Kitabu cha ukweli - Mlango wa ine: "CHEM CHEM"
MULANGO WA INE :
CHEM CHEM
[ 1 ]
1 . Ametakasika Mwenyenzi Mungu, aliye tangulia bila kuanza ajili ya kukamilika.
2. Ni mwenyi kuenea katika yote tafauti na upungufu wote.
3. Amejaa milki kamilifu ambae huweza yote na hujua yote.
4. Mamlaka kubwa ajabu ya utendaji wa vyote yenyi kuongoza ulimwengu.
5. Bila yeye kutangulia (kupatikana) hakungeli patikana chochote, ndio maana ameitwa"chemchem"ya upatikanaji wote na maisha yote..
6. Mwanzo wa vyote, kadiri ya milki ichipuayo kadiri ya taa iangazayo.
7. Hakika ametukuzika sana Mwenyenzi Mungu, mzima peke yake ulimwenguni.
(2)
1. Mwenyenzi ni mtawala wa wote pahali pote, bwana wa majeshi asiye jumuika angani wala ukiwani.
2. Kutojumuika katika upungufu sio kukosekana, hayo husababishwa na ukamilifu wake.
3. Mkamilifu hastahili kuchangikana na wapungufu asiye kunajisika.
4. Hali yake hii tukufu hutokana na ukubwa wa daraja yake, bwana wa mabwana.
5. Ndio maana hazingatiwe katika upungufu sababu ya kutojumuika humo wala kufanana na chochote.
6. Kadiri hewa inavyo zingatiwa
kwa vitimbi vyake, ndivyo pia enzi inavyo zingatiwa kwa matendo yake.
7. Hakika Mungu Mwenyenzi ni mkubwa sana mwenyi mamlaka ya ajabu,mtakatifu asiye najisika.
(3)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, wa pekee anaye jumuisha pasipo kujumuika.
2. Mkombozi anaye fungua waja wake kutokana na vifungo vya shetani.
3. Na kuwajaza afya kimwili na kiroho ,na kuwaingiza katika bustani ya neema.
4. Mtukuzeni Mola aliye umba kila kitu, chemchem ya nuru ulimwenguni.
5. Hakuna aliye juu yake, muheshimiwa,anaye stahili kupelekewa shukrani zote.
6. Mumilki aliye imara na daima katika tendo kua kadiri ya uzima kinyume na maisha.
7. Hakuna aliko tokea wala anako endea ,mtangulizi kadiri ya mwanzo wa vyote, mwenyi kuenea.
(4)
1. Enyi wanaadamu, abuduni wote Mola wa ulimwengu aliye enzini.
2. Wala usiweke kiumbe pa fasi ya muumba wako.
3. Wala usifanye zihaka katika ibada usije ukaangamia.
4. Wala kuimba na kucheza sio kusali, wala mlio wa vyombo vya mziki sio dhikri.
5. Kila ibada iko na kawaida yake ambae Mola wenu kawafunzeni.
6. Kumsifu Mungu katika nyimbo ni jambo nzuri sana, lakini iko na fasi yake pia na wakati wake, katika mpango maalumu.
7. Watu wasio abudu vilivyo ni wale wasio amini vilivyo wameamini sehemu na wamepinga sehemu ya ujumbe wa Mola wao.
(5)
1. Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu, mkamilifu, anaye miliki vyote ulimwenguni.
2. Vyote huanzishwa naye na vyote hukomeshwa naye.
3. Ni yeye peke yake anaye jua sababu ya kuumbwa kwa kila kiumbe.
4. Kumbi usimlaumu mola wako ajili ya kuumba kiumbe fulani.
5. Hakuna ukamilifu katika umbiko : kama uyu ni chukizo maishani mwako, nawe pia ni chukizo maishani mwa wengine.
6. Hayo hutokana na asili ya umbiko ambae ni upungufu, lakini Mungu aliwawekeeni silaha ya kuchora nayo upungufu.
7. Silaha hiyo ya nuru ndio neno la Mungu, ambae huchora pumzi kadiri ya roho takatifu.
(6)
1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, mjuzi wa kila kuumba.
2 Mwingi wa huruma anaye samehe watumishi wake kadiri ya toba zao.
3. Heri Mutu anaye acha makosa yake bila kuirudilia tena.
4. Jitihada ya kujenga imani itawale maisha yote.
5. Sala na dhikri ifanyike kila siku popote ulipo ,ili nafsi yako ijae nuru ya Mungu.
6. Mola wenu ametosheleza haja ya kila kiumbe wala hakuna msaada badala yake.
7. Mungu wa miujiza anaye tenda kwa idhni : mumilki na mshindi aliye na uzima.
[ 7 ]
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mwokozi, anaye jaa mamlaka ya kila namna.
2. Kauli yake imeokoa wote wanao itumia kama dira ya maisha.
3. Zoezi ya kuisoma kauli yake hii kila mara kadiri ya dhikri inaleta heri ya kila namna kufatana na manuizi.
4. Hakika amefaulu kabisa mutu anaye hifadhi moyoni mwake sura na aya kadhaa ambae huisoma kila mara.
5. Ujumbe wake ndio nuru kubwa ambae huondoa ujinga unao tokana na vitimbi vya shetani.
6. Nuru yake ni elimu ambae huteketeza ujinga, ndio maana ni sharti kutumia neno lake ili mupate kuzingatia bayana uzima
wake.
7. Hakuna kimbilio ingine badala yake, bwana wa majeshi anaye miliki vitu vyote.
(8)
1. Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu, mlinzi mwema, anaye tosheleza haja zote wakati wote.
2. Pasipo msaada wake hakuna ambae angeli okolewa,Mola wa karne na karne,muhifadhi wa milele.
3. Ametenda yote kwa idhni yake, wala hazaufike kwa kufanya shuruli yoyote.
4. Milki yake ni juu ya vitu vyote, hakuna mfano wake wala Diko mwenzake,wala jerani yake.
5. Amestawi milele kiushindi tafauti na kuishi, m'bora wa kuenea kadiri ya uzima.
6. Hana mwanzo wala mwisho, wa pekee anaye kamilika.
7. Hakika utukufu wote unamustahili yeye peke yake, wala hakuna mwengine kama yeye,wa muujiza aliye juu.
(9)
1. Enyi wanaadamu ! ,ingieni wote katika dini ya Mungu.
2. usilimu ndio usalama wa nafsi katika mapenzi ya Mungu.
3. Atakaye kataa kusilimu amekataa kuingia katika dini ya Mungu.
4. Hatua ya kwanza katika usilimu ni shaada.
5. Kukiri moyoni na kushaidilia waziwazi kwamba Mungu Mwenyenzi ni m'moja tu,hakuna mwengine kama yeye.
6.Na hatua ya pili ni kupokea ujumbe wake wote na kuutumia maishani.
7. Mwenyenzi ndio mkamilifu anaye tawala angani na ukiwani, baba wa salama aliye salama milele na milele.
(10)
1. Amejaa utukufu Mwenyenzi Mungu,mkamilifu anaye jitenga na upungufu wote.
2. Kutenda kwake sio sawa na kutenda kwao viumbe. Hawa hutenda kizaifu na yeye hutenda kimilki.
3. Kwa wao kuzingatia uzima wa Mungu ilibidi wa pewe ujumbe wake kadiri ya kusema kwao.
4. Matendo yote ya viumbe ni katika upungufu, hayapatikane kamwe katika ukamilifu.
5. Kama kutenda kwake hufananishwa sio ila namna ya kusikilizisha ili mupate kutimilika.
6. Kuona kama lugha ni umbo, ndio maana hakuna lugha ya Mungu.
7. Na kama Mungu Angeli kua na lugha fulani bila shaka angeli kua na umbo fulani, lakini mtukufu wa daraja amejitenga mbali na uzaifu huo.2. Mtukufu wa kauli anaye jaa milki kamilifu ambae huongoza wote kwa njia ya neno lake.
3. Ole wao wanafiki wanao geuzageuza neno la Mungu, wamefikia hata kubadiri maana ya andiko kwa kuzingizia tafsiri ya kiroho.
4. Hafahamu mambo ya kiroho ispokua aliye jazwa roho takatifu.
5. Tafsiri ya neno la Mungu pasipo ufunuo ni uwongo mtupu.
6. Wameangamia wote wanao jidai unabii pia na utume kwa ugumu wa nyoyo zao na ilihali hawakufunuliwa na Mungu.
7. Tumieni wote kweli yake hii na hekima : musiongeze wala musipunguze.
(12)
1 .Mwenyenzi Mungu ndio mufalme wa siku ya kiyama,hakuta bakia ispokua Enzi tukufu peke yake.
2. Nani anaye kanusha matukio ya kiyama ? Hakika ni upumbafu kushakia kauli ya mjuzi wa yote.
3. Mungu ndio mkweli wa kauli,hasemi ispokua ukweli peke yake.
4. Siku hiyo Mwenyenzi atawafufua wote wapumuao baada ya kuwauwa.
5. Kufufua sio tendo la ajabu kuzidia kuumba:hakuna kigumu kwake yeye aliye na milki kamilifu.
6. Atakapo idhinia jambo ndipo hutukia kwa rafla jambo hiyo sambamba na idhni yake.
7. Siku hiyo ndio siku ya malipo kila mutu atavuna yale ambae alipanda.
(13)
1. Tumsifu Mungu aliye na ujuzi wa kuumba, mufalme wa ajabu tafauti sana na kila kitu.
2. Kutokeza toka sifuru ni tendo la ajabu ambae hufanyika na mwenyi ukamilifu.
3. Mpungufu hana uwezo wala fahamu ya kutokeza toka sifuru sababu amekumbwa na uzaifu mkubwa.
4. Heri Mutu anaye nyenyekea mbele ya muumbaji wa pumzi na mwili.
5. Hakika mamlaka yake ni kubwa zaidi ambae hutenda kwa idhni bila kutumika kazi.
6. Ombeni yote kwake mumilki, utapewa kwa wingi bila hesabu,kimwili ao kiroho.
7. Mwenyenzi ndio tajiri wa vyote, mwenyi uwezo wa vyote, hakuna mwengine kama yeye.
(14)
1. Mwenyenzi Mungu ndio mufalme wa ajabu anaye zidia wote ulimwenguni.
2. Hakuna mfano wake popote kwani yeye tu ndio mkamilifu wengine wote ni wa pungufu.
3. Ole kwao wapumbafu ambae humlinganisha muumba na kiumbe fulani.
4. Hakika anaye muita mjumbe wa Mungu kua ndio Mungu wake ni sawa na kafiri anaye abudu sanamu.
5. Mungu hagusanake na umbo yoyote wala hageukake hali wala hapumuake hewa.
6. Ukamilifu wake humtenganisha na kila kitu, hawezi kujumuika mbinguni wala hadezeni wala duniani.
7. Kwa yeye kuketi maala fulani inabidi vyote vilio kutwa huko vipotee namna ya kukosekana, maana milki yake kamilifu
hufuta upungufu wote kandokando yake.
(15)
1. Uzima wa Mungu ni muujiza wa maajabu : ametangulia kimuujiza na ameumba kwa maajabu.
2.. Mola anaye stawi katika dhati yake mwenyewe hali ya kua Mwenyenzi.
3. Ukaona kiumbe kinacho ishi mbinguni kiumbe hicho ni mwanahewa_halisi.
4. Na kinacho ishi duniani bila shaka nimwanahewa_haramu.
5. Na vivihivyo pia kinacho ishi hadezeni ni mwanahewa_haramu.
6. Usilinganishe umbo yoyote na Mola wa ulimwengu ,hafanane na yeyote wala chochote.
7. Hakika mola wenu ni tafauti sana na kila kitu : yeye ni mkamilifu na wengine wote ni wapungufu.
(16)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, chemchem ya baraka ambae hupatiana sifa na heshima kwa amtakaye.
2. Usiku ni wake na mchana ni wake, ameona muda wote pahali pote, wala hapitiwake na chochote.
3. Uhai na kifo hutokea kwake, ni yeye anaye fufua wafu kwa neno litokalo kwake na kumjaza roho takatifu amtakaye.
4.. Hakuna mwengine kama yeye ,muumba wa anga na ukiwa atawalaye Milele na milele.
5. Ombeni idhni ya Mwenyenzi ipate hufanyika maishani mwenu.
6. Hakika idhni yake juu ya jambo fulani, ni utimilifu wa jambo hiyo.
7. Ee Mola wangu ! Unizidishie elimu,na unizidishie nuru na unizidishie riziki,yote kadiri ya idhni yako.
(17)
1. Mwenyenzi Mungu ndio taa ya ulimwengu, mjuzi wa mambo yote.
2. Ndiye msimamizi wa kila kitu, mwenyi mamlaka isiyo pungua wala kuongezeka ajili ya kuenea.
3. Muanzishaji na mkomeshaji ,aliye pasipo yeyote milele na milele.
4. Ole wake yule asiye zingatia uzima wa Mola wake.
5. Tumieni utaalamu kifikara ili upate kuzingatia njee ya mwili.
6. Akili ndio macho ya kiumbe ambae huzingatia kiroho
7. Yeyote asiye zingatia kiroho hana akili ndio maana hana imani.
(18)
1. Utakatifu ni wake Mwenyenzi Mungu, mfariji,anaye ruzuku kila kiumbe.
2. Mungu wa miujiza anaye tenda kwa maajabu.
3. Mlinzi mwema anaye tosheleza haja za waja wake, anaye rehemu na anaye kirimu.
4. Alikua, yuko na atakua,mwenyi kuenea.
5. Mtukufu afanyaye apendavyo,hakuna wa kumsambisha wala wa kumuhukumu.
6. Upende haupende upo chini ya mamlaka yake, mteza nguvu, aliye na uwezo wa kuenea.
7.. Bingwa wa mabingwa anaye miliki falme zote ulimwenguni, wa pekee aliye juu.
(19)
1.Shukrani kwa Mwenyenzi Mungu, mpanaji wa pumzi, anaye kadirisha maisha ya kila kiumbe.
2. Umri ni zawadi kutoka kwake yeye anaye patikanisha kwa idhni bila kutaabika na kazi.
3. Hakuna mbele yake wala nyuma yake, mtangulizi wa milele.
4. Tajiri wa vyote, anaye pagaa watumishi wake mafuta ya kiroho na kuwapandisha katika daraja.
5. Chemchem ya nuru ambae humulika ulimwenguni.
6. Hana baba wala mama,si mwanaume wala si mwanamuke, hana ukoo wala Kabila ...
7. Hafanane na yeyote maana yeye ndio mkamilifu wengine wote ni wapungufu.
(20)
1. Mwenyenzi Mungu ni uzima kadiri ya ukamilifu.
2. Mamlaka yenyi kuenea katika yote itokezayo kwa idhni ambae hakikuwa popote.
3. Dhati yake ni uwezo wa vyote, namna ya kuenea katika yote.
4. Mtukufu wa ajabu asiye kurubiwa na uzaifu wowote, Mutakatifu aliye peke yake enzini.
5.Hakuna mwengine kama yeye ,mzima, anaye tangulia katika yote imara na daima.
6.. Mumilki wa anga na ukiwa, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.
7. Mola wa pekee anaye stahili kuabudiwa, mwenyi milki kamilifu, anaye kirimu wanahewa wote na wazila hewa wote.
(21)
1. Kitabu hiki ni ufunuo kutoka mbinguni, ukweli usio na shaka.
2. Maneno yake huletewa na malaika saba,kila yule na ujumbe ambae hujenga kweli moja.
3. Mungu amefanya mawasiliano baina ya mbingu na dunia katika dhati yangu nipate kua muonyaji.
4. Uchoraji wa pumzi ufanyike katika maunganio ya anga na ukiwa ili mutu apate utimilifu.
5. Yeyote atakaye tumia kauli tukufu ya kitabu hiki pumzi yake itafanyika roho takatifu.
6. Kuzingatia uzima wa Mungu ndio kumuona Mungu, yeye hazingatiwe kimwili sababu hana mwili.
7. Mwili ni umbo zaifu sana, ujinga mtupu, kadiri ya uchafu ambae haumkurubie kamwe mtukufu aliye enzini.
63
(22)
1. Shukrani yote inamustahili Mwenyenzi Mungu, mkamilifu, anaye chagua miongoni mwa watumishi wake na kumtuma
amtakaye.
2. Masingizio na mazarau ya makafiri na wanafiki haiwezi kubadiri chochote katika neema ya Mungu iliye juu ya shahidi wake.
3. Yule ambae Mungu amemtukuza ,hakuna atakaye weza kumzalalisha.
4. Na yule ambae Mungu amemzalalisha hakuna atakaye weza kumtukuza.5. Kinacho tatiza watu sana ni chuki na kiburi, hawataki kavumu ya mutu mwengine.
6. Ole wao makafiri na wanafiki wanao wa tungia uwongo mitume, hakika hadeze ndio makao yao,humo itakua ni kilio na kusaga meno.
7. Heri wanyenyekevu wanao pokea ujumbe kwa furaha, hakika wao ndio vyombo halisi vya mchoraji ,watarithi bustani ya neema kwa kishangwe.
(23)
1. Neno la Mungu ni mfano wa maji safi,na ibada ni mfano wa matumizi yake.
2. Uchafu wa shetani ambae hujaribu kunajisi watumishi wake hutakaswa na neno la Mungu katika ibada.
3. Tegemeeni kwa Mola wenu katika shida yote, hakika hakufanyike lolote ispokua kwa idhni yake.
4. Kuto kua urakibuni pia na kukosa tumaini ya Mungu ndio mambo ambae hutenganisha watu na karama ya Mola wao
5. Neno la Mungu ni kinga na utajiri maishani,jikingeni kwa kuisoma aya zake kwa wingi.
6. Na itumieni aya zake kama chakula pia silaha ya kuteketeza falme za giza zinazo taka kujiinua.
7. Kauli tukufu ya kitabu hiki imeleta nguvu na ushindi kwa yule anaye isoma kila mara.
(24)
1. Mwenyenzi Mungu ndio tumaini la walimwengu ambae hulea viumbe vyote kwa usawa.
2. Ni amri kumuabudu kila siku asubui na jioni na kumtukuza usiku na mchana.
3. Wanafiki wameabudu kwa udanganyifu na ilihali moyoni hakuna hata chembe ya imani.
4. Abuduni Mungu kwa moyo wako wote na nia ya kupata wokovu hiyo siku ya mwisho.
5. Uwe katika usalama ama katika magumu,simama imara, usibadirike sababu ya vitimbi vya dunia.
6. Mola wako atakuvika taji la utukufu,na kukuweka katika kundi ya walio heshimishwa.
7. Tumainia Mungu peke yake katika shida zote ,wala usimchanganye na yeyote wala chochote
(25)
1. Mwenyi enzi ni tafauti sana na kila kitu, hakuna mfano wake popote ulimwenguni.
2. Yeye sio umbo maana kila kilicho umbwa ni kipungufu.
3. Amepatikana kadiri ya kuenea, mtukufu anaye zidia wote kwa jumla.
4. Mshindi anaye kamilika bila mwanzo wala mwisho.
5. Ukamilifu umetokana na Enzi ambae ni uwezo wa vyote na pia ujuzi wa vyote.
6. Kuweza yote na kujua yote ndio kumiliki vyote.
7. Hakika Mwenyenzi Mungu ni mshindi juu ya kila kitu ,mufalme wa ulimwengu.
(26)
1. Uzima ni wake Mwenyenzi Mungu, mtukufu anaye kamilika milele.
2. Mola ndio mwanzo wa vyote, chemchem ya kila fahamu.
3. Mfano wa taa ya ulimwengu, mwenyi kujua yote.
4. Elimu yote hutokea kwake, anaye patikanisha na anaye kosekanisha.
5. Usimlaumu mola wako kwa lolote yeye anaye kamilika katika busara.
6. Hauzingatie chochote ispokua kwa ruhusa yake.
7. Mola wa miujiza anaye jaa mamlaka ,hakuna mwengine kama yeye,wa pekee aliye juu.
(27)
1. Enyi wanaadamu ! Aminini Mungu ukweli wa kuamini.
2. Kua na imani ni kua katika mapenzi ya Mungu.
3.Kutumia maamrisho yake na kujitenga mbali na makatazo yake.
4. Mungu amewaalikeni wote katika nuru yake ndani ya dini yake.
5. Mujichugulie fadhila nyingi kutoka kwa Mola wenu.
6.. Mungu ndio tajiri wa vyote anaye ruzuku wanahewa wote, hakuna maisha pasipo msaada wake.
7. Hakika mwokozi ni Mungu peke yake, wala hakuna mwengine kama yeye wa milele aliye juu.
(28)
1. Ujuzi ndio chemchem ya umbiko ulimwenguni.
2. Mjuzi ndio mtokezaji wa kila umbo, la wazi na la siri,kadiri ya mwanzo wa vyote.
3. Hakuna kisicho kua chake,angani na ukiwani, tajiri wa vyote, m'bora wa kuumba.
4. Ni yeye aliye kutwa hapo awali tayari amekwisha Tangulia bila msaada wa yeyote.
5. Mwenyi uzima, anaye jaa milki kamilifu, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.
6. Amepatikana kadiri ya kuenea bila maanzio wala makomeo,jalali ulimwenguni.
7. Hakika Mungu ni mkubwa sana, tegemeo na kimbilio la wa silimu.
(29)
64
1. Sauti ya Mungu ni yenyi mamlaka ya ajabu, yenyi kutimiliza kwa rafla jambo anaye idhinia.
2. Mungu hasemake kifikara Bali yeye husema kiujuzi,hali ya kuenea katika fahamu.
3. Kusikia sauti ya Mungu ni neema ya kukutana na wokovu.
4. Ametakasika kabisa yule aliye msikia Mola wake ,maana ameingia katika nuru yake.
5. Mutu anaye sema na Mungu ni mwenyi kuinukia;laiti mungeli muzingatia Nabii Mussa.
6. Kuzungumuza naye ndio kukurubishwa sana naye, zaidi ya wengine wote.
7. Amejumuika katika sehemu ya kwanza ya bahadhi la juu angani.
(30)
1. Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu, hakimu mkamilifu.
2. Mtukufu anaye tenganisha adili na batili pasipo kasoro.
3. Ni yeye atakaye ingiza makafiri hadezeni na kuwakosekanisha baadaye.
4. Na ni yeye atakaye waingiza waaminifu mbinguni na kuwapatia maisha ya milele.
5. Amekufuru yeyote anaye kanusha moto wa jahanamu,bila shaka hadezeni ndio motoni.
6. Kadiri moto unavyo poteza kuni,ndivyo pia hadeze inavyo poteza umbo.
7. Hakika sifa zote zina mustahiki Mwenyenzi Mungu ,muumba wa viumbe vyote.
(31)
1. Mungu amestawi juu sana mbali na viumbe vyote, hakuna jerani yake.
2. Ukamilifu wake umemtenganisha kabisa na upungufu wa aina yote.
3. Ametangulia kadiri ya kuenea, hakuna alipo anzia wala alipo komea.
4. Enzi yake imewaka na kurarua upungufu wa aina yote kandokando yake.
5. Mamlaka yake imetawala pahali pote ulimwenguni, wala hatumikake kazi kwa kutenda.
6. Mapenzi yake hutosheleza kiutendaji,hodari aliye na starehe ya ajabu.
7. Hakuna Mola mwengine kama yeye,mwokozi, anaye rehemu na anaye kirimu.
(32)
1. Aliye arshini haonekanake kimwili sababu ya kutokua na mwili.
65
2. Macho ya kimwili hayazingatie ispokua miili peke yake.
3. Kumbi usitumie macho ya mwili wako kwa kutaka kumuona kimwili sababu yeye hana mwili wala pumzi.
4. Mutu hawezi kumuona Mungu kimwili , Mola wenu ni tafauti kabisa na umbo zote ,wa pekee aliye enzini.
5. Mungu hana mwili wala pumzi, na ndio maana haiwezekane kumuona ana kwa ana maana yeye ni wa pekee.
6. Kukosa mwili na pumzi sio kukosekana Bali kuko hali ingine tukufu ajabu tafauti kabisa na umbiko,inayo itwa Enzi kadiri ya
uzima wake Mungu.
7. Ni kawaida kumtazama Mungu kiroho ili upate kuzingatia uzima wake, ndio maana mutu hawezi kuamini ispokua aliye na
akili.
(33)
1. Enyi walio amini ! Fanyeni ibada kwa wingi ili mupate kujazwa nuru ya Mungu .
2. Aliye na nuru ya Mungu huzingatia bayana uzima wa Mungu, maana yeye ni katika mapambazuko .
3. Amefunuliwa wazi_wazi siri ya ufalme wa mbingu, akiwasiliana na wa takatifu wa mbinguni.
4. Ndio maana mitume wa Mungu ndio mashaidi wa uzima wake humu duniani.
5. Ni amri kwa kila mutu kumuamini Mungu Mwenyenzi na pia kuwaamini mitume wake wote.
6. Kila mtume iko na kitabu, yaani iko na maneno aliyo funuliwa na Mungu.
7. Hakuna mjumbe pasipo ujumbe, wala hakutumwa yeyote pasipo elimu ya neno la Mungu.
(34)
1. Mwenyenzi ni mwenyi mamlaka ya ajabu, ametenda yote, zaidi ya wote, pahali pote.
2. Hazaliwe wala hakufe yeyote pasipo ruhusa yake.
3. Uwingi wa viumbe haumusumbue kwa kutosheleza haja zao, tajiri wa vyote.
4. Milki kamilifu hutimiza mambo yote kwa rafla, bila kutumika kazi.
5. Hakuna wa kumfichama wala wa kumponyoka,maana uwezo wake umezienea anga na ukiwa.
6.Daraja yake hailingane na yeyote, mshindi, anaye kusanya vyote katika ujuzi wake.
7. Hakika mwenyenzi Mungu ni mkubwa sana, bwana wa mabwana, hakuna mwengine kama yeye.
(35)
1. Mola wa ulimwengu ndio tegemeo la haki,amekua yote katika yote, mwenyi kutosheleza.
2. Katika shida yote, weka tumaini lako kwa Mungu, mapenzi yake ikafanyika tu shida yote humalizika.
3. Ametibu magonjwa isiyo tibika na watu, mganga mkamilifu, anaye umba kila magonjwa na dawa yake..
4. Kisomo kitukufu kadiri ya dhikri ,katika kitabu hiki ,ni tiba ya kila magonjwa.
5. Uchache wa imani ndio jambo ambae husababisha uzaifu wa kila aina pia na majaribu.
6. Juhudi ya ibada katika urakibu inaleta wokovu maishani mwa watu.
7. Muweza wa vyote ni Mungu peke yake, tumkimbilie na tumaini letu lote katika mambo yetu yote, hakuna mwengine kama yeye.
(36)
1. Mwenyenzi ni mufalme wa ulimwengu mwenyi uwezo wa ajabu.
2. Amepatikana kadiri ya kutangulia bila mwanzo wala mwisho.
3. Ni ajili ya kua na milki ya ushindi, ndio maana amekamilika mbali na upungufu wote.
4. Kua na mwanzo pia na mwisho ni kua na upungufu, namna ya kuto kamilika.
5. Utukufu wa kujua yote na kuweza yote ndio unao mfanya aeneane katika yote hali ya kua mwanzo wa vyote.
6. Hakuna Kitakacho mtokeza yeye aliye tangulia vyote, wala kitakacho mkomesha yeye anaye kamilika katika yote.
7. Hali yake hii ya kuenea ndio uzima ambae ni umungu, bingwa mshindi anaye miliki vitu vyote.
(37)
1. Enyi walio amini ! Mtukuzeni Mungu na kumshukuru kwa wingi ajili ya neema aliye wapeni.
2. Kuamini Mungu ni neema kubwa, hakuna bahati maishani zaidi ya kufikiwa na imani moyoni.
3. Hakuna mwenyi akili kumzidia yule anaye amini uzima wa Mungu.
4. Asiye amini Mungu ni sawa na mnyama ambae hukosewa akili.
5. Kule kutokua na utaalamu kifikara, ndio humfanya ashindwe kuzingatia kiroho.
6. Yeye ni mfano wa kipofu ambae uzingatiaji wake hukomea katika mwili, hawezi kutazama kiroho. 7. Kama angeli kua na akili bila shaka angeli mzingatia Mungu Mwenyenzi, baba wa siri aliye kwa siri.
(38)
1. Ulimwengu ni jumla ya sehemu tatu :Enzi, Anga na Ukiwa.
66
2. Wanahewa wote huzingatia ajili ya fikara iliye ndani ya pumzi zao.
3. Fikara yao huzidiana kulingana na umbile zao.
4. Pumzi isiyo changikana na chochote ni kubwa tena bora zaidi ya ile inayo changana na mwili.
5. Ndio maana wanahewa_halisi ni pumzi takatifu, kubwa tena yenyi utaalamu kifikara ambae huzingatia vema zaidi ya
wenzao.
6. Amezingatia bayana mbinguni, hadezeni na duniani na piahuzingatia njee ya umbiko, enzini, ajili ya kupatikana na macho ya
kiroho inayo itwa akili.
7. Mutu atakaye jazwa pumzi halisi atakua na ginsi ya kuzingatia umbiko na pia muumba wake.
(39)
1. Mutu anaye silimu ni mfano wa nuru inayo meremeta ,amezaliwa upya kiroho.
2. Amejaaliwa neema yakujumuika katika hesabu ya wanyenyekevu ambae hufanikiwa na jaza la mbinguni.
3. Muumba wa anga na ukiwa ni mwingi wa rehema,msaada wake hutarajiwa na wote wanao pumua.
4. Ibada ndio charamata ya nuru, kila anaye abudu Mungu vilivyo hukurubiwa na roho takatifu.
5. Hakuna aliye mwema kama vile Mungu mwenyi rehema ya kuenea.
6. Heri mutu anaye mshukuru kwa kila jambo, kila ulicho nacho ulipewa na Mungu.
7. Hakika nampenda Mola aliye ni umba, bila yeye kama mimi si chochote.
(40)
1. Mola wangu amenipa kazi ya kutangaza habari ya uzima wake.
2. Watu wengi hawana yakini na uzima wake, wamejaa mashaka ajili ya kutomzingatia kimwili.
3. Wengine wanasilimu kwa udanganyifu na ilihali hawana yakini (na uzima wake ) moyoni.
4. Atakaye amini ujumbe huu,bila shaka atakua yakini kwamba Mungu yupo na atajazwa roho takatifu itakayo mfanya aishi
milele.
5. Sema :katika daraja ya kiroho mimi ni walii wa Mungu.
6. Na katika kazi ya kiroho mimi ni mjumbe wa Mungu Mwenyenzi.
7. Hakika shukrani zote zinamustahili Mwenyenzi Mungu, mufalme mwema, anaye jua yote na anaye weza yote.
(41)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, Mola wangu na Mola wenu pia na Mola wao.
2. Mungu wa ma nabii na mitume wote, chemchem ya upatikanaji wote na maisha yote.
3. Aliye mtuma Ahmad ili asadikishe qur'ani na pia atabiri ujio wa Kalonda.
4. Hakika Ahmad ni mjumbe wa Mungu aliye kuja baada ya Nabii mutukufu Muhammad ,kabla ya kuzaliwa kwa Kalonda;
asema roho wa Mungu.
5. Mutu anaweza kua Nabii na ilihali yeye sio mtume, na pia anaweza kua mtume na ilihali yeye sio Nabii.
6. Na mwengine anaweza kua Nabii pia mtume, na ndio mutukufu zaidi : kama vile ,Mussa ,Yesu masiya,Eliya, na Muhamadi...
7. Mtume asiye kua Nabii ni miongoni mwa mawalii watukufu.
(42)
1. Musifuni yeye aliye umba kila kitu, mtegemewa ,anaye stiri kila nafsi, angani na ukiwani.
2. Maisha pasipo nuru yake haiendelee lakini hukoma,maana giza ni mfano wa uchafu ambae huchafua nafsi.
3. Aliye nuruni hufikiwa na heri nyingi na aliye gizani hufikiwa na shari ya kila namna.
4. Nuru imeleta usalama ajili ya uzuri wa malaika na roho.
5. Na giza imeleta hasara ajili ya ubaya wa Shetani na muzimu.
6. Amefaulu kabisa mutu anaye amini mjumbe wa Mungu, ijapokua hafafanue baina ya Nabii na Mtume.
7. Kinacho hitajika ni imani, mutu anaye kubali ujumbe wa Mola wake hujazwa nuru ya mbinguni.
[ 43 ]
1. Mponyaji ni Mungu peke yake, mganga wa magonjwa yote, wala hapone yeyote ispokua kwa idhni yake. 2. Ee Mola wangu ! Uniponye kwa rafla kadiri ya idhni yako ibakie ishara kwa watu watakao kuja nyuma.
3. Na unikinge na kila uchawi:wakutia na wakupuliza,hakika wewe ndio mujibu wa dua.
4. Mungu ndio ukingo wangu ngao ya miujiza anaye ni kinga na hatari ya kila namna, usiku na mchana.
5. Watu wa dunia hawamsadiki Mungu ila kwa mashaka na ndio sababu wamekanusha ujumbe wake.6. Ondoeni mashaka ,enyi watu wa dunia, kwa nini hamuamini na hali mumezingatia?vyote munavyo viona vilifanyika naye bila msaidizi.
7. Amepatikana kadiri ya kuenea, bila maisha wala mauti,bila kimo wala kipimo,lakini mkamilifu awezaye na ajuaye.
(44)
1. Enzi, Anga na Ukiwa ndio hujenga ulimwengu.2. Enzini hupatikana utukufu wa ajabu, ukamilifu kadiri ya uzima.
3. Na Anga ndio kambi la Hewa, maala penyi shuruli ya kila namna ambae hupatikana maisha.
4. Na Ukiwa sio sifuru lakini utupu kimwili kadiri ya ganda,umbo isiyo Linda pumzi ndani mwake.
5. Aliye Enzini hafanane na yeyote, yeye ndio mkamilifu lakini wengine wote ni wapungufu.
6. Mungu hafanane na yeyote wala chochote, amepatikana kadiri ya kuenea.
7. Mamlaka yake ni juu ya kila kitu, mteza nguvu anaye zidia kushinda,wa miujiza aliye juu.
(45)
1. Mwenyenzi Mungu peke yake ndio mwenyi kuenea katika tendo kua hali ya kua mzima.
2. Kupatikana ao kujumuika ao kuishi sio kua na uzima.
3. Unaweza kupatikana namna ya kujumuika ulimwenguni na ilihali hauna uzima.
4. Kua na uzima ni kua na ukamilifu, namna ya kuenea kimllki na kibusara,yaani kuweza yote na kujua yote.
5. Wala kuishi sio kua na uzima maana sio kukamilika.
6. Anaye ishi ni yule anaye pumua hewa yaani yule anaye fikiri.
7. Shuruli ya aina yote ni uzaifu na ndio maana ni kwao viumbe, haipatikane kwa Muumba kamwe.
(46)
1. Neno la Mungu ni nakala ya ufunuo ambae hujaa kweli.
2. Ni ujumbe wa mjuzi ambae ndani mwake hamna kasoro wala doa lakini ukweli usio na shaka.
3. Kila atakaye tumia neno lake, atakua mtaalamu ,mwenyi nguvu ya ushindi .
4. Mungu atafumbua macho yake kwa kumjaza nuru ya mbinguni.
5. Pumzi yake itakomazwa na roho takatifu na ndio maana ukaguzi wa andiko itakua jambo raisi kwake.
6. Mengi ni mafumbo ambae hudai tafsiri, na pia mengi ni wazi_wazi, ndio maana hudai mwenyi akili.
7. Kutumia neno la Mungu ndio kutumia nuru ya Mungu namna ya kujitenga na giza.
(47)
1. Mwenyenzi yupo,ndiye mwenyi uzima katika ulimwengu.
2. Amepatikana kadiri ya kuenea hatua na upungufu wa aina yote.
3. Mungu hawezi kujumuika na vitu vizaifu asije kulingana nao katika kuzaufika.
4. Mola wenu ni yote katika yote zaidi ya yote kuliko wote, mufalme wa wote.
5. Macho yako haiwezi kumuona ana kwa ana,sababu ya kua tafauti sana naye.
6. Wewe ni mwenyi mwili na pumzi, lakini yeye hana mwili wala pumzi.
7. Amepatikana katika upekee,njee ya Anga na ukiwa, katika utukufu usio kurubiwa na yeyote, Enzini.
(
67
48)
1. Macho ya mwanaadamu haizingatiake vitu vyote vilivyomo ulimwenguni.
68
2. Siokwamba jumla ya vitu unavyo viona ndio walimwengu wote.
3. Kuko aina nyingi ya viumbe ambae mwanaadamu hazingatiake bayana, utazamaji kimwili ni wenyi uzaifu mkubwa.
4. Mwilini hamna ispokua ujinga mtupu, na ilihali ujinga hauzingatiake Bali hupitiwa.
5. Viumbe vyenyi kua karibu naye angani na ukiwani hawezi kuzingatia vyote bayana kefule yeye mshindi aliye njee ya umbiko
!.
6. Hapana kujingikiwa ajili ya kuto mzingatia kimwili yeye asiye kua na mwili,tena aliye mbali sana na dunia.
7. Mola wenu amejifunua ku watu kupitia wajumbe wake ili watu wapate kuzingatia uzima wake.
(49)
1. Mwenyenzi Mungu ni mumoja hana baba wala Mama, sio muzila hewa wala mwanahewa.
2.. Mungu hafanane na yeyote wala chochote katika ulimwengu, yeye peke yake ndio mkamilifu lakini wengine wote ni
wapungufu.
3. Dhati yake ni tukufu ajabu, haigusanake na chochote wala haigeukake hali.
4. Kitu kinacho badiri hali ni zaifu,hubadirika ajili ya uzaifu wa kuto eneana.
5. Mungu hawezi kugeuka kiumbe, kua kiumbe ni kua zaifu.
6. Hasara ilio_je kwao wanao abudu mtume wa Mungu ! Wanamshirikisha Muumba na kiumbe alicho kiumba .
7. Ingawa kama hawata acha ibada hiyo ya sanamu,bila shaka wataangamia siku ya kiyama.
(50)
1. Ametakasika Mwenyenzi, m'bora wa wanao bariki,mjuzi anaye geuza pumzi kua roho takatifu.
2. Mapenzi yake ndio msaada mkubwa ambae kutosheleza haja zote,mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu.
3. Mjuzi anaye kadiria maisha ya kila anaye pumua.
4. Alitangulia mwenyewe kadiri ya kuenea pasipo uzaifu wa kuanza na kukoma.
5. Kupatikana milele bila mwanzo wala mwisho ndio kukamilika hali ya kua na uzima.
6. Mungu ndio mwanzo wa vyote ambae huenea katika tendo kua, hakuna kabla yake wala baada yake.
7. Hakika ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu aliye na uhuru : anaye miliki shuruli na wakati, m'bora wa kuenea.
.
(51)
1. Mutu wa dunia amekanusha uzima wa Mola wake sababu y'a kupatikana pasipo kuanza namna fulani2. Hali hii ya kutangulia ndio ukamilifu, namna ya kuweza yote na kujua yote.
3. Kuanza ni uzaifu wa kua sifuru kabla yake ,na pia kukoma ni uzaifu wa kua sifuru baada yake.
4. Kua na mwanzo pia na mwisho ni kua mpungufu kadiri ya umbiko, ambae asili yake ni sifuru.
5. Kama italazimika kila yule kuanza namna fulani, ni kwamba imelazimika kila yule kuumbwa ,na ilihali haiwezekane viumbe
kupatikana pasipo muumba kutangulia.
6. Muumba ni yule asiye umbika , anaye kamilika kimilki kinyume na uzaifu wa kushindwa.
7. Milki yake hiyo ya ajabu isiyo shindwa na chochote ndio inayo mkamilisha pasipo upungufu wa kuto kua muda fulani, na pia
ndio inayo mfanya atokeze ambacho hakika popote.
(52)
1. Ole wao wajumbe wa Shetani, ambae baada ya kutumia njia mbali mbali ya ushirikina ,hutumia kwa unafiki kitabu cha
Mungu ili wa pate hanasa ya dunia.
2. Wamejidai unabii na utume na ilihali wao ni mishirikina .
3. Na wanapo piga ramli,watu wa dunia wamezani ni unabii.
4. Na wanapo fuma ufumu wao kwa kutibu ,watu wa dunia wamezani ni maombi.
5. Udanganyifu kama huo ndio mafunzo ya Shetani ili wapate kuwapoteza walio amini.
6. Alama yao ni kutowaletea watu "maneno ma takatifu”, na ndio maana hawana vitabu kadiri ya nakala ya ufunuo wao.
7. Wamezingizia kusoma vitabu vya Mungu,na kudanganya kufanya ishara ndogo kutokana na mizimu yao, ajili ya upofu wa
watu wa dunia.
(53)
1. Umungu ni uzima, yaani ukamilifu.
2. Ni utangulizi kadiri ya kuenea katika yote.
3. Kutangulia vyote ndio kupatikana milele.
4. Na hapatikane milele ispokua yule asiye kua na upungufu (uzaifu) wowote.
5. Na asiye kua na upungufu wowote ni yule awezaye yote na ajuaye yote.
6. Na yule awezaye yote na ajuaye yote ndio mkamilifu, kadiri ya " mwanzo wa vyote "
7. Naye ndiye muanzishaji wa kila kitu aliye muumba wa vyote anaye itwa Mungu Mwenyenzi.
(54)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba, aliye tokeza kila kinacho patikana ulimwenguni.
2. Milki yake kamilifu ni mamlaka ya ajabu ambae huhukumu kila upatikanaji na maisha ulimwenguni.
3 .Utukufu wake huu wa ajabu unamtenganisha na vitu vyote, hafanane na chochote wala hachangie fasi na yeyote.
4 .Amestawi katika utukufu wa dhati yake mwenyewe hali ya kua wa pekee.
5. Alitangulia kila kitu, namna ya kuenea kadiri ya uzima.
6. Hakuna kabla yake wala baada yake sababu ya kuenea namna ya kukamilika.
7. Hakika Mungu Mwenyenzi ndio mwenyi uzima, mufalme mkamilifu,hakuna mwengine kama yeye.
(55)
1. Ujumbe wa Mungu ni mfano wa nuru ambae huondoa giza,yaani elimu ambae huondoa ujinga.
2. Atakaye kanusha ujumbe wa Mungu, atakua gizani siku zote wala hawezi kuzingatia.
3. Kila mara baada ya mtume, Mola wenu analetaka Mja nyuma ili kusadikisha ujumbe wake.
4. Roho takatifu anasaidiaka waaminifu katika njia mbali mbali,lakini sio kwa kuwapatia karibuni wote kazi ya utume.
5. Waaminifu na waubiri wote sio ma Nabii wala Mitume ,hapana kujidai unabii ao utume ajili ya kufanya kazi ya Mungu.
6. Dini ambae waubiri wote wameitwa ma Nabii ao mitume ni dini ya uwongo.
7. Ogopeni Mungu ukweli wa kuogopa,wala usimzingizie kwa lolote, wala usipinge lolote katika kauli yake.
(56)
1. Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu, mtukufu wa daraja, anaye inukia walimwengu wote kwa jumla.
2. Ameteremsha nuru yake hii katika umati huu ili ukweli upate kutawala duniani pote.
3. Ukafiri wa kukanusha uzima wa Mungu hauna tena fasi kwani uwongo umekwisha toweka.
4. Someni wote kitabu hiki ili mupate kuzingatia uzima wa Mola wenu.
5. Hakungeli patikana yeyote wala chochote bila Mungu kutangulia ulimwenguni, maana ndiye muanzishaji.
6. Mumilki asiye hitaji kwa yeyote, ambae wote huitaji kwake.
7. Alikua, yuko na atakua, mwenyi kuenea ; hakuna mwengine kama Mungu.
(57)
1. Mola wa ulimwengu amekua yote katika yote kuliko vyote, m'bora wa kuenea.
2. Ukamilifu ni hali tukufu ajabu, uwezo wa vyote kadiri ya mamlaka ya milele.
3. Fikara ya viumbe ni fahamu ndogo sana, haiweze kukagua siri ya utukufu wa ujuzi.
4. Upungufu hauwezi kupatikana bila ukamilifu kutangulia, kamwe upatikanaji na maisha pasipo utangulizi wa uzima.
5. Hakika viumbe haviwezi kupatikana pasipo Muumba kutangulia, ndiye chemchem ya upatikanaji na maisha.
6. Pasipo Mungu kama sifuru ingeli tawala milele, maana kungeli kosekana mwanzo wa vyote.
7. Umungu ni utukufu wa ajabu tafauti sana na kila kitu, hakuna mwengine kama yeye.
69
(58)
1. Abuduni Mola wa ulimwengu kila siku kwa kusali : asubui na mangaribi pia na usiku. Na umtukuze mchana kadiri ya uwezo
wako.
2. Ni lazima kwa kila mutu kuonesha shukrani na heshima kwa Muumba wake Aliye juu.
3. Nabii Muhamadi alifundisha watu sala ili wapate kukurubishwa na Mola.
4. Mwalimu wa usilimu,aliye kua na silimusha watu kwa maneno na matendo.
5. Heri mutu anaye amini mjumbe uyu na kuitumia qur'ani kama chakula ya roho.
6. Mungu alimupa kazi kubwa katika nuru kubwa na kumpa heshima kubwa mbinguni.
7. Anaye silimu ndio anaye muamini,hatua ya kwenda mbinguni.
(59)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, chemchem ya nuru, anaye angazia mitume na nuru itokayo dhatini mwake.
2. Kama alivyo mjaza yesu masiya nuru kubwa sana, na kumfanya umbo laini yenyi imani timilifu kadiri ya mapenzi yake. 3. Akamtakasa kadiri ya neno lake, na kumtukuza kadiri ya roho yake.
4.Mnyenyekevu na mpole wa moyo,hapazake sauti anapo sema ,lakini maneno yake imeinukia ya wenzake.
5. Hiyo siku ya kiyama, bwana Yesu atasaga milima kuisawanisha ardhi sawa sawa, hakuta baki bonde wala kisuguu.
6. Hakika Yesu masiya ni bwana, mufalme mwenyi daraja kubwa na heshima kubwa sana mbinguni.
7. Anaye silimu ndio anaye muamini,hatua ya kwenda mbinguni.
(60)
1. Enzi sio sifa yake Mungu, lakini dhati yake Mungu. Na dhati yake Mungu ndio umungu.
2. Hakuna kiumbe chenyi kua na Enzi ndani mwake.
3. Umungu ni katika upekee kadiri ya ukamilifu,hakuna wana_Enzi ispokua "Mwenyenzi" peke yake.
4. Ni kwamba habari ya Enzi tukufu ndio habari ya Mwenyenzi Mungu.
5. Katika umungu ndio Enzini, umoja tafauti sana na uwingi.
6. Hakika Mungu ni wa pekee, hachangie fasi na yeyote wala hafanane na chochote.
70
7. Yule atakaye mfananisha Mungu na mwanahewa ao muzila hewa, atakamatwa na kutupwa hadezeni, kadiri kapi inavyo ogotwa na kutupwa motoni.
(61)
1. Dini ya Mungu ni usilimu,kuingia katika dini ya Mungu ndio kusilimu ,na anaye silimu ndio musilimu.
2. Dini ingine yote ni ya uwongo maana imetokea kwa yule mudanganyifu.
3. Mungu ni mumoja na dini yake ni moja, wala jumuiya la kidini sio dini ya Mungu.
4. Kila Nabii ao mtume anaye hubiria watu kwamba mwanakondoo wa Mungu ndio Mwenyenzi bila shaka ni Nabii ao mtume
wa uwongo.
5. Dini ambae hawaabudu Mungu mwenyenzi ,wala hawaamini mitume, wala hawaamini siku ya kiyama ni dini ya uwongo.
6. Dini ambae hawashaidilie uzima wa Mungu ,wala hawasome sura za ufunguzi,wala hawasujudu katika sala, ni dini ya
uwongo.
7. Kutoa shaada ndio tendo la msingi wa imani, na kusujudu ndio tendo la msingi wa ibada.
(62)
1. Ujumbe wa Mungu umepatikana katika vitabu vyake vitukufu.
2. Vitabu vitukufu ni nakala ya ufunuo wa Mungu, sio fikara ya kibinaadamu.
3. Kitabu chochote kinacho andikwa pasipo kufunuliwa na Mungu sio kitabu kitukufu.
4. Neno la Mungu ni mfano wa maji ya kunywa ,ambae hupatikana katika kisima cha Mungu.
5. Kuona kama kisima kinaweza kuchafuka,ndio maana Mwenyenzi anatumaka wajumbe ili kusafisha kisima chake mara na
mara.
6. Ole wao waandishi wadanganyifu,ambae huongeza ao hupunguza katika maandiko ma takatifu.
7. Tumieni wote kitabu kitukufu hiki, "ukweli" ambae Mungu mwenyewe kaushuudia,ili mupate kuokolewa.
(63)
1. Kauli tukufu hii "ukweli" ni ujumbe wa Mungu ku watu wote.
2. Asiye amini Mungu ,na yule anaye amini Mungu, wao wote wamealikwa kusoma kitabu hiki ili wapate kuzingatia uzima wa
Mola wa ulimwengu.
3. Kukosa yakini moyoni kunaleta unafiki katika imani.
4. Elimu ndogo inaleta uzaifu katika imani, na ndio maana matendo ya musilimu asiye kua na elimu haiachane na matendo ya
kafiri.
5. Kama Mungu haonekane kimwili ni kwa sababu hana mwili, sio kwamba kukosa mwili ndio kukosekana.
6. Tazameni kiroho ili mupate kuzingatia uzima wa Mola wenu.
7. Mola wa ulimwengu sio mwili wala pumzi, lakini mwenyi "Enzi".
(64)
1.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu, mwenyi uzima, atanguliaye kadiri ya kuenea.
2. Kauli yake ni tukufu ajabu, imefadhilisha kila nafsi inayo itumia.
3. Atakaye mtukuza Mungu katika kuzisoma aya za kitabu hiki kwa wingi,atakua miongoni mwa wazaliwa wa sehemu ya
kwanza ya bahazi la juu angani.
4. Sifa ya Mungu inayo andikwa katika kitabu hiki ndio tukufu zaidi,kifaa maalumu cha maisha.
5. Ni bora zaidi kufanya dhikri ya kisomo cha kauli hii hali ya kua na matendo mazuri,ili upate kuzingatia utendaji wa Mola
wako bayana.
6. M'bora katika watu ni yule aliye katika mapenzi ya Mungu, hatakiwe amani mbinguni ispokua yule anaye takia watu wenzake
amani duniani.
7. Kilicho muimu maishani ni mapendo :hamfitini ndugu yake ispokua yule asiye mpenda nduguye.
(65)
1. Ushindi ni wake Mwenyenzi Mungu, mtukufu aliye na mamlaka ya ajabu.
2. Ndiye mneemeshaji ,anaye bariki mchaguliwa wake pamoja na uzao wake bila ukomo.
3. Ma Nabii na mawalii wanaweza kuzaa kimwili na pia wanaweza kuzaa kiroho.
3. Mungu ndio mkweli wa kauli,hakuna atakaye vruga mpango wake wala kuiba baraka yake.
4. M'bora wa kuumba anaye tokeza,kadiri ya matamshi yake, kila kitu kinacho patikana.
5. Ameporomosha ujumbe wake kwa kila umati maana yeye ni taa isiyo fifia wala kuzimika.
6. Mjuzi na mshindi anaye kadirisha kila kinacho fanyika ulimwenguni.
7. Hakuna mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu Mwenyenzi peke yake.
(66)
1. Mwenyenzi Mungu ndio chemchem ya nuru, kadiri ya taa ya ulimwengu.
2. Neno lake ndio nuru maishani,litumieni kwa kila jambo kauli tukufu ya kitabu hiki, ili mupate ushindi.
2. Ni yeye peke yake anaye pana cheo kwa amtakaye,hakuna mamlaka kinyume na idhni yake.
3. Unabii na utume umetoka kwake, ameteremsha ujumbe kwa muja wake kuhusikana na majira ya umma wake.
4. Amekadirisha neno lake kulingana na ukaguzi wa watu wa ule umati ili wapate kuzingatia.
5. Mola wenu hawatakieni kamwe yaliyo mazito ispokua yaliyo mepesi.hakika Mungu ni mwema sana na zaidi.
6. Roho takatifu ndio zawadi ya Mungu kwa watumishi wake, ambae husindikiza nafsi zao hadi utimilifu.
7. Ni karama ya Mungu kutoka mbinguni, ili walio silimu wasiangamie lakini wapate wokovu.
(68)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mwalimu mkamilifu anaye fundisha wanahewa wote kwa njia mbali mbali.
2. Ujumbe wake huu ni elimu ya namba ya juu inayo wa husu watu wenyi akili.
3. Utazamaji kiroho unafanya wazingatie duniani pia na inje ya dunia.
4. Ni mwenyi nuru ya Mungu,musilimu anaye soma sura ao aya kadhaa ya kitabu hiki kitukufu,usiku kama vile mchana.
5. Sema :Yesu Masiya ndio simamizi la neno la Mungu,na Muhamadi ndio simamizi la ibada ya Mungu:umpende nani na umkatae nani?
6. Muaminifu wa kweli ni yule anaye amini Mungu na mitume wote pia na vitabu vyote.
7. Hakuna mtume wa dini for wala hakuna kitabu cha dini fulani, mitume wote na vitabu vyote ni vyake Mungu mumoja katika dini yake moja ya usilimu.
(69)
1. Uzima ndio ukamilifu, ni uwezo wa vyote tafauti sana na uzaifu wote.
2. Mwenyi uwezo wa kumiliki kila kitu, hakuna mfano wake popote ulimwenguni.
3. Utukufu wa ajabu usio kadiriwa na yeyote ndio umungu, ushindi katika yote milele na milele.
4. Kulazimisha Mungu aanze mu namna fulani ni kulazimisha Mungu apungukiwe ao azaufike mu namna fulani.
5. Ni upofu wa kuto zingatia mwanzo wa vyote,hakungeli patikana chochote pasipo Muumba kutangulia ulimwenguni.
6. Milki kamilifu ndio mamlaka ya umungu ambae katangulia vyote bila msaada wa yeyote.
7. Utangulizi ndio ukamilifu kadiri ya uzima, mamlaka itokezayo kuujaza ulimwengu.
(70)
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, muhitajiwa ,anaye tosheleza walimwengu wote maala pote.
2.. Uwezo wake Mwenyenzi hauna kipimo ,ndiye mtokezaji wa mapya asiye dondoka wala kushindwa.
3. Mjuzi anaye jua yaliyo mbele yao na yaliyo nyuma yao, pasipo shuruli yoyote wala msaada wowote.
4. Alikua, yuko na atakua, mwenyi kuenea hali ya kua uzima.
5. Mtukufu asiye onekana kimwili, aliye tafauti sana na umbiko.
6. Pahali pake hakuna mwengine,Mwenyi kumiliki walimwengu wote milele.
7. Mwenyenzi Mungu ni mkubwa sana, chemchem ya upatikanaji na maisha, hakuna mwengine kama yeye.-
Maoni
Chapisha Maoni