIDA

1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu Mjuzi wa kuumba ,anaye kadiria kila mwanahewa fikara ya sawa na maisha yake 2.Fikara yao huwatosheleza katika utetezi wao,kulingana na umbo zao
3.Na ndio maana maitaji yao ni tafauti ajili ya utafauti wa umbile zao,kila yule hufanya shuruli ya namna yake 4.Mungu peke yake ndio anaye jua mradi wa kuumbwa kwa kila kiumbe

5.Hakupendelea yeyote pasipo haki,bali vyote hufanyika katika kawaida la umbiko

6.Atakaye kanusha ujumbe huu sio ila kafiri mkuu, wala hawata nusurika wale wanao husudu, wata rundikwa hadezeni sababu ya kuipinga haki

7.Heri mutu anaye amini kweli hii ambae hupata yakini ya uzima wa Mungu,na kufunika mabaya kwa mema,miguu urakibuni siku zote. 59. ChUKI

1.Ametakasika sana na zaidi yule aliye umba mbingu na dunia kwa kauli yake tukufu
2.Mjuzi wa kukadiria ,anaye jaalia waja wake neema ya kila namna
3.Atakaye vizia kunyanganya ao kuvruga neema aliye pewa mwenziwe,ukomo wake ni hadezeni 4.Mushirikina aliye na elimu ya Nyota anaye zingizia kutabiri ni sawa na wafumu wengine wote. 5.Wao wote wametumia wakaaji wa zimuni,ndio maana wanayo kazi moja ya kurogana. 6.Utazani ameombeana kumbi amerogana,na utazani muaminifu kumbi muovu mkuu.
7.Chuki imejaa moyoni mwake,wala hawatakie wenziwe amani kamwe.

60. TAMAA YA DUNIA
1.Nani aliye pumbafu kuliko yule anaye taabikia maisha ya dunia peke yake?

2.Utamuona ametamania kila kitu, hashukuru wala hatosheke
3.Mizimu anayo sharikiana nayo humzidishia wasiwasi ili kuivruga zamiri yake
4.Ni kwa sababu amekaribiza wakaaji wa hadeze ndani mwake ndio maana amechafuka 5.Ame helekezwa upande ambae mwenyewe kautarajia.
6.Atakaye kataa neno la Mungu ajili ya kuipenda sana dunia, amepotea mbali na njia. 7.Tumaini ya Mungu peke yake moyoni ndio matumizi ya njia iliyo nyooka.

61. NIA
1.Shukrani ,sifa na heshima humustahili Mwenyenzi Mungu pekeyake,mlinzi mwema 2.Atakaye penda kuona utukufu wa Mungu maishani mwake basi afanye "Nia" 3.Hatua ya kumtegemea na kumtumikia Mungu maisha yako yote
4.Na kua na desturi ya kuamuka usiku kwa kufanya ibada.

5.Kumtukuza katika kisomo na dhikri kwa wingi pia na maombi katika mpango maalumu
6.Mola wa ulimwengu atajitukuza kwake na kumupatia zawadi ya kiroho
7.Na bila shaka atazingatia bayana utukufu wa Muumbaji wake; hakuna mwengine aliye na uwezo kama yeye.

62. MWENYE KITI
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu bingwa (Mshindi) aliye huru kufanya yote anayo penda katika ulimwengu 2.Ni yeye anaye miliki falme zote,utupu wa Enzi,kinyume na uzaifu wa aina zote
3.Anacho kishika hujaa nguvu ,na anacho kiacha hukosa nguvu
4.Yeye ndio yote katika yote,”mwenyi kiti”,anaye simamia jumla ya viumbe .
5.Mkaguzi wa mambo yote, anaye endelesha na anaye komesha maisha ya viumbe
6.Ameinuka juu zaidi ya kila kitu ,wa pekee anaye stahili kuabudiwa
7.Bwana wa mabwana ,mwenyi uwezo wa kuenea, wa miujiza aliye juu.

63. NUSRA
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu muweza na mujuzi anaye kamilika peke yake ulimwenguni 2.Mganga mkuu,anaye ponya kila magonjwa kwa kauli yake tukufu
3.Neno la Mungu ndio dawa kubwa,yenyi kutibu magonjwaya mwili na ya roho.
4.Umungu ndio nusra ya walimwengu, mamlaka ya ajabu inayo okoa na shari ya kila namna 5.Kamanda wa majeshi anaye irikisha warozi kwa kauli yake tukufu
6.Kisomo kitukufu na dhikri ni miongoni mwa silaha za nuru ambae huteketeza falme za giza 7.Someni kwa wingi aya za kitabu cha "UKWELI", ili mupate kupokea zawadi ya kiroho.

22

64. MTATUZI
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu Mshindi aliye na utasi juu ya yote,anaye tokeza na anaye angaza
2.Uzima wake husababisha upatikanaji wa viumbe vyote, na kuvilinda
3.Ni yeye aondoaye dhiki, atatuaye utata wa kila aina angani na ukiwani
4.Ombeni msaada kwake yeye aliye na uwezo wa vyote ,magumu ya aina yote hukomeshwa naye kwa idhni bila kutaabika na

kazi yoyote
5.Mlinzi mwema anaye tarajiwa na wote, tajiri wa vyote, anaye tosheleza katika shida zote, mwingi wa rehema na mwingi wa

ukarimu
6. Heri mutu anaye mtegemea Mwenyenzi peke yake bila kumchanganya na chochote 7.Hakuna mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki kama yeye,mwokozi aliye juu

65. TAA ISIYO ZIMIKA

1.Mwenyenzi ametakasika sana na zaidi , amestawi mbali na uchafu wa aina yote;
2.Enzi yake ni tafauti na kila kitu, uwezo wa kuenea
3.Hakuna kunajisika kwake aliye kamilika; mamlaka ya milele pasipo mabadiriko yoyote
4.Mwenyenzi ni kiongozi mwenyi busara kamilifu, anaye jua yasiyo fahamika na yeyote
5.M'bora wa kukadiria anaye fanya yote katika usawa , hakuna kisicho kua sawa miongoni mwa alivyo viumba 6.Watu hawamzingatie Muumba wao ajili ya kuzorota kwa pumzi yao mwilini

7.Mungu ndio Bwana wa mabwana,taa ya ulimwengu inayo angazia bila kufifia wala kuzimika milele na milele 66. KIFO

1.Ametakasika sana Mwenyenzi Mungu M'barikiaji,anaye tawala maala pote ulimwenguni 2.Mbingu na dunia hushangilia jina lake, wa milele mwenyi sifa kamilifu
3.Hasahau chochote wala hashindwe na chochote wala hakuna wa kumzidia kwa lolote 4.M'badirishaji wa majira,anaye geuza umbo ya mwanaadamu baada ya kufa kwake

5.Kifo cha mutu sio mwisho wa maisha ya mutuangani lakini ukiwani,maana ni mtengano wa mwili na pumzi 6.Pumzi ya mutu hufanyika roho urakibuni ama muzimu uatiduni,na mwili wake ndio hukoma baada ya kifo 7.Na hiyo siku ya kiyama ndio ukomo wa Shetani na mizimu,isipokua malaïka na roho ndio watakao kua hai

8.Kuzila neno la Mungu ndio kufa kiroho;maana pumzi yako sio mtotowa roho,bali mtoto wa muzimu. 9.Tumieni neno la Mungu katika kawaida yake ili mupate kurithi ufalme wa mbinguni.

67. UFUFU KO
1.Sema : kufufua wafu ni jambo raisi sana kwa Mungu Mwenyenzi, atakapo idhinia itafanyika kwa rafla kadiri ya idhni

(mapenzi)yake
2.Kutokeza toka sifuru ndio jambo kubwa ajabu lakini kurudishia kitu hali yake ya zamani sio jambo ngumu zaidi ya kuumba

3.Kwa nini makafiri wamefanya ubishi kuhusu habari ya ufufuko? aliye na uwezo wa kuumba atashindwaje

kukiamusha tena alicho kilaza?
4.Hiyo siku ya kiyama kila nasfi itaonja mauti,ispokua dhati yake tu ndio itakayo bakia, maana Mwenyenzi peke yake ndio

mkamilifu
5.Na punde kidogo,ndipo atakapo fufua wote ili kutenganisha adili na batili.
6.Uwezo wa Mungu ni wa ajabu sana,wala yeye hatumikake kazi kwa kutenda jambo
7.Atakavyo hutukia kwa rafla kadiri ya idhini yake,m'bora wa kuumba
8.Mutu anaye didimia katika zambi,akaamini na kutubu,tendo hili ni ufufuko kiroho
9.Amezaliwa upya maana alikua amekwisha fariki kiroho,mfano wa mauti inayo puliziwa pumzi ya uhai.

ndio kawaida ya neno la Mungu 69. DINI YA UWONGO

1.Ondokeni wote katika ma dini ya uwongo na njooni wote katika usilimu,dini ya kweli ya Mungu Mwenyenzi 2.Dini ya uwongo yote huletewa na mitume wa uwongo,ambae hujidai utume na ili hali hawakutumwa na Mungu 3.Watu hawa ndio waovu wakuu ambae wamekwisha chagua Hadeze(Jahanamu) kua makao yao ya milele 4.Wamepoteza watu wengi na uwongo wao ambae hupinga kweli ya Mungu:

23

68. KAWAIDA YA NENO
1.Mwenyi uzima ni mmoja na dini yake ni moja,wala hakutaanza dini mupya njee ya Usilimu maana hakuta tokea Mungu

mwengine
2.Na yule atakaye silimu kiisha akajipatia dini ingine ambae hutoka njee ya kauli tukufu yeye sio ila mnafiki
3.Amedanganya kusilimu na ili hali hana imani.
4.Mwenyi imani hawezi kukataa mafundisho ya Mitume ya Mungu
5.Tumieni neno la Mungu maishani katika usawa,enyi walio silimu; hakika maisha pasipo neno la Mungu ni hasara kubwa 6.Ma Nabii na Mitume ndio wengi lakini dini ya Mungu sio nyingi bali moja tu.
7.Kuishi katika kawaida ya neno la Mungu ndio kuishi katika dini ya Mungu.
8.Kuchinja, kutokula haramu na kutovunja amri ya Mungu na kadhalika ni katika mwili na katika roho sio kimwili tu wala sio

kiroho tu
9.Na vivihivyo pia kuhusu Hija, ibada hii inayo tafsiri yake kiroho, ni amri kwa watu wote kuitimiliza kimwili na kiroho pia:

5. Bahadhi miongoni mwao humpachika mtume wa Mungu daraja ya umungu, na wengine husema kuna wa Mungu wengi 6.Na wengine humkanusha Nabii aliye pewa Qur'ani, na wengine hukanusha mbingu na hadeze,na hukanusha siku ya Kiyama 7.Hakika ni muimu kuchunguza kauli yao na matendo yao pia ili mupate kugundua hakika ya roho zao.

70. JAMAA MOJA
1. Kuamini Mitume mbalimbali walio tumwa katika ma umati mbalimbali kusiwatenganishe,hakika wote walitumwa na

Mumgu mmoja
2. Miongoni mwao hakuna aliye na dini yake, lakini wote ni katika dini moja ya Usilimu

3.Mungu hakuwapa Mitume ispokua kazi ya kusilimusha watu wa dunia, yaani kuwaingiza katika usilimu, dini ya Mungu Mwenyenzi

4.Atakaye kataa kusilimu ndio anaye kataa kujumuika katika dini ya Mungu
5.Jihadharini na manabii wa uwongo,ambao huwaondoa watu wa dunia katika njia na kuwapoteza mbali sana. 6.Mbinguni hakuna mtengano wowote lakini umoja,wamejaa upendo wa ajabu

7.Watu wote wanao muamini Mungu Mwenyenzi peke yake na Mitume wake wote ndio wandugu wa kiroho, jamaa moja la mbinguni.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kitabu cha ukweli - Mlango wa saba : "KAULI TUKUFU"

Kitabu cha ukweli - Mlango Wa pili "ENZI TUKUFU"

MWANDISHI WA KITABU: