Kitabu cha ukweli - Mlango wa tano : "NJIA YA MUNGU"


MLANGO WA TANO: NJIA YA MUNGU



(1). AHMADIYA

1. Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu, mkamilifu anaye jitenga na upungufu wote milele.
2. Mkweli wa kauli ambae tamko lake hutokeza kitu ambae hakikua popote.
3. Mutu atakaye amini na kutenda mema bila shaka ataingizwa mbinguni.
4. Na yule atakaye kufuru na kutenda mabaya ndio atakaye ingizwa Hadezeni.
5. Ole kwao wanao tumainia kuokolewa kwa neema, hakika kila mutu atavuna yale aliyo panda. 6. Kilicho muimu katika imani ni matendo mazuri.

72

7. Imani pasipo matendo mema ni unafiki mtupu.
8. Kila mutu analazimishwa kutenda mema, haimufae mutu ispokua matendo yake mwenyewe.
9. Matendo ya mutu mwengine haiingie katika hesabu ya mutu mwengine, ispokua mazao yake.
10. Kama unaingiza mutu katika dini, utapewa pia sehemu katika yale atakaye ya chuma ndani ya dini.
11. Na kama unaingiza mutu katika urozi, utapewa pia sehemu katika yote atakaye ya chuma ndani ya urozi ulio mupa.
12. Mitume wote walifanya kazi moja ya kuondoa watu kwenyi giza na kuwapeleka kwenyi nuru.
13. Kuamini mtume wa Mungu fulani ni kutumia mafundisho yake bila kuongeza wala kupunguza.
14. Atakaye ongeza ao kupunguza katika mafundisho yake, amemsemea uwongo mtume wake .Na kumsemea uwongo mtume ni kumsemea uwongo Mungu aliye mutuma.
15. Mwenyenzi Mungu ni baba wa salama aliye salama, tendeni salama ili mupate usalama wa milele.
16. Mungu ni mkubwa sana, mufalme wa ulimwengu wote, asiye lingana na yeyote ajili ya ushindi.
17. Maagizo yake ndio nguvu inayo tokeza,hakipatikane chochote ispokua kadiri ya agizo lake.
18. Enzi inayo patikana ndani mwake ndio mamlaka yake ya ajabu ambae humiliki vyote.
19. Atakaye abudu Mungu vilivyo atajazwa nguvu ya ushindi ndani mwake, na kuinuliwa katika sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani.
20. Pumzi yake itajazwa nuru mfano wa mkaaji wa mbinguni, kinvuli cha Enzi tukufu.
21. Mungu Amestawi arshini kiupekee,milki yake ndio hutawala vitu vyote fasi yote.
22. Nuru ya Mungu haipatikane fasi yote wala ndani ya viumbe vyote.
23. Ndio maana kuna patikana maala pa nuru na maala pa giza,na pia viumbe vya nuru na viumbe vya giza.
24. Mola wa ulimwengu ni wa pekee ,mwenyi uhuru, umbalimbali na viumbe vyote kwa jumla.
25. Mwenyi uwezo wa kuenea, ambae milki yake imewaka kimuujiza na kupoteza kwa rafla uzaifu wa aina yote kandokando yake.
26. Mwenyenzi ni mumilki, mutukufu na mshindi, bingwa wa ma bingwa.
27. Ee Mola wangu ! Unijaalie kuacha yote ninayo chupa,na unipatie nguvu ya kushinda tamaa ya nafsi yangu.
28. Wala usiniache kua na chuki mbele ya wale ulio wa neemesha.
29. Wala usinifanye kua na kiburi ajili ya neema ulio nipa.
30. Mola wangu ! Unifanye kua mnyenyekevu na mpole wa moyo,miongoni mwa wachaguliwa wako.
31. Roho alinichugua na kunipeleka,tukafika katika uwanja wenyi nuru kubwa.
32. Nikatazama, naangalia,nikaona mtoni mbele yetu.
33. Roho akaniambia, akisema : tazama kule ngambo ya mtoni.
34. Nikatazama ngambo ya mtoni,nikaona watu wengi walio vaa makanzu na viremba na mitama.
35. Watu wale walikua na hali ya upole sana, walipo niona ,wakaanza kuniita kwa kunisihi sana ili nipate kuvuka upande huo. 36.:Roho aliye nipeleka akaniambia, akisema : wasilimu wale unao waona upande huo ndio wa Ahmadiya.
37. Wasilimu wale walikua wapole sana, wengi ,na pia upande huo kulikua nuru pia.
38. Wakati walipo zidi kunisihi ili nipate kujumuika kambini mwao ,nikaanza kufikiri kama ni vuke ao hapana.
39. Roho aliye nipeleka, akaniambia ,akisema:tazama pia upande wetu. Nikatazama. Nikaona nuru kubwa tena maala ambae humeremeta sana.
40. Punde kidogo nikaona watu wote wananyamaza hali ya kutetemeka,wakaanza kutazama juu.
41. Na mimi pia nikatazama juu, nikaona roho mfano wa mutu aliye vaa kanzu mweupe ,anakuja akiporomoka toka juu mbinguni.
42.Roho yule akateremuka na kutua juu ya maji ya mtoni huo ulio tenganisha upande wangu na upande wa Ahmad.
42. Alipo tua juu ya maji ya mto hakugusa maji ya mto huo,lakini alininginia hewani namna ya kuketi kwa kukunja miguu.
43. Akaita watu wa pande zote mbili, upande wetu ulikua kuume kwake, na upande wa Ahmadi ulikua kushoto kwake, maana alihelekeza uso wake chini ya mtoni.
44. Akasema : Nimetumwa na Mungu ili ni pate kuwaamua.
45. Nimemupa mkubwa wa Ahmadiya talankha hii ili amupokeze Kalonda
46. Kama kijana uyu (Kalonda) anaipokea bila ayo kugusa maji ya mtoni, ni kwamba imeruhusiwa Kalonda kwenda upande wa Ahmadiya.
47. Lakini kama talankha hii inagusa maji ya mtoni mbele ya Kalonda kui pokea ,ni kwamba haistahili Kalonda kwenda upande huo wa Ahmadiya.
48. Kiisha roho aliye tua juu ya maji akainua vitanga vyake na kunyanyua macho yake juu, akaomba Mungu bila kupaza sauti. 49.Alipo maliza kuomba,akachugua talankha hiyo na kumupokeza mkubwa wa Ahmadiya ili anipokeze, ilikua mfano wa kalamu.
50. Wakati huo wasilimu wa pande zote wakaanza kuomba Mungu ili nipate kujumuika upande wao.
51. Mkubwa wa Ahmadiya kiisha kuipokea ,akaninyooshea mkono wake wa kuume ili anipokeze pia.
52. Na mimi pia nikamunyooshea mkono wangu wa kuume ili nipate kuipokea.
53. Nilipo karibia kuipokea ,ikamuponyoka na chongo yake ikagusa maji kabla ya mimi kuipokea,ndipo nikaikamata baada ya

73

yao kugusa maji.
54.Roho aliye tua juu ya maji akasema:Kalonda ameketi upande wake huu ,na Ahmadi upande wake ule.
55. Wasilimu walio kua na niita upande wa Ahmadi walisikitika sana,
56. Na wasilimu walio kua upande wangu pamoja na roho aliye nipeleka wakafurai sana.
57.kiisha roho aliye tua juu ya maji ya mto akanyanyuka na kupaa juu mpaka mbinguni.
58. Nilipo amuka wakati wa sala ya asubui.
59. Niliona umbo ,mfano wa mutu ,yenyi sura ya urembo sana zaidi ya wanaadamu .
60. Alikua amevaa nguo mweupe yenyi kufunika kiwiliwili chake tangu kumabeka mpaka kuvikanyako .
61. Fasi ya mikono yake kulikua kwenyi kuvimba utazani ni mabawa.
62. Alikua na ogelea hewani bila kutembea na miguu yake.
63. Alipo ni kurubia ,nilifunga macho yangu kwa kuogopa, lakini nilikua na muona kama anaye tazama, nilipo fungua macho nikazidi kumuona.
64. Hakika shukrani na heshima humustaili Mwenyenzi peke yake, Hakuna Mola mwengine kama yeye.
65. Ee Mola wangu ! Unipe kila la heri na unikinge na kila la shari na unijaalie mwisho mwema.
66. Usiku ni wako na mchana ni wako, wala Hakuna kisicho kua chini ya uwezo wako.
67. Mungu wa Ibrahimu na Kalonda, aliye pasipo yeyote juu ya maala pa juu.
68. Muumba wa viumbe vyote, aliye tangulia kadiri ya kuenea,mwenyeji wa ulimwengu.
69. Heri mutu anaye amini Mungu Mwenyenzi peke yake.
70. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu Mwenyenzi peke yake.

(2). DIRA

1. Mwenyenzi Mungu amenipatia kazi ya kuhubiri habari ya uzima wake.
2. Watu wengi hawasadiki kwamba Mungu ni mwenyi uzima.
3. Hawaamini kwamba Mungu yupo sababu hawamuonake kimo chake,wala kumsikia sauti yake, na pia ajili ya kuto jibiwa palepale pindi wanapo muomba.
4. Watu hawa humuitaji kimwili kulingana na hali zao,wamezani amelingana na umbo.
5. Hawatambue ya kama Mola wao ni wa pekee tafauti sana na vyote kadiri ya Muujiza wenyi kustaajabisha.
6. Huonekana kimwili yule aliye na mwili.
7. Mungu haonekane kimwili ajili ya kuto kua na mwili wala pumzi mfano wao.
8. Hayo ni kwa sababu yeye ni tafauti sana na umbo zote,sio mwanahewa wala sio muzilahewa
9. Amepatikana mbali sana na viumbe, katika upekee, enzini.
10. Hakuna anaye lingana naye katika tendo kua, peke yake ndio mwenyi uzima na mwenyi uwezo wa kufanya kila kitu, na peke yake ndio anaye jua yote.
11. Huonana ana kwa ana wanao lingana katika busara : kwamba kadiri ya fahamu ya uyu ndio pia kadiri ya fahamu ya yule. 12. Na ndio maana Mutu hazingatie bayana ispokua viumbe vyenzake,maana wote hulingana.
13. Fikara yao ni ndogo sana, haiwezi kuzingatia bayana njee ya anga na ukiwa.
14. Ndio kisa cha mutu kuto muona ana kwa ana Mola aliye njee ya anga na ukiwa, mtukufu anaye hifadhika katika Tabaka la Enzi.
15. Na kusema ni tendo la wanahewa, la muusiano baina yao ambae huweka wazi mawazo yao.
16. Ajili ya uchache wa fikara yao, watu hawafahamiake yaliyomo vifuani mwa wenzao pasipo kusema nao kwa sauti ao kwa mfano.
17. Wametumia misemwa kadiri ya lugha mbali mbali ili wapate kusikilizana,namna ya kusaidiana katika utetezi wao (maisha yao).
18. Haya hutokana na uzaifu wa umbo zao, ambae huitaji msaada kwa kuishi.
19. Na pia hayo humaanisha uchache wa fahamu yao ambae hudai mafunzo kwa kufahamu.
20. Kuzungumuza baina yenu ni miongoni mwa utetezi kifikara, namna ya kuishi.
21. Kua na sema na watu sauti kwa sauti katika haja za watu ni namna ya kuishi pamoja nao.
22. Mungu Mwenyenzi hagusike na uzaifu huo wa kuishi hata kidogo,maana yeye ni mkamilifu mwenyi uzima.
23. Wala hasemake kifikara maana yeye hana fikara, ndio maana haongeake na viumbe vyake kuhusikana na shuruli zao kama anaye fikiri mfano wao.
24. Kusema kwake sio sawa na kusema kwao viumbe, maana Mungu haseme ila kijuzi,bila kazi ya kufikiri wala kutamka kwa pumzi wala kwa ulimi.
25. Akapenda mutu asikie maneno fulani kwa jina lake, sauti hutokelea kwa rafla kutamka maneno yale kadiri ya idhni yake.
26. Sio kwamba hutamka kwa pumzi ama kwa kufungua kinywa ;Mola wenu hana pumzi wala kinywa hana mdomo wala ulimi,wala kiungo chochote, atakalo hutukia kwa rafla.
27. Na kama mutu anasikia sauti yake sio kwamba hutokea dhatini mwake, lakini mapenzini mwake.
28. Na mapenzi yake ni miongoni mwa nuru yake, : kadiri ya roho yake, kadiri ya neno lake.
29. Roho yake na neno lake sio uzima wake, lakini nuru yake takatifu.

74

30. Sauti yake ingeli kua na tokea dhatini mwake, kama angeli kua na shurulika katika kutamka mfano wao viumbe.
31. Hapo angeli kua na ishi namna ya kujitetea mfano wao viumbe,maana shuruli ao kazi haifanyike ila na mwenyi fikara, yaani kwake aliye na maisha.
32. Na maisha haipatikane ispokua kwao viumbe wasio kua na ujuzi, ambae hufikiri.
33. Kwake yeye asiye kua na fikara, hakuna shuruli ao kazi yoyote,atakalo hutukia kwa rafla kadiri ya idhni yake bila kutumika kazi.
34. Kuonekana kimwili na kusema kifikara ndio kua kiumbe chenyi maisha, hali dhalili tafauti sana na Muumba.
35. Kutenda kwake Mwenyenzi ni kwa ajabu hakulingane hata kidogo na kutenda kwao viumbe, maana hawa ni wa zaifu na yeye ni muweza.
36. Watu wa dunia hulazimisha umungu ulingane na umutu, bila kutambua kama uzima ni utukufu wa ajabu usio lingana hâta kidogo na hali dhalili ya maisha.
37. Kama utamlaumu Mungu ajili ya kuto fanya jambo fulani ni vema ujibashiriye mwenyewe kama ni kweli tendo lile hustahili kutendeka na mkamilifu.
38. Mengi wanao mlaumu Mungu haya stahili katika uzima Bali hustahili katika maisha.
39. Mungu ni mwenyi milki kamilifu : anaweza yote na anajua yote, hali ya kua na uhuru, mbali na shuruli yote.
40. Kama Mwenyenzi hufananisha tendo fulani na utendaji wao ni katika mfano ili mupate kuzingatia.
41. Lugha yao viumbe sio ila tafsiri ya utendaji wao ambae ni tafauti kabisa na utendaji wake Mwenyenzi.
42. Hakuna kosa katika uumbaji wake, maana ujuzi wake unao umba ni fahamu kamilifu isiyo gusika na upungufu wowote.
43. Kilicho muimu kwao viumbe ni utiifu ,kutumia maamrisho na kutupilia mbali makatazo, ili wapate wokovu.
44. Majibu ya Mwenyenzi huzingatiwa rasmi na watu kiroho, maana hutendeka kwa njia ya ujuzi tafauti kabisa na fikara.
45. Aliye na roho ndani mwake huzingatia bayana utendaji wa Mola wake kwani yeye sio kipofu.
46. Na yule asiye kua na roho dhatini mwake ndio kipofu asiye zingatia chochote katika ukarimu wa Mola wake.
47. Kwa kujazwa roho takatifu inabidi utumie neno la Mungu katika kawaida yake.
48. Neno lake ndio nuru yake ambae huondoa giza, namna ya kufumbua macho.
49. Muaminifu ni mwenyi kua na ginsi ya kuwasiliana na watakatifu wa mbinguni kwa njia mbali mbali wakati wowote.
50. Anaweza kuonana na malaika pia na roho na Kuzungumuza nao bila panzia ao nyuma ya panzia.
51. Wakaaji wa mbinguni ni wenyi kazi ya kuwasaidia wale wanao amini uzima wa Mungu na kutii sheria yake.
52. Mutumishi wa Mungu anajibiwaka na Mola wake kwa njia mbali mbali kulingana na daraja ya imani yake.
53. Na majibu ya Mola wenu sio katika fikara, lakini katika ujuzi.
54. Kila atendalo mjuzi ni la ajabu maana huzidia fikara ya viumbe.
55. Na ndio maana matendo ya Mola wenu haiheleweke wala kuzingatiwa ispokua na wenyi akili.
56. Na yeyote asiye amini uzima wa Mungu hana akili, ispokua yule anaye tumia neno la Mungu kama dira ya maisha yake ndio mwenyi akili.
57. Mwenyi akili ni yule aliye wa roho ambae hujaa nuru ya taa ya ulimwengu isiyo zimika.
58. Utaalamu wake unamufanya ahepukane na shari na kumukutanisha na Heri.
59. Amepata maisha ya milele sababu amefanyika roho ambae ni miongoni mwa nuru yake Mwenyenzi.
60. Heri mutu anaye pokea karama kutoka mbinguni.
61. Atakaye shika maneno ya kitabu hiki, hali ya kua amejitenga na ushirikina pia na unafiki, atapewa zawadi ya kiroho.
62. Roho amemkurubia yule anaye amini ujumbe huu na kukaa ndani mwake.
63. Mungu Amestawi enzini, juu kupita mbingu, mbali sana na dunia.
64. Ni wa pekee asiye kurubiwa na asiye jumuika, mumilki aliye tangulia kadiri ya kuenea.
65. Yeye ndio mwanzo wa vyote, anaye tokeza bila kutokezwa ,mfinyanzi wa ulimwengu.
66. Mamlaka yake imetawala pahali pote ulimwenguni, wala hakuna asiye milikiwa naye.
67. Uzima wake ni muujiza, na utendaji wake ni maajabu.
68. Mwenyi ujuzi, anaye ona yote na anaye sikia yote.
69. Anga na ukiwa vilifanyika naye bila msaidizi, muweza wa vyote.
70. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu Mwenyenzi peke yake,na hakika Kalonda ni mjumbe wake.

(3). MEZA KUBWA


1. Amejaa utukufu Mwenyenzi Mungu, mjuzi wa kuumba, hakuna kilicho patikana bila hufanyika naye.
2. Uzima wake ni muujiza wa maajabu mbele ya viumbe ajili ya kuenea kimilki.
3. Kuenea ndio kukamilika, yaani kuto kua na upungufu wowote.
4 .Hali yake hii ya kuenea katika tendo kua ni milele kadiri ya kutangulia.
5. Utukufu wa kuto pungukiwa hâta kidogo ndio ukamilifu.

6. Uwezo wake Mwenyenzi umestaajabisha watu ajili ya kuzidia fikara yao.
7. Uzingatiaji wao hutokana na asili yao ya upungufu.
8. Neno la Mungu huletewa katika mifano maana umungu ni muujiza wa maajabu mbele yao viumbe.

9. Mithali ili kufahamisha,  maana lugha zenu sio ila tafsiri ya fikara yenu na matendo yenu, ambae ni tafauti sana na ujuzi wake pia na uwezo wake.

10. Kunapatikana tafsiri ya kimwili na pia tafsiri ya kiroho, sambamba na umbo lake mutu.

11. Pumzi yake ni sehemu ya anga,na mwili wake ni sehemu ya ukiwa; yaani changachanga ya pumzi na mwili.

12. Utazani imepingana kimwili na ilihali haipingane kiroho,maana mwili ni mfano wa giza na roho ni mfano wa nuru. 13. Gizani munamo mashaka ajili ya upofu wa kuto zingatia ; lakini nuruni hakuna ma shaka ajili ya kuzingatia bayana. 14. Kuona kama umungu ni utukufu wa ajabu, ndio maana nuru yake pia sio jambo ndogo.
15. Nuru yake inayo tafsiri nyingi, maana ni jambo kubwa, inahusikana na matazamio.

16. Enzi kadiri ya taa na hewa kadiri ya nuru yake.

17. Ama ujuzi kadiri ya taa na fikara kadiri ya nuru yake.
18. Katika taswira ya ulimwengu inabidi tafsiri zote ili watu wapate kuzingatia.
19. Pumzi inaweza kua nuru na pia inaweza kua giza kulingana na umbile pia na kazi yake.
20. Mwenyenzi aliweka kifaa maalumu ambae hutakasa uchafu unao najisi pumzi.
21. Neno la Mungu ndio hutakasa kabisa pumzi inayo itumia katika kawaida yake.
22. Hâta ikifikia kugeuka roho takatifu hali ya kua nuru yake Mwenyenzi.
23. Watu wote wamealikwa katika nuru yake, na wote wanaweza kua nuru yake ispokua watakae kataa wenyewe.
24. Heri mutu anaye silimu na kutubu, maana ameingia katika nuru, hatua ya kwanza katika njia iliyo nyooka.
25. Kuamini Mungu na malaika zake na mitume yake wote, na vitabu vyake vyote ndio imani ya kweli.
26. Neno la Mungu ni kweli moja inayo fundisha Mungu mmoja na dini moja ya usilimu.
27. Niliona katika ndoto, mutu ananikurubia,na kuniambia,akisema : kuja twende ili nipate kukuonesha !
28. Akaniuliza, akisema : unanifahamu?nikamjibu ,nikisema : hapana. Akasema : hakika mimi ni Roho takatifu wa Mungu.
29. Akanichugua,tukaenda pamoja, tukafika kwenyi mukutano wa watu wengi .
30. Nikaona kumewekwa” meza kubwa “ ya muviringo mbele ya uwanja wa mukutano,ambae juu yake kuliketi watu wa tatu. 31. Nikaona mumoja wa wale watu watatu walio keti juu ya meza akasimama,alikua amevaa kanzu mweupe ; akaanza kuhubiri neno la Mungu kwa kupaza sauti.
32. Wakati huo watu wote walio huzuria mukutano walikaa kimya wakimtekeleza;alipo maliza kuhubiri ,akaketi chini juu ya meza.
33. Ndipo yule mwengine aliye kua pa kati yao akasimama,naye pia alivaa kanzu mweupe, akaanza kuhubiri neno la Mungu namna ya kupaza sauti.
34. Naye alipo maliza kuhubiri, alikaa chini juu ya meza,ndipo alipo simama yule wa tatu :
35. Alikua amevaa kikwembe kyeupe(weupe wa kadiri),akifunika bega lake la kushoto pamoja na mkono ispokua kitanga.
36. Na akaacha wazi bega lake la kuume na mkono wake wote,pasipo kufunika na nguo hiyo mweupe.
37. Akaanza kuhubiri neno la Mungu na sauti ya chini sana na hali ya upole sana tena mwenyi kulainika sana na zaidi, ili bidi kutega sikio kwa kusikia aliyo kua na hubiri.
38. Roho aliye nipeleka akaniambia, akisema :uyu unaye muona akiubiri kwa sauti ya upole sana ndio bwana Yesu.
39. Ameubiri na sauti ya upole sana lakini maneno yake ni yenyi kuinukia ya wenzake wote.
40. Nilipo zidi kumtazama,moyoni mwangu muliingia ulainifu na unyenyekevu.
41. Roho akaniambia, akisema : kuja twende,tukaenda katika njia mbukani,mbuka île ili kua na visuguu vingi na miti mirefu mingi.
42. Nikasikia shindo kubwa sana nyuma yetu, nikageuka na tazama,nikaona ardhi inakuja na geukageuka namna ya kupinduliwa.
43. Milima,miti na mabonde vyote vinageuzwa na kusawanishiwa sawa sawa, nyuma yake hakukubakia bonde wala kisuguu. 44. Roho akaniambia akisema : kweli Nina kuambia ,hiyo siku ya kiyama, bwana Yesu atasaga milima na kusawanisha ardhi, hakuta bakia bonde wala kisuguu.
45. Roho akaniambia akisema : twende. Tukaenda, tukafika kwenyi muji ambae sikuona humo ispokua wanaume.
46. Watu wale walikua kikundi wima uwanjani:walikuja kutupokea na shangwe kubwa, baada ya kusalimiana tukaanza kupita ; 47. Nikaona mutu mumoja aliye keti chini barazani akasimama,akaja kutupokea kwa furaha, akisema : karibu mpenzi wa Mungu, tunafurahi sana kukupokea katika muji wetu, maana tulikua na kungojea ,basi subiri nikuletee chakula, hauta pita na njala.
48. Tukamsubiri,akaingia nyumbani, akaleta muhogo mubichi ambae hauja menyewa,akanipatia akisema : pasula na ukule.
49. Nikachugua muhogo ule ,nikaupasula na vidole vyangu ,na tazama ndani ya muhogo, nikaona mume jaa maandiko ma takatifu yenyi sifa kubwa ya Mungu.
50. Nikamuuliza roho aliye nisindikiza ,nikisema :ndani ya muhogo huu mume jaa maandiko ma takatifu yenyi sifa ya Mungu. 51. Roho akaniambia akisema : soma maandiko Yale yote na imetosha kwako.
52. Nikasoma maandiko Yale yote,ambae yalikua na ongezeka kama nikafika ku mwisho mpaka vile niliimaliza yote.
53. Nikatazama ndani ya muhogo huo, nikaona mizizi tatu, nikamuuliza roho aliye nisindikiza,nikisema : muhogo huu uliumbika namna gani ? Ndani mwake hupatikana maandiko matakatifu pia na mizizi tatu pahali la muzizi mmoja kama kawaida ?

75

54. Roho akaniambia akisema : sikia maana ya hii mizizi tatu.:huu muzizi wa kwanza ndio bwana Yesu. Na huu muzizi wa pili ndio bwana yesu.na huu muzizi wa tatu ndio bwana Yesu.
55. Nikaona kama nimeamuka,nikaanza kufasiria yale nilio yaona,kumbi nilikua bado sija amuka,nikingali katika usingizi ndotoni.
56. Mumoja kati yao akasimama akisema : sikia maana ya maono yako:
57. Maneno ya Mungu yenye unafundishaka, inapandaka huko juu, hiyo siku ya kiyama itakua ndio chakula chako, hauta sikia njaa wala kiu.
58. Nilipo amuka sasa kikweli ,ni kasali rakaa mbili, ni kamuomba Mungu anifunulie wazi maana ya maono haya.
59. Nilipo jitandaza tena kwa kulala, nikamuona tena roho mtakatifu aliye nipeleka,akaja kunichugua na kunipeleka, tukaenda tukafika katika muji ambae watu walikua na zungumuza neno la Mungu barazani.
60. Aliye kua mkubwa kati yao akasimama, akawakataza kelele, akisema : ivi mume zoza Kalonda hâta sikia maana ya yale aliyo funuliwa.
61. Kiisha kutupokea,akamsimamisha mumoja kati yao akisema : ewe mukristu,simama umufasirie Kalonda maana ya maono yake.
62. Yule aliye amrishwa akasimama na kunihelekea akisema : sikia maana ya ndoto yako ewe mpenzi wa Mungu.
63. Fungua kitabu cha warumi sura yake ya kumi na tatu, aya yake ya kumi na mbili, ili upate kufahamu maana ya maono yako. 64. Sema : Yesu masiya ndio njia ya kwendea mbinguni.
65. Hakuna atakaye ingia mbinguni pasipo kutumia neno la Mungu Mwenyenzi.
66. Kuamini Mungu na mitume yake na vitabu vyake vyote, ndio kutumia neno la Mungu.
67. Imani ikaingia ndani ya mutu na kuketi moyoni mwake ,pumzi ya mutu uyu ni miongoni mwa roho takatifu.
68. Yesu masiya ni neno la Mungu, na ni roho ya Mungu. Na ni njia ya Mungu.
69. Jihadharini na imani mbaya ya kumpachika aliye tumwa daraja ya yule aliye mtuma.
70. Mungu ni mumoja, hakuzaa wala hakuzaliwa,mkamilifu asiye zaufika wala kubadirika,wa pekee aliye juu.


(4). KISWAHILI


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, mumoja, atanguliaye ulimwenguni.
2. Mola mwenyi uwezo wa ajabu kuzidia vyote, wala hakuna kilicho mkurubia katika mamlaka.
3. Ni yeye anaye nusuru muja wake kwa namna ya miujiza.
4. Na kuwaangamiza mahasidu na wanafiki wanao piganisha maisha ya mtumishi wake bila sababu.
5. Shetani ni adui wa watu, anaye ingia katika nyoyo za watu wasio tumia urakibu.
6. Na kuwaimiza kufanya ufisadi wa kila namna, ambae ndani mwake hamna ispokua ubaya.
7. Ni muimu kwa kila mutu kujitenga mbali na adui yake (shetani) asiye onekana kimwili.
8. Anaye onekana kiroho peke yake, ambae hujificha ndani ya umbo ingine ili apate kudanganya watu.
9 . kujitenga na adui uyu ni kunusuru nafsi yako na shari ya kila namna.
10. Ukingo wa kweli ili adui uyu asivamie nafsi yako hasa ni imani na ibada ya Mungu.
11. Kuwa yakini moyoni na uzima wa Mola wako, na kumkumbuka kila wakati popote ulipo.
12. Na kumsifu kwa wingi na kumshukuru kwa yote anayo kufanyia.
13. Hakika shukrani zote zinamustahili Mwenyenzi Mungu, muweza wa yote.
14. Na umsujudie Mungu peke yake, wala usisujudie mwengine badala yake.
15. Na ndio maana ni amri kwa kila mutu kuhelekeza mawazo yake yote kwa Mungu katika sala.
16. Hakika sala ndio ibada kubwa, tendo kubwa la unyenyekevu mbele ya Muumba.
17. Hali yake Mungu ni muujiza ambae fikara ya viumbe haiwezi kuukagua.
18. Amezidia wote katika mambo yote maana Hakuna mwengine aliye na milki kamilifu kama yeye.
19. Watu wamestaajabu sana uzima wake ambae ni tafauti sana na maisha yao.
20. Vyote vinavyo patikana katika umutu ,havipatikane hata kidogo katika umungu.
21. Watu wa dunia wamestaajabu sana hali yake ya ukamilifu ya kutokua na mila.
22. Kua na mila fulani ni kua na umbo fulani hali ya kua kiumbe.
23. Mila ni jambo ambae hupatikana katika upungufu ,haina fasi katika ukamilifu.
24. Usawa wenyi kuenea haupatikane ispokua katika umungu
25. Vyote ambae hupatikanakatika umutu sio katika usawa wenyi kuenea ajili ya kuto kamilika.
26. Fikara sio ila shuruli kadiri ya utetezi ,namna ya utafiti wa utimilifu.
27. Uzuri huangamiza ubaya ,na ubaya pia huangamiza uzuri.
28. Mkamilifu ni mtukufu aliye huru kabisa hakuna cha kumuangamiza ,wa pekee aliye tafauti kabisa na mila yote.
29. Mungu aliye juu ni mwenyi uwezo wa vyote,na ndio maana inabidi kumpelekea ,yeye peke yake, maitaji yenu yote .
30. Maombi ya muaminifu sio katika shari lakini katika heri ,amemtukuza mola wake na kujisihi kwake kwa siri na kwa wazi. 31. Hawezi kumuendea mchawi kwa shida ya kiroho ,asije akavamiwa na shetani.

77

32. Mola wenu amewapendeni sana na ndio maana huwaleteeni ujumbe ili mupate wokovu.
33. Pasipo uzima wake hakungeli patikana yeyote miongoni mwa viumbe.
34. Ni amri kwa watu wote kumuamini na kumuabudu yeye aliye tangulia,mfalme anaye miliki upatikanaji wote na maisha yote.
35. Heri mutu anaye vumilia pindi anapo jaribiwa ,bila shaka atavikwa taji la utukufu baada ya ushindi.
36. Katika maisha kuna kupanda na kushuka ,wala usimlaumu Mola wako ajili ya madhara fulani kukupata.
37. Asili ya kila umbo ni upungufu ,hakuna ukamilifu katika umbiko.
38. Mungu ndio mufalme wa ulimwengu anaye anzisha na anaye komesha kila kitu .
39. Ni yeye atakaye mtuma Yesu masiya siku ya kiyama na kazi kubwa ya kusawanisha ardhi sawasawa ,ikuwe yenyi unyoofu kabisa.
40. Kuifanya ardhi ikuwe nyoofu,katika usawa pasipo utafauti wowote ndio kugeuza dunia kua bustani ,namna ya kuondoa matatizo yote na kuleta amani ya milele.
41. Watu wema ndio watakao keti katika ardhi hii mupya nyoofu,kadiri ya bustani,na kuishi humo milele.
42. Na waovu ndio watakao tupwa njee ya usawa ,katika uharibifu hadezeni.
43. Humo hadezeni ,hufikiwa na kifo cha pili ,kadiri ya upotevu wa nafsi.
44. Katika bustani hupatikana uhai kadiri ya utimilifu wa umbo .
45. Kuichora ardhi kadiri ya bustani sio jambo ngumu kwa Muumba.
46. Wala kuichora pumzi ya mutu hali ya kua roho takatifu sio jambo ngumu kwa muumba.
47. Siku ya kiyama nafsi ya mutu haita kua kama ilivyo kua baada ya kifo .
48. Muumba atamurudishia mutu umbo lake ,yaani atamfufua.
49. Mutu hata kua tena mwili peke yake kama alivyo kua kaburini ,wala hata kua tena pumzi peke yake kama alivyo kua barazani baada ya kuihama dunia.
50. Mwanaadamu atakua kama alivyo kua duniani,changachanga ya pumzi na mwili .
51. Mwenyenzi Mungu ni mwenyi uwezo wa kufanya yote ,wala hakuna mfundi mwegine zaidi yake.
52. Mola wenu ni mwenyi uwezo wa kuweka bustani katika ardhi hii mupya ,hata mukipatikana starehe ya milele .
53. Kadiri bustani ilivyo leo huko mbinguni hailinde ndani mwake ispokua pumzi tukufu ,yaani mwanahewa halisi peke yake. 54. Kwa ginsi ipate kulinda mutu ambae amekwisha kufufuliwa kadiri alivyo kua duniani ,huchanga bustani na ardhi nyoofu.

55 Kama alivyo changa ardhi yenyi usawa na bustani ,na hata ikapatikana Edeni,eneo lenyi kua na ginsi ya kumlinda Adamu na Eva ,ambae ni wanahewa_haramu.
56. Mwenyenzi ndio m'bora wa wanao ruzuku ,,mwenyi rehema za milele.
57. Amebarikia wanao amini bila wasiwasi wala mashaka,ambae hujitaidi kwa kutenda mema.

58. Wanao simama katika kisomo cha ufunguzi ,na kumsujudia pia na kushaidilia upekee wa Mungu mwenyenzi . 59 .Asiye abudu Mungu kwa kutumia taratibu kama hii imani yake ni ya bure kabisa .
60. Musilimu ni mnyenyekevu anaye abudu Mungu mfano wa wakaaji wa mbinguni.
61. Muskiti ndio nyumba inayo jengwa ajili ya ibada ya Mungu mwenyenzi.

62. Ibada inayo fanyika humo muskitini ni :sala,maubiri,dhikri,kisomo na maombi.
63. Matandiko bora ndani mwake ni misala ,na mfano wa hayohumo hamustahili viti na mameza ao vitanda,maana ni maala pa kumsujudia Mungu.
64. Kumsifu Mungu katika kisomo ao katika nyimbo ni jambo la kawaida kabisa ,panafasi yake .Hapana kuimba ndani ya sala. 65. Ni lazima moyo wa musilimu kufanana na muskiti ,ambae ndani mwake hufanyika ibada ya Mungu.
66. Muskiti ni nyumba tukufu ya ibada ya jamaa la kidini,kuacha kujumuika muskitini ni kuvunja alama ya dini ya Mungu.
67. Mungu mwenyenzi ndio tajiri wa vyote ,ma kabila yote ni yake wala hakuna lugha isiyo kua yake .
68. Kila mtume wa Mungu alifunuliwa katika lugha yake yenye anasemaka,ili asikie na afahamishe watu.
69. Kauli tukufu hii imefunuliwa katika kiswahili sababu Kalonda anasemaka kiswahili,sio mkazo ku watu kutumia lugha ya mjumbe wao katika sala ,ispokua kipenda_roho.
70. Heri yule anaye tumia ukweli huu maishani mwake.

5). ROHO


1. Mwenyenzi Mungu ndio mshindi ,hakuna mwengine kama yeye ,muumba wa anga na ukiwa ,wa milele aliye juu.
2. Ujuzi wake unamfanya atokeze aina nyingi sana ya pumzi ,halisi na haramu ,kadiri ya idhini yake.
3. Kila anaye pumua hewa ,ndani mwake hupatikana fikara ,na ndio maana ni mwenyi maisha.
4. Umbo la kihewa linalo itwa pumzi humfanya apumue na afikiri ,yaani apate kuishi.
5. Nafsi isiyo kua na pumzi sio kihewa lakini kimwili ,na ndio maana ni miogoni mwa wazilahewa ,njee ya maisha.
6. Heri mutu anaye kagua baina ya nafsi kihewa ,ambae hutafautisha wakaaji wa mbingu na wakaaji wa hadeze.
7. Mungu aliumba mbingu na thamani kubwa,na wakaaji wake pia ni watukufu.
8. Malaika na roho ni viumbe vitukufu maana hutokana na nuru yake takatifu.
9 Pumzi zote sio roho ,kunapatikana umbile za kihewa tafauti.
10. Nafsi kihewa inayo patikana ao inayo fanyika ,kadiri ya neno ao kwa njia ya neno la Mungu ndio "Roho".

78

11. Nafsi kihewa ,yaani pumzi,inayo patikana ao inayo fanyika kinyume ama tafauti na neno la Mungu sio roho,lakini muzimu. 12 .Na malaika sio roho,bali ni umbo mbili tafauti.
13. Na shetani sio muzimu,bali ni umbo mbili tafauti sana.
14. Malaika ni mwenyi mabawa,lakini roho hana mabawa.

15. Na shetani ni mwenyi mapembe ,lakini muzimu hana pembe.
16. Roho ni jaza la nuru ,na muzimu ndio jaza la giza.
17. Mungu amestawi peke yake arshini,hakuna wa kujumuika naye wala jerani yake.
18. Wengine wote ni umbo alizo ziumba ,hakuna atakaye weza kukurubia dhati yake tukufu.
19 .Roho ni miongoni mwa viumbe vyake vitukufu ambae hupatikana mbinguni
20. Enzini hamuna roho wala malaika ,wala kiumbe chochote .
21. Ni maala pa upekee penyi kujaa milki kamilifu, umbo zote huyeyuka ,namna ya kufutika,kandokando mwake ,hakuna ginsi ya kujumuika enzini.
22. Watu wasio kua na elimu wamemfananisha Mola wao na roho ,bila kutambua kama mwenyenzi halingane na umbo yoyote. 23. Roho ni nafsi kihewa kadiri ya pumzi tupu.ndani mwake hamna Enzi bali hewa ambae ni nuru ya Enzi
24. Ni mwanahewa_halisi aliye umbwa kwa hewa ,anaye ishi hewani kwa kupumua hewa,kadiri ya neno lake.
25. Mola Aliye pasipo yeyote, juu ya maala pa juu ni mjuzi wa kutokeza mapya wakati wowote kadiri apendavyo .,
26. Kama anaruhusu upatikane kua mutu wakati huu kadiri ulivyo ni amri kwako kumshukuru kwa wingi
27. Angeli penda usijumuike ulimwenguni kama wewe ni sifuru ,haungeli kua chochote .
28. Na kama Mungu anaita mutu fulani kua ndio roho yake, ni kwa kuonesha ukubwa wa imani ya mutu yule, ameishi kwa njia ya neno lake kadiri ya nuruyake.
29. Ndio maana Mungu amemuweka katika fungo la viumbe vyake vitukufu vinavyo itwa Roho.
30. Na kama Mungu anajitapia kiumbe fulani kua chake,sio kwamba viumbe vingine sio vyake, wala haimaanishe ya kwamba kiumbe hicho ndio yeye.
31. Hayo humaanisha ukubwa wa daraja ao thamani ambae Mola kajaalia umbo île.
32. Ametakasika kabisa Mwenyenzi Mungu na Yale yote wanao mshirikisha nayo.Mola mwenyi ukamilifu, wa pekee aliye juu. 33. Mbingu, hadeze na dunia ni mazao ya idhni yake mwenyewe, pasipo mshauri wala msaidizi wa kazi.
34. Ni yeye anaye Lea maisha ya wanahewa wote, kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.
35. Kumuabudu yeye peke yake na kuacha maovu yote ndio kuichora pumzi yako kua roho takatifu.
36. Mungu ndio mwenyi uzima, kujiuliza kama ni kweli Mungu iko ,ni alama ya kukosa akili, hali ya upofu.
37. Pasipo Mungu kutangulia, hakungeli patikana chochote ulimwenguni.
38 .Kwa kitu kutokezwa toka sifuru ,inatakika kupatikane kabla ya yote,yule awezaye yote na ajuaye yote, atakaye kitokeza.
39. Hakuwezi kutokezwa kitu bila fundi wa kukitokeza kutangulia kupatikana mbele ya yote.
40. Kitu kisicho dai wa kukitokeza ni kîle kilicho kamilifu, ambae hujieneza katika yote bila upungufu wowote.
41. Kingeli dai msaada kwa kyao kupatikana kama kisingeli weza kutokeza toka sifuru, maana kingeli kua na uzaifu mfano wao viumbe.
42. Hakika kushakia uzima wa Mola na hali uko na zingatia viumbe alivyo viumba, ni upofu, hali ya kukosa macho ya kiroho inayo itwa "akili".
43. Mungu Mwenyenzi ndio m'bora wa kutenda, mjuzi anaye jaza tabaka la anga na maisha ya kila namna.
44. Kujiuliza kama Mungu anaweza ni kukosa imani, amejaa ma shaka ajili ya kukosa yakini.
45. Vyote kwa jumla hutendeka kwa idhni yake, lau kama hasingeli Patiana nguvu ya utendaji, bila shaka viumbe visingeli weza kufanya lolote.
46. Na kama viumbe visingeli weza kujikusuru kiutendaji kama hakungeli patikana maisha yeyote ulimwenguni.
47. Kilicho mfanya atangulie bila kuanza na atokeze ambacho hakikua popote ni île milki kamilifu aliyo nayo ambae ni mamlaka ya kufanya anayo penda,pasipo kushindwa na chochote.
48. Mungu ndio muweza yote kadiri ya mwanzo wa vyote, pasipo yeye hakungeli patikana wala kufanyika chochote.
49. Mungu ndio mjuzi wa vyote ,ambae vyote ni vyake, wala hakuna kisicho kua chake,kwani ndiye muanzishaji wa kila kitu. 50. Yeye ni mwenyi mamlaka ya utendaji, anaye anzisha na anaye komesha .
51. Hakuna mwengine kama Mungu, wa miujiza na wa milele.
52. Alitangulia kadiri ya kuenea katika mamlaka yake mwenyewe, kabla ya ulimwengu na baada ya ulimwengu,mwenyi kukamilika.
53. Mufalme anaye enea katika tendo kua,mtukufu asiye badirika.

54 .Mungu Mwenyenzi sio mwenyi maisha wala sio mwenyi ukiwa, lakini mwenyi uzima. 55. Ni mwenyi kuenea katika yote mbali na upungufu wote.
56. Mamlaka yake humiliki kila kitu, vitu vyote ni chini ya uwezo wake.
57. Hakuna mwengine kama yeye ,wa pekee atanguliaye ulimwenguni.

58. Ukamilifu wake unamfanya aenee katika tendo kua pasipo kabla yake wala baada yake, na atokeze vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani bila kuiga mfano popote wala kutumika kazi yoyote .

79

59. Kama si ukamilifu wake,hakungeli patikana chochote Bali sifuru ingeli tawala milele.
60 . Mpungufu hawezi kutokeza toka sifuru maana ni mwenyi uzaifu hafahamu chochote wala hawezi lolote bila msaada wa mfinyanzi wake.
61. Ujumbe huu ni ukweli usio kua na shaka ambae Mungu kaushuudia mwenyewe.
62. Kuna patikana umungu ambae ndio ukamilifu kadiri ya uzima.
63. Ni utukufu wa ajabu, mamlaka ya milele inayo patikana kimuujiza bila msaada wa yeyote.
.64 Hakungeli patikana yeyote wala chochote bila milki kamilifu kama hii kutangulia ulimwenguni.
65. Mutu asiye amini Mungu ni sawa na mnyama ambae hukosewa akili.
66. Na waaminifu wote ni katika fungo moja na wanahewa_halisi, watakatifu wenyi hidaya kadiri ya jaza la nuru yake Mungu. 67. Tumieni wote ukweli huu ili mupate kuzingatia uzima na kujumuika mbinguni.
68. Hakika Mungu iko mzima,mufalme wa milele, aliye tangulia kadiri ya kuenea.
69. Heri mutu anaye silimu na kutubu maishani mwake,ambae humsujudia Mola wake usiku kama vile mchana.
70. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mwenyenzi Mungu peke yake.


(6). MUUSIANO


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,Mjuzi aumbaye ,wa pekee anaye stawi katika dhati yake mwenyewe .
2. Mwokozi aliye na mamlaka juu ya kilakitu, mwalimu wa wote.
3. Ni yeye anaye letea watu ujumbe kuwanusuru na shari ya giza
4. Kumuamini aliye tumwa na Mungu mwenyenzi ni neema,jambo muimu kwa watu wote .
5. Kama ni wa uwongo mutamutambua kwa matunda yake .
6. Na Hakika kumzingizia Mungu kwamba kakutuma na ilihali hakukutuma ni zambi kubwa sana, wala mutu hafikie kiasi hicho ispokua kafiri mkubwa.
7. Na wengine walio kufuru hawaamini mtume yeyote sababu hawa kujionea wala kujisikilia wakati walipo funuliwa na Mungu.
8. Usilazimishe kukutanika wanapo funuliwa kwa wewe kuamini ,utajionea ao kujisikilia namna gani na hali sio wewe ulio funuliwa?.
9. Lau kama ni ushahidi wa mambo ya kidunia anakubali kwa haraka bila kulazimisha kukutanika yeye mwenyewe .
10. Hayo humaanisha ukafiri mtupu ,amejaa kiburi sababu ya kupewa muda ,hakika atajuta kwa yale aliyo kua akiyafanya.
11. Mjumbe wa Mungu ni mwenyi elimu ya juu,mwenyi utaalamu wa kiroho.
12. Ameinukia wengine maana ni uvuli wa ujuzi, nuru ya taa ya ulimwengu.
13. Neno anaye toa sio lake Bali la yule aliye mtuma, na ndio maana ni lenyi kuinukia.
14. Basi jihazarini na upinzani musije kuwapinga mitume wa Mola,musifikie kuanguka pembeni yao mfano wa makapi.
15. Na wanao kanusha wajumbe wote ndio makafiri wanao kanusha uzima wa Mola wa walimwengu.
16. Aminini Mungu Mwenyenzi aliye umba mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo.
17. Ni yeye aliye tangulia kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho.
18. Hakuna mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyenzi peke yake.
19. Hakika wengi miongoni mwa watu waliingia katika hasara alipo tumwa Ahmad, kila mutu aliye mpinga ni mwenyi hasara. 20. Mungu amemtuma malaika aniagize neno hili:hakika Ahmad ni mjumbe wa Mungu, wala musiwe na shaka juu yake.
21. Basi aliye na masikio ya kusikia asikie .
22. Mwenyenzi ndio mumilki, mpanaji wa nguvu anaye tegemewa na walimwengu wote kwa jumla.
23. Mola wa karne na karne,Hakuna kisicho milikiwa naye, mshindi wa popote na milele.

24. Ni yeye anaye fanya muusiano baina ya sehemu zote za ulimwengu ili maisha ipate kutimilika.
25. Amejaa utukufu wa ajabu, mchungaji mwema anaye rehemu na anaye kirimu .
26. Achanikaye mbinguni huonana na watakatifu wa mbinguni na kusharikiana nao pia, wakingara namna moja kama matonge ya nuru.
27. Na yule achanikaye hadezeni, huonana na wakaaji wa hadezeni na kusharikiana nao pia, wakififia wote kama matonge ya giza.
28.muusiano wa mbingu na dunia ndio ufunuo ambae huambatanisha mutu na nuru.
29. Na muusiano wa dunia na hadeze ndio ushirikina ambae huambatanisha mutu na giza.
30. Mutu atakaye wasiliana na mbingu atatukuzika mpaka kufikia daraja ya juu ya viumbe vyote.
31. Na mutu atakaye wasiliana na hadeze atazalalika mpaka kufikia daraja ya chini ya viumbe vyote.
32. Muusiano na mbingu umeleta baraka,na muusiano na hadeze umeleta laana.
33. Hakika ni bora kwa mutu kuchagua Heri kuliko shari.

34 .Mola wenu amekua yote katika yote, juu ya yote kuliko wote ,m'bora wa kuenea. 35. Ukamuomba heri atakupatia ,na ukimuomba shari atakupatia.
36. Maisha ya mutu ni utetezi baina ya mema na na mabaya.
37. Akili yako ndio itakayo kuweka huru ao mtumwa.

38. Lau kama watu wangeli ona ginsi mizimu inavyo taabishwa na shetani humo zimuni,kama watu wote wangeli ogopa kutenda zambi.

39. Na lau kama wangeli ona ginsi roho inavyo shangiliwa na malaika humo mbinguni,kama watu wote wangeli pupia kutenda mema.

40. Maana Hakuna furaha sawa na hiyo ya mbinguni,na pia hakuna mateso sawa na hiyo ya hadezeni.

41. Hakika Mola wenu ni m'bora wa mahakimu : humlipa kila mmoja wenu sawa sawa na matendo yake.

42. Tumieni urakibu maishani mwenu,enyi walio silimu, hakika hii ndio njia iliyo nyooka.

43. Aliye katika njia iliyo nyooka hana tegemeo ingine badala ya Mungu Mwenyenzi.

44. Matendo yake imeambatana sana na maamrisho ya Mungu ,tafauti kabisa na makatazo yake.
45. Mnyenyekevu ni yule anaye fuata sheria ya Mungu, ameogopa kutenda zambi asiye kupotea njia.

46. Mwenyenzi ni mkaguzi wa mambo ya siri na ya wazi, Hakuna asilo lijua.
47. Mtefuzi wa kila zamiri, chemchem ya fahamu ulimwenguni.
48 . Ufunuo utokao mbinguni ndio mwongozo wa maisha ya watu.
49. Hakuna utimilifu wa maisha pasipo imani, wala hakuna wokovu njee ya nuru yake. 50. Cha muimu mbele ya yote ni kusilimu na kutubu.

51. Dini inayo undwa pasipo ufunuo ni makila ya shetani.
52. Watu wengi wamefichamia katika neno la Mungu, wakidanganyia kuhubiri na kuombeana . 53. Wanapo piga ramli, hudanganyia kutabiri maono,wamezani kupata kumbi kupatikana .
54. Hakika hawadanganye ispokua nafsi zao wenyewe ,watajuta kwa Yale walio kua wakiyafanya.

80

55.Mutu atakaye ingia katika dini isiyo fundisha umoja wa Mungu, amepotea njia.
56. Na yule atakaye ingia katika dini isiyo fundisha namna ya kumsujudia Mungu peke yake ameangamiza nafsi yake mwenyewe.
57. Hakuna imani moyoni mwa mutu pasipo matumizi ya shaada na sijida.
58. Mungu amewapenda sana wanyenyekevu wanao muabudu yeye peke yake.
59. Mitume wote walikua na shaidilia umoja wa Mungu na pia wote walikua na msujudia yeye peke yake.
60. Atakaye tenda umbalimbali na mafundisho ya mitume ya Mungu ni miongoni mwa makafiri, pumbafu anaye potea njia. 61.Roho aliniita,tukaenda,tukafika maala ambae mutu alikua na hubiri ,alikua mnene,akivaa shati na suruhali,ya rangi ya kahawa.
62. Roho akaniambia akisema :mutu uyu anaye hubiria hili kundi la watu ndio Kadima ya Nzambi.
63. Mutu uyu amedanganya watu kwamba alitumwa na Mungu na ilihali Mungu Mwenyenzi hakumutuma .
64. Maneno anaye hubiri inasikilika na watu wa dunia kama ni maubiri ,lakini mbinguni maneno yake imesikilika kama matusi makubwa anayo mtusi Mola wa ulimwengu.
65. Hakika nakuambia mutu uyu ni Nabii wa uwongo tena mchawi mwenyi laana kubwa .
66. Nilipo sikia hayo nikamuambia roho tuondoke pahali hapo ,tulipo anza kwenda ,yule Nabii wa uwongo akageuka kutuangalia,akaanza kututukana na kutukania kutuiba sehemu ya nyota yetu .
67. Roho akaniambia akisema : usiogope hana uwezo wowote mbele yetu.
68. Zama hizi watu wengi wamemzingizia Mungu kwamba kawatuma na ilihali Mungu hakuwatuma .
69. Uwaambie watu wafanye angalisho na ma nabii wa uwongo,
70. Wajumbe wa uwongo wamewadanganya wale wanao amini kwa kuona miujiza ,ambae huamini ya kama Mungu anaweza kujigeuza mutu,wao ndio mateka ya masih dajali.

(7) JARIBU


1. Ametakaskka mwenyenzi Mungu ,mfalme wa ajabu anaye patikana kadiri ya kuenea,bila mwanzo wala mwisho.
.2 Utangulizi wa dhati yake ulimwenguni ndio uzima ambae ni umungu.
3. Mshindi anaye zidia wote kimilki na kiufahamu.,ambae vyote humuitaji .
4. Pahali alipo hakuna mwengine, wa pekee bila mfano wake wala diko mwenzake ,wala jerani yake.
5. Mtukufu wa ajabu aliye yote katika kujua na yote katika kuweza ,muujiza wa maajabu ulimwenguni.
6. Mola wa mashariki yote na magharibi yote,mwenyi mamlaka ya milele.
7. Katika ulimwengu kunapatikana hali mbili tafauti: ukamilifu na upungufu.
8. Ukamilifu ndio uzima ,kadiri ya kuenea.Hali tukufu ya kumiliki vyote pasipo uzaifu wowote.
9. Na upungufu ndio hali dhalili ya Ukosefu wa Mamlaka ya kuenea .Na kuto enea ndio uzaifu wa kushindwa.
10. Ukamilfu ni utukufu ,mamlaka ya kuweza yote na kujua yote
11. Na upungufu ni udhalili ,uzaifu wa kushindwa na yote ,ambae hudai msaada kwa kufanyika na kwa kufanya .
12. Kuanza husababisha kua sifuru kabla yake.
13. Na kukoma husababisha kua sifuru baada yake.
14. Kuanza na kukoma ndio alama kubwa ya uzaifu wa kitu ,upungufu wa kutokamilika
15. Na ndio asili ya kila umbo ,tafauti kabisa na muumbaji .
16. Kuona kama Mungu hana uzaifu wowote ndani mwake, ndio maana hakuna kabla yake wala baada yake

81

17. Mungu ni mwenyi kukamilika tafauti sana na upungufu wa aina yote.
18. Na ndio maana yeye peke yake ndio mwanzo wa vyote,yaani muanzishaji wa kila kitu.
19. Pasipo ukamilifu wake kama sifuru ingeli tawala milele.
20. Katika upungufu hamna ispokua uzaifu mkubwa ,na ilihali uzaifu hauwezi kutokeza toka sifuru.
21. Kama kuna patikana ulimwengu na walimwengu (yaani umbiko)ni kwa sababu Mwenyenzi Mungu alitangulia namna ya kuenea pasipo uzaifu wa kuanza na kukoma.
22. Shangilieni uzima wa Mola wenu aliye juu ,muweza yote na mujua yote ,wa pekee anaye kamilika.
23. Mungu peke yake ndio mwenyi uzima tafauti kabisa na kila kitu, hakuna anaye fanana naye .
24. Fikara ya viumbe ni jambo dhalili mbele ya ujuzi wake, wala haizingatie chochote ispokua kwa ruhusa yake.
25. Mwenyenzi ni mkamilifu anaye stirika milele ,ambae hafikiwake na asicho kitaka kamwe.
26. Na ndio maana huzuni na hasira hukomea kwao viumbe ,alama ya uzaifu kama hii haipatikane enzini kamwe .
27. Amelinganishwa na viumbe katika hayo kupitia mapenzi yake ambae huzingatiwa kadiri ya nuru yake.
28. Malaika na roho ni mfano wa nuru yake ambae hutimiza mapenzi yake,
29. Katika upungufu wa ubinaadamu,watu wamezani kama kile kinacho wa huzunisha ao kinacho wa kasirisha , ni vivihivyo pia na kwake mwenyenzi maana wao ni uvuli wake.
30. Kwa kufikia mapenzi yake mshindi lazima kuiga mila ya malaika na roho ,ambae humnukulu.
31. Atakaye tenda kinyume na mila ya watakatifu wake ,bila shaka atakua amepotea njia .
32. Watakatifu wake wa mbinguni ni mfano wa nuru yake lakini sio mfano wa Enziyake
33. Ni tafauti sana na dhati yake,maana wao ni viumbe na yeye ni muumba.
34. Matendo ya viumbe hailingane na matendo ya muumba kamwe
35. Mila nzuri huwaingiza watumishi wake katika utimilifu sio katika ukamilifu.
36. Kama malaika na roho hupatwa na huzuni pia na hasira sio kwamba uzaifu huo utamgusa mtukufu wa daraja aliye enzini. 37. Mwenyenzi ni muujiza wa maajabu aliye pasipo yeyote ,juu ya maala pa juu,hafanane na yeyote .
38. Amekua na milki kamilifu ambae hutenganisha kutenda kwake na kutenda kwao viumbe.
39. Kutenda umbalimbali na mafunzo ya watakatifu wa mbinguni ni kutenda sawa na mafunzo ya Shetani.
40. Kinacho tafautiana na nuru kimelingana na giza.
41.Tumieni maamrisho ya Mungu na itupilieni mbali makatazo yake ili mupate wokovu.
42. Mungu ndio anaye stahili kutumainiwa zaidi ya wote maana ndiye peke yake awezaye yote.
43. Heri mutu anaye simama imara katika njia ya Mungu.
44. Hasara ilio je kwao vigeugeu wenyi kua mguu njiani mguu porini .
45. Unafiki ni sumu maishani ,maana hufupisha umri wa mwanaadamu .
46. Mungu ni mwenyi uwezo juu ya kila kitu ni vema kua yakini naye.
47. Vyote viliumbwa naye na vyote humilikiwa naye na pia vyote hukomeshwa naye.
48. Ni amri kwa watu wote kuamini kwamba Mungu iko.
49. Hakuna Mola mwengine kama yeye,mkamilifu aliye pasipo yeyote ,milele na milele..
50. Ni mtukufu wa ajabu ambae dhati
yake huunguza kadiri ya kufuta umbo zote kandokando yake.
51. Amengara zaidi ya nuru ,taa tukufu ya ulimwengu isiyo lingana na chochote .
52. Nuru yake ni kubwa ajabu ambae hupofoa jicho linalo jaribu kumchungulia.
53.Amejidhihirisha kwao kwa namna ya mifano na pia kwa njia ya neno lake.
54. Bila yeye kujifunua kwenyi wajumbe wake kama watu hawangeli zingatia uzima wake.
55. Anaye sikia sauti ya Mungu ndio anaye muona Mungu ,amemzingatia kupitia kauli yake.
56. Hapana kulazimisha ukamilifu ukuwe sawa na upungufu,ambae ni kamilifu ni muujiza mbele ya wapungufu.
57.Anaye kanusha ujumbe na kulazimisha tu kumuona kimwili ni kafiri anaye mkanusha Mola wake kwa kusudi .
58. Katika maisha ya watu kuna patikana kipindi cha majaribu, ni lazima kuizingatia na kuihepuka.
59. Shetani anajipindaka na ushambulizi kujaribu kuwaangusha wasilimu katika imani yao.
60. Kupatwa na madhara fulani ni jambo la kawaida kwa watu wote,hapana kumkufuru Mungu.
61. Shari na mema yote imetoka kwa Mungu, kilicho muimu kwako ni kuamini na kuabudu na kuomba Mungu.
62. Na kupewa uchawi bila wewe kutaka pia ni jaribu .kilicho muimu kwako ni kuukataa,yaani kutoutumikisha kwa kurogana. 63. Atakaye utumikisha baada ya kuambukizwa atakua ameshindwa na jaribu .
64. Ni lazima kwako kuzidisha ibada ya sala na Saumu na dhikri ya kisomo cha kitabu hiki kitukufu.
65. Mola wako atakusafisha ,mamlaka yote ni yake, wala hashindwake na chochote kamwe.
66. Kauli tukufu ya kitabu cha ukweli ni yenyi nguvu na ushindi ambae huunguza kila falme za giza.
67. Kama unajitenga na mabaya na kutumia kauli tukufu hii katika mpango maalumu, bila shaka utafanikiwa katika maombi yako.
68. Hakika dawa ya kutibu nayo jaribu ni subira na ibada .
69 Kitabu hiki ni ukweli kutoka kwa Mola wa ulimwengu.

70. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu Mwenyenzi peke yake


8. MUHAMADI


1.Roho alinichugua, tukaenda pamoja,tukafika pahali walipo
kua wakichoma nyama ya bei.
2.Nikapenda niuze nyama ile, lakini Roho aliye nipeleka
akanikataza
3.Nikamuuliza kwa nini nisiuze ambae wasilimu wameuzisha ?
4.Akanijibu akisema :sio halali,kuna wasilimu wanao tumiaharamu bila kufahamu ; 5.Mara huruhusu makatazo na mara hukataza maamrisho.
6.Tukaenda ,tukafika muskitini,tukaingia na kusali .
7.Tulipo maliza tukatoka uwanjani.
8.Katika uwanja kulikua Muti mukubwa tena mrefu.
9.Roho akanionesha muti ule, akisema : Muti huu ndio
Muhamadi ,
10.Katika ardhi yote unabaki uyu peke yake,ingine yote

imekwisha anguka.
11.Nikachugua mpanga,nikakata tawi moja ya Muti ule ili niupandikize.
12.Nikaona Roho ya uwalii inakuja haraka na kutua mbele yangu,ikisema : kwa nini unakata muti huu ? 13.Nikamjibu,nikisema :nime kata tawi hii moja ili niupandikize

fasi mbali mbali, maana ivi unabaki umoja,kunahatari ya
kupoteza hii aina ya Muti.
14.Roho akafurai, akisema,unafanya vizuri ;sasa wende na patia watu vipande vya tawi ili wakusaidie kuuotesha,wale watakao penda. 15.Nami nikafanya kadiri Roho aliniambia.

16 .Nikamupatia mutu mumoja Aliye kuja haraka ili anisaidie.
17 .Kiisha kumupa ndio nikaenda kutafuta wengine wa kuwapatia. 18 .Na mimi nikabaki na tawi kubwa nikaiotesha mwenyewe.
19 .Nilipo tazama mbele yangu,nikaona Roho anakuja na

ogelea hewani, katika nuru kubwa.
20 ..Alikua mfano wa mutu,akivaa kanzu mweupe na mtama weupe na suruhali mweupe.
21 ..Na nyuma yake kulikua sahafa ya watoto wadogo wakivaa sawa naye (makanzu,mitama na ma suruhali,mweupe).
22 .Roho akaniambia, akisema :uyu unaye muona ndio « Yasini ». 


9. SAFARI


1.Uzima ni wake mwenyenzi Mungu,mkadirishaji wa karama .
2. Anamupatia amtakaye,na humunyima amtakaye.
3.Ndiye chemchem ya uhai wote,pia ya mauti yote.
4 .Vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini hutukuza jina lake 5.Ni yeye anaye simamisha na ni yeye anaye angusha, wala

hakuna msaada kinyume na idhni yake.
6 .Upatikanaji wa vyote ni katika uumbaji wake,tajiri wa vyote
Ulimwenguni.
7.Mtukufu anaye enea kabisa: alikua, iko na atakua, Mwenyi uzima .
8 .Mutu Hana uzima, yeye ni hunusu ao kipande.
9 . Hunusu ni kwake Aliye na maisha ya milele,iko na mwanzo Lakini Hana mwisho.
10 .Na kipande ni kwake asiye kua na maisha ya milele, ambae hupatikana na mwanzo pia na mwisho. 11 . Maisha ya mutu ni mfano wa safari ; anatoka apa na anaenda pale.
12. Heri Mutu anaye tumia urakibu , maana ni Mwenyi maisha ya milele
13. Alikua Duniani anaenda mbinguni hali ya kua hai.
14. Urakibu ndio Njia ya kwenda mbinguni.

82

15. Na uatidu ndio Njia ya kwenda hadezeni. 16.Tembea urakibuni ili upate kufika mbinguni. 17. Kambi bora lenyi starehe ya milele. 18.Amani ya Mungu kwa wasilimu wote. 


10.KISTARI CHA USAWA

83

1.Ametakasika mwenyenzi Mungu,m'bora wa kauli na matendo, wa pekee anaye kamilika.

2. Ukamilifu haupatikani kwa kiumbe sababu hakina Uwezo
wala ujuzi .
3. Hali yake hii ndio Sura ya Enzi, mfano wa kistari cha usawa, kisicho kua na mwanzo wala mwisho,bila fundo wala lukumba.
4 . Tafauti sana na sura ya umbiko ambae ni upungufu, mfano wa kistari kilicho na mwanzo pia na mwisho,chenyi fundo na lukumba.
5 . Milki kamilifu ndio hufanya kitu kitangulie bila kuanza,na kutokeza toka sifuru ,kwani ni mamlaka ya vyote.
6 .Kuweza yote ndio kuenea na kutoweza yote ndio kutoenea
7. Na kuenea ndio kukamilika na kutoenea ndio

Kua mpungufu.
8 .Na kukamilika ndio kua na uzima na kua mpungufu ndio kukosa
uzima.
9. Na uzima ndio Umungu,ufalme wa ulimwengu, haupatikane ispokua kwa Muumba peke yake. 10. Kistari mfano wa fahamu ( wazo ).Na nukta mfano wa kisa.
11. Mufululizo wa visa katika usawa ni namna ya fahamu.
12. Asifiwe mwenyenzi Mungu Aliye uzima, fahamu ya vyote pasipo Kipimo

11. SALA YA JAMAA

1. Kauli tukufu ambae ni ujumbe wa Mungu ndio njia ya kupitia kwa kwenda kwa Mungu.

2. Njia hii ni kwa watu wote,wanaume na wanawake
3. Wametenda zambi wanaume wanao wa ziwilia wanawake kusali muskitini.
4. Hakika sala ya jamaa ni muimu kwa watu wote wanaume kama vile Wanawake , maana ni yenyi thawabu nyingi.
5. Mungu ni mwema sana,amezidisha malipo kwa kila muaminifu na Kuwaletea wajumbe wake kila umati,ili wawasafishie njia.
6. Tumieni maamrisho na acheni yote mliyo katazwa ili mupate kufuzu starehe ya mbingu.
7. Fanyeni ibada wote kwa jumla,wala msitindiane riziki,
8. Na usikose kuchuma udhu mbele ya kusali :kwa maji ao kwa

udongo,ao kwa manuizi.
9. Hakika amefaulu kila yule anaye tenda mema.


12. MAPASA


1. Usilimu ni katika matumizi ya ibada ya Mungu kimwili.
2. Na uaminifu ni katika matumizi ya ibada ya Mungu kiroho.
3. Mutu hawezi kusilimu kikweli bila kuamini.
4. Na mutu hawezi kuamini kikweli bila kusilimu.
5. Atakaye jidai Usilimu pasipo kuamini ni mnafiki.
6. Na atakaye jidai uaminifu pasipo kusilimu ni mnafiki.
7. Ni kawaida kwa mtumishi wa Mungu kusilimu na kuamini.
8. Maana Usilimu na Uaminifu ni mfano wa mapasa
9. Aliye kuja mbele ni Usilimu ,na aliye kuja nyuma ni Uaminifu.


13.   BILA YEYE NI SIFURU


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.

2. Bila yeye kuumba kama mimi na wewe pia na yule hatupatikane ulimwenguni.

3. Shukrani zote zina mustahili yeye peke yake, mkamilifu aliye juu.

4.Ni muimu kwetu kumuabudu Mungu peke yake.

5. Tusimfananishe na yeyote wala chochote, wala tusimuombe mwengine badala yake.

6.Mola wa wanahewa na wazilahewa, aliye mwenyeji wa ulimwengu.

7.,Ndiye muweza anaye miliki ufalme wote, Hakuna mwengine kama yeye, wa popote na milele.


14.  ATENDAYE BILA KAZI


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.

2. Anaye takasa nafsi bila kazi ya kusugua.

3. Na kuponesha magonjwa bila kazi ya kutunza.

4. Kutumika kazi ni alama ya uzaifu, dalili ya kukosa uwezo wa vyote.

5. Aliye na uwezo wa vyote hatumikake kazi kwa yeye kutenda jambo.

6. Idhni yake ni yenyi uwezo wa vyote, hutokeza kwa rafla kile anacho idhinia.

7. Anaweza kutangulia bila kuanza,na anaweza kutenda bila kutumika (kazi).



15.  BILA MWANZO WALA MWISHO


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, mzima, aliye pasipo yeyote muda wote.

2. Hakutokezwa na fulani, wala fasi fulani, wala muda fulani.

3.Amepatikana kadiri ya kuenea, namna ya kukamilika.

4. Ndio sababu  vyote vilitoka kwake kwani yeye ndio mwanzo wa vyote.

5. Dhati yake iliye uwezo wa vyote humfanya apatikane kadiri ya uzima.

6. Angeli kosa uwezo kama angeli anzishwa sawa na kiumbe.

7. Lakini kuona kama yeye ni mwenyi Enzi, ndio maana hukamilika bila upungufu wa kuanza na kukoma.


16.  MTAYARISHAJI


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.

2. Aliye tayarishia mwanadamu vifaa vya maisha, kimwili na kiroho.

3. Vifaa vya maisha ya mutu kimwili,humpatia starehe duniani.

4. Na vifaa vya maisha ya mutu kiroho, humpatia starehe mbinguni.

5. Starehe ya duniani ni ya muda, sababu mwili ni umbo dhalili.

6. Na starehe ya mbinguni ni ya milele sababu roho ni umbo tukufu.

7. Ni lazima kumshukuru Mungu ajili ya wema wake,hakuna anaye kupenda zaidi ya Mola wako.


17.   VYOTE NI BURE


1. Utakapo hubiriwa ukweli wa Mungu, ni amri kwako kuyashika na kuyatumikisha.

2. Kukataa neno la Mungu ni kujitindia riziki,hasara kubwa ya kupoteza umbo lako.

3. Maisha ya dunia isikudanganye,ewe mwanadamu.

4. Hakika vya dunia vyote ni vya bure, maana utaviacha baada ya muda mchache.

5. Mutu ni kama mpita njia duniani, kambi lake maalumu hupatikana mbinguni.

6. Atakaye kataa ukweli huu ndio mjinga anaye tumikia dunia peke yake.

7. Yeye ni mfano wa kipofu asiye zingatia mbele ya safari,atajikwaa na kutumbukia shimoni.


18.   OGOPA MUNGU


1. Ewe mwanadamu ! ogopeni Mola wako ukweli wa kuogopa.

2. Usimzihakie wala usimzingizie kamwe mufalme wa wafalme.

3. Yeye ndio m'shindi afanyaye apendavyo popote na milele.

4. Mtukufu anaye jaa milki kamilifu, anaye zidia vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini.

5. Usijifananishe naye wala usishindanie naye, vyote ulivyo navyo ulipewa naye.

6. Hata nafsi yako imepatikana kwa ruhusa yake, mumilki wa jumla ya matendo.

7. Kadiri alivyo na uwezo wa kutokeza toka sifuru kila kitu,ndivyo alivyo na uwezo wa kupoteza (kufuta)kwa rafla kila kitu ulimwenguni.


19.  JICHO


1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, mtukufu asiye zingatiwa na kipofu.

2. Mola wa ajabu anaye zingatiwa na wenyi kua na macho ya kuona peke yake.

3. Kuona ni kufahamu,na kutokuona ni kuto fahamu.

4. Na kuonekana ni kufahamika,na kutoonekana ni kuto fahamika.

5. Kupenda kumuona Mungu ni kupenda kumfahamu Mungu.

6. Kama mutu anakulazimisha umuoneshe Mungu ni kwamba amekulazimisha umfahamishe hali ya Mungu.

7. Hapo inakubidi kumsomea kitabu cha ukweli, ambae hufasiria waziwazi uzima wa Mungu ,ili apate kuzingatia.

8. Ukweli wa Mungu hauwahusu ispokua wenyi akili, maana ndio wenyi macho ya kuona, 

9. Kukosa akili ndio kukosa macho, yaani ndio kua kipofu.

10. Atakaye sema kama yeye haaminiake kwamba kipo ispokua kile anacho kiona na kiungo cha mwili wake kiitwacho jicho ,ni mnafiki anaye kanusha uzima wa Mungu kwa kusudi na kiburi.

11. Kwani vyote anavyo amini kwamba vipo,hakuvizingatia na hicho kiungo cha mwili wake kiitwacho jicho.

12. Ameamini kwamba hewa,sauti,onjo,arufu...vipo na ilihali hakuvizingatia na kile kiungo cha mwili wake anacho kiita jicho.

13. Jicho la kiumbe linalo fanya kizingatie bayana ni fikara timamu inayo itwa"Akili".

14. Aliye na akili huzingatia ijapokua kisicho kua na mwili,hata kiwe mbali njee ya dunia.

15. Hakika kumkanusha Mungu aliye kuumba ni kukosa akili.

16. Heri mutu anaye amini ukweli huu unao leta yakini moyoni.


20.  HERI NA SHARI


1. Kumbuka mola wako popote ulipo, wala usimusahau, hakika yeye ndio mpanaji wa maisha.

2. Nafsi yako na riziki yako na umri wako umepewa na Mungu.

3. Hakungeli patikana yeyote wala  chochote pasipo Mwenyenzi  kutangulia na milki kamilifu.

4. Anaruzuku kila kiumbe na anakinga kila kiumbe na shari ya kila namna.

5.Katika maisha ya mwanaadamu kunapatikana heri na shari.

6. Heri imepatikana ndani ya maamrisho,na shari imepatikana ndani ya makatazo.

7. Anaye tumia maamrisho hupatikana ndani ya ulinzi wa Mungu.

8. Na anaye tumia makatazo , hupatikana njee ya ulinzi wa Mungu.

9. Kua katika ulinzi ndio kua katika heri,na kua njee ya ulinzi ndio kua katika Shari.


21.   UPENDO


1. Jambo muimu katika maisha ya musilimu  ni upendo.

2. Mutu asiye kua na upendo ku watu wenzake sio musilimu wa kweli.

3. Ni amri kupendana wote,bila ubaguzi wa rangi, wala ubaguzi wa kabila...

.4. Hauwezi kufuraikia magumu ya mutu unaye mpenda,

5. Hauwezi kumchukia,wala kumzingizia,  wala kumchekelea, wala kumuuwa, wala kumuiba mutu unaye mpenda...

6. Upendo unamziwilia mutu kutenda mazambi mengi,ngao ya kujikinga na zambi.

7. Heri mutu anaye wapenda watu wote,walio kuume kwake na walio kushoto kwake.


22.    MATUMIZI YA SHAADA


 1. Mwenyenzi Mungu ndio kimbilio la wasilimu wote.

2. Mfariji anaye leta amani kwa wote wanao tumikisha shaada zao.

3. Kuwa yakini na uzima wa Mungu sio kwa midomo tu bali kwa matendo.

4. Anaye amini kikweli humtumainia yeye peke yake,na hujiweka chini ya mamlaka yake.

5. Na humpelekea maitaji yake yote, yakini kwamba atasikia na atajibu.

6. Wala hamzihakie kutaka amufanyie kile ambae amekwisha mfunza namna ya kujifanyia mwenyewe.

7. Na humsujudia mola wake kila siku: asubui na mangaribi,pia na usiku.

23.     MATUNZO

1. Sema : kukataa kutunzwa na hali upo mgonjwa,ni kujizulumu mwenyewe.

2. Na kumuendea mganga ili akutunze sio zambi,lau kama hauta mshirikisha mola wako na chochote.

3. Kuna aina mbili ya matunzo: matunzo  ya kimwili na matunzo ya kiroho.

4. Na pia kuna aina mbili ya waganga :waganga wa mwili na waganga wa roho.

5. Wajumbe wa Mungu na watumishi wa Mungu ndio waganga wa roho;Na matunzo yao ni maubiri na maombi.

6. Na wanasayansi wanao tumikisha miti ama vidonge,ao zinguo ...ndio waganga wa mwili.

7. Ni halali kwenu kutunzwa matunzo yote, ya mwili na ya roho.


24.   KUKOSA  DINI


1 .  Hakika wa uminu ni wenyi kunipendeza sana,asema roho wa Mungu.

2. Nikamuuliza wanakupendeza kwa nini ? ni maubiri yao ao matendo yao ?

3. Roho akanijibu, akisema:sisemee wale wa zamani bali nimesemea hawa wa sasa.

4. Wale wa zamani wamejiita waaminifu ,hali ya kua mbali na usilimu.

5. Nimesemea uaminifu ambae umeanzisha wewe:kwani unafundisha imani ndani ya dini, lakini wao hufundisha njee ya dini.

6. Hakika nimekuambia uaminifu bila usilimu ni ukafiri na unafiki mtupu.

7. Kuamini bila kusilimu ni kijidai imani bila shaada, yaani kuamini bila kua yakini na uzima Mungu.

8. Kukataa usilimu ni kukataa dini ya Mungu.

9. Na kukosa dini  ni kua katika ukafiri wa namba ya juu.


25.    KISA CHA USILIMU


1. Jina ya dini sio uaminifu lakini usilimu.

2. Uaminifu hauzingatiwe bayana na watu duniani,bali huzingatiwa bayana mbinguni na Malaika na roho.

3. Kuto kuzingatia imani bayana kunamfanya mutu ashindwe kutambua ni nani aliye na imani ya kweli.

4.  Usilimu ndio matendo mema ambae hudhihirika, lakini imani iliye moyoni haidhihirike bayana.

5. Na kuona kama usilimu ndio unaye zingatiwa bayana na watu, ndio kisa cha usilimu kufanyika dini ya Mungu duniani.

6. Utazani kama mutu fulani ni mwenyi imani , kumbi hana imani.na yule usiye muamini , ajili ya kujitenga na unafiki,kumbi ndio mwenyi imani.

7. Matumizi ya imani ndio matendo mema kadiri ya usilimu,haiwezekane kutumikisha imani bila kudhihirisha matendo mema.


26. HAKUZAA WALA HAKUZALIWA


1. Mungu Mwenyenzi ni yule aliye umba anga na ukiwa pamoja na vilivyomo.

2. Asiye kua na uwezo wa kuumba hastahili kuitwa Mungu.

3. Aliye tangulia kinyume na kuanza ndio mwenyi uwezo wa kutokeza toka sifuru.

4. Haowake wala haolewake,kwani yeye sio mwanaume wala yeye sio mwanamuke.

5. Kuona kama haungake ndoa na yeyote ndio maana hazalake.

6. Na kuona kama haungake ndoa wala hazalake ndio maana hana bibi wala bwana wala mtoto.

7. Mwenyenzi Mungu mtukufu amejitenga mbali kabisa na uzaifu huo wa kuzala na kuzaliwa.


27. WA PEKEE KATIKA UPEKEE


1.Ametakasika Mwenyenzi Mungu, M'bora wa kuumba.

2. Atanguliaye kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho.

3. Viumbe vyote vilimukuta tayari amekwisha enea katika ulimwengu.

4. Mwenyi uzima, ambae peke yake hukamilika katika tendo kua,wa milele na milele.

5. Yeye ni muweza wa vyote anaye jua yote.

6. Wa pekee katika upekee bila mfano wake wala jerani yake.

7. Sifa yake imezidia vyote, mtukufu anaye heshimiwa na anaye sujudiwa.


28. KAULI MUIMU


1. Sema :samahani Mola wangu kwa yote ninayo chupa !

2. Hakika mimi siwezi kuokoka pasipo huruma wako.

3. Unifungue katika vifungo vya Shetani.

4. Na unipatie nguvu ya kushinda adui !

5. Na unihelekeze kwako maisha yangu yote.

6. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyenzi peke yake.

7. Na  hakika Kalonda ni shahidi wa Mungu Mwenyenzi.


29. ULINZI NA UTAJIRI


1. Enyi walio amini ! kumbukeni Mola wenu kila mara popote mtakapo kua.

2. Wala musi muasi mola wenu ajili ya ugumu wa maisha ya dunia.

3. Yeye ndio mpanaji, anaye ruzuku kila nafsi angani na ukiwani.

4. Mutu anaye mtegemea Mungu peke yake, ndio anaye pokea zawadi ya kiroho.

5. Amepata ulinzi na utajiri wa milele ,kwani yeye sio tena yatima.

6. Nafsi yake haita vamiwa na yeyote wala haita kua katika dhiki.

7. Hakika amefaulu kabisa mutu anaye muabudu Mungu Mwenyenzi peke yake pasipo kumchanganya na chochote.


30. MAALA TAKATIFU

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mwalimu wa walimwengu.

2. Anaye chagua viongozi vya umati mbalimbali katika mitume yake.

3. Na ndiye anaye chagua maala takatifu ya kila umati.

4. Na kuwaalika walio silimu kuitembelea,na kufanya ibada ya hija kwa walio na ginsi.

5. Maala takatifu yote ni kwa watu wote, lakini iliye muimu kwenu ni ya umati wenu.

 6. Jihadharini na hila ya Shetani asikuingizeni katika ushirikina,kama alivyo wa poteza watu wa kabla yenu.

7. Na wakaanza kuabudu kiumbe maala hiyo bila kufahamu.

8. Hakuna Mola mwengine anaye stahili kuabudiwa ila Mwenyenzi peke yake.






Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kitabu cha ukweli - Mlango wa saba : "KAULI TUKUFU"

Kitabu cha ukweli - Mlango Wa pili "ENZI TUKUFU"

MWANDISHI WA KITABU: