Kitabu cha ukweli - Mlango wa sita : "UZIMA"
1 MWANZO WA VYOTE
1.Mungu ni mmoja sababu yeye ndio mwanzo wa vyote.
2. Hakuna ginsi mwanzo wa vyote upatikane tena na mwanzo wake ungine.
-
Ni wa pekee ajili ya kua na milki kamilifu,fahamu ya vyote ambae hutokeza toka sifuru.
-
Hakuna kinacho patikana bila kufanyika naye.
-
Ni Mungu pekee aliye na ujuzi,fahamu isiyo shindwa na lolote;mamlaka ya uumbaji.
-
Mungu ni mwenyi uzima sababu ya kupatikana na milki kamilifu.
84
-
Milki yake hufanya atangulie ; yaani apatikane bila kuanza wala kukoma.
-
Hakuna wa Mungu wengi sababu umungu ni ukamilifu,Hakuna utafauti wala mipaka,Hakuna maanzio wala makomeo,ajili
ya kuenea.
9. Uwingi ni katika viumbe,na upekee ni katika umungu.
10. Ni yule aliye umbwa ndio kawekewa wenziwe wa kushiriki naye katika matumizi.
11. Na yeye asiye umbika hawezi kua na wenzake sababu hakuna wa kuwajaza ili wawe wengi.
12. Muumba ndio mwenyi mamlaka ya kuwajaza (ili wawe wengi) kadiri apendavyo.
13. Mungu ni kama taa ya ulimwengu,ambae huangaza maala pote kwa nuru yake.
14. Pahali penyi kua taa hupatikana sehemu tatu:Taa, Nuru na Giza
15. Kila sehemu ni tabaka,na jumla ya hizo tabaka tatu ndio ulimwengu.
16. Mgawanyiko huu wa ulimwengu umesababishwa na busara ambae katangulia.
17. Taa hiyo ndio ujuzi na nuru yake ndio fikara,na giza ndio ujinga.
18. Hakutukie chochote pasipo fahamu kamilifu kuya tenda.
19. Kuona kama busara kamilifu ndio ujuzi,na aliye na ujuzi ni Mungu peke yake,ndio maana Mungu peke yake ndio aliye fanya ulimwengu upatikane.
20. Ni lazima watu kugundua jambo ambae husababisha upatikanaji wa viumbe ili wapate kuzingatia ulimwengu ambae ni uzima,maisha na mauti.
21. Ni mwenyi uzima aliye na ujuzi,na ni mwenyi maisha aliye na fikara,na ni mauti aliye na ujinga.
22. Kupatikana bila uzima wala maisha ndio kua mauti,yaani kua bila ujuzi wala fikara ndio kua na ujinga kadiri ya mauti.
23. Hakika upatikanaji ( mauti) na maisha ni matunda ya idhni yake Mjuzi;
24. Hakufanyike lolote pasipo utangulizi wa fahamu ya vyote ambae ni uwezo wa vyote.
25. Hakukua,hakuna na hakutakua mwengine badala ya Mungu Mwenyenzi.
26. Hakuna nguvu wala fahamu bila msaada wa ujuzi maana vyote ni katika fahamu ya mtangulizi
27. Ujuzi ndio taa,na uvuli wake (ao mwangaza wake ) ndio fikara,na kinyume cha mwangaza wake ndio giza ambae ni ujinga.
28. Katika matazamio ingine: ujuzi ndio Enzi ,na fikara ndio Anga yaani hewa,na ujinga ndio ukiwa.
29. Kuona kama ujuzi ndio ukamilifu,ndio maana Mjuzi ni mwenyi uwezo wa vyote,hashindwake na yeyote wala chochote.
30. Mwenyi mamlaka ya uumbaji,atokezaye mapya ambae hayakua popote,bila shuruli kupatikana ndani mwake.
31. Mola wa jumla ya viumbe,aliye hodari na wasaa ,anaye stawi enzini katika uhuru,aliye na kasi la uwezo wa kutenda,mzima.
32. Enzini ni maala pa juu kupita mbingu,wala hakuna kilicho inuka mfano wake ulimwenguni.
33. Mwenyi daraja la juu kuliko vyote,mtukufu atanguliaye kadiri ya kuenea.
34. Hodari asiye jumuika katika umbiko,M'bora wa katangulia.
35. Mbingu ni bahazi la kiroho linalo patikana angani.
36. Na dunia ni bahazi (kambi) la kimwili linalo patikana ukiwani
37. Katika utazamaji kiroho:dunia imefunikwa na giza, na mbingu
imemeremeta na nuru.
38. Hakika anga (hewa) ndio nuru na ukiwa ndio giza.
39. Utakatifu ni wake Mwenyenzi,M'bora wa kuumba Mola wa anga na ukiwa,haimjuzu kutokea wala kuendea, muhodari juu
ya arshi yenyi heshima ,imara kukadiria; mtukufu mwenyi uwezo na ushindi.
40. Mustawi aliye na mamlaka juu ya yote,huko juu ya maala pa juu,Mungu mzima asiye kosekana muda wowote,mshindi aliye
juu.
41. Mungu alitangulia kuenea bila mwanzo wala mwisho sababu ya kupatikana na fahamu ya ajabu isiye shindwa
42. Na baada ya utangulizi wake,akatokeza viumbe vyote kwa njia ya mapenzi yake.
43. Kwa sababu hakufanyike jambo kinyume na idhni yake,hutakika uzima upatikane kwa ulimwengu kutimilika.
44. Kuona kama Mungu pekee ndio mwenyi uzima,ndio maana yeye peke yake ndio mwenyi uwezo wa kuumba.
45. Ametokeza kwa rafla kiumbe ambacho hakikuwaka popote ulimwenguni.
46. Mungu haonekaniake viumbe ajili ya kutokurubiana naye katika fahamu.
47. Mungu ni Mjuzi,lakini viumbe havijue.
48. Viumbe hufikiri tafauti na kujua,walio na pumzi; na hupitiwa wasio kuwa na pumzi.
49. Mola mtukufu ni muweza bila msaidizi wala muchoko, mu miliki wa ulinzi na karama.
50. Shuudieni Mwenyenzi Mungu,uzima ushindaye,Mola wa mashariki na magharibi ,mamlaka katika yote pahali pote ulimwenguni.
51. Hakika ujuzi ndio ukamilifu ambae ni uzima kadiri ya umungu.
52. Ni muujiza wa maajabu ambae hupatikanisha kila kitu,wala hakuna cha faida mfano wake,wala utasi kinyume naye.
53. Mola atulizaye tatizo kwa hudumu lake,msemeleaji wa viumbe.
54. Aliye umba mbingu angani kama vile tungi ,ambae huzagaa na nuru.
55. Na akaumba dunia ukiwani kama ganda yenyi kujaa giza.
56. Hakika Mungu ndio mwenyi kuwako imara na daima ulimwenguni,wa milele aliye juu.
85
57. Haiwezekane viumbe ambae havijue vipatikane na Muumba ajuaye akosekane.
58. Hakiwe kiumbe ila kilicho umbika na Muumba.
59. Tumieni maamrisho ya Mungu ili Mwenyenzi akuamrishe kuishi milele.
60. Na atumiaye makatazo hufupisha umri wake,na pia hujiangamiza mwenyewe.
61. Kama utatenda mabaya usizani kama unam'buguzi Mungu,hakika umejizulumu mwenyewe.
62. Mungu sio mfano wa kiumbe ambae hutaabika na kasirani,uzaifu kama huo haum'kurubie kamwe.
63.Anaye chukizika,hulia;na anaye furahi,hucheka .Mtukufu aliye juu,hujitenga mbali sana na uzaifu huo wa kulia na kucheka.
64. Mola wa ulimwengu sio mvuguvugu katika hali yake,hapungukake wala haongezekake,kwa maana yeye ni Mkamilifu.
65. Mungu ni mwenyi uhuru,baba wa salama aliye Salama,hafikiwake na yale asiyo yataka.
66. Hali yake Mungu ya uhuru haimziwilie kuongoza viumbe vyake kuwawekea maamzi, namna ya kutenganisha adili na batili.
75. Kwa kufahamu neno la Mjuzi ni lazima kutimilika kikafara;yaani kua na akili.
76. Neno la Mungu hufanyika kifikara kadiri ya kusema kwa watu ili wapate kulisikia.
77. Na ndio maana hakika ya kadiri yake haikadiriwe ispokua katika mifano.
78. Neno lake ndio nuru inayo angazia watu, hufanya wamzingatie mwenyi uzima ulimwenguni.
79. Hakuna wala hakukua,wala hakutakua mola mwengine badala yake ,sababu hakuna kabla wala baada ya umungu.
80. Hutukuka jina lake ulimwenguni,Mola mkamilifu katika yote,mlezi wa viumbe.
81. Umungu ni mamlaka ya ajabu,utukufu wa namna yote,katika yote,pahali pote ulimwenguni.
82. Anaye tawanisha hewa katikati ya ulimwengu kadiri ya idhni yake,ndiye Mola wa arshi tukufu.
83. Hakuna kilicho kurubia uwezo wa Mungu ambae mchoko haumguse,ambae hukadiriana vipimo ajili ya kujua yaliyo mbele
yao na yaliyo nyuma yao.
84. Na akataaye kipimo cha Mwenyenzi Mungu na kutarajia tamaa ya nafsi yake ndio mzalili,umbo ya hadezeni.
85. Mola wa Anga na Ukiwa hatendake kadiri mutu anavyo tenda,lakini hutenganisha nuru na giza bila kudanganyika wala
kusambisha.
86. Aliumba mutu katika umbile la katikati juu yake pumzi na chini yake mwili.
87. Na silaha ya utetezi kifuani mwake,ili asiangamie ajili ya uziwi na upofu.
88. Akili huapa kwa jina la ujuzi,na humsujudia Mola wake katika yakini.
89. Na muguu wake wa kuume juu ya maji,na muguu wake wa kushoto juu ya udongo na moyo wake katika hifadhio la adili.
90. Huamini Mungu katika yakini,na zamiri yake ndani ya mipaka ya neno la Mungu.
91. Na ndio maana matendo yake hubarikiwa na nuru hutiliwa ndani mwake.
92. Kuamini Mungu kwa yakini ndio tendo kubwa,hutimiliza nafsi yako kua roho.
93. Roho ni nuru,hakuna shaka ndani mwake ajili ya kuzingatia.
94. Uvuli wa Enzi tokea uzimani,silaha ya utetezi na dira kwa wamchao Mungu.
95. Ni neno la Mungu ndio huleta uhai rohoni na mauti mwilini.
96. Na kuamini Mungu kwa mashaka ndio tendo mbaya,huzaufisha nafsi yako kua mauti.
97. Kuona kama mwili ni giza,kuna mashaka ndani mwake ajili ya kutozingatia.
98. Mwenyenzi Mungu ni mshindi,hodari katika arshi yake,jalali ulimwenguni.
99. Huenea katika yote,muda wote,maala pote,mwenyi uzima,imara na daima milele na milele
100. Huinuka ulimwenguni ajili ya milki kamilifu,ambae ni mamlaka ya kuenea katika yote ulimwenguni.
101. Karama zote ni zake Mungu,ambae peke yake ndio mzima,wa pekee aliye huru kutenda kila apendalo.
102. Watu hawamfahamu mwenyi daraka ulimwenguni ajili ya kuvaa miili.
103. Hakika Mungu Mwenyenzi kudiriki vyote ulimwenguni.
104. Mola mtukufu asiye na doa, ambae huzagaa juu ya ulimwengu,mtawala wa anga na ukiwa,mfinyanzi wa jibini
ulimwenguni.
2. ULIMWENGU
86
1. Ulimwengu ni jumla ya sehemu tatu: Enzi,Anga na Ukiwa.
2. Enzi ndio chemchem ambae katokeza Anga pia na Ukiwa,yaani mwanzo wa vyote.
3. Ujuzi wake ndio uwezo wa vyote ambae hutokeza toka sifuru Anga na Ukiwa kadiri ya kambi mbili tafauti.
4. Enzini munamo hali moja tu,ya upekee pasipo utafauti wala mipaka,ni uwezo wa ajabu usio zaufika wala kushindwa,utukufu wa milele na milele.
5. Umungu ndio uzima kadiri ya ukamilifu.
6. Mkamilifu ni yule asiye kua na upungufu wowote,ambae huweza yote na hujua yote,anaye miliki ulimwengu na walimwengu pasipo kumilikiwa.
7. Hakuna tarehe ya kuanza kwake wala tarehe ya ukomo wake.
8. Hakika kuanza na kukoma ndio alama kubwa ya upungufu,ni uzaifu wa kushindwa kujieneza katika yote.
9. Muweza yote ni mwenyi milki ya ushindi ambae hutangulia kadiri ya kuenea.
10. Utangulizi wa ujuzi mbele ya vyote kupatikana ulimwenguni ndio «Uzima»
11. Yeyote aliye anza sio mzima na ndio maana hawezi kutokeza chochote toka sifuru.
12. Mungu mwenyi uzima ndio aliye na uwezo wa kuumba.
13. Aliumba tabaka la Anga chini yake,na akaumba tabaka la ukiwa chini ya Anga.
14. Enzi yake inapatikana juu ya ulimwengu,na Anga katikati ya ulimwengu,na Ukiwa unapatikana chini ya ulimwengu.
15. Akaumba viumbe vingi sana na kuvigawanya sehemu mbili yafauti: sehemu katika Anga na sehemu katika Ukiwa.
16. Na viumbe aliye wa pangiza angani ni wale ambae hupumua hewa,ambae hupatikana na pumzi ndani mwao.
17. Na viumbe aliye wa pangiza ukiwani ni wale ambae hawapumue wala hawalinde pumzi ndani mwao.
18. Wakaaji wa Anga wameitwa «wanaanga» ao «wanahewa»
19. Na Wakaaji wa ukiwa wameitwa «wakiwa» ao «wazila hewa».
20. Kunapatikana aina mbili ya wanahewa,na pia kunapatikana aina mbili ya wazilahewa.
21. Kuna wanahewa halali (halisi) na pia kuna wanahewa haramu.
22. Na kunapatikana wazilahewa halali,na pia kuna wazilahewa haramu.
23. Kuona kama angani munamo aina mbili ya viumbe ndio maana kunapatikana pia kambi mbili tafauti.
24. Katika tabaka la Anga,kunapatikana maala pa tukufu na kunapatikana maala pa dhalili.
25. Maala pa tukufu ndio mbingu,na maala pa dhalili ndio Hadeze.
26. Maana kunapatikana maki ya mbingu,inayo tenganisha sehemu hiyo mbili.
27. Huko juu ya maki ya mbingu ndio mbinguni na huko njee,chini ya maki ya mbingu,ndio "Hadezeni" .
28. Na huko chini, njee ya Hadeze, katika maunganio ya Anga na Ukiwa,ndio «Dunia».
29. Dunia ndio sehemu ndogo sana,maunganio ya Anga na Ukiwa:juu yake ni angani na chini yake ni ukiwani.
30. Duniani munapatikana wanahewa-haramu na wazilahewa (wakiwa).
31. Ni mkiwa-halali (muzilahewa- halali) yule anaye timiza sharti za mtengano na hewa,ambae hata chembe ya hewa haitumike umboni mwake.
32. Na pia ni mkiwa haramu(muzilahewa-haramu) yule ambae chembe ya hewa hushiriki umboni mwake pasipo kulinda pumzi.
33. Hiyo nusu ya hewa inayo tumika umboni mwa mkiwa haramu ni ndogo sana,ndio maana humsaidia tu kwa kugua (kuvuma) sio kwa kufikiri, sababu ya kutolinda pumzi ndani mwake.
34. Umbo lake halina ginsi ya hupumua ajili ya kutolinda pumzi,na ndio maana umbo hii haifikiri.
35. Umbo za wanahewa-haramu ni changachanga ya pumzi na mwili.
36. Mwanahewa haramu amepumua na amekula,hupumua ili pumzi ijenge umboni,na kula ili mwili ujenge sawa umboni mwake.
37. Hewa ndio nuru ya Enzi na mwili ndio giza ambae ni kinyume cha nuru.
38.Mfano wa Anga ni kama mwanga wa moto:ni mwanga katika utazamaji,na ni joto katika ugusaji.
39. Ndio mfano wa Anga uvuli wa Enzi:utazani ya kama hewa ni tafauti sana na fikara na ili hali ni kitu kimoja.
40. Kila kiumbe kinacho tumia hewa na kulinda pumzi ndani mwake hufikiri.
41. Na kila kiumbe kisicho tumia hewa wala kulinda pumzi ndani mwacho hakiwezi kufikiri.
42. Maana pumzi ni jengo la hewa ,na jengo kihewa ndio jengo la fikara
43. Asiye kua na mjengo kihewa,yaani asiye kua na pumzi hana fikara.
44. Na aliye na pumzi umboni mwake ndio mwenyi fikara.
45. Hewa humpa nguvu ya utendaji na pia humpa nguvu ya uzingatiaji.
46. Asiye kua na pumzi ndani mwake hafahamu chochote na pia hawezi lolote,anapatikana kadiri ya kupitiwa ,hana ginsi ya
kutenda.
47. Na ndio maana wanahewa ni wakubwa kuliko wazila hewa. Na wanahewa-halali ni wakubwa kuliko wanahewa-haramu
,maana wao ni watimilifu kifikara kuliko wenzao ambae huzaufishwa na mwili.
48. Wanahewa -halali wame pumua pasipo vituo maana ni pumzi tupu.
49. Na wanahewa-haramu ndio wanao pumua katika vituo ajili ya kuchangikana na mwili.
50. Na ndio maana wanahewa haramu hufikiri na pia hupitiwa,yaani wamezingatia na wame lala,
51. Kuzingatia ni tendo la pumzi,na kulala ni tendo la mwili.
52. Inapo changikana pumzi na mwili kua umbo moja,hushirikishwa fikara na ujinga.
53. Wakaaji wa Anga hujumuika angani na Wakaaji wa ukiwa hujumuika ukiwani.
87
54. Ispokua wanahewa-haramu ndio hujumuika katika maunganio ya Anga na Ukiwa.
55. Viumbe wanao jumuika angani ni Malaika na Roho,pia na Shetani na muzimu,na pia Mutu,nyama,ndege,vidudu,samaki...
56. Malaika na roho mbinguni;na Shetani na muzimu Hadezeni; na pia mutu,nyama,ndege,vidudu na samaki katika dunia
57. Na viumbe wanao jumuika ukiwani ni :udongo, maji,jiwe,muti,mumea,ujoga...
58. Hakika Mwenyenzi Mungu ni Mjuzi,mwenyi uwezo wa vyote,M'bora wa kuumba.
59. Ametokeza toka sifuru viumbe vingi sana bila kuiga mfano kwa yeyote,mkamilifu aliye juu.
60. Wanahewa-halali ni Malaika na roho...
61.Wanahewa-haramu ni:Shetani,muzimu,mutu,nyama,ndege,samaki,vidudu...
62. Viumbe ambae hujitenga na hewa mdio viumbe halisi vya ukiwa.
63. Na viumbe ambae hujitenga na mwili ndio viumbe halisi vya Anga.
64. Wanahewa-haramu ni changachanga ya pumzi na mwili.
65. Kujitenga kwa pumzi na mwili ndio kifo duniani na ndio kuzaliwa mbinguni ao Hadezeni.
66. Mwili ndio unao mfanya mutu ajumuike duniani.
67. Na pumzi ndio inayo mfanya mutu ajumuike mbinguni ao Hadezeni.
68. Hakika kupumua hewa ndio kutumia fikara, asiye pumua hewa hawezi kufikiri hata kidogo.
69. Hewa huchamusha ukiwa namna ya kuguisha kwa msaada waji itakayo mawinguni.
70. Katika tabaka la Anga kunapatikana: mbingu,hadeze na sehemu (chembe) ya dunia.
71. Kila kambi huko juu angani iko na baraza yake ambae ni upande wa nyuma ya maki yake.
72. Upande wa nyuma kugusiya maki ya mbingu ndio baraza la mbingu.
73. Na upande wa nyuma kugusia maki ya hadeze ndio baraza la hadeze.
74. Ni kwamba baraza hizo ni katika maunganio ya mbingu na Hadeze,mfano wa kituo kabla ya kuingia kambini.
75. Huketi katika baraza la mbingu pumzi urakibuni.
76. Na pia huketi katika baraza la Hadeze pumzi uatiduni.
77. Mbingu humeremeta na nuru kubwa maana anga yake ni ya kumwanzo karibu na kisima cha nuru.
78. Na ndio maana wakaaji wa mbingu ni wenyi fikara kubwa zaidi ya viumbe wenzao,kwani wametumia nuru ya ku shina karibu na ujuzi.
79. Na Hadeze ni yenyi kuchakaa hali ya kuzoroteka kabisa,ni yenyi kufifia kadiri ya giza ajili ya kupatikana njee ya mbingu,mbali na chemchem ya nuru.
80. Na ndio maana wakaaji wa hadeze ni wenyi fikara zaifu sana yenyi kufifia sana;lakini huchugua nafasi ya pili ajili ya asili yao,(ya ulimi wa moto)
81. kwa maana mbingu ni juu na hadeze ni chini,mfano wake ni mlima na bonde ;
82. Nilazima kupanda kwa kufika mlimani na pia kushuka kwa kufika bondeni.
83. Na kuona kama mbingu na hadeze ni angani,matendo ya kupanda na kushuka ni hewani.
84. Mutu amepatikana pa shina ya mlima na bonde
85. Malaika na roho mlimani husimamia uzuri,na Shetani na muzimu bondeni husimamia ubaya.
86. Hualika watu mlimani kwa njia ya ukweli,na pia hualika watu bondeni kwa njia ya uwongo.
87. Wametetea watu ili wapate kundi la kujumuika nalo kambini mwao.
88. Na watetezi wa Shetani na muzimu ni wenyi husda na kibri na pia wachawi.
89. Watetezi wa malaika na roho ndio ma Nabii na Mitume.
90. Na atakaye fuata ma Nabii na Mitume,hupaa mlimani.
91. Na atakaye fuata ma hasidu na wachawi,huporomoka bondeni.
92. Mlimani kuna heshima na amani ya milele,lakini bondeni kuna aibu na mateso.
93. Malaika na roho huporomoka kwa kumjaa mutu duniani maana hutokea juu.
94. Na Shetani na muzimu hupanda kwa kumsibu mutu duniani maana hutokea chini.
95. Malaika amekaribiza roho ya mutu kwa kishangwe,na kumuweka katika starehe ya milele.
96. Na Shetani amevamia muzimu wa mutu kwa kasirani kubwa,na kumuingiza kama mfungwa ndani ya jela.
97. Eh Mwenyenzi Mungu Mtukufu! unifanye kua roho takatifu na kunikaribiza mbinguni kama mfalme ,na kumeremeta kama
jua,ni kifinikwa bawa la mfalme wa malaika zako.
98. Ufalme wa ulimwengu wote umekustahili peke yako muweza yote anaye tosha watu katika vifungo vya wachawi na
kuwasafisha walio najisika.
99. Mola wangu! ni nusuru kutokana na zulma pia na masingizio ya watu wa dunia.
88
100. Na unipatie nguvu ya kushinda falme za giza,na ujitukuze ndani mwangu kama ulivyo jitukuza ndani yaMussa,na ndani ya Eliya ,na ndani ya Muhamadi,na ndani ya Ibrahimu...
101. Na ndani ya Yesu Masiya,mwana kondoo wa Mungu ,nabii mwenyi ufalme.
102. Mola wangu! uwasamehe wote walio nikosea,kwa rehema zako wala yeyote miongoni mwao asiangamie ajili yangu lakini ajili ya nafsi yake mwenyewe.
103. Mapenzi yako yafanyike,sio kama ninavyo taka mimi ispokua kadiri ya idhini yako tukufu .
104. Ee Muumba wangu! ulinzi wa Anga na Ukiwa ni katika uwezo wako, kwa uwingi wa rehema zako amani hunifikia,na kwa njia ya neno lako maisha hunipitia, unisamehe, na unibarikiye, na uniokoe Ee Muumba wangu,maliza shauku langu kunipatia kinywaji.
105. Mola wangu! unikinge na kila hatari na unijaalie mema ya ulio niumbia,na unifanye kua wokovu wa watu. .
3 . MAJIRA
1. Nuru ya Mwenyenzi Mungu imetawanyika pahali pote katikati ya ulimwengu,ni utukufu wa dhati yake m'shindi aliye juu.
2. Hujikusuru waliyemo nuruni kuliko waliyeko njee,ajili ya kuzingatia.
3. Furaha ilioje kwao wenyi pumzi! hakika wao ni wenyi ginsi ya kujikusuru na kuzingatia kwa msaada wa jaza lao.
4. Nuru hutokea ndani ya taa ya ulimwengu,humeremeta wote wanao jumuika.
5. Hakika pumzi ni jengo la hewa iliye umbwa kwa anga kadiri ya gandamano kihewa.
6. Hewa ni mfano wa umeme,kama bado hauja tiliwa chomboni hauwezi kutenda,lakini kukapatikana umbo inayo hitaji
hewa,ndipo hewa hutumika ndani mwake.
7. Hewa iliyeko karibu na Enzi ndio kubwa zaidi ya hiyo ya huko karibu na ukiwa.
8. Na hewa ya inchikavu hailingane na hewa ya baharini.
9. Na kama mutu anaingia ndani ya maji atazania kama hamuna hewa.
10. Maki ya hewa ya huko,kutolingana na umbo lake,anazania kama sehemu hiyo hakuna hewa.
11. Mwanahewa-haramu anaye ishi ndani ya maji,ni tafauti kabisa na yule anaye ishi inchikavu.
12. Wa inchi kavu hawezi kupumua ndani ya maji na pia wa mu maji hawezi kupumua inchikavu,ispokua umbo la kati na kati
ambae kaumbwa namna hiyo.
13. Kazi ya hewa imehusika na Fasi ya kutumikia,kukakutanika maki ingine fulani,hewa hufifia,ajili ya kuchangikana.
14. Hewa haimalizikake,lakini umbo lake lika bomolewa husalia hewa tupu katika kawaida yake na umbo hiyo hupotea.
15. Hewa haiweze kumalizika yote namna ya kukauka sababu ni nuru ya taa isiyo zimika.
16. Kuzimika kwa taa ndio kumalizika kwa nuru .Ajili ya utukufu huo,maisha ya milele hupatikana angani,namna ya kutozimika.
17. Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu aliye umba anga na ukiwa kadiri ya tabaka mbili tafauti.
18. Akafanya hewa kadiri ya nguvu,na Akafanya ukiwa kadiri ya uzaifu.
19. Aliye na nguvu ndio anaye mumiliki aliye zaifu ,ndio maana hewa hutumikisha ukiwa.
20. Hakika mwili pasipo pumzi ni bure kabisa,pumzi ndio hutumikisha mwili maishani.
21. Utazani roho yamutu hunyanyua ardhi na mikono yake miwili juu.
22. Pumzi ya mutu ni yenyi nguvu ya kutetea namna ya kutumia umbo zote za kiukiwa.
23. Nguvu ya hewa ndio hunyanyua ardhi juu,na pia ndio inayo nyanyua kila umbo lenyi uzito kimwili na kulibandikiza kwenyi
ardhi ambae ndio mwili mzito zaidi.
24. Na ajili ya nguvu ya hewa,hakiponyoke chochote kwa kuanguka ijapokua kuzunguuka kwa ardhi angani.
25. Hewa huchamusha ardhi,hata maji ikichamuka ndani mwake na kupasua ardhi kadiri ya chemchem na kutiririka juu yake
kadiri ya mtoni.
26. Hata ikifikia muvuki ufumuke ardhini na kupanda juu na kugeuka wingu la nvua.
27. Mwenyenzi Mungu hutafautisha nyakati maala mbali mbali kwa kufanya vitimbi hewani ,ambae hupoza ukali wa mwanga
wa jua viongezekapo,na vipunguapo mwanga wa jua huzidi kua mkali.
28. Wakati huo mawingu huyeyuka na ukali wa mwanga wa jua,hata kukipatikana maji itokayo mawinguni,inayo itwa nvua.
29. Na pia mawingu hugandana wakati mwanga wa jua hupozwa na vitimbi vya hewa.
30. Sema: ni ajili ya utafauti wa umbo za wapumuao ndio maana hawafanane kifikara:kila yule huvuta hewa kadiri ya umbo lake.
31. Ni mfano wa umeme ,ukitiliwa mu pasi hutoa joto ndani mwake,na katika taa ,hutoa mwanga ndani mwake...haufanye
lolote kama hauja tiliwa chomboni
32. Ndivyo pia kuhusu hewa umboni,kila yule hufikiri kadiri ya umbo lake.
33. Mwenyenzi Mungu hapana mwengine ila yeye-mwenyi kugawanya fadhila yake duniani kama vile mbinguni. Akifanya vitimbi hewani kwa nyakati maalumu,mara huongezeka na mara hupunguka.
34. Na pengine huimarisha vitimbi vya hewa pasipo mabadiriko yoyote.
35. Na pengine hukosekana huo mchamuko kihewa hata vitimbi vyake hukosekana pia.
89
36. Sababu hiyo,utakuta maala « nvua» hunyesha na ambae hainyeshe.
37. Maala ambae nvula hunyesha muda fulani na ambae hainyeshe muda fulani,hata kukipatikana nyakati tafauti.
38. Aliye na pumzi umboni mwake ndio mwenyi maisha ajili ya kufikiri.
39. Kuona kama kufikiri ndio kuishi,yeyote asiye fikiri hana maisha.
40. Maisha ya mutu ni tafauti na maisha ya wanahewa haramu wengine.
41. Mutu ametetea ili apate kufuzu starehe ya mbinguni,kinyume na utetezi huo,maisha yake hukoma.
42. Hufuzu starehe ya mbinguni yule anaye amini Mungu Mwenyenzi na kumuabudu yeye peke yake.
43. Wanahewa-haramu wengine hawana akili na ndio maana hawakupewa neno la Mungu.
44. Neno la Mungu halikuja ispokua kwa wenyi akili,asiye kua na akili hawezi kuamini wala kuabudu ,na ndio maana hawana
maisha ya milele.
45. Uzima ndio umungu,hali tukufu ajabu isiyo zaufika wala kufananishwa,mamlaka ya vyote juu ya yote,milele na milele
46. Angani kuna maisha ya muda na maisha ya milele
47. Maisha ya muda ni kwao wasio muamini Mungu ambae hawana akili.
48. Na maisha ya milele ni kwao wenyi akili ambae humuamini Mungu Mwenyenzi na kumuabudu yeye peke yake.
49. Maisha ya milele ni hali ya kuanza bila kukoma,mfano wa nuru ya taa isiyo zimika.
50. Ni kama kistari (cha usawa) kilicho na mwanzo pasipo hatimaye,mfano wa hunusu.
51. Na maisha ya muda ni kama kistari (cha usawa) kilicho na mwanzo pia na mwisho,kadiri ya kipande.
52. Kuona kama hakuhelekea Enzi,ndio maana huatarika kwa kupatwa na ukomo.
53. Na upatikanaji ni mfano wa jangwa,ndani mwake hamuna chemchem wala nvua,mboleo wala mimea,yeye sio kistari ajili
ya ukosefu wa fahamu.
54. Mpatikanaji ni yule asiye kua na maisha,ambae hana fikara ajili ya kutokua na pumzi,bali hujumuika kiumbile namna ya
kupitiwa.
55. Muumba kawafarijini kwa jaza lake maalumu,hewa ,ambae kuogelea humo Aina na aina ya viumbe.
56. Pasipo hewa mwanga hauwezi kuangaza,wala sauti kusikilika,maana hakuna kifaa kingine cha kutawanyikia.
57. Mwanga na sauti hutembea hewani, wala haoni wala hasikie ispokua aliye na pumzi.
58. Ndege na vidudu...hutembea hewani,namna ya kuogelea kwa kuvua na mabawa yao, na samaki kwa vipepe vyake majini.
59. Hakuna ufundi bila hewa,wala tendo lolote kwa mwanahewa pasipo hewa.
60. Na hewa na maji,muvuki na wingu linalo yeyuka,ndege hewani na samaki majini, jua na mwanga wake hewani.
61. Pumzi mwilini,sehemu mbili umboni mwa mutu,fikara na ujinga.
62. Hakika Muumba wa viumbe ni muujiza wa maajabu,uwezo usio na kipimo,mwenyi uzima.
63. Humiliki vyote kwa idhni yake,wala hakuna ligumu kwake,Mola wa pekee bila mfano wake.
64. Viumbe vyote humtegemea,Mtukufu asiye zingatiwa na wapumbafu,Mola wa Enzi tukufu ,mwenyi kuachana na umbo zote.
65. Aliye fanya pumzi ichamushe mwili na ku usimamia kimatumizi.
66. Mungu huendelea ngambo zote kadiri ya kuenea ,mwenyi ukamilifu kuliko vyote.
67. Mwenyi ukarimu,mnara wa nuru juu ya ulimwengu,atakasikaye na ashindaye.
68. Ametenda katika kujua ,ulimwengu na walimwengu sio chochote wala lolote pasipo Mungu.
69. Hupatikana viumbe ajili ya Mungu kutangulia .na ingawa kama hasingeli tangulia,sifuru ingeli tawala milele.
70. Hakika upatikanaji wa viumbe ni miongoni mwa alama ibainishayo uzima wa Mungu.
71. Mungu alimupatia mutu pumzi yenyi ginsi ya kumzingatia ili apate kumuabudu.
72. Ni heri mutu anaye zingatia vitimbi vya Muumba wake na kumuabudu katika yakini.
73. Na anaye zingatia utukufu wa Enzi sio wa mwili bali wa roho.
74. Nuru hutawanyika angani na giza hutawanyika ukiwani;ndio maana hufifia Anga iingiliwaye na giza,na hungara ukiwa
uingiliwayo na nuru.
75. Jaza la nuru ya uzima katika urithi wa Shahidi wake;na mtiririko wa maji umefungua panzia la mbingu,hata ikinishukia baraka yake tokea mbinguni.
76. Na agano la Mungu,na taji la utukufu wake juu ya kichwa chake.
77. Ee mola wangu! unisamehe,na unibarikie na uniokoe,naeunitimizie mapenzi yako duniani na mbinguni.
4 .KADARA
1. ulimwenguni kuna Mungu aliye tangulia, mfano wa chemchem ya upatikanaji na maisha.
2. Yeye ni muujiza wa maajabu:alitangulia kimuujiza na akatokeza toka sifuru kwa maajabu.
3 . Hali yake ni uzima, hana maanzio wala makomeo, M'bora wa kuenea.
4 .kuanza kwa kitu ni kuumbwa kwacho,na yeyote aliye umbwa ni kiumbe.
5. Mungu atalazimika kuanza,hulazimika kua kiumbe;Eti hakustahiki kuwako Muumbaji ispokua viumbe peke yao?
6. Kwa kiumbe kupatikana,inatakika kutangulie mjuzi atakaye kitokeza.
7. Hakungelipatikana kiumbe hata kimoja pasipo utangulizi wa mwenyi ujuzi,maana kungeli kosekana fundi wa kutokeza.
8. Mungu ndio mwanzo wa vyote,angelikua na mwanzo wake hasingelikua muumba lakini kiumbe.
9. Mungu hana mwanzo wala mwisho sababu yeye ni Mkamilifu.
90
10. Kua na mwanzo pia na mwisho ni kua mpungufu.
11. Huweza yote ajili ya kujua yote, Mkamilifu aliye Enzini.
12. Enzi yake hutawala maala pote, nuru yake tele angani,ni yeye muweza na Mjuzi,aliye na uzima.
13. Itakua-je kwa yule aonaye fikara kiisha aka kanusha ujuzi? ao kwa yule aonaye hewa kiisha aka kanusha Enzi? ao kwa
yule aonaye mwanga kiisha aka kanusha taa?
14. Hakika uvuli haupatikani pasipo kitu chenyewe kutangulia,wala viumbe pasipo Muumbaji.
15. Utangulizi mbele ya vyote ndio mamlaka ya umungu .
16. Anaye tangulia yote,huzidia yote.
17. Hakika Mungu ni mwenyi ushindi juu ya kila kitu,Mtukufu wa popote na milele.
18. Mungu ndio mwenyi kuona pasipo kupitiwa na chochote muda wote,pahali pote ulimwenguni
19. Viumbe hutazama kwa kuzingatia,hawaoni ispokua kidogo tu ajili ya uzaifu wa macho yao.
20. Haonani na Malaika uso kwa uso ispokua mwenyi akili timamu,na pia haonani na Shetani uso kwa uso ispokua pumbafu.
21. Huonana uso kwa uso ambae hulingana katika fahamu.
22. Kuona ni kufahamu,na kuona yote ni kujua .
23. Hakika muonaji wa vyote ulimwenguni ni Mungu ambae peke yake hujua yote.
24. Mungu hayupo angani sababu yeye sio mwanahewa ,wala ukiwani sababu yeye sio mkiwa.
25. Mola wenu hustawi katika utukufu wa ajabu,Enzini ,mahala ambae hakujumuike mwengine wala kukurubiwa,ajili ya
ushindi na uhuru .
26. Hasingeli kua huru kama angeli jumuika na kushurulika,na ili hali mshindi aliye huru ni mkamilifu ;hastahili kuchangia fasi
na yeyote wala hastahili kukumbwa na shuruli yoyote ile.
27. Hali kama hiyo ya kutojumuika humfanya awe katika uhuru,hali ya kujua pasipo kufikiri na pia kutenda pasipo kutumika.
28. Yeyote anaye fikiri ao anaye tumika hana uhuru.
29. Mungu ni hodari mwenyi utukufu,huepukana na utetezi ajili ya kukamilika.
30. Hakuna kosa katika kuumba kwake,vyote ni sawa katika maisha ya jumla ya viumbe.
31. Ambae ni mubaya kwako,ni nzuri kwa mwengine.
32. Ni kwamba hakuna asiye pendeza wala asiye chukiza,miongoni mwa wanahewa (viumbe).
33. Humlaumu Mungu ajili ya kuumba umbo fulani yule aliye na elimu ndogo, na pia yule asiye jali maisha ya mwengine.
34. Ni bora zaidi utafauti wa umbo kadiri alivyo umba,kuliko kurudishia umbo moja moja tu,na ili hali mjuzi anaye umba
hashindwi kutokeza mapya.
35. Kuona kama kuna viumbe vingi ndio maana kuna patikana vifaa vingi vya maisha ya mutu.
36. Kila kiumbe ambae hupatikana kimependwa na Mungu.
37. Sio kwamba kupendwa na Mungu ni kufanya mapenzi yake tu,lakini hasa ni kuumbwa.
38. Kuona kama wenyi mila nzuri ndio watakao pewa maisha ya milele,husemekana wao ndio wa pendwa wa Mungu
Mwenyenzi.
39. Maadamu wazuri huishi milele,ni kwamba mapenzi ya Mungu ambae hupatikanisha ni juu yao siku zote.
40. Na kuona kama wenyi mila mbaya ndio watakao pewa mauti, husemekana wao ndio wakataliwa wa Mungu Mwenyenzi.
41. Maadamu wabaya watakosekana milele,ni kwamba mapenzi ya Mungu ambae hupatikanisha hukosekana kwao baadaye.
42. Lakini kama angali na ishi yeyote, hupendwa na Mungu;maana kinacho mfanya aishi ni hiyo mapenzi ya Mungu ambae
hupatikanisha.
43. Mila nzuri hulazimika kwa watu sababu ya kusalamisha umbo zao kwa kupata maisha ya milele.
44. Na mila mbaya hukatazika kwa watu sababu huhatarisha nafsi zao kwa kupata mauti ambae ni ukomo na upotevu.
45. Ni kwamba ubaya huatarisha na uzuri husalamisha nafsi .
46. Heri utetezi wako ukupatishe maisha ya milele,ukipata kufuzu mazao ya zamiri yako.
47. Maisha ya Mutu ni katika masanganjia: kuume kwake mema,na kushoto kwake mabaya,ni tayari kwako njia utakayo
chagua.
48. Shuudieni uzima wa Mungu kikweli,wala usikufuru katika masemi yako wala katika matendo yako.
49. Usimlaumu Mungu ajili ya ku kuumba ulivyo wala usitamani umbo ya mwenzako na kukataa umbo lako mwenyewe.
50. Amekufanya ujaze hapa na yule ajaze pale ili kila yule afae katika jumuiya la wapumuao.
51. Hakuna urithi katika umungu maana mamlaka yake haina ukomo.
52. Shuudieni Mwenyenzi Mungu, Mufalme wa ajabu,ambae humhelekea kwa kumkimbilia wote wanao pumua,Mola wa
karne na karne, tumaini la walimwengu.
53. Mungu kufanya siku ya mwisho sio kuchoka kusimamia,bali hutenganisha adili na batili, ili kila yule apate kuvuna aliyo ya
panda.
54. Hali yake Mungu ni uzima,ni utangulizi wa ujuzi,uwezo wa kuenea.
55. Kipimo hakipatikane ndani mwake,akadiriaye pasipo kukadiriwa,na kumiliki bila amri ya yeyote,na kutawala juu ya palipo
juu,Mtukufu azidiaye na awezaye.
56. Ni yeye ajuaye yalio pita,ya sasa na yatakayo kuja, hajifunze wala hasahau,ijapokua ni mbele ao nyuma ya wakati miongoni
91
mwa nyakati. Mjuzi asiye kadiriwa.
57. Muweza ni Mungu,mamlaka ya kumiliki,ni ajabu maarifa yake,ushindi wa milki yake.
58. Sura ya Mungu ni ukamilifu,namna ya kuenea katika yote.
59. Tumaini na nguvu ya kila umbo,hakuna mamlaka kinyume naye,wala msaada badala yake,Mubora wa wanao ruzuku.
60. Rangi ya Mwenyenzi ni utukufu wa dhati yake: Mungu kama taa na rangi yake ndio nuru yake.
61. Aliye jipakaa rangi ya Mwenyenzi ni yule aliye wa roho,ambae hujaa imani.
62. Utajiri wa mutu sio mwilini mwake lakini rohoni mwake.
63. Roho ya mutu ni pumzi urakibuni,wingi wa wema wake ndio wingi wa mali yake.
64. Uumbaji hauna ukomo wake maana ujuzi unao umba hauna ukomo; kadiri idhni yake huendelea ndivyo pia uumbaji wake
huendelea.
65. Mungu sio roho,lakini uzima.
66. Uzima ni ukamilifu kadiri ya kuenea kimilki,uwezo wa ajabu usio zaufika ambae hutenda bila kutumika,mamlaka ya vyote
ulimwenguni.
67. Shina la vilivyomo kadiri ya ulinzi wa upatikanaji na maisha:milki ichipuayo taa iangazayo.
68. Neno la Mungu ni dawa ya kila magonjwa,matumizi yake ni matibabu ya nafsi.
69. Penda Muumba wako zaidi yako mwenyewe,na jerani yako kama unavyo jipenda mwenyewe.
70. Anaye mpenda Mungu zaidi yake mwenyewe,hupupia kutimiza amri ya Mola wake kuliko shuruli zake binafsi,akihifazi
mipaka yake kinyume na tamaa ya nafsi yake, akimkumbuka Mola wake kila wakati na kumuabudu kila siku.
71. Ibada ndio mwanya wa waaminifu,na Shirki ndio mwanya wa makafiri.
72. Jihadharini nafsi zenu musije kumlaumu Mwenyenzi ku vyovyote : wala musiseme kwanini Mungu amefanya ivi, ao
«pahali Mungu angefanya ivi».
73. Hakika kumlaumu Mungu ni zambi,kufru ya namba ya juu.
74. Kadara ya Mungu ni makadirio yake kwa watu ambae ni yale anao taka yafanyike kwenyi kiumbe chake mutu,yaani sheria
yake yenyi maamrisho na makatazo.
75. Ni amri kila mutu Kuamini kadara ya Mungu.
76. Na kuamini kadara ya Mungu ni kukubali kwamba shari na mema imetoka kwa Mungu.
77. Kukubali ndio kutii,na shari ndio makatazo na mema ndio maamrisho ya Mungu.
78. Ni kwamba kukatazika na yale ambae Mungu kakataza na kutumikisha yale ambae Mungu kaamrisha ndio kuamini kadara
ya Mungu.
79. Na kufikiwa na yale usio helewa wala usio ya taka ambae hauna elimu wala uwezo wa kuyahepuka bila wewe kumlaumu
Mungu wala kukufuru.
80. Ukisimama imara kwa kusubiri na kushukuru,yakini kwamba muweza yote na mjuzi wa yote ni Mungu peke yake.
81. Ni kuamini kadara, maana umetumia maamrisho ya Mola wako ya kusubiri bila kukufuru wala kulaumu.
82. Hekima na elimu ya kutojilinganisha na Mola katika fahamu wala katika uwezo,yakini kwamba wewe ni m'pungufu asiye
kua na uwezo wa vyote wala fahamu ya vyote.
83. Yakini kwamba shida na magumu ni kawaida kumufikia kila mutu ajili ya uzaifu wake ndio kufanya mapenzi ya
Mungu,yaani kuamini kadara.
84. Atakaye kufuru ao kumlaumu Mola wake katika magumu ao katika shida ndio asiye amini kadara,maana ametenda zambi.
85. Ni upumbafu sana,baada ya kutenda zambi,useme: ni kadara ao iliandikwa.
86. Jihadharini nafsi zenu na masingizio musije mkamuzingizia Mola wa ulimwengu.
87. Atakaye tumia maamrisho ya Mungu,bila shaka,atakutana na heri.
88. Na atakaye tumia makatazo ya Mungu,bila shaka,atakutana na shari.
89. Mwenyenzi Mungu- hakuna mwengine ila yeye pekee, mtoaji wa neno ambae huongoza kwa pumzi itokayo kwake,ngome
mazubuti la waaminifu.
90. Tabaka la Enzi ni siri ku watu wa dunia ajili ya giza iliyemo duniani,na ni bayana ku watu wa mbingu ajili ya nuru iliyeko
mbinguni.
91. Hakika ya mutu,sio mwili wake,lakini roho yake na ndio maana uzuri wa mutu sio urembo wa mwili wake,lakini urembo
wa roho yake.
92. Hakuna mauti mbinguni ajili ya uzuri,na pia hakuna maisha ya milele hadezeni ajili ya ubaya.
93. M'bora wa kuumba alipenda kupatikane umbo la kati na kati.
94. Akaweka mutu pa masanganjia,kuume kwake uzuri na kushoto kwake ubaya.
95. Akamupodoa kwa kumupatia akili, ili apate ginsi ya kujichagulia njia.
96. Mola hakupenda masanganjia ibaki wazi pasipo umbo maalumu.
97. M'bora wa kuumba ambae harudishie umbo moja moja katika kuumba kwake,bali hutokeza aina na aina za viumbe,sura na
kazi tafauti ijapokua idadi yao,bila kujifunza wala kuiga maana yeye ni Mkamilifu mwenyi kujua yote.
98. Mola wenu ni Mjuzi,Mtukufu asiye kua na doa,shina la vyote vilivyomo,ambae vyote humuitaji Mshindi aliye juu.
5 . PANZIA
1 Mungu aliumba viumbe vingi sana na kuvipangiza maala mbali mbali kufatana na umbile zao.
5.Akatenganisha wakaaji wa mbingu na wakaaji wa Hadeze,pia wakaaji wa Dunia.
6.Akawakabiza Malaika na roho bahazi la mbingu.
7.Na akawakabiza Shetani na muzimu bahazi la Hadeze kua kambi lao.
8.Na akamukabiza mutu na minyama...Dunia kua kambi lao. 9.Akatenganisha kambi zao kwa panzia na ili hali wote hujumuika angani.
10.Panzia hizo huwafanya wasizingatiane sawa sawa.
11.Wakaaji wa dunia hawaoni ila duniani tu ajili ya kutazama kimwili.
12.Na wakaaji wa hadeze huzingatia hadezeni pia duniani ajili ya kutazama kizimu.
92
13. Na wakaaji wa Mbingu huzingatia mbinguni na duniani ajili ya kutazama kiroho.
14. Mutu aliye katika mwanga haoni ispokua maala pake,lakini aliye katika giza huzingatia maala pake pa giza na pia
huzingatia pahali palipo mwanga.
15. Haiwi nuru ambae hufumba macho,wala sio giza ambae hufumbua macho.
16. Ambae ni nuru kimwili,ni giza ki roho,na hivi hivyo pia kizimu
17. Ndio mfano wa wanahewa-haramu,wamezingatia tu duniani,wala awazingatie mbinguni ijapokua sehemu zote mbili
hupatikana angani
18. Hayo kusababishwa na utafauti wa fikara yao.
19. Kwa kuwaona wanahewa halali,inabidi watu watumie taa zao namna ya kuwachanika.
20. Kuona kama mbingu na hadeze ni tafauti,taa zao pia ni tafauti.
21. Taa ya kuchanika ili upate kuzingatia mbinguni ndio « Ibada » ambae hufungua panzia ya mbingu na kuwa dhihirisha
malaika na roho.
22. Na taa ya kuchanika ili upate kuzingatia hadezeni ndio Uchawi (urozi) ambae hufungua panzia kuwa dhihirishia ma shetani
na mizimu.
23. Atumiaye ibada hujumuika mbinguni baada ya pumzi yake kuachana na mwili,hali ya kua « roho « .
24. Sio hali ya kua malaika kabisa ajili ya utafauti wa asili yao.
25. Na atumiaye uchawi,hujumuika hadezeni baada ya pumzi yake kuachana na mwili wake,hali ya kua « muzimu >.
26. Sio hali ya kua Shetani kabisa ajili ya utafauti wa asili yao
27. Kuona kama Malaika na roho ni umbo mbili tafauti,kambi zao pia ni tafauti
28. Fasi anapo keti muzimu humo hedezeni ndio Zimu.
29. Na fasi yenye Shetani anapo ishi humo hadezeni ndio «Zalala» ao « Zwalamu ».
30. Na fasi anapo ishi Malaika humo mbinguni ndio «Zamana».
31. Na fasi anapo ishi Roho huko mbinguni ndio «Bustani».
32. Bustani ni kambi la mbinguni ambae hujumuika watu wema wafanyao ibada duniani.
33. Na Zimu ni kambi la hadezeni ambae hujumuika watu wabaya watenda zambi duniani.
34. Katika bustani hupatikana starehe kubwa maana zamana ni ulinzi wa bustani.
35. Na Zimuni hupatikana magumu ya kila aina sababu zwalamu (zalala) ni uangamizi wa zimu.
36. Ni kwamba malaika hulinda vizuri Roho bustanini akijifanya mtumishi wake.
37. Na Shetani huangamiza sana mizimu Zimuni akijifanya bwana wake.
38. Malaika zamanani na Roho bustanini,katika sehemu ya juu angani
39. Na Shetani zalalani (zwalamuni) na muzimu zimuni katika sehemu ya chini angani.
40. Na mutu duniani katika maunganio ya Anga na Ukiwa masanganjiani.
41. Humtetea Mutu kwa uzuri zamanani,pia humtetea mutu kwa ubaya zalalani.
42. Sehemu ya juu Angani hupatikana utukufu na katika sehemu ya chini Angani hupatikana udhalili.
43. Kambi mbili tukufu hupatikana mbinguni (sehemu ya juu angani), jaza urakibuni.
44. Na dhati mbili dhalili hupatikana Hadezeni (katika sehemu ya chini angani),jaza uatiduni.
45. Katika utukufu kuna dhati kimalaika na dhati kiroho.
46. Na katika udhalili kuna dhati kishetani na dhati kizimu.
47. Dhatini mwa malaika hutokea «Unabii»,na dhatini mwa roho hutokea «Uwalii».
48. Na dhatini mwa shetani hutokea «Uhasidu»,na dhatini mwa muzimu hutokea «Urozi».
49.Nabii wa Mungu ni yule ambae Mungu amemchagua na kumteremushia wa malaïka,ambao humuinua na kumtuma ku watu.
50. Na Walii ni yule ambae Mungu amemteremushia Roho namna ya kumuinua ku watu
51. Kuna aina tatu ya uwalii : usidiki, ushahidi na usalihi
52. Walii anaye inuliwa na kutumwa,yaani anaye pewa utume ni miongoni mwa Mitume yake Mwenyenzi.
53. Utume umepatikana sana katika usidiki na ushahidi.
-
Na ma Nabii wengine hufunuliwa kwa namna ya kuachana,lakini nguvu ya Mungu ndani mwao ni Malaïka pia na Roho.
-
Malaïka alimtangulia Roho dhatini mwake Nabii.
-
Na Roho alimtangulia Malaïka dhatini mwake walii.
-
Na Hasidu ni yule anaye jazwa na Shetani na kusharikiana naye.
93
-
Na mrozi ni yule anaye jazwa na mizimu,namna ya kusharikiana nayo.
-
Ma Hasidu na warozi ndio watetezi wa Shetani,ambae humsaidia kupoteza watu mbali na njia.
-
Shetani alitangulia muzimu dhatini mwake hasidu.
-
Na muzimu alimtangulia Shetani dhatini mwake mrozi.
-
Maki ya mbingu ni mfano wa tungi kandokando mwa taa ambae huzagaa.
-
Taa haitoi ndani mwake ispokua nuru ambae ni sehemu ya utukufu wake.
-
Nabii wa Mungu ni mwenyi elimu na hekima,na maarifa zaidi ya watu wengine.
-
Yeye ni neno,nuru na nguvu ya Mungu Mwenyenzi.
-
Mfano wa milima ardhini,mamlaka ya uongozi ili ardhi ipate kusimama sawa.
-
Hakuna umati pasipo Nabii,wala Nabii pasipo umati.
-
Mwongozo uliwafikieni nyinyi wote kutoka kwa Mungu, haikuchelewa kaumu hata moja.
-
Kitabu hiki ni nuru kubwa ambae huwafanya watu wakuwe na yakini.
-
Kukosa yakini kunawafanya wakuwe makafiri na wanafiki.
-
Ukafiri ni kwa yule ambae bado kupokea neno la Mungu.
-
Na unafiki ni kwa wale walio silimu bila yakini.
-
Hakuna ulizo mbaya kuhusu Mungu,na Malaïka zake pia na Roho zake.
-
Wala hakuna ulizo mbaya kuhusu ma Nabii na Mitume,yaani kuhusu neno la Mungu.
-
Wala Hakuna ulizo mbaya kuhusu ulimwengu na walimwengu.
-
Uliza yale usiyo ya fahamu ili upate kuhelewa,na ujibie yale unayo fahamu utakapo ulizwa.
-
Asie kua na masikio ya kusikia neno la Mungu na asiye kua na macho ya kuzingatia uzima wa Mungu ni mauti.
-
Enyi wanaadamu! Someni neno la Mungu na pia tafuteni yakini.
-
Nuru ya Mungu imekwisha angazia watu wote: weupe,wekunda,weusi bila ubaguzi.
-
Kilicho muimu apa sasa ni kutafuta yakini, ukweli huu ni uyakini wa uzima wa Mungu pia na neno lake.
-
Ni nuru ambae humshukia shaidi wake KALONDA juu ya mlima Karombwe.
-
Nuru ya mwezi na nyota na jua inayo angaza duniani.
83. Na atakaye amini ujumbe huu atakua «Yakini» na uzima wa Mungu pia na ujumbe wake ,ndio maana nafsi yake
itameremeta mfano wa nuru.
6 . UMUTU
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,muanzishaji wa ulimwengu,atanguliaye kwa mamlaka yake mwenyewe.
2.Mwenyi kuenea kadiri ya uzima,amekua yote katika kuwako na yote katika kuweza na yote katika kujua,mtukufu aliye
juu.
3. Ujuzi wake ni mamlaka kubwa zaidi ya kila kitu, haujumuikake ajili ya utukufu wake wa ajabu.
4. Hakuna umbo itakayo weza kulinda ujuzi nafsini mwake bila kufutika na kukosekana ulimwenguni.
5. Ni uwezo wa ajabu kadiri ya muujiza unao waka na kurarua zaidi ya moto
6. Utukufu wake umefanya ajae katika yote,mwenyi kuenea
7. Enzi yake haiwezi kuingia ndani ya mutu,wala ndani ya malaïka,wala ndani ya roho wala ndani ya Shetani,wala ndani ya
muzimu...
8. Enzi sio mfano wa hewa ambae huingia ndani ya umbo mbali mbali na kujenga kumo kadiri ya pumzi
9. Umbo yote ni zaifu haistahili kukurubia milki kamilifu
10. Maana kugusana na uzaifu ao upungufu ni kuzaufika ao kupungukiwa
11. Hayo ni mbali kabisa na sifa yake,hazaufikake wala hashindwake, Mzima aliye juu
12. Ujuzi haupatikane angani wala ukiwani,ispokua Enzini peke yake
13.Kwa maana Mungu mwenye Enzi ndio Mjuzi,hakuna mwengine kama yeye
14. Na yeyote atakaye jidai ujuzi ni kafiri mkubwa,maana amejilinganisha na Muumba wake
15. Mwenyenzi Mungu ni nuru ya ulimwengu, Mtukufu anaye angazia jumla ya wapumuaye
16. Viumbe vyote vimepatikana kwa ufundi wake, M'bora wa kuumba
17. Mshindi aliye na mamlaka ya ajabu, Anga na Ukiwa pamoja na vilivyomo hupatikana kwa idhni yake
18. Hakuna mwengine kama yeye,Mjuzi aliye na uwezo wa vyote
19. Mwenyi kuwako kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho,wapekee aliye kamilika
20. Amekua yote katika yote,anaye fahamu kila kitu, Mwalimu wa walimwengu
21. Ni yeye anaye funulia watu mambo yote,akiwaletea neno lake kadiri ya nuru ili umbo zao zipate kutimilika
22. Mtukufu anaye stiri umbiko kwa idhni yake,hakuna atakaye faulu njee ya Mwongozo wake
23. Lau kama watu wangeli ona ginsi pumzi zao zinavyo timilizwa pindi wanapo silimu kama wote wangeli pupia kusilimu
94
bila kuritadi maishani mwao
24. Hakuna jambo bora katika maisha ya mutu kama vile imani
25. Tumieni urakibu katika maisha yenu, bila shaka hii ndio njia iliyo nyooka yenyi Baraka na nuru
26. Na anaye tembea katika uatidu amepotea na bila shaka yeye ni maskini mnyonge, atakaye nyimwa fadhila yote,wala hawezi
kuishi milele
27. Makafiri wamezembea sana kwa kuamini, wamejaa mashaka ajili ya uchache wa elimu
28. Wanalazimisha kutimiziwa maitaji yao pale pale wanapo omba
29. Hawatambue kama hayo hutokana na yakini iliye moyoni.
30. Jisafisheni kwa ibada ili dua zenu zikubalike
31. Matendo yako yote yawe mema na moyo wako ujae yakini ya uzima wa Mungu(ili dua ijibiwe bila kusita)
32. Na ogopeni Mola wako ukweli wa kuogopa,wala usimlahumu kwa lolote
33. Hakuna Mola Mwengine ila Mwenyenzi peke yake ,Mzima aliye na mamlaka juu ya kila kitu.
34. Watu wamejaa wasiwasi ajili ya tamaa ya maisha ya dunia,hawana yakini na maisha ya mbinguni.
35. Mola wenu amekwisha weka siku ya mwisho duniani ambae kila yule atavuna yale aliyo ya panda
36. Haijuzu kuwalipa watu kabla ya siku hiyo ili mpango wake utimilike usije kuvrugika
37. Mungu angeli kua na jibu pale pale kama taratibu hii isingeli timilika,maana dunia ingeli ondolewa kabla ya siku iliyo
wekwa
38. Kazi munayo fanya duniani malipo yake ni mbinguni mumetetea ili mupate maisha ya milele
39. Ndio maana Mungu anajibiaka maombi ya watu namna ya ajabu,akiwapa sehemu kidogo apa duniani na kiwango (sehemu)
kikubwa huwalindia mbinguni
40. Ni bora zaidi kuomba yanayo husu roho yako maana ndio dhati yako ambae kuishi
41. Na atakaye tetea mwili na kusahau roho yake ndio maskini ambae hana akiba yoyote
42. Kuna maombi nzuri na pia kuna maombi mbaya lakini watu wengi hawafahamu
43. Mara unaweza kuomba shari kwako ajili ya tamaa ya mwili bila wewe kufahamu
44. Mola wenu ni mlinzi mwema,amewahepusha watu na shari ya kila namna,ambae wamezingatia na ambae hawazingatie
45. Maisha ya dunia ni matayarisho ya maisha ya mbinguni
46. Kumbe usitegemee sana mwili wako ni bora zaidi kustiri roho yako kwa matumizi ya neno la Mungu
47. Ama yule atakaye shuudia mungu mwengine badala ya Mwenyenzi pia ni kafiri mkubwa
48. Andiko imeuwa wengi miongoni mwa watu wale ambae huitumia kwa uziwi na upofu
49. Mungu ni Mmoja aliye Enzini, milki kamilifu isiyo fanana wala kugusana na yeyote wala chochote
50. Mungu ni mwenyi mamlaka juu ya kila kitu, Mtukufu anaye simamia walimwengu wote
51. Funguo ya heri na ya shari imepatikana kwake atakavyo hufanyika, Mshindi aliye juu
52. Atakaye tenda mema atakutana na heri na atakaye tenda mabaya atakutana na shari
53. Usalama wa nafsi unapatikana kwa njia ya kusilimu, na mateso ya nafsi imepatikana kwa njia ya kukufuru
54. Umutu ni mfano wa <<mwendo na njia >>.
55. Mwendo wa mutu ni matendo yake,na njia ya mutu ni mila yake.
56. Hutembea katika njia,matendo kadiri ya mila.
57. Mwendo pasipo njia ni bure,na njia pasipo mwendo ni bure
58. Ukubwa ulio-je neema ya Mungu kwenyi umbo la kati na kati ,ukingoni mwa Anga!
59. Mutu hutumia mwendo fulani na njia fulani ili apate kufika mbinguni ao hadezeni
60. Hakika maisha ya dunia ndio safari ya kwenda mbinguni ao hadezeni
61. Maadamu mila inayo aina mbili,hupatikana pia aina mbili ya njia
62. Kila mara huchuguana matendo na mila ya mutu
63. Atumiaye njia nzuri,mwendo wake ni muzuri vile vile
64. Na atumiaye njia mbaya,mwendo wake ni mubaya pia
65. Njia ya uzuri ndio "Urakibu"
66. Na njia ya ubaya ndio "Uatidu"
67. Njia ya uzuri hupanda mlimani,na njia ya ubaya hushuka bondeni
68. Utumiwapo urakibu ndipo uatidu hufifia,na utumiwapo uatidu ndipo urakibu hufifia nafsini
69. Ni wa mlimani urakibuni,na bondeni uatiduni
70. Matumizi ya urakibu ni sura ya malaika mbinguni
71. Na matumizi ya uatidu ni sura ya Shetani hadezeni
72. Matendo yako ya leo ni akiba yako ya kesho
73. Yote munayo yatenda duniani hulindwa huko juu,hiyo siku ya kiyama itakua ndio chakula na kinywaji kwenu
74. Ole wao wanafiki ambae hudanganya watu kuamini na ili hali hawana imani
75. Hakika hawadanganye ispokua nafsi zao wenyewe,maana watajuta kwa yale walio kua wakiyafanya
76. Mpelekeeni Mola wenu shukrani kwa wingi enyi watu,hakika Mungu Mwenyenzi ni mwema sana
95
77. Msemeleaji wa viumbe,anaye nusuru nafsi ukingoni mwa bonde,na kuinyanyua juu mpaka mlimani,hakuna mwokozi kama
yeye
78. Ustaarabu ulio-je na akili urakibuni katika uvuli wa Enzi,hayo sio ila utimilifu wa nafsi
79. Anuiapo mutu kufanya ibada,Malaika Mbinguni hujiandaa kumsaidia
80. Na anapo nuia kufanya uovu Shetani hadezeni hujiandaa kumuvamia
81. Jihadharini na ushirikina pia na uovu,musije mukavamiwa
82. Hakika Mungu Mwenyenzi ni Mtukufu sana,M'bora wa kuumba,anaye jenga hewa kadiri ya pumzi mbalimbali
83. Mola anaye stawi Enzini pekee; katika utukufu usio kadiriwa,Mshindi aliye na mamlaka ya ajabu
84. Ni mfano wa taa,kadiri taa hutoa mwangaza ndivyo pia Enzi inavyo toa hewa
85. Enzi ndio kitu chenyewe,na hewa (Anga) ndio uvuli wake: ni mwanzo utokezaye kadiri ya shina la vyote vilivyomo
ulimwenguni
86. Ni tabaka lenyi uwezo wa vyote ambae hutenda kwa idhni bila kutumika kazi
87. Hakika Enzi tukufu ndio dhati yake Mungu, Milki kamilifu yenyi ushindi milele na milele
88. M'bora wa kuumba ambae kaumba dunia katika maunganio ya Anga na Ukiwa
89. Akapangiza humo wanahewa-haramu wenyi pumzi na mwili umboni mwao
90. Mwili hufanya wajumuike duniani kama chombo cha kuikalia,na itakapo jitenga pumzi na mwili,huondoka duniani na
kuingia mbinguni ao hadezeni
91. Kila Mwanahewa hutetea namna ya kusalamisha nafsi yake ili apate kudumu
92. Mungu aligawanya fikara kwa kila yule kadiri ya umbo lake ili apate kujikusuru katika kutimiza maitaji yake
93. Aliye Mtukufu tena hodari ni yule anaye pokea zawadi tokea mbinguni
94. Uyu ni mwenyi ginsi ya kutetea maisha yake na ya wengine duniani namna ya usimamizi
95. Ameshukiwa na nuru tokea mbinguni ambae humjaza nguvu ya kiroho yenyi kustiri nafsi.
7. MWENYENZI
1.Enzi imepatikana juu ya maala pa juu ulimwenguni,ni chemchem ya nuru ambae huangazia walimwengu.
2.Enzi ndio dhati ya Mwenyenzi Mungu,ndio ukamilifu ambae ni uzima
3.Kwake hakuna upungufu wala uwingi,lakini upekee kamili
4.Umungu ni muujiza wa maajabu,uwezo na fahamu bila kipimo
5.vyote huanza kadiri ya idhni yake na vyote hukoma kadiri ya idhni yake
6.Mshindi asiye kua na uvuguvugu katika milki yake,Mtukufu asiye badirika.
7.Uzima ni mamlaka yenyi kuzidia uwezo na fahamu ya vyote,ambae katangulia bila kuanza,na pia katangulia bila kukoma. 8.Hana mwanzo ajili ya ujuzi,wala mwisho ajili ya uwezo
9.Hakutukie lolote pasipo utangulizi wa fahamu,ni lazima kutangulie ujuzi utakao anzisha upatikanaji wote na maisha yote.
10.Hakika fahamu ya vyote ndio uwezo wa vyote.
11.Kama si utangulizi wa ujuzi,hakungeli patikana chochote.
12.Lakini kuona kama Mjuzi katangulia ndio maana kumepatikana ulimwengu na walimwengu
13.Utangulizi wake ndio uzima,muujiza wa kuenea namna ya kupatikana bila kuanza,namna ya ukamilifu
14.Hakika hutangulia mwenyi kuenea kimilki na kibusara, yaani mkamilifu .
15.Enzi tukufu ndio dhati yake,na uzima ndio hali yake ya kuenea.
16.Utangulizi mbele ya vyote kupatikana ndio mamlaka ya uumbaji.
17. Ni milki ya ushindi ambae huweza yote,ikijiweza yenyewe namna ya kuwako bila kufanyika,na iki jiepusha kiushindi na
uzaifu wa kukoma.
Hakika hutangulia mwenyi kuenea kimilki na kibusara,yaani Mkamilifu
Enzi tukufu ndio dhati yake, na uzima ndio hali yake ya kuenea
Utangulizi mbele ya vyote kupatikana ndio mamlaka ya uumbaji, fahamu yenyi tayari kutokeza kadiri ya idhni yake
18. Hali hii ya ushindi mbele na nyuma, ndio umungu: ukamilifu katika milki na katika fahamu.
19. Kuweza yote na kujua yote ni ajabu mbele ya viumbe,ajili ya uchache wa fahamu yao wamekiri kwamba ni muujiza wa
maajabu
20. Pasipo uzima,ulimwengu si chochote; maana hakungeli patikana chochote wala lolote.
21. Kuona kama kuna uzima katika ulimwengu ndio maana kumepatikana Umungu.
22. Mungu hutangulia mwanzoni kinyume na kuanza mwanzoni
23. Kama angeli anza,hasingeli umba; maana uwezo wa vyote ungeli mkosa,na hapo angeli dai msaada kwa yeye
kupatikana,mfano wa viumbe.
24. Milki kamilifu humfanya namna ya kuenea pekee pasipo msaada wowote,hujipatikanisha kimuujiza na hupatikanisha
viumbe kwa maajabu.
25. Sio kama uzaifu ambae hudai msaada wa muweza ,ambae hufanyika na mwengine,ambae kabla ya kufanyika hakuwaka
chochote
26. Hakutokee chochote katika sifuru,mpaka kutangulie fahamu fulani ya kujua kutenda ndio kutatokea kifulani.
27. Kuuliza kuanza kwa Mungu ni kuuliza kuumbwa kwake ni kama kumulinganisha na kiumbe: maana kuanza kwa kitu ni
kuumbwa kwacho.
96
28. Ni vema kuuliza kutangulia kwake ,maana ndio hali yake.
29. Aliye tangulia ni yule aliye kuwako kabla ya uumbaji ambae milki yake hutokeza bila kutokezwa.
30. Ni mwenyi uzima ambae ndani mwake hakuna palipo wazi ambae pangeli dai kujazwa na msaada wa mwengine,lakini
ukamilifu wa ajabu,usio pungua wala kuongezeka ajili ya kuenea.
31. Mamlaka yake ni juu ya falme zote,wala hakuna mfalme ila mtumishi wake mdhalili.
32. Muumbaji pasipo hatia,mfalme wa mabingwa ambae huzagaa maala pa juu sana ulimwenguni.
33. Mungu ni Mjuzi ambae hufahamu pasipo kufikiri.
34. Hakika fikara ni kinvuli cha ujuzi mfano wa nuru yake.
35. Haijuzu kitu kukaa ndani ya uvuli wake wala kutokea humo, bali uvuli wa kitu ndio utokao ndani mwake.
36. Wala kinvuli hakiwezi kugeuka kitu chenyewe,ndio maana yeyote anaye pumua hewa ni mwanahewa tu,hata kuwaka
kamwe Mwenyenzi.
37. Mungu amehepukana na uzaifu wote wa ugeugeu,milki kuu itendayo kadiri ya idhni yenyi mamlaka ya ajabu.
38. Penda Mola wako zaidi ya vyote,wala usiweke kipenzi badala ya Muumba wako,maana neema yake iliye juu yako ni kubwa
sana hauzingatie ukubwa wake ajili ya uzaifu wako; kila ulicho nacho ni neema kutoka kwa Mungu.
39. Mwenyenzi Mungu-hakuna mamlaka kinyume naye mpweke, hakika ya uhodari ambae nuru humfumuka kwa wingi,
vikijipakaa viumbe utukufu wa dhati yake:utangulizi pekee,uzima ulimwenguni ,ndiye Mtukufu Mfalme asiye tegemea
40. Mungu ni baba wa siri aliye kwa siri,amefanya siri kwa siri,muujiza wa maajabu ulimwenguni,aliye pasipo yeyote juu ya
maala pa juu... Akienea maala pote kiujuzi; chemchem ya upatikanaji na maisha,ambae hakuanza wala hatakoma, muweza wa
vyote ulimwenguni
41. Hii ni nuru kubwa,neno la kweli kutoka kwa Mola wako ,Mtukufu aliye juu
42. katika utukufu wa nuru yake wokovu huwa fikia,na katika neema yake huwashukia baraka ya Mola wao ajili ya kupokea; ni
fadhila kutoka kwa Mwenyenzi Mungu,Mola wa walimwengu
43. Mungu hupodoa waja wake na rangi yake takatifu zawadi tokea Enzini
44. Mwenyi reheme za kuenea,ambae huongoza kaumu zote kwa ishara zake,akizungumuza kweli yake kwa ukarimu wa jaza
lake,na kufumbua macho yao kwa ukubwa wa nuru yake. katika idhni yake tukufu,maisha na mauti hutokelea,muabudiwa wa
haki ulimwenguni.
45. Ni yeye aingizaye Anga ukiwani na Ukiwa angani,akiwa kadirieni katika kawaida yake,ushindi wa neno lake.
46. Hakika Mungu Mwenyenzi ni muujiza wa maajabu: alitangulia bila kuanza kimuujiza,na akaumba viumbe vyote kwa
maajabu.
47. Hana hatia katika kuumba kwake,wala tatizo kwenyi milki yake, Hodari katika ufalme wake.
48. Mungu-ni Yeye asiye tegemea ambae idhni yake hutenda,Mola wa arshi yenyi utukufu.
49. Mwenyenzi Mungu ni Mshindi anaye miliki walimwengu kwa amri yake. Atakavyo hutukia kwa rafla. Ndani mwake
munamo uwezo wa maajabu, na hakuna kinacho fahamu ila kwa niaba yake, mamlaka itokezayo kuujaza ulimwengu. Ni yeye
mwenyi utasi tafauti na mategemeo ambae hujieneza kinyume na shuruli. Mola wa Anga na Ukiwa ajaaye sifa dhatini mwake:
karibu naye hujaa baraka na mbali naye hujaa laana, mfariji anaye tegemewa na jumla ya viumbe, mwenyi kujibu kadiri ya
maitaji kinyume na kuuliza. Muumba wa nuru na giza anaye simamia kwa usawa, ndiye mkuu atanguliaye.
50. Huu ni utukufu wa Mungu Mwenyenzi,Msifiwa aliye na milki ya kuenea pote,mamlaka ya milele.
51. Mwenyi kujua bila kusahau ,na kuweza bila kushindwa, mzibiti wa hesabu ya walimwengu kwa rafla bila shuruli ambae
walimwengu humtumainia.
52. Wa pekee aliye huru ulimwenguni,ambae peke yake hujua pasipo shuruli wala hataabike wala hagusike na mafikiri.
53. Mwenyi kutosheleza viumbe na fadhila yake,umaskini na utajiri watokea kwake,ni yeye anaye ruzuku kuondoa dhiki; anaye
watimizieni sambamba na ahadi zake.
54. Uzima ni kama kistari cha usawa kilicho kamilifu,ambae hakuna kilicho anzia wala kilicho komea,fundo wala
lukumba,ameenea katika yote kadiri ya ukamilifu.
55. Hakika kuna Muumbaji aliye pekee ambae katangulia na katawala kwa uwezo wake mwenyewe .
56. Aliye umba mbingu na dunia kwa idhni yake,Akapangiza mbingu angani na dunia katika maunganio ya Anga na
Ukiwa,vyote maala pengine hatua na kambi lake tukufu.
57. Mbingu,Hadeze na Dunia sio ulimwengu wote,bali kunapatikana tabaka lingine tukufu zaidi,ndio «Enzi tukufu», fasi yenye
Mungu anastawi milele.
58.Uongofu haupatikane pasipo busara,na busara kamilifu ndio ujuzi, ni kwamba Mungu aliye na ujuzi ndio kiongozi pekee wa
jumla ya viumbe .
59. Na ambae huongoza walimwengu ndio mfalme wa wote,mwenyi mamlaka ya ajabu.
60. Mungu alitia akili ndani ya umutu na kuifanya zamiri kua dira. atakapo badiri mutu zamirini mwake kuelekezwa kwenyi
maitaji yake.
61. Mungu ni mwanzo unao tokeza bila kutokezwa,milki isiyo tokea wala kuendea,mwenyi kukamilika ambae ukubwa wa
uwezo wake ni kama muujiza.
62. Ni yeye aliye anzisha kila umbo; la wazi na la siri, asikiaye kwa rafla masemi ya walimwengu wote ijapokua idadi yao,
97
Mola Mlinzi wa viumbe,M'pweke aliye juu.
63. Hana kimo wala umbo,tatizo wala woga; Mola mkamilifu katika yote, Mshindi aliye juu.
64. Hakika ukamilifu umepatikana Enzini,na upungufu ndio unao patikana angani na ukiwani.
65. Ni timilifu maisha ya Mutu anaye tumia kawaida ya neno la Mungu,na utimilifu sio ukamilifu.
66. Maisha ya kiumbe ambae asili yake ni upungufu ndio inayo weza kufikia utimilifu.
67. Ukamilifu ndio uzima,hali tukufu tafauti na upungufu wa aina yote.
68. Kila kilicho na mwanzo ni kipungufu kadiri ya unusu na kipande ni kipungufu ajili ya kutokamilika lau kama kingeli
kamilika kisingeli fanyika.
69. Halitimie ambae ni kamilifu,wala kukamilika ambae ni timilifu
70. Ni tafauti kabisa ujuzi na fikara,ujuzi katika ukamilifu,na fikara katika upungufu.
71. Mungu hana mila wala tamaa,hana njaa wala kiu,wala mfano wa hayo,wala mwengine mfano wake,Mtukufu aliye na
ushindi.
72. Mzima ni Mungu peke yake ambae uweji wake haudai msaada wowote,aliye tangulia kikamilifu namna ya kuenea pote
pasipo chochote kinyume naye.
73. Hakuna kiumbe chenyi uzima bali kuna kiumbe chenyi maisha na pia kuna kiumbe ambae hakina maisha.
74. Viumbe vyote kwa jumla si chochote wala lolote pasipo Mungu,maana hayuko haï wala mauti miongoni mwao ila kwa
uwezo wa Mungu Mwenyenzi.
75. Tazameni kiroho hali ya kua umetupilia mbali matazamio kimwili,ili upate kuzingatia uzima ulimwenguni.
76. Kutazama kimwili humfanya mutu azingatie duniani,na utazamaji kiroho humfanya mutu azingatie njee ya dunia.
77. Uzima ni ukamilifu,uwezo wa vyote ambae katangulia kuenea,ushindi katika yote milele na milele.
8. LUGHA
1. Umungu ni uzima,na uzima ndio ukamilifu,hali ya kuenea
katika yote bila upungufu wowote.
2.Aliye kamilika ni mwenyi uwezo wa vyote na ujuzi wa vyote.
3.Yaani ni mwenyi mamlaka juu ya kila kitu,mufalme wa ulimwengu .
4.Mwenyi uwezo wa vyote ndio mwenyi uhuru,anaye fanya apendavyo, 5.Hamilikiwe na yeyote wala chochote,na pia hamtegemee yeyote wala
chochote,
6.Hana mwanzo wala mwisho sababu ni mwenyi Kuenea.
7.Hashindwake wala hadanganyikake, wala hapumzikake, mshindi aliye tangulia .
8.Vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini hutukuza jina lake.
9.Mtukufu anaye tengana na vitu vyote,wa pekee kadiri ya muujiza wa
maajabu.
10.Uzima humfanya apatikane bila hitaji ya msaidizi.
11.Asiye kamilika hawezi kutangulia ajili ya upungufu wa kuto enea.
12.Mpungufu ana anzaka, na mkamilifu ana tanguliaka.
13.Kila mpungufu alikua sifuru kabla yake,na ndio maana inabidi aumbwe kwa yeye kupatikana ulimwenguni.
14.Na mkamilifu ni yule asiye kua na kabla yake wala baada yake,ambae
huenea Katika tendo kua.
15.Fasi yenye iko mwengine hawezi kufika.
16.Yeye ni Mola wa ulimwengu wote ;hana Kabila, wala asili, wala lugha.
17.Jina lake hupatikana katika lugha zote.
18.Lugha zote zimependwa Sana na Mungu.
19.Hakuna lugha dhalili wala tukufu,yote ni Sawa mbele yake.
20.Na majina yake yote ambae hupatikana Katika kila lugha ni bora.
21.Mungu ni mleta Amani,hawataki Watu wanao kosesha wenzao amani.
22.Kulazimisha Watu lugha ya kigeni ni kuwafanya watumwa.
23.Kujifunza lugha ya kigeni ni vema .
24. Lakini kukaza Watu na lugha ya kigeni sio vema.
25. Someni katika lugha zenu ili elimu yenu itimilike.
26.lugha ya kigeni huzaufisha elimu,katika utafiti.,Na huzaufisha uhuru, katika maisha.
27.Na kutumia lugha ya kigeni katika neno la Mungu ,huzaufisha Imani.
28.Mungu hawatakieni kamwe mazito lakini mepesi.
9 . ALIYE
1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,mzima ,aliye tangulia kadiri ya kuenea.
2. Ni yeye aliye umba vyote kadiri ya idhni yake,bila kuiga kwa yeyote wala
kutumika kazi.
3. Lakini yeye hakuumbika Bali alitangulia kwa mamlaka yake mwenyewe.
4. Hutangulia ajili ya kua na milki kamilifu,muweza yote na mujua yote.
5. Anaye weza yote na kujua yote ndio mkamilifu,uzaifu na upungufu havina fasi ndani mwake.
6. Kuumbwa ni kushindwa kutangulia.
7. Na kushindwa kufanya jambo fulani ndio alama ya uzaifu na upungufu.
8. Kama uzaifu wa kushindwa upo,kumbi na uwezo wa kushinda upo.
9. Ndio maana kunapatikana kiumbe,na pia kunapatikana Muumba.
10. Kiumbe ni katika uzaifu na Muumba ni katika uwezo.
11. Haiwezekane kiumbe kipatikane na Muumba akosekane.
12. Kukosekana kwa Muumba kungeli sababisha kukosekana kwa viumbe vyote.
13. Kupatikana kwa Muumba ndio husababisha upatikanaji wa viumbe.
14. Kama unaona viumbe,tambua kama Muumba iko mzima.
15. Kuona kama viumbe ni katika upungufu, ndio maana haviwezi kutangulia.
16. Anaye kubali upatikanaji wa viumbe hali ya kua amekanusha upatikanaji wa Muumba,ni pumbafu wa namba ya juu.
17. Mungu peke yake ndio mkamilifu, mwenyi kujieneza katika yote,m'zima; Hakuna mwengine kama yeye.
10.ASIYE NA UMRI
1.Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu, anaye tawala mbingu, hadeze,na dunia.
2. Hazaufikake wala hachokake, m'shindi afanyaye apendavyo.
3. Hakuna wa kumkaripia wala wa kumuhukumu, m'kuu anaye staajabisha.
4. Humtukuza vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini, mufalme
wa wafalme wote.
5. Kutumainia Mola mwengine badala yake ni ujinga mtupu.
6. Hakuna Mola mwengine kama yeye,wa pekee aliye juu.
7. Ujuzi ni katika ukamilifu,unapatikana katika Umungu hali ya kua
uzima.
8. Alipatikana kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho,bila umri
wala umbo.
9. Kuona yote na kusikia yote ni kujua.
10. Kukosa kuona yote na kukosa kusikia yote ni kufikiri.
11. Mwenyi kujua ndio Mungu,na mwenyi kufikiri ndio mwanahewa.
12. Mungu ni mfalme wa milele, anaye tawala ulimwengu wote bila
mipaka.
13. Mtukufu asiye lingana na kiumbe chochote, ambae uzima wake
hustaajabisha viumbe.
14. Kumfananisha Mungu na kiumbe fulani ni ujinga Sana,ni Sawa na
yule anaye mfananisha mutu na chombo alicho kiunda.
15. Mutu hawezi kulingana na chombo alicho kiunda.
16. Kadiri mutu hawezi kulingana na vyombo alio vitengeneza ,ndivyo
pia Mungu hawezi kulingana na viumbe alio viumba.
17. Kadiri kulivyo hatua kubwa kati ya mutu na chombo, ndivyo kulivyo
hatua kubwa kati ya Mungu na kiumbe.
18. Hakuna kiumbe kilicho mfanana Mungu mwenyenzi.
11. MUZIMU
1. Ametakadika Mwenyenzi Mungu m''bo wa kuumba, aliye umba wanahewa na wazilahewa,ambae Mwenyewe hakuumbika.
2. Kutoumbwa sio kukosekana,lakini kutoundwa ni kukosekana.
3. Kuhusu kiumbe,kinacho mfanya aumbike ni uzaifu.
4. Na kuhusu Muumba, kinacho mfanya asiumbike ni uwezo.
5. Sifuru ndio shina la uzaifu,na uzima ndio shina la uwezo.
6. Ndio maana sifuru haitokeze,ispokua uzima ndio hutokeza.
7. Hakuna atakaye lingana naye maana kila yule ni kiumbe chake.
8. Uzima sio maisha, ndio maana Muumba sio kiumbe.
9. Kulazimisha uonane na Mungu uso kwa uso ni kulazimisha
Mungu awe na uso kama wewe.
10. Kila kile kinacho patikana katika umutu ,hakipatikane kamwe katika
Umungu.
11. Kupatikana kadiri mutu alivyo patikana na anavyo tenda,ni
99
kumfanana mutu.
12. Kukosa umri kadiri ya uzima ni Muujiza.
13. Mola wenu ni wa pekee, tafauti na kila kitu.
14. Umungu haulingane na umutu kamwe : umutu ni upungufu,na Umungu
ni ukamilifu.
15. Heri mutu anaye amini Mungu kwa moyo wake wote na kumuabudu
yeye peke yake.
16. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa ila mwenyenzi peke yake.
17. Na hakika Mussa,Eliya,Yesu na Muhammadi...ni mitume ya Mungu.
18. Jihadharini na ushirikuna, usitumainie yeyote wala chochote zaidi ya Mola wako.
19. Usiabudu wakaaji wa mbingu, wala wakaaji wa hadeze, wala wakaaji
wa dunia.
20. Kutumia majini ni Sawa na kutumia mizimu.
21. Muaminifu ni yule anaye tumia malaika na roho , kadiri ya nuru
na nguvu ya Mungu.
22. Walio silimu wamepotea ajili ya kutumia majini ambae ni mizimu.
23. Wamezani kama wametumia viumbe vyenyi Mila nzuri ajili ya upofu.
24. Watu wenzao tu hawafahamu ni nani muaminifu wa kweli kefule
majini wasio iona bayana !
25. Kua muzimu ao jini ni kua kafiri ao mnafiki ,na kua roho ndio kua
muaminifu.
26. Fanyeni ibada ya Mungu na kisomo cha UKWELI huu ili mupokee
roho takatifu.
12 .KITU CHENYEWE
1.Aya za kitabu hiki ni rehma na nuru maishani mwako.
2.Tumieni Kauli tukufu hii kila siku kwa kuisoma kadiri ya dhikri ili upate ushindi.
3.Kila andiko ni yenyi nuru,nguvu ya ushindiinayo teketeza falme za giza.
4.Milango saba ndani ya UKWELI wake, kadiri ya mbingu saba ndani ya NURU yake.
5.Hakika asiye jua kitu sio kitu.
6.Mwenyenzi Mungu ndio KITU CHENYEWE,mwenyi uzima.
7.Upatikanaji wowote njee ya dhati yake ni miongoni mwa viumbe vyake.
13. KIWE NA KINAKUWA
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.
2. Mjuzi wa vyote na muweza wa vyote, anaye patikanisha na anaye kosekanisha ulimwenguni.
3. Aliye tokeza ulimwengu na walimwengu peke yake bila msaidizi.
4. Mumilki asiye tumika kazi kwa kutenda, ambae idhni yake hutosheleza.
5. Kiwe na kinakuwa ndio namna ya kutenda kwake.
6. Mwenyi kuenea, namna ya kutangulia bila mwanzo wala mwisho.
7. Yeye ni bwana wa mabwana na bingwa wa mabingwa,wa popote na milele.
14. DHATI
1. Mwenyenzi ndio mwenyeji wa ulimwengu ambae vyote ni vyake.
2. Enzi yake ni mamlaka ya ajabu inayo patikana kimuujiza hali ya kuenea katika yote.
3. Milki yake imewaka zaidi ya moto wa aina yote,bila mfano wake.
4. Dhati yake haigusanake na chochote,kitakacho jaribu kuisogelea hufutika kwa rafla.
5. Enzi yake ingeli sogelea mbingu, hakungeli kua tena mbingu kwani ingeli futika,na vivihivyo kwenyi hadeze na dunia.
6. Na ndio maana haingiake ndani ya kiumbe chochote,na pia hakuna kiumbe kitakacho ingia ndani mwake.
7. Ni wa pekee juu ya maala pa juu,enzini.
8. Yeye ni tafauti sana,tena mbali sana :hana jerani wala mfano wala kipimo.
9. Dhati yake inayo itwa Enzi hupatikana kimuujiza na hutenda kwa maajabu.
15. UMOJA WA MUNGU
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu Mola wa wanahewa na wazilahewa, mamlaka itokezayo ulimwengu.
2. Uwezo wake hauna kipimo,na ndio maana haudai kutumika kwa kutenda.
3. Na ndio hufanyika kwa rafla kile anacho idhinia.
4. Hakuna aliye jazwa enzi ndani mwake,popote ulimwenguni.
5. Angani na ukiwani hupatikana wanahewa na wazilahewa.
6. Mola wa viumbe amestawi peke yake enzini.
7. Hakika Mungu ni mumoja,hakuna mfano wake popote ulimwenguni.
16. UWEZO
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, aliye milele bila uzaifu wa kuanza na kukoma.
2. Enzi yake ni uwezo wa usio gusika hata na chembe ya uzaifu.
3. Uwezo kama huo ndio unao mfanya atangulie kupatikana kadiri ya kuenea pasipo maanzio wala makomeo.
4. Angeli anza kama ingeli dai wa kumuanzisha amtangulie kwa yeye kupatikana, maana angeli kutwa sifuru kabla ya kuanzishwa.
5. Na kama angeli anzishwa, hasingeli kua mkamilifu kadiri ya Muumba,bali angeli kua mpungufu kadiri ya kiumbe.
6. Kukosa uwezo wa kutangulia ndio kukosa uwezo wa kuumba, maana ni kua kiumbe.
7. Uwezo wa kutangulia bila kuanza ndio uwezo wa kutokeza toka sifuru hali ya kua Muumba.
17. UBORA WA UMBIKO
1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.
2. Muumba wa anga na ukiwa pamoja na vilivyomo, aliye kadirisha sawa sawa umbiko lote.
3. Ameumba kadiri ya kufumba,hakuna awezaye kukagua umbiko ila kwa njia ya ufunuo wake.
4. Ujuzi wake umemfanya atokeze vyote bila kasoro, wala hakuumba chochote bila faida yake wala maana yake.
5. Na ndio maana haifae kumlaumu Mungu kuhusu kuumba kwake, anajua ambae wengine wote hawajue.
6. Mutu hafahamu ispokua yale ambae Mwenyenzi kamfundisha ; elimu yote na nguvu yote imetoka kwa Mungu.
7. Ogopeni Mola wako ijapokua kwa kutazama umbiko ! ukubwa ulio-je ujuzi wake unao tokeza vyote pasipo kuiga mfano popote !
18.IBADA NI WEMA
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, Mwalimu mwema, aliye mfunza mutu ginsi ya kumuabudu.
2. Ndipo mutu alipo simama kwa kumuimidi.
3. Na kufunika mabaya kwa mema,
4.Na kumnyenyekea kwa moyo wake wote.
5. Roho ya upendo hutawala nafsini mwake.
6. Anampenda jerani yake aliye kuume kwake na aliye kushoto kwake
7. Wala hafanye ibada yoyote ila kwa kutanguliza wema, sambamba na kauli tukufu ya Mola wake.
19. ASIYE GUSIKA
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, anaye stawi juu ya maala pa juu, enzini.
2. Dhati yake ni mamlaka ya ajabu, uwezo wa vyote tafauti na vyote.
3. Malaika na roho hawana uwezo wa kugusana na Enzi yake.
4. Milki yake hufuta umbo zaidi ya kuunguza ,na ndio sababu ya kuto gusika na chochote.
5. Usidanganyike na andiko iliye tolewa kwa mfano ili kusikilizisha watu.
6. Mola wenu ni mtukufu wa ajabu hagusanake wala kukurubiana na yeyote,bali mbali kabisa na umbo zote.
7. Angalisho na wajumbe wa shetani wanao chugua andiko iliye tolewa katika mfano kuhusu mengine, na kulipachika fasi isiyo stahili na lengo kunajisi neno lake.
20. MASOMO 18
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, aliye umba mbingu, hadeze na dunia kwa idhni bila kutumika kazi.
2. Kitabu cha ukweli ni nuru kubwa sana ambae Mwenyenzi alikuteremushia.
3. Milango saba ya mbingu saba inayo hifadhika na muhifadhi wa milele.
4. Ukweli huu ni somo kubwa miongoni mwa masomo kumi na nane.
5. Na wewe ni shahidi wa Mungu, ambae husimamia shaada yake.
6. Tangaza uzima wa Mola wako kwamba ni tafauti na maisha yote;na uwapige marfuku mishirikina wa aina yote.
7. Hali ya Mola wako,na mamlaka yake,na kambi lake,ni tafauti sana na kila kitu,wa pekee aliye juu.
21. JITIHADA
1. Enyi walio silimu ! jitahidini kujenga imani ndani ya nyoyo zenu ili mupate maisha ya milele.
2. Na jambo la kwanza ni kuwa yakini na uzima wa Mungu.
3. Na kuwa yakini kwamba shida zote hutoshelezwa naye.
4. Hakuna atakaye kuvamia kama upo yakini na ulinzi wa Mola wako.
5. Na kumpenda Mwenyenzi zaidi ya wote, maana ndiye anaye kupenda zaidi ya wote.
6. Na kujitahidi kutimiza mapenzi yake sambamba na kauli yake tukufu.
7. Jitahidini pasipo kuchoka, maana mafanikio yako hulingana na jitihada yako.
22. WA POPOTE NA MILELE.
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.
2. Anaye tokeza ma elfu ya viumbe kila siku.
3. Mkomeshaji, anaye poteza ma elfu ya viumbe kila siku.
4. Mjuzi aliye mbali na kufikiri pia aliye mbali na kupitiwa. 5. Ni muweza asiye jikaza kwa kutenda na asiye choka kutenda.
6. Mkamilifu asiye kua na kabla yake pia asiye kua na baada yake.
7. M'bora wa kutangulia anaye enea kadiri ya uzima,wa popote na milele.
23. MLETA HABARI
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.
2. Aliye umba viumbe vyote bila kasoro,mkadirishaji wa maisha.
3. Mjuzi asiye jifunza kwa kutokeza,toka sifuru,kitu ambae hakikua popote.
4. Mleta habari, aliye mtuma Kalonda duniani na habari ya uzima wake,na kumpatia kitabu kitukufu.
5. Ni mufalme anaye miliki walimwengu kwa uwezo wake na ujuzi wake Mwenyewe.
6. M'bora wa kuenea, anaye jitosheleza mwenyewe katika mambo yote.
7. Mola asiye omba shauri kwa yeyote, ambae wote huomba shauri kwake,wa pekee aliye kamilika.
24. WA TAYARI NA MILELE
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.
2. Aliye umba mbingu hadeze na dunia bila kuiga mfano popote.
3. Mwenyi uwezo wa ajabu,utendao kwa rafla anacho idhinia, M'bora wa wafundi.
4. Wote husalimu amri kwake, wa pekee anaye stahili kusujudiwa.
5. Mjuzi wa yote, anaye jua yaliyomo vifuani.
6. Ukafikiri tu, tayari ameyajua .na ukasema tu, tayari ameyasikia.na ukatenda tu, tayari ameyaona.
7. Hakika Mungu Mwenyenzi ni mkamilifu,wa tayari na milele.
25. MUUMBA ALITANGULIA
1. Mungu aliumba wote bila kuumbwa na yeyote.
2. Anaye umbwa ndio kiumbe na anaye umba ndio Muumba.
3. Kiumbe iko na mwanzo wake ambae ni wakati wa kuumbwa kwake.
4. Lakini Muumba ambae hakuumbika,hana mwanzo wake,sababu hakuna wakati wa kuumbwa kwake.
5. Kupatikana bila kuumbwa ndio kutangulia ulimwenguni.
6. Na ndio kukamilika, hali ya kuenea katika tendo kua,bila upungufu wa kuanza na kukoma.
7. Kama viumbe hupatikana ni kwa sababu Muumba aliye viumba alitangulia ulimwenguni.
26. NDOA
1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu mjuzi wa kuumba.
2. Aliye umba mume na muke na ginsi ya kuzaana ili dunia ijae na watu.
3. Na kuwafanya watu kua wasimamizi (wa wanahewa-haramu na wazilahewa) katika ardhi.
4. Akamfundisha mutu kweli yake ili apate kumuabudu.
5. Na kumuruhusu kuowa mutu mwenzake tu :asiowe wala kuolewa na jini, wala mnyama...
6. Na wala asiowe wala kuolewa na mwanaume mwenzake,na pia asiowe wala kuolewa na mwanamuke mwenzake.
7. Na kumuruhusu mwanaume kumpa mchumba wake mahari kabla ya ndoa.
8. Na asiowe wala kuolewa mbele ya umri kutimia.
9. Na pia asiowe wala kuolewa na mutu asiye mupenda,ni lazima wapendane kimwili na kiroho.
10. Bwana ampende sana bibi yake,na bibi amtii sana bwana yake.
11. Na talaka hairuhusiwe ispokua kwa yule anaye chupa na uovu, zaidi sana uzinifu,na ushirikina,na ukafiri.
12. Ni amri kwa aliye silimu kumusilimusha mwenzake ;wasikose kusilimu na wasiritadi baada ya kusilimu.
Maoni
Chapisha Maoni