Kitabu cha ukweli - Mlango wa tatu "NURU TAKATIFU"

MULANGO WA TATU : NURU TAKATIFU


1.UITO

1.huu ni ujumbe kutoka kwa Mungumwenyenzi:
2.Mimi Kalonda , nilisikia sauti toka juu kuniita nilipo itika akasema: ni mimi Mungu wako! nime kubariki kama nilivyo mubariki ibrahim.
3.Na nimekutuma uwaubirie wale utakao wa kuta wakibishana kuhusu uzima wangu.
4. Ni kamuuliza, nikisema:niwahubirie maneno gani?
5.Mungu akanijibu akisema:yale utakayo fahamu kuhusu uzima wangu.
6.Kwelikweli ninakwambia hauta fahamu lolote kunihusu mimi ispokwa ukweli peke yake.
7.Akaniambia, akisema, unasikia ninayo kuagiza?nikajibu, nikisema ndio nimesikia.
8.Mungu akaniambia, akisema:usikose kuwafikishia kweli yangu.
9.Nilipo maliza kuzungumuza na Mungu maneno hayo, nikaona nuru kubwa mbele yangu.
10.Ni katazama, katika nuru ile, nikaona mwanamuke mumoja ameketi chini udongoni.
11.Alikua mtu mweusi mnene mwenye kimo cha kadiri, akivaa kanzu ya kitenge.
12.Alikua ndani ya jengo la msingi wa nyumba, iliyo jengwa kwa matofari ya kuchomwa.

13.Tulikua na tazamana mimi na yule mwanamuke.

14.Punde kidogo nikaona maji tokea juu mbinguni,ikamushukia (mwanamuke yule) kichwani pake,ikimimilika kama vile maji itokayo katika mulonge.

15.Wakati maji ilimushukia toka juu,nikamuona kama aliye na mimba.

16. Na maji ile ilitiririka mwilini mwake,akalobana yeye wote,mpaka udongoni.

17. Na ilipo gusa udongo,maji ile ikasambaa (udongoni)bila kulobanisha udongo wala kuzama.

18. Wakati huo,nilisikia mzozo wa watu wengi wakipiga kelele kwa kishangwe,wakisema :amebarikiwa... amebarikiwa !!!...

19. Nikasikia sauti toka juu kuniambia,ikisema:tazama,ewe Kalonda, ginsi baraka yako itakavyo patikana.

2.UVULI

1.Ametakaslka Mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba aliye umba nuru kadiri ya uvuli wake.
2.Kinvuli cha mwenyenzi huzingatiwa kadiri ya matazamio yenu, na ndio maana nuru yake hutajwa namna tafauti. 3.Kama matazamio yako humzingatia Mungu kadiri ya enzi tukufu, nuru yake huzingatiwa kadiri ya hewa (anga) 4.Na kama utazamaji wako humzingatia Mungu kadiri ya ujuzi, uvuli wake ama nuru yake nifikara.
5.Na kama humemzingatia kadiri ya uzima, nuru yake ao uvuli wake ni maisha (uhai)
6.Mbingu ni kambi takatifu, sehumu yakwanza ya bahazi la juu angani;
7.Ndio sehemu kubwa ya tabaka la anga, tukufu inayo jumuisha falme mbili takatifu;
8.Kuna mahala anapo patikana malaika, na pia sehemu anapo keti roho humo mbinguni.
9.Malaika na roho ni pumzi hai yenye fikara timilifu iliyo umbwa kwa uvuli wa enzi tukufu.
10.Kuona kama ilifanyika kwa nuru ya taa ya ulimwengu, umbo hizi ndio nuru ya mwenyenzi inayo angazia dunia. 11.Hiyo fikara timilifu kadiri ya neno lake takatifu iliye ndani mwao ndio mwangaza unao angazia.
12.Ufunuo wake ndio mwangaza mboleo ya maisha ya watu.
13.Wamefaulu kabisa walio silimu kwa shaada yao, ambae umpelekea mola wao shukrani.
14.Ni mkubwa sana mwenyenzi Mungu m'bora wa kukadiria anaye jaa mamlaka.
15.Utukufu wa dhati yake umezienea mbingu na ardhi, na vilivyomo hutamania uvuli wake.
16.Mufalme wa wafalme aliye na ushindi, ambae kauli yake hufanya yote pasipo shuruli, m'bora wa kuumba.

44

3.M'BORA WA KUUMBA

1.Ametakasika mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba ,mtukufu ambae hatumiake kifaa chochote cha njee ya alivyo viumba kwa kuumba.
2.Lau kama angeli tumia kifaa ambae hajue kukitokeza hasingeli itwa muumbaji bali angeli itwa muundaji.
3. Mumilki anaye tokeza ambacho hakikua kwa kutumia idhni yake peke yake.
4.Kustawi kwake katika dhati yake mwenyewe humfanya upekee pasipo kuchangikana na chochote wala ku fanana na chochote wala kutumia chochote cha umbali mbali naye.
5.Mufalme anaye enea katika yote kwa mamlaka yake mwenyewe, mtukufu aliye na miliki kamilifu.
6.Wengi miongoni mwa watu hawawezi kuamini ambae njia tano ya fikara kupitia mwilini haidhatiti.
7.Ndio maana wamepatikana mbali sana na nuru: sehemu moja ya watu humkanusha Mungu.
8.Na sehemu ingine ya watu humpachika mujumbe wa Mungu daraja isio yake ya umungu.
9. Awa wote ndio wasio amini kweli kikweli, nivema kushuudia kweli vilivyo kihakika.
10.Kumpachika mtume fulani umungu ni sawa na kuabudu sanamu ,zambi kubwa zaidi ya yote.
11.Mshindi katika yote hujitenga mbali na upungufu wote, hakuna kilicho mfanana.
12.Jihadharini sana maishani mwenu na ibada ya masanamu, hakika ushirikina ndio upotevu wa bayana.
13.Umungu ni katika upekee, tafauti na umbo zote, wala uzaifu wa kujumuika haumkurubie kamwe mtukufu aliye enzini. 14.Hakika utakatifu ni wake mwenyenzi, mtukufu ambae nuru humfumuka kwa wingi, vikijipakaa viumbe utukufu wa dhati yake.
15.Mwenye kuenea katika yote kuliko wote, mufalme wa wafalme wote.
16.Hakuna mwengine kama yeye, mwenyi mamlaka ya ajabu, anaye weza yasio wezekana kwa viumbe, m'bora wa kuumba.

4.AKUNA LAWAMA

1.Ametakasika mwenyenzi Mungu m'bora wa kuumba anaye fanya yote kwa usawa bila hitaji ya msaidizi.
2.Mkamilifu ajaaye utukufu, anaye podoa na anaye tuliza nafsi ya walio silimu.
3.Mjuzi anaye kadiria jumla ya viumbe pasipo kudondoka, kiongozi mwenye kukamilika.
4.lakini watu wa dunia humlaumu Mungu muumba kwa kuwaumbia shetani ambae huwaangamiza.
5.Na ilihali maisha yao(watu)pia nimfano wa maisha ya shetani mbele ya viumbe vingine.
6.hayo hutokana na upungufu asilia ambae huzikumba umbo zao wote kwa jumla.
7.Na wanapo angamiza viumbe ajili ya starehe ya nafsi zao, hufurai bila kujali kilio chao.
8.Kadiri watu wanavyo laumu kuumbwa kwa shetani ,ndivyo pia viumbe vingine vinavyo laumu kuumbwa kwa mutu. 9.Minyama ,ndege,samaki,vidudu...wanalia kwa uchungu wanapo uwawa na watu .kama vile watu wanavyolia kwa uchungu wanapo vamiwa na shetani.
10.Kama kweli Mungu hakustaili kuumba shetani sababu huangamizana ,ni kwamba hakustaili pia kuumba mutu sababu

45

huangamizana pia.
11.Viumbe vyote huangamizana ajili ya upungufu asilia unao tafautisha maisha yao.
12.Ambae ni mbaya kwa uyu ni nzuri kwa yule,katika maisha ya jumla ya viumbe.
13.Hakuna kisicho pendeza wala kisicho chukiza miongoni mwa viumbe.
14.Eti ni kweli kabisa Mungu alifanya makosa kuumba viumbe?
15. Hapana kumlaumu Mungu kwa lolote maana mola wenu ni mjuzi wa vyote anaye tenda katika usawa kila jambo.
16.Wala usitafute kua mkamilifu kama Mungu ambae hagusiwake na upungufu wowote ,na ilihali wewe ni tunda la upungufu.

 17.Ni amri kwa kila mutu kumsifu sana Mungu na kumshukuru kwa wingi ,hapana kumlaumu Mungu ku vyovyote.
18. Mutu atakaye amini Mungu kwa moyo wake wote na kumuabudu kila siku,na akawa na moyo safi ,bila shaka nafsi yake itageuzwa roho atakapo ihama dunia.
19.Tetea namna ya kupata utimilifu wa nafsi yako ,sio ukamilifu,lakini neema ya kupata maisha ya milele.

5.MTENDAJI

1.Ametakasika yeye aliye umba mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo.
2.Mwenyi kustawi katika utukufu ,juu ya palipo juu ,hakuna mfano wake ulimwenguni.
3. Amejaa katika kua,nyuma na mbele ,bila mabadiriko yoyote.
4. Hakuna macho iwezayo kumtazama ana kwa ana ajili ya utukufu wake wa ajabu.
5. Macho itakayo jaribu kumtazama,hupofoka bila mafanikio yoyote .
6. Nuru juu ya nuru mtukufu anaye angaza kadiri ya taa ya ulimwengu .
7. Mkamilifu asiye gusika na upungufu wowote ,m'bora wa kuenea .
8. Baba wa siri aliye kwa siri kadiri ya muujiza wa maajabu, ambae hali yake hustaajabisha walimwengu.
9.Amejaa uwezo wa vyote wala hakuna asilo liweza,mwenyi mamlaka ya utendaji.
10. Kila tendo liko na tafsiri yake inayo maanisha ujuzi wake.
11. Hatendi lolote ispokua katika kujua,muweza na mjuzi,anaye wezesha na anaye fahamisha kila umbo la kihewa .
12.Watu wangeli fahamu mradi wa kuumbwa kwa kila umbo, hakika wange muogopa Mungu na kumsifu na kumshukuru. 

13.Ameumba kadiri ya kufumba, wala hakague ispokua aliye funuliwa naye.
14.Mkuu aliye na ushindi juu ya kila kitu, shina la vilivyomo ulimwenguni.
15.Majira ya ulimwengu, imetokana naye, ni yeye anaye badiri kipindi katika wakati.
16.Hakuna Mungu mwengine kama yeye, bwana wa mabwana, anaye hifadhi kwa milele.
17.Mola wa anga na ukiwa, mumilki, ambae nguvu yote hutokea kwake.
18.Wa pekee katika utukufu usio kurubiwa, msifiwa aliye kamilika, anaye patikana juu ya daraja zote,mwenyi uwezo na ushindi.
19.Wengine wote walifanyika naye, wala hakuna mwengine kama yeye, mzima, anaye pimiana muda bila yeye kupimiwa na yeyote.
20.Mwenyi kuenea katika tendo kua, kuzidia wakati, m'bora wa kutangulia.


6. SIMAMA IMARA

1.Utukufu ni wake mwenyenzi Mungu, kiongozi mwenyi hekima kamilifu.
2.Amejifunua kwao wanaadamu kwa namna tafauti, wamaajabu anaye fanya raisi jambo ngumu, na kuifanya ngumu jambo raisi.
3.Hawamzingatie ila kidogo tu, kwani nuru yake aiwafikie kama kawaida ajili ya giza ambae ni mwili ujengao nafsi zao.

 4.Anga ndio sehemu ya ulimwegu kadiri ya mwangaza wake na wanaanga wamekuwa na ginsi ya kujikusuru kadiri ya kutenda. 

5.Pumzi zao zimekua nguvu na zimekua fahamu, ndio maana ni wenyi maisha.
6.Hii ni miongoni mwa faida ya nuru yake, ambae huthamanisha umbiko.
7.Watu wa dunia wamekataa neno la Mungu lenyi nuru na baraka, wamekubali vishawishi vya shetani ambae hufunika.
8.Ni kwa sababu hawamzingatie shetani bayana kadiri alivyo umbwa, anayo desturi ya kujificha.
9.Shetani ni umbo mbaya ajabu, yenyi kutisha, lau kama angelikua na onekana bayana, hakuna mutu ambae angeli penda imusogelee.
10.Umbo lake ni uchafu, na matendo yake ni machafu, na kambi lake ni chafu ajabu, maana yeye ni kapi.
11.Ubaya wa aina yote ni ndani mwake, mfano wa yalala, ambae hulinda uchafu wa aina yote.
12.Pahali ya pumzi yake kuleta ladha nafsini mwake iliyo mjaa, yao humletea maumivu na wasiwasi.
13.Matendo yake yote ni kinyume na usawa, wala hatendi ispokua ubaya.
14.Yeyote anaye sharikiana naye ndio anaye fanana naye, katika mila na matendo, analeta wasiwasi katika jamii la watu. 

15.Amewafunza urozi wa kila namna na kuwapambia hata wakiupanga majina mazuri ili watu wautamanie.
16.Na pia huuingiza katika dini;kuwafananishia ramli na utabiri wa maono,na kuwafananishia zinguo la kizimu na uponyaji wa maombi.
17.Hayo ndio mafunzo ya shetani, mambo ya giza ambae mwisho wake ni hasara.
18.Ole kwao watembeaye gizani ,hakika ni mbaya sana makao yao siku ya mwisho.
19.Na wana pupia kusukumana gizani ajili ya chuki, wala hawataki uongofu.

46

20.Na wanapo karibiza watu mezani, hutia urozi ndani ya chakula ili wawaambukize wengine.
21.Hakika kupatiana uchawi ni zambi kubwa sana zaidi ya kuuwa mutu.
22.Ni kujiwekea akiba ya zambi, maana zambi yote atakao ichuma na uchawi ulio mupa, nawe pia utapewa sehemu.
23.Na yule uliye mupatia urozi kama unapatiana pia, utapewa pia na zambi ya yule mpaka mwisho.
24.Usitafute kurudisha kisasi kwa kupezana uchawi kama walivyo kupatia wewe, na ili hali wale unao wapatia sio yule alio kuambukiza.
25.Na kama wana kuambukiza uchawi(urozi) bila kutambua wala kutaka, usikate tamaa, lakini zidisha ibada na usimame imara mpaka mwisho wa umri wako.
26.Hakika mola wako atakutakasa na kukuneemesha, ukipewa bustani kua makao yako ya milele.
27.Atakaye simama imara katika urakibu pasipo kurogana na uchawi walio muambukiza ndio shujaa anaye pewa daraja ya kiroho, ambae ameshinda majaribu.
28.Na yule atakae shindwa kusimama imara katika njia ya Mungu baada ya kuambukizwa uchawi, kiisha akaanza kurogana, ndio maskini kiroho anaye shindwa na jaribu.
29.Simameni imara enyi walio silimu ili mupate kupokea zawadi ya kiroho.
30.Aliye pokea roho takatifu hawezi kunajisika(kiroho) ijapokua wakusudie kumunajisi.
31.Giza aifukuzake nuru lakini nuru ndio yenye nguvu ya kusukuma giza mbali.
32.Imani ya kweli humfanya mutu ateremkiwe na watakatifu wa mbinguni.


7. USHAIDI

1.Shuudieni kweli hii, enyi watu hakika mola wenu yupo pamoja na washuudiao.
2.Mungu amenifunulia kweli hii na kuishuudia mwenyewe ,hakuna shaka ndani Yake.
3. Mimi ni shahidi wa Mungu mwenyenzi ,nimetumwa ku watu wote bila ubaguzi.
4. Nimeleta ushahidi wa uzima wa Mungu ili kila yule atakaye upokea apate uzima wa milele.
5. Hapana kushakia habari hii ya ukweli,wala usizanie kama ni akilia ya kibinaadamu.
6. Wala usizani kama kutomuona na macho ya mwili wako ndio kukosekana kwake,hayo humaanisha ukubwa wa daraja yake pia na utafauti uliyeko baina ya wewe na yeye.
7. Mungu ni uzima kadiri ya Enzi tukufu,lakini wewe ni changachanga ya pumzi na mwili.
8. Mwili ni ukiwa kadiri ya utupu wa ujinga,yaani uzaifu na upungufu,ganda isiyo Linda fahamu yoyote.
9. Na pumzi ni mjengo kihewa ambae kafanyika kwa uvuli wa enzi,yaani fikara kadiri ya uvuli wa ujuzi.
10. Fikara yenyi thamani ya uvuli ichangikane tena na mwili ulio ujinga mtupu ,itawezaje kuzingatia bayana umungu ambae ni muujiza wa maajabu?
11. Ndio maana Mungu mwenyi ujuzi alichugua hatua ya kuwatumieni ujumbe na watu wenzenu ili mupate kuzingatia uzima wake.
12. Wajumbe wake ndio mashahidi wake ambae humsikia na masikio yao nahuona utukufu wake na macho yao.
13. Neno ni ngumu kimwili ,lakini mwepesi kufahamika kiroho.
14. Mwili ni giza na roho ni nuru,aliye wa mwili hutembea gizani,na aliye wa roho hutembea nuruni.
15. Aliye wa roho ni mwepesi kuzingatia uzima sababu yeye ni katika mapambazuko.
16. Alie wa mwili hawezi kuzingatia uzima maana yeye ni gizani,macho yake imefumbwa na ujinga.
17. Na ijapokua musilimu azaufike katika maisha ya dunia,yeye ndio chombo halisi,umbo tukufu la mbinguni.
18. Na ijapokua kafiri atukuzike katika maisha ya dunia ,sio kwamba anakua chochote,yeye ni kapi tu ,umbo dhalili ya hadezeni.
19. Hakika Mungu ni mwenyi kuwako,mzima,anajua yote na anaweza yote,halingane na yeyote.
20. Makafiri wanafikiria ya kwamba Mungu amefanana na kiumbe ,ndio maana wamelazimisha yafanyike kwake kama inavyo fanyika kwenyi viumbe.
21. Hakika kupatikana kwake kadiri ya kutangulia pia na kutenda kwake kadiri ya kutokeza toka sifuru ni muujiza wa maajabu,tafauti sana na kupatikana pia na kutenda kwao viumbe.
22. Mungu ni mwenyi mamlaka ya ajabu ,anga na ukiwa vilifanyika naye bila kutumika kazi.
23. Akaamuru kitu fulani kifanyike mara moja kinakua.
24. Uzima wake hauna asili,Bali yeye alitangulia kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho,wala hakudai msaada wowote kwa yeye kuwako.
25. Utukufu wake huu umemtafautisha na vitu vyote kwa jumla,wa pekee bila mfano wake.
26. Kama unafikiria kuhusu hali yake ,tambua ya kama hakuna umbo yenyi kumfanana ku vyovyote.
27. Hayo ni kwa sababu yeye peke Yake ndio mwenyi ukamilifu ,na wengine wote ni wapungufu,hakuna ginsi ya wao kulingana.
28. Mchoraji haweze kulingana na chombo kilicho chorewa naye.
29. Ndio maana mutu hawezi kumuona muumba wake ana kwa ana;kitu kilicho fanyika kina patikana chini sana,mbali kabisa na daraja ya yule aliye kifanya,hawawezi kulingana kamwe.
30. Kama yule aliye fanyika angeli pewa ginsi ya kuzingatia hali ya yule aliye mufanya,Angeli staajabu sana.

31. Hali ya yule aliye mfanya ni tukufu ajabu kubwa sana na zaidi tafauti kabisa na yule aliye fanyika. 32. Hakika uwezo wa muumbaji ni mwingi mno hakuna hâta namna ya kuukagua.
33. Kweli kabisa mwenyenzi ni muujiza wa maajabu,hakuna ginsi ya kumkurubia ku vyovyote.

47

8. MASIYA

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,mneemeshaji ,anaye mtukuza amtakaye miongoni mwa watumishi wake.
2. Mimi kalonda nilikua na zoezi ya kuamuka usiku kwa kusali.
3. Siku moja roho akanijia katika ndoto ,akaniambia akisema:hakika ibada unayo fanya ni kubwa na malipo yake ni kubwa .
4. Na kama utapenda kuinuliwa,basi upande mlimani,ukafanye ibada kama hii usiku na mchana kadiri ya uwezo wako.
5. Nilipo amuka,nikajiandaa kwenda mlimani kwa ajili ya ibada ya Mungu muda wa siku tatu.
6. Nilipo kua katika kisimamo ndani ya sala,usiku huko mlimani,nilisikia sauti toka juu kuniita :kalonda!
7. Nilipo itika akasema:kati ya zawadi hiyi mbili chagua unayo penda upewe:
8. Kuna zawadi ya kimalaika na zawadi ya kiroho.
9. Zawadi ya malaika ni hii:jibrilu ,mikailu na asrafilu.
10. Na zawadi ya roho ni hii: Yesu masiya,Mussa na Eliya.
11. Nikajibu ,nikisema :Mungu mwenyewe anichagulie île iliye bora kwangu anipatie.
12. Ni bora kwako île utakayo ichagua mwenyewe,chagua unayo penda upewe.
13. Akaanza kunifasiria kuhusu zawadi ya kimalaika:akamtapa jibrilu hali yake na kazi yake na daraja yake.na akamtapa mikailu,kuonesha hali yake na ufalme wake na vivihivyo kwa malaika asrafilu.
14. Kiisha akanifasiria kuhusu zawadi ya kiroho kunionesha utukufu wa nabii Mussa ,daraja yake na kazi yake.
15. Na akanionesha utukufu wa Yesu masiya daraja yake na kazi yake humo mbinguni, hakika Yesu ni mfalme.
16. Na pia akanionesha utukufu wa nabii Eliya,daraja yake na kazi yake humo mbinguni.
17. Ndio akaniambia,akisema:baada ya kufahamu ubora wa zawadi yote mbili,chagua sasa zawadi unayo penda upewe.
18. Nikataka kuchagua ya kimalaika lakini nilipo tizama ukubwa wa daraja ya Yesu masiya nikachagua zawadi ya kiroho,yaani Yesu masiya,Mussa na Eliya.
19. Ma nabii hawa ni wenyi utukufu wa namba ya juu mbinguni.
20. Wakati huo nilikua nimeendelesha sala mpaka mwisho.
21. Kiisha nikalala,nikaona katika ndoto,mwangaza mkubwa umeniangazia,
22. Nilipo tazama juu,nikaona nuru mfano wa jua ya asubui.
23. Nikatazama ndani ya île nuru iliye kua mfano wa jua ya asubui,nikaona mutu humo ndani.
24. Nuru île ilikua na teremuka toka juu mbinguni.
25. Wakati huo nilijikuta juu ya muti mkubwa,katika majani ya chongo ya tawi lake .
26. Mutu yule aliye kua na poromoka ndani ya nuru ,alishangiliwa sana na watu walio kua chini ardhini.
27. Wakisema:yesu masiya ! mwana kondoo wa Mungu ! Mfalme wa mbinguni, mpenzi wa Mungu,njia ya mbinguni,roho ya Mungu...
28. Roho akaniambia,akisema:tazama Yesu masiya, mwana kondoo wa Mungu aliye haï,anaye kuja duniani ili kuondoa zambi za watu .
29. Na tazama ,alikua na shukia upande ambae uguta ulitenganisha upande nilio kua na upande alio kua na shukia hewani.
30. Alipo kurubia sehemu hiyo ,tawi nilio kua ili nepa upande huo alikua na shukia,kutambuka ukuta huo ulio tutenganisha.
31. Ndipo Yesu masiya alipo ni chugua,akinishika na mikono yake miwili na kunipitisha upande wake wa kulia pembeni yake. 

32. Tukawa tumeketi ,kadiri wanavyo keti juu ya kiti ,hewani.
33. Watu walio kua huko chini ardhini waka shangilia sana ,wakimtukuza sana Bwana Yesu.
34. Hakika karibu na Yesu masiya kuna hewa yenyi ladha nafsini.

9. MALINGANIO

1. Utakatifu ni wake mwenyenzi Mungu ,m'bora wa kuumba.aliye umba anga na ukiwa na ilihali hakukua kwa yeye kuigia mfano.
2. Vilivyomo angani navilivyomo ukiwani hushangilia dhati yake,mkuu aliye na ushindi.
3. Heri mutu anaye mnyenyekea muumba wake na kuitakasa dini yake ,maana atatukuzwa kuanzia duniani mpaka mbinguni.
4. Hakika makafiri ni wapumbafu ,kama wanasikia jina la Mungu hutukuzwa ,nyoyo zao hujaa huzuni na hasira.
5. Na kama wana sikia sifa ya shetani huburudika nyoyoni mwao.
6. Wao ndio wajinga ,wanao fanya nyoyo zao kua makao ya shetani.
7. Ni wenyi mioyo migumu ajabu,yenyi kujaa kiburi,wala hawata amini ijapokua waubiriwe ao hapana.
8. Hawafikiri ispokua ubaya:huchukia kila jambo nzuri,na hutamania kila jambo mbaya,umbo dhalili ya hadezeni.
9. Waaminifu ndio wanao furahi sana wanapo sikia sifa ya Mungu mwenyenzi.
10. Neno la Mungu ni chakula ya kiroho nafsini mwao,wameitumia kila siku ili kuzijenga roho zao.
11. Na huchukizika sana wanapo sikia maneno ya upuuzi wa shetani ,maana kwao ni mfano wa sumu ambae huaribu afya ya roho zao.
12. Waliumbwa kwa kauli tukufu na wameishi kwa matumizi ya kauli tukufu ,umbo tukufu ya mbinguni.

13. Wamechukia mabaya yote ,na wametamania mazuri yote;wao ni mfano wa mboleo ya uzuri,vipenzi vya Mungu. 

14. Anaye zingatia uzima wa Mungu na kuushuudia ni mwenyi akili.
15. Na yule asiye zingatia uzima wa Mungu ndio pumbafu.
16. Utimilifu hupatikana mbinguni na uaribifu hupatikana hadezeni.

17.Ndio maana wanao silimu na kutenda mema ,hujumuika mbinguni ,na wanao kufuru na kutenda mabaya,hujumuika hadezeni,baada ya kuihama dunia.

18. Mola wenu ametakasika zaidi ya kila kitu,hakuna wa zaidi yake wala wa sawa yake ambae Angeli msaidia.
19. Shuudieni uzima wa mwenyenzi katika yakini,ndiye mtawala wa ulimwengu.

20. Amekua yote katika yote,mwanzo wa vyote,chemchem ya upatikanaji na maisha ulimwenguni.

10. MAFUNDISHO

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, mtangulizi anaye jumuisha kila apendacho ulimwenguni.
2. Ni yeye anaye angazia mbingu na ardhi ,chemchem ya mwangaza kadiri ya taa ,ujuzi wa kila kitu.
3. Nuru ya Mungu sio mfano wa mwangaza kimwili,lakini fahamu ambae huondoa ujinga.
4. Kitu ambae ni nuru kimwili ni giza kiroho,hakika mwili na roho ni umbo mbili tafauti kabisa.
5. Nuru ya Enzi imewahusu wanahewa ambae kaumbwa kwa baki la uvuli wake.
6. Enzi ni ujuzi,na nuru yake ni hewa kadiri ya fikara.
7. Naam ! Fahamu ambae huondoa ujinga.
8. Neno la Mungu huzagaa namna ya kuelimisha viumbe.
9. Kutumia neno la Mungu ndio kutumia nuru maishani.
10. Haikuja nuru kwa mjumbe ila ajili ya watu wote bila ubaguzi.
11. Tumieni wote ukweli huu ili mupate Kufanyika roho takatifu mutakapo ondoka duniani.
12. Mutu anaweza kufahamu kwamba Mungu yupo kwa njia ya ufunuo ao kwa njia ya mafundisho. 

13. Kama mutu ana amini Mungu bila kuhubiriwa na mutu yeyote ni msaada wa roho takatifu.
14. Roho anaweza kumkurubia mutu na kumsaidia katika shuruli zake bila mutu mwenyewe kutambua.

 15. Huzingatia msaada wa roho yule aliye wa roho.
16 . Mutu ni mfano wa kipofu ,macho yake imefumbwa na giza.
17. Mungu ni baba wa siri aliye kwa siri,inabidi kumtazama kiroho kwa kuzingatia uzima wake.
18. Ujumbe huu ni nuru kubwa ambae humsaidia mutu kwa kuzingatia uzima wa Mungu.

48

11. TOBA

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,hakimu mkamilifu,anaye tenganisha adili na batili.
2. Mutu halaumike ajili ya kutenda zambi ispokua yule aliye pewa akili.
3. Ujuzi wake ambae ni busara kamilifu ndio unao jua yule anaye stahili kusamehewa na pia yule anaye stahili kuhukumiwa.
4. Na ndio maana maamzi ya watu inafanyika na Mungu peke yake.
5. Mungu mujuzi amekuwekeeni maamrisho na makatazo.
6. Amekuwekeeni maamrisho ili ukutane na Heri,na amekuwekeeni makatazo ili uhepukane na shari.
7. Katika vile alivyo viumba ,kuna ambae husalamisha nafsi yako na ambae huhatarisha nafsi yako.
8. Kadiri sumu inavyo haribu mwili wa mutu,ndivyo pia zambi inavyo haribu roho ya mutu.
9. Kama upo yakini kwamba Mungu ni mjuzi wa yote,mbele na nyuma,haustaili kumpinga kwa lolote,Bali unastaili kumtii.
10. Na kama haufaamu mradi wa amri yake fulani,ni ajili ya upungufu wako unao tokana na asili ya umbo lako.
11. Kila asemalo Mungu ni kweli na haki maana yeye ni mkamilifu.mpungufu hastaili kumlaumu kamwe.
12. Utazania upo katika kundi ya wanao stahili kusamehewa kumbi wewe ni katika kundi la wanao stahili kuhukumiwa.
13. Na mara utazani utaangamia ,kumbi utaokolewa.
14. Hakika ataangamia yule anaye tenda maovu kwa kusudi,ambae hataki kuacha wala kutubu.
15. Yule atendaye zambi kwa ujinga ama kwa kukazwa bila ya idhini yake ndio anaye samehewa upesi.
16. Fanyeni toba namna ya kujilaumu kwa matendo yako,na kunuia kutoirudilia tena,hali yakua umejisihi sana kwa mola wako ili akusamehe.
17. Kiisha ujitolee kuzidisha wema,na pia kumtukuza mola wako kwa wingi.
18. Bila shaka mola wako atakutakasa,hakika yeye ndio msamehevu na mrehemevu.
19. Muaminifu ni yule anaye muamini Mungu na mitume yake ,na pia anaogopa kutenda zambi.
20. Anaye tenda zambi kwa siri ao kwa wazi,sio muaminifu,ijapo kua ajidai mwenyewe.
21. Na wengi huzingiziwa na makafiri ili kuwaaibisha na pia kuwavunja moyo wanao hitaji kauli tukufu.
22. Kila aliye tumwa na Mungu alizingiziwa,kama wanavyo mzingizia Kalonda yale asiyo ya fanya.
23. Kumsemea aliye tumwa uwongo ni kumkebei yule aliye mtuma,zambi kubwa sana.
24. Haisamehewe zambi hii mpaka atubu mbele ya watu kwamba alimsemea wongo mjumbe .
25. Utukufu unatokana na nuru ya Mungu:mutu anaye jazwa malaika ao roho ndio mutukufu.
26. Na kitabu ambae huandikwa ujumbe,ambae malaika na roho humfundisha Mjumbe ni kitukufu.
27. Na Fasi ambae hujumuika malaika na roho ni maala pa takatifu.

28. Mungu ndio bwana wa ulimwengu wote mfalme wa ajabu,anaye simamia wote sawa sawa. 

29. Hakuna upatikanaji wala maisha njee ya idhini yake.
30. Wala hakuna anaye tukuzika ulimwenguni kama yeye, bwana wa mabwana.
31. Alikua, yuko na atakua,mwenyi kuenea;hakuna mwengine kama yeye,wa pekee aliye juu.

49

12 .  UNAFIKI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu ,anaye endelea kuleta mwongozo wake duniani.
2. Huu ni uma bora wenyi majira ya bustani,ambae roho huninginia hewani kutafuta wa kumshukia .
3. Humshukia mnyenyekevu ,anaye amini ujumbe huu mwenyi yakini na uzima wa Mungu.
4. Atakaye hifadhi kauli tukufu ya kitabu hiki,na kuyafanya kama dhikri namna ya kuyarudilia kwa wingi katika kisomo,ataona miujiza ya Mungu.
5. Mwenyenzi atatosheleza maitaji yake kwa namna ya ajabu,lau kama yeye sio mshirikina wala mnafiki.
6.wanafiki ndio wanao zalalisha kazi ya Mungu ajili ya unafiki wao.
7. Ni mfano wa mayatima wasio kua na mlinzi ,ambae hudanganyia kwamba ulinzi wao ni Mungu na ilihali hawafuate sheria ya Mungu.
8. Wamemkimbilia adui wao mkubwa ili awalinde,bila kutambua kama wamejitoa wenyewe mateka.
9. Wamesema tume amini na ilihali katika nyoyo zao hamna hâta chembe ya imani.
10. Na wamesema tumeokoka na hali wao ndio kuni ya jahanamu.
11. Shetani amewataabisha ajili ya kukosa imani,ndio maana wamekosa msaada wa Mungu kwani wao ni wanafiki.
12. Muaminifu wa kweli hataabishwe na shetani ispokua katika kipindi cha majaribu.
13. Shetani hana uwezo wowote mbele ya Mucha Mungu ,maana uyu ni nuru ambae humuondoa yule aliye giza.
14. Hapana kutia unafiki katika imani yako usije ukanyimwa fadhila yote.
15. Na atakaye amini kweli ataona msaada wa Mungu.
16. Ishara kubwa kutoka kwa Mungu itafanyika naye,sio kwa mapenzi yake,lakini kwa idhni ya mola wake.
17. Mungu ndio mtendaji mkuu ,ambae vyote hutokana na idhni yake.
18. Mtukufu anaye tawala bila mpinzani,na kuhukumu bila faragha,m'bora wa viongozi.
19. Utukufu wa Mungu unaendelea kuonekana kila siku kwa ukarimu wa jaza lake.
20. Ajabu ilioje matendo yake Mungu anaumba aina nyingi sana ya viumbe,wala hakuna kwa yeye kuigia mfano.
21. Muumba wa anga na ukiwa kadiri ya pumzi na mwili.
22. Akitokeza asili ya kila umbo kadiri ya idhni yake, na ilihali mwenyewe hana asili yake,mola wa juu ya daulati ,mshindi aliye juu.
23. Mwenyi uzima ,anaye inukia kila kitu,mamlaka katika yote milele na milele.
24. Ni mutukufu wa daraja anaye stawi katika arshi ,asiye kurubiwa na yeyote.
25. Hakuna mwengine mfano wake ulimwenguni,mumilki wa kila jeshi.
26. Ameenea bila kasoro ,juu ya maala pa juu,kadiri ya kistari cha usawa bila mwanzo wala mwisho,na bila fundo wala lukumba.
27. Hakuna wa kumbuguzi wala wa kumsaidia katika uzima wake,amejitosheleza mwenyewe katika yote namna ya kukamilika. 

28. Ni mkubwa wa wakubwa wote,aliye na utasi wote ,pahali pote ulimwenguni.

13.   MLIMA WA HEKIMA

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,mjuzi ,ajengaye umutu baina ya anga na ukiwa.
2. Sehemu ya anga umboni mwake ndio pumzi, na sehemu ya ukiwa ndani mwake ndio mwili.
3. Ukiwa sio sifuru ,lakini upatikanaji usio kua na fikara ndani mwake,kadiri ya ujinga mtupu.
4. Ni umbo isio kua na maisha ajili ya ukosefu wa pumzi ndani mwake.
5. Na ndio maana anaitwa muzilahewa,umbo isiyo linda pumzi ndani mwake.
6. Muumba alifanya mwili wa mutu mfano wa ardhi,wenyi mboleo ioteshaye viungo.
7. Kadiri maji itokayo mawinguni inavyo fufua mimea iliyo kufa,ndivyo pia neno litokalo mbinguni linavyo fufua matunda ya kiroho iliyo kufa nafsini.
8. Mutu ni umbo la kati na kati,changachanga kiumbiko,amekumbwa na uzaifu wa mwili sababu ya kuketi duniani.
9. Na hujaa nguvu nafsini ajili ya pumzi,umbo la angani.
10. Hufanikiwa na mazao ya zamiri yake yule aonekanaye katika sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani.
11. Utaalamu wake ndio hunyanyua umbo lake juu,kwani ametumia nuru itokayo mbinguni.
12. Jengeni mlima wa hekima duniani,na aina tatu ya udongo:kadiri ya mnara wa uongozi katika uharamu kihewa.
13. Sehemu ya udongo mweusi na sehemu ya udongo mweupe na sehemu ya udongo mwekunda.
14. Hakika ardhi husimama sawa pasipo kuyumbayumba majini ajili ya milima.
15. Ujuzi ni wake mwenyenzi Mungu m'bora wa kuumba atanguliaye ulimwenguni.
16. Hakuna alipo anzia wala atakapo komea,mwenyi mamlaka ya ajabu,mshindi aliye juu.
17. Hazaufikake hâta kidogo maana yeye ni mkamilifu,tafauti na wapungufu wote.
18. Hutendeka kwa rafla anacho idhinia,mwenyi uhuru wa milele.

19. Yeye ndio mwanzo wa vyote kadiri ya muujiza,anaye fanya yote kadiri ya maajabu. 

14. KISIMA

50

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu Chemchem ya nuru ,anaye funulia watumishi wake siri ya mbinguni.
2. Niliona katika ndoto,roho amenikurubia ,akaniambia ,akisema:kuja twende nikuoneshe kisima cha Mungu.
3. Nikaenda pamoja naye ,tukafika kwenyi kisima.
4. Roho aliye nipeleka akaniambia :hiki ndio kisima cha Mungu,tazama ginsi kimechafuka!
5. Nikatazama ndani mwake, nikaona mumejaa uchafu,na majani imeota juu ya maji .
6. Na sehemu ndogo ndio iliyo safishiwa vizuri na maji yake ili kua safi kabisa.
7. Roho aliye ni peleka akaniambia,akisema:sehemu île iliyo safishwa ndio kazi aliyo ifanya nabii muhamadi.
8. Nabii uyu alifanya kazi kubwa ya kusafisha kisima cha Mungu, ili watu watumie maji safi.
9. Lakini hakumaliza,Bali alisafisha sehemu ndogo tu.
10. Na wewe ingia ndani ya kisima, usafishe pia sehemu utakayo wezeshwa na Mungu.
11. Akanipatia upanga ,nikaingia ndani ya maji ya kisima,nikaanza kusafisha lakini siku maliza,Bali sehemu ndogo tu.
12. Roho aliye nipeleka akaniita,akisema: ewe Kalonda ! Tazama ,akafungua kitanga châke cha kuume kunionesha.
13. Na tazama,nikaona wembe unageuka nuru mfano wa mwezi.
14. Nikatazama ndani ya mwezi ule ,nikaona watu wawili ndani mwake.
15. Mmoja alikua amevaa mfano wa kamanda wa jeshi,na mwengine mfano wa roho mwenyi sura ya urembo sana.
16. Roho aliye ni peleka akaniambia ,akisema:uyu unaye muona ndio nabii muhamadi.
17. Akasema:kweli ninakuambia muhamadi ndio bwana wa wote.
18. Nilipo amuka nikaenda mlimani kwa ajili ya ibada muda wa siku tatu.
19. Nikanuia kuomba Mungu zawadi ya kiroho , ambae nilikua nimekwisha chagua:yaani Yesu,Mussa na Eliya. Na anipatie pia muhamadi .
20. Nilipo kua katika kisimamo cha sala ya usiku ,mlimani, nilisikia sauti toka juu kuniita,akisema:Kalonda ! unapenda Muhamadi akushukie?nikasema,ndio.
21. Mungu akaniuliza, akisema:unapenda aje katika upepo ao aje katika nvua?chagua
22. Nikajibu nikisema :aje katika nvua.
23. Nikasikia watu wengi wameshangilia ,chini ya mlima,wakisema:amebarikiwaa , amebarikiwaa...barakaa,barakaaa...
24. Kiisha wakaanza kusema: Laa ilaha ila laha,muhamadi rasululah,laa ilaha ila laha,kalonda rasulu laha...
25. Mungu akaniambia,akisema:" tangu leo umepewa usanii ".
26. Nilikua nasikia masauti yao lakini sikua na waona.
27. Kiisha nikamalizia sala yangu,na nikafanya dhikri kwa wingi ,ndio nikalala


15. KISOMO

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, muanzishaji wa ulimwengu.
2. Kadiri alivyo tangulia bila hitaji ya msaada,ndivyo alivyo umba viumbe bila hitaji ya msaidizi.
3. M'bora wa kuumba anaye fanya kawaida ya umbiko,hâta kukipatikana usawa katika maisha ya jumla ya viumbe. 

4. Hakuna kudondoka kwa mjuzi,vyote hufanyika kwa usawa.
5. Kiumbe hâta kimoja hakifahamu ispokua kwa msaada wake,mwalimu wa siri na wazi.
6. Mtukufu anaye stahili kusifiwa ,mwenyi hâtua na lawama yote.
7. Karibu naye hupatwa na mwangaza,na mbali naye hufinikwa na giza.
8. Mola mwenyi hekima ya ajabu ,ambae hustaajabisha ajili ya kuzidia , mjuzi.
9. Ameendelesha maisha ya dunia ajili ya kutohukumu papu kwa papu.
10. Maisha ya mbingu ni utetezi wenyi kutimia,kazi maalumu ya nuru ambae ni kufukuza giza.
11. Starehe ilioje katika sehemu ya kwanza ya bahazi la juu angani.
12. Ni kambi lenyi utukufu ,ambae ndani mwake hupatikana Maisha ya milele.
13. Tetea namna ya kujumuika mbinguni ,ukipata kufuzu kwa mazao ya zamiri yako.
14. Utetezi bora ni matumizi ya neno la Mungu:ukifanya aliyo kuamrisha na kuacha aliyo kukataza.
15. Hakika aliye silimu ndio mwenyi akili na aliye kufuru ndio mjinga.
16. Someni maandiko matakatifu ya kitabu cha ukweli ili mupate kujazwa.
17. Na itakapo somewa kauli tukufu ya kitabu hiki, ndipo huwafikia nusra kutoka kwa mola wao.
18. Kisomo kinayo faida kubwa huwapatieni nguvu na ushindi, na huwarejesha nyuma wanao shindana nanyi.
19. Amefaulu kabisa yule anaye tumia maneno ya kitabu hiki kadiri ya kifaa maalumu cha maisha.


16. TUMAINI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu, bwana wa kila jeshi,anaye neemesha wote walio amini.
2. Tumaini ndio iletayo heri nyingi maisha ni,maana ndio msingi wa imani.
3. Mutu anaye kosa tumaini ya Mungu moyoni mwake ndio maskini,hakuna la Heri maishani mwake.
4. Ni bora kumtumainia Mungu katika kila jambo ,ukawa yakini kwamba ndiye anaye raisisha na ndiye anaye kwamisha.

51

5. Moyoni mwako usijiweke mbali naye,lakini karibu naye,katika ulinzi wake.
6. Helekeza mawazo yako yote kwake,ukijiuliza moyoni mwako kama yote unayo tenda ni katika mapenzi yake ao hapana.
7. Kuweni na zoezi ya kumkumbuka na kumtukuza moyoni,na tumaini ya kua hauko peke yako Bali malaika na roho wamekuzunguuka.
8. Kama unafaulu katika shuruli zako umshukuru Mungu yakini kwamba ni msaada wake.
9. Na kama unakosa usimlaumu mola wako wala usikate tamaa,lakini umshukuru Mungu na kumuomba masamaha na msaada wake.
10. Na uzidishe ibada hali ya kua na tumaini ya kutoshelezwa na Mungu peke yake.
11. Usiwe na wasiwasi kutaka kujibiwa palepale,wala usisahau ya kama mjuzi ni yeye peke yake,mara utazani ni shari kumbi ni Heri.
12. Wala usijali zarau ao lawama ya watu ,lakini kumbuka ya kama uchoraji wa pumzi yako unabidi makapi kuanguka kandokando yako.
13. Simama imara katika kumuabudu mola wako,ijapokua ugumu wa maisha.
14. Mpelekeeni mola wenu shukrani kwa wingi,mufalme tajiri, anaye miliki vyote kwa jumla.
15. Ndiye mwenyeji wa ulimwengu, mchana ni wake na usiku ni wake,wala hakuna kisicho kua chake.
16. ukategemea umbo fulani,umetegemea kile alicho kiumba,wewe sio ila pumbafu wa kweli.
17. Vyote vitapita,itabakia dhati tukufu ya mola wa ulimwengu.
18. Tukuza jina la mola wako kila siku,na umsujudie na kumshukuru kwa wingi,hakika yeye ndio anaye stahili kuabudiwa.
19. Angeli penda ukosekane duniani kama aungeli zaliwa,lakini amekujaalia maisha kwa ukarimu wa jaza lake.
20. Na akapenda kubadiri hali yako ,utageuzwa kwa rafla,hakuna mwengine aliye na utasi kama yeye.
21. Basi kumbatia kauli ya mola wako kwa kishangwe ,wala usiritadi baada ya kusilimu, wala usiabudu kinyume na muumba wako.


17. UJENZI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,hakimu mkamilifu ,anaye jua Yale ambae wanahewa hawafahamu.
2. Mutu asitafute kujiamua mwenyewe wala kumuamulia yeyote na ilihali hafahamu ya nyuma wala ya mbele ya wakati.
3. Wala usifanye kiburi sababu mola wako anajua yote na hali wewe haujue kama yeye.
4. Ni bora kwako kuamini na kutenda mema na kumuomba.
5. Hayo huonesha matunda mazuri ya zamiri yako na msimamo wako katika imani.
6. Kadiri unavyo tumika kazi ili upate kujenga mwili wako ,ndivyo unavyo pashwa kufanya ibada ili upate kujenga roho yako. 

7. Kama mutu anakataa kuoga maji,na kufua nguo yake,mwili wake utaharibika .
8. Na vivihivyo kama mutu anakataa kusilimu na kutenda mema,roho yake itaharibika,hawezi kuishi milele kamwe.
9. Mwenyi akili ni yule anaye tumia vifaa vya mwili wake na pia vifaa vya roho yake ,kadiri mola wake alivyo muamrisha.
10. Na mjinga ni yule anaye tenda kinyume na maamrisho ya mola wake.
11. Umbalimbali wa mutu na mnyama ni akili:atakaye amini na kutenda mema ndio mwenyi akili.
12. Na atakaye kufuru na kutenda mabaya ndio mjinga,asiye kua na akili,mfano wa mnyama.
13. Neno la Mungu ndio chakula ya roho , itumieni katika kawaida yake ili roho zenu zipate afya njema ya kuishi salama milele.


18. MUTI WA UNABII

1. Utakatifu ni wake mwenyenzi Mungu, mkadiriaji wa karama, aliye pasipo yeyote.
2. Nilijikuta katika ndoto, chini ya muti mukabambi wa rangi ya kimanjano,na majani ya mayiyasombe.
3. Muti ule ulikua na Matawi tatu ,yenyi kuzidiana unene.
4. Nikamuona roho pembeni yangu, akaniambia,akisema:huu ndio muti wa unabii,panda juu yake.
5. Nikapanda juu ya muti ule katika tawi moja,nikatokelea njiani mpaka mbinguni.
6. Nikakutana na mutu aliye vaa kanzu mweupe, aliye kua na kimo cha kadiri.
7. Mutu yule akanikaribisha kwa furaha,akisema:mimi ndio nabii Mussa.
8. Nimetumwa ili nikuoneshe nyumba ya nabii ibrahimu ,tazama nyumba yake kadiri ilivyo.
9. Nyumba île ili kua nzuri sana ambae sijapata kuona,katika bustani ya karibu yetu.
10. Na kiisha ,akanifundisha maneno mengi. Alipo maliza,tuka agana,nami nikarudia.
11. Nikajiona nimeteremuka kwenyi muti huo nilio pandia,na kushuka mpaka chini ardhini.
12. Vijana wa wili ,walio kua na tembea kwa ushujaa wakanikaribia,walivaa mikalabanda kuvikanyako,na mashati na masuruhali.
13. Mmoja kati yao akaniuliza,akisema : nabii Mussa alikua na kuzungumuzia maneno gani mbinguni ?
14. Nikamufasiria kwa kifupi,wote wa wili wakaamini, nao wakajiandaa kupanda katika muti huo wa unabii.


19. WAZI WAZI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu mufalme wa ajabu,aliye ni chagua na kunituma ili nipate kufasiria wazi wazi habari yake. 

2. Wengi miongoni mwa watu wamenajisi utukufu wa mola wa ulimwengu kwa kumufananisha na viumbe.

3.Mungu mwenyenzi hafanane na yeyote ,yeye sio roho ,wala sio neno ,wala nabii ,wala malaika,wala yeye sio shetani wala muzimu.

4. Amepatikana kadiri ya kuenea,mamlaka yenyi uzima,hakuna anako tokea wala anako endea.
5. Wote mnao wataja walifanyika kwa idhni yake ,kuwatokeza toka sifuru

6. Pahali alipo hakuna mwengine, mshindi anaye stawi arshini.

7.. Ingieni wote katika usilimu,dini ya Mungu mwenyenzi;ni vema kumuabudu yeye peke yake ,msifiwa aliye juu.


20. USALAMA WA NAFSI

1.Shuudieni kwa yakini mwenyenzi Mungu,mumoja,atanguliaye ulimwenguni.
2. Anaye amini Mungu peke yake hawezi kuabudu kingine ispokua muumba peke yake,wala hachanganyi nuru na giza. 

3. Na ameamini mitume wote,wala hamkanushe yeyote miongoni mwa wale walio tumwa na Mungu.
4. Kuamini mitume ni kusadiki maneno waliyo kuja nayo na kuitumikisha.
5. Na kuamini maneno ya mitume wote ndio kuamini vitabu vya Mungu vyote.
6. Anaye tumia vilivyo maneno ya vitabu vya Mungu amesalamisha nafsi yakekuingia mbinguni.
7. Na kusalamisha nafsi katika mapenzi ya Mungu,ndio kua katika dini ya Mungu.


21. SHABAA

1. Enyi walio silimu,unganeni katika kamba moja wala musiachane,mola wenu huwapenda sana walio na umoja.
2. Hapana kuunda kikundi cha kidini ajili ya shabaa ya kidunia.
3. Wala musitumie neno la Mungu kama kizingizio na ilihali shabaa yenu ni mambo mengine.
4. Tumieni neno la Mungu ajili ya kutafuta wokovu wa roho zenu ,mupate kuingia mbinguni baada ya kuihama dunia.

 5. Mambo ya kimwili yote ni ya bure,maana itabaki duniani,ispokua mambo ya kiroho ndio inayo dumu milele.
6. Dini nyingi hutokana na uchache wa imani pia na uchache wa elimu.
7. Mungu ni mumoja na sheria yake ni moja ,haipinganake kamwe.


22. WA PEKEE

1. Shuudieni ukweli huu,enyi watu wa dunia,hakika hii ni nuru tokea Enzini.
2. Ni kauli tukufu yenyi utimilifu ,mwongozo na wokovu kutoka kwa Mungu.
3. Mungu ndio mwenyi uzima peke yake,mufalme wa ajabu asiye lingana na yeyote.
4. Mtukufu asiye kua na mwili wala pumzi ndani mwake.
5. Na ndio maana hachangie fasi na yeyote,wa peke aliye enzini.
6. Wengine wote ni tafauti sana naye, pumzi yao na miili yao huwafanya wajumuike angani na ukiwani. 

7. Mungu amehepukana na upungufu wote , maana amestawi arshini milele.


23.SILAHA

1.Mamlaka ni yake mwenyenzi Mungu m'bora wa Viongozi.
2.Mungu wa maajabu anaye tendea waja wake miujiza ya kila namna.
3.hakuna unaso utakao nasa wa chaguliwa wake.
4.wachawi hubaki bumbuwazi wakati waaminifu wanapo okolewa kimuujiza.
5.neno lake hupanguza uchafu wa aina yote, kadiri nuru ipanguzavyo giza.
6.pakizeni nguvu ya ushindi nafsini mwenu kwa ibada ya sala na dhikri, hakika neno la Mungu ndio silaha ya wachamungu. 

7.Mola wenu ni muweza wa kila jambo, mwenyi mamlaka kuliko vyote ulimwenguni.

52

24 . WALII

1.Nilipo kua nime lala, roho alinichugua na kunipeleka, katika ndoto, akanifikisha kwenyi mukutano mkubwa wa watu wengi sana.
2.wengi miongoni mwao walivaa mavazi matakatifu makanzu na viremba ma Juba....
3.roho alisimama mbele ya mukutano akaanza kuhubiri neno la Mungu.
4.Alipo maliza, akinisimamisha mbele ya mukutano na kuniruhusu niwaubirie neno la Mungu.
5.Nika wa ubiria kuhusu umungu, na nilipo maliza nikaona yule mkubwa aliye keti katika kiti cha ufalme, akasimama, wakati huo watu wote walistaajabu sana elimu yangu.
6.Na kuni kurubia na kunipatia mukono wake wakulia, akisema: sikiliza, ewe mpenzi wa Mungu:
7.utakapo hubiri ujumbe huu, watu wa dunia wata kuuliza:wewe u' nani ?usiseme ' u' nabii, sema : u' walii.
8.maana wewe nimtoto wa walii, baba yako mzazi ni walii wa Mungu mwenyenzi.
9.nikaona roho ya uwalii inakuja na ninginia hewani, ikanisogelea na kunieleza, ikisema:
10.Ewe mpenzi wa Mungu usiongeze wala usipunguze katika yale unayo funuliwa.


25 .BABA WA SALAMA

1.ametakasika mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba, mtukufu anaye ondoa aibu na kuleta heshima kwa mtumishi wake aliye zingiziwa.
2.Na ni yeye mjuzi anaye konyeza mutu aliye tetwa na kumsimamia aliye achwa.
3.Mola mtatuzi wa shida zote, mwokozi, anaye nusuru kutokana na shari ya shetani.
4.ameondoa, kwa kauli yake, mashaka na wasiwasi moyoni, hali ya kua mfariji wa milele.

5.baba wa salama aliye salama, mlinzi mwema anaye simamia wote kwa usawa.
6.Neno lake ndio chakula ya roho, mtukufu wa kauli na matendo, ajengaye pumzi urakibuni.
7.Mungu mwenye enzi tukufu, anaye sikia na anaye jibu maombi ya watumishi.

26. HODARI

1. Mwenyenzi Mungu peke yake ndio aliye tangulia kadiri ya kuenea bila mwanzo wala mwisho.
2. Lau kama Alianza ,hasingeli kamilika ,maana Angeli kumbwa na upungufu fulani ,namna ya kukosekana muda fulani. 

3. Na angeli kua na uzaifu fulani,hasingeli weza kuumba chochote,maana angeli kosewa milki itokezayo toka sifuru.
4. Uwezo wa kuumba ni mamlaka ambae haistahili hata chembe ya uzaifu wowote ndani mwake.
5. Alama ya uzaifu fulani ni dalili ya umbile fulani,na ilihali kiumbe hakina uwezo wa kuumba.
6. Mwenyi uzima ni muujiza wa maajabu,mutukufu anaye patikana kadiri ya kuenea,ambae idhini yake kutenda.
7. Hakika Mungu ni wa peke,hodari asiye jumuika.


27. MLINZI MWEMA

1. Abuduni Mungu Mwenyenzi aliye umba kila kitu,unacho kiona na usicho kiona
2. Yeye ndio bwana wa mabwana,ambae maisha na mauti hutokea kwake.
3. Mlinzi mwema,asiye sinzia wala kulala,anaye okoa kutokana na vitimbi vya shetani.
4. Dunia haimzingatie kabisa ,ispokua mbingu ndio humzingatia kidogo tu.
5. Malaika na roho humsujudia kwa unyenyekevu,namna ya kutetemeka mbele yake.
6. Watu wa dunia hawamuabudu kama inavyo stahili,ispokua walio silimu kwa shaada zao za uyakini. 

7. Umbo iliye njee ya nuru haizingatie uzima wa Mungu sababu hufunikwa na giza.


28..M'BORA. WA. WAFUNDI

1. Ametukuzika sana na zaidi mufalme anaye stawi arshini milele.
2. Mtakatifu mwenyi ujuzi wa yote,anaye jaa kweli na haki ndani mwake.
3. Muweza aliye tandaza mbingu angani na dunia ukiwani kadiri ya kambi mbili tafauti.
4. Na kujaza ndani mwake viumbe vya kila aina,m'bora wa wafundi,asiye iga kwa yeyote,ambae wote huiga kwake. 5. Mutu hagundue wala haunde chochote pasipo mwongozo wake,mwalimu wa walimu wote.
6. Heri yule anaye funuliwa na Mungu maana hufundishwa na mjuzi,na ndio maana ni mwenyi kuinukia .
7. Watakieni rehma na Amani mitume wote ,ni kubwa tena bora kabisa kazi waliopewa na Mungu.

53

29. UTATUZI

1. Ametakasika mwenyenzi Mungu,mwokozi ,anaye fungua maisha iliyo fungwa,na kumponesha aliye gonjwa ,ushindi wa

neno lake.
2. Hakuna utata pahali penyi utatuzi wake mutukufu aliye enzini.
3. Mujibu wa dua anaye anaye rehemu viumbe.
4. Amemnusuru muja wake kutokana na majaribu,falme ya giza haina Fasi ndani mwake ajili ya ibada. 

5. Kisomo na maombi hukinga na huponya kwa namna ya ajabu.
6. Someni kila mara kitabu hiki cha ukweli ili mujazwe nguvu ya ushindi.
7. Na kusali kila siku asubui na jioni,na kumtukuza Mungu usiku na mchana.


30. MTOTO

1. Niliona,katika ndoto ,nimeingia nyumbani.
2. Nikamukuta roho ndani ,kati ya sebule,na watu wengi pamoja na ndugu zangu muma pembeni.
3. Roho akaenda ku kona ya sebule maala ambae kulikua kashiki ya maji ya kunywa.
4. Akaingiza mikono yake miwili ndani ya kashiki iliyo kua na maji ya kunywa.
5. Akatoa mtoto mchanga ndani ya kashiki ,alikua mtoto mwanaume.
6. Kiisha akamuweka mu sahani iliyo kuwa na maji safi, kati ya sebule.
7. Mtoto akafungua kinywa chake,maji ikatokota midomoni pake.
8. Roho akawaambia: Tazameni kadiri anavyo sema.
9. Kweli kweli Nina waambia,mtoto uyu atasema .
10. Ndugu zangu wakaanza kujiuliza,uyu ni mtoto wa nani?
11. Roho akawajibu ,akisema:uyu ni mtoto wa Kalonda atakaye sema maneno.
12. Roho akaniambia ,akisema:habari hii hata wa kubwa yako walio kutangulia zamani waliipokea :
13. Nilikua natembea njiani,nikakutana na mwanamuke kigumba.
14. Ni kamuchugua,katika siku tatu akabeba mimba ,akazaa mtoto mwanamuke jina lake Mariamo.
15. Roho wa Mungu akaandika jina hili hewani,maandiko meupe yakaonekana hewani yakiandikwa "Myriam". 

16. Roho wa Mungu akaniambia,akisema:soma jina unayo iona hewani.Nikasoma ,nikisema :Myriam.
17. Roho akaniambia, akisema:utampanga mtoto wako jina hili atakapo zaliwa.

31. URAKIBU

1. Ukubwa ni wake yeye anaye stawi arshini,Mola wa karne na karne,mkukufu atanguliaye kadiri ya kuenea .

 2. Ni yeye aliye na utasi juu ya kila kitu,mumilki ,ambae hashindwake na chochote.
3. Watu ndio wazaifu katika fikara,hawawezi kabisa kumtegemea vilivyo ajili ya upungufu asilia.
4. Ndio maana hufikiwa na madhara mbalimbali ajili ya udhalili wa dunia .

5. Lau kama wangeli weza kusimama imara kama walivyo wakaaji wa mbinguni,tatizo lisingeli msibu yeyote. 6. Maisha yao ingeli timilika kadiri ya starehe ya milele ,hakuna kilio mbinguni .
7. Basi tumieni njia bora ya urakibu,yenyi kujaa nuru,ili mupate kurithi ufalme wa mbinguni.

6. Ni kwamba waaminifu ndio wenyi akili ,ambae wameona bayana kiroho ndio maana wamemuamini Mungu.

 7. Kuona kama makafiri hawana akili ndio maana hawaamini uzima wa Mungu ajili ya kuto zingatia kiroho.

54

32. MSAADA

1. Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu,Muumba wa roho na mwili,anaye bariki wachaguliwa wake.
2. Atakaye tumia nuru bila kuichanganya na giza maisha yake yote,hubarikiwa pamoja na uzao wake.
3. Jitengeni na upuuzi wa shetani :usimuendee mpiga ramli wala usimshirikishe na chochote.
4. Hakuna"msaada"njee ya radhi yake Mwenyenzi,maana vyote hutokana na idhni yake.
5. Magumu ya maisha ni kawaida kumgusa kila mutu,imetokana na uzaifu wa mwili,asili ya mwanaadamu.
6. Kama ni msiba shukuru Mungu bila kurombokeza, Na kama ni magonjwa,tumia maombi ao matunzo,hapone yeyote ispokua kwa ruhusa yake.
7. Na kama ni ukosefu ama tatizo lolote,fanya ibada na kazi,ukijaa tumaini ya msaada wa Mungu.


33. MPONYAJI

1. Amini Mungu Mwenyenzi ,aliye umba mbingu na ardhi pamoja na vilivyomo bila kuitaji ya msaidizi. 2. Hakuna anaye ishi pasipo ruhusa yake,muweza wa vyote .
3. Kila yule amehitaji msaada wa Mola wake,tumaini na kimbilio,tajiri wa vyote.
4. Mungu ndio mponyaji wa kila nafsi,mkarimu anaye ondoa machungu moyoni.
5. Tumieni neno lake,katika kawaida yake,ili upate kuona utukufu wa Mola wako.
6. Linapo tukuzwa sana jina lake ,ndipo hufanyika ishara yake ya kila namna.
7. Mwenyenzi ni mfariji wa milele,Mufalme mkamilifu,asiye hitaji chochote kwa yeyote.


34.   AKILI

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,mpenzi wa watu,amemtukuza kila anaye amini uzima wake na kutii sheria yake. 2. Makafiri hawana yakini na uzima wa Mungu ajili ya kuto mzingatia kimwili.
3. Huzingatiwa kimwili kile kilicho na mwili ,na huzingatiwa kiroho kile kisicho kua na mwili.
4. Kuona kama Mungu hana mwili ,ni lazima kumtazama kiroho ili upate kuzingatia uzima wake.
5. Akili ndio macho ya kiroho inayo zingatia Enzi tukufu namna ya kudhatiti uzima wake.

35.  BAYANA

1. Mutu aliye na akili ni yule anaye zingatia uzima ulimwenguni bila kulazimisha muujiza kwa yeye kusilimu. .

2 .Muujiza mkubwa uliye”bayana” ni kuumba kwako na pia kuumba kwa viumbe vyote uvionavyo.
3. Hakungeli patikana kiumbe chochote ,angani na ukiwani,pasipo muumbaji kutangulia( kupatikana ) ,maana kungeli kosekana fundi.
4. Kuna utafauti mkubwa kati ya Muumba na kiumbe.
5. Muumba ni mwenyi ukamilifu ,na kiumbe ni mwenyi upungufu.
6. Ukamilifu ni namna ya kuenea katika uwezo na katika fahamu,na upungufu ni namna ya kutoenea katika milki na katika busara( fahamu ).
7. Kuenea katika uwezo na katika fahamu ndio kuweza yote na kujua yote, mamlaka itokezayo kuujaza ulimwengu.


36.   NYOTA

1. Niliona ,katika ndoto, mwangaza mkubwa umeniangazia toka juu.
2. Nikanyanyua macho yangu juu, nikatazama, nikaona nyota ine kubwa yenyi kuunganishwa na vistari vine.
3. Nyota moja upande wa mashariki na nyota ingine upande wa mangaribi ,na ingine upande wa kaskazini na ingine nyota upande wa kusini.

4. Humo ndani ya vistari vilio unganisha zile nyota ine,mulikua makundi ya nyota ndogo,na mwezi uliandama ndani ya kundi moja ya nyota humo ndani ya jengo lile la zile nyota ine kubwa.
5. Roho akanichapia nyota zile ine kubwa ,pahali pa vistari akachapa nyota ndogondogo zilizo unganisha zile nyota ine kubwa 6. Roho akaniambia ,akisema:vile vistari ni mufululizo wa nyota ndogo ndogo zinazo unganisha zile kubwa.

7. Roho akaniambia akisema:hakika nyota hizi unazo ziona ndio watoto.* 

37. KARAMA

1. Sema:kuna daraja ya kiroho na pia kuna kazi ya kiroho .
2. Daraja ya kiroho ni unabii na uwalii .
3. ,Na kazi ya kiroho ni utume na utumishi .
4. Unabii ni daraja kubwa ,karama ya nuru kubwa ,ambae humfanya azingatie mambo yatakayo tokea mbele ya wakati,na
kuwaonya watu.

5. Na utume ni kazi kubwa sana ya kiroho ,ya kufundisha watu neno la Mungu kwa njia ya ufunuo,yaani kwa kupokea ujumbe kwa Mungu.
6. Mtume anaweza kua na daraja ya uwalii ao anaweza kua na daraja ya unabii .
7. Na yule anaye tumikisha ao anaye fundisha watu neno la Mungu kwa njia ya maandiko, yaani bila kupokea ujumbe kwa Mungu ,yeye ndio Mtumishi.


38. UZAO WA MBINGUNI

1.Mwenyenzi Mungu ni nuru ya anga na ukiwa,mjuzi atawalaye ulimwenguni.
2.Yeye ndio chemchem ya kila upatikanaji ,mufalme wa pekee anaye enea kadiri ya uzima.
3. Ameletea watu mwangaza namna ya upodozi wa nafsi.
4. Tumieni wote nuru hii,ili nafsi zenu zipate kufikia utimilifu,mupate kua watukufu wa mbinguni. 

5. Mbinguni hakuna kuzaa wala kuzaliwa,lakini wakaaji wa bustani huzaliwa duniani.
6. Atakaye amini Mungu na mitume yake yote,ndio mzaliwa kiroho wa mbinguni.
7. Atageuka roho takatifu,atakapo ihama dunia,na kujumuika mbinguni.


39. JITIHADA

55

1. Mwenyenzi ni mshindi aliye na mamlaka ya ajabu, mwenyi uwezo wa kuokoa ijapo kua dakika ya mwisho.

2. Hapana kukata tamaa ajili ya maovu iliyo tangulia ,ni bora kujitaidi kutubu na kutenda mema ili upate kusamehewa.
3. Usijiamulie mwenyewe kua wa hadeze na ilihali hauja kufa,kukingali wakati wa kukuokoa lau kama utaamini .
4. Wala usijiamulie mwenyewe kua wa mbingu na ilihali ungali na ishi duniani,labda imani yako haikubalike ,na wenda utadondoka baadaye.
5. Usiwe na majivuno wala usiwe na unyonge,lakini ujitaidi kuzidisha wema ili upate ushindi.
6. Kama uko katika jitihada ya kutumia nuru vilivyo,usisahau kwamba unaweza kujaribiwa .
7. Na utakapo jaribiwa na yule mwovu ,ujitolee kushinda majaribu kwa subira na ibada, ukiomba masamaha na wokovu .


40.   ZAMIRI

1. Imani ya kweli ni kusadiki uzima wa Mungu ,na pia kutumikisha mafundisho ya mitume wote.
2. Kinacho haribu imani ya watu ni uchafu wa nyoyo zao pamoja na ushirikina .
3. Ni lazima kutakasa zamiri yenu kwa kuondoa :kiburi,chuki ,nongo,choyo,hila,fitna,na tamaa mabaya . 

4. Na utakapo jitenga na mambo haya na yaliyo mfano wa hayo, ujitolee kufanya ibada kwa wingi .
5. Usijidai utumishi na ilihali moyo wako umejaa takataka ya kila namna .
6. Mbingu ni pahali patakatifu,hakuwezi kuingia kichafu .
7. Mwenyenzi Mungu huchunguza zaidi zamiri ya watu,anafahamu sana yaliyo moyoni mwa kila mutu .


41. MATUMIZI

1. Abuduni Mungu mwenyenzi peke yake wala usiabudu mwengine badala yake .
2. Watumishi wa Mungu wengi wamepotea ajili ya kutumia kafara ya shetani .
3. Kutumikisha mizimu (ma jini) kwa siri ao kwa wazi ,ni ujinga wa kujitoa mateka .
4. Kwa nini kutumikisha jeshi la hadezeni na hali munatambua matata ya hadeze ?
5. Kwa nini hamutumikishe tu jeshi la mbinguni na hali munatambua fadhila ya mbingu?
6. Mara ni kushindwa kutumia njia nzuri ya urakibu;maana kutumia maamrisho ya Mungu ni vigumu kwa wenyi wasiwasi na tamaa ya dunia .
7. Na mara ni kukosa tumaini ajili ya uchache wa imani ,hawana yakini na uzima wa Mungu Mwenyenzi .


42. MILKI ICHIPUAYO

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu,M'bora wa kuumba,aliye muumba Shetani kwa ulimi wa moto,na akamuumba Malaika kwa Anga takatifu.
2. Na akamuumba Mutu kwa udongo .
3. Hakuna Mjuzi mwengine kama yeye na ndio maana hakuna anaye weza kuumba ispokua yeye peke yake .
4. Anatokeza viumbe vingi sana ,wala hasahau hâta kitu kimoja,mlezi wa jumla ya viumbe .
5. Anajua na anatosheleza haja ya kila umbo inayo ishi .
6. Mtukufu atanguliaye kimuujiza ,afanyaye maajabu ,aliye na uhuru , aliye na ushindi .
7. Chemchem ya upatikanaji na maisha , kadiri ya milki ichipuayo ,kadiri ya taa iangazayo .


43. MUSKITI MTAKATIFU

1. Roho wa Mungu alinikurubia ,akaniambia,akisema:maono haya hâta wakubwa yako walio kutangulia waliyaona .
2. Nikatazama juu , nikaona mbingu imefunguliwa ,naangalia ,nikaona jicho mfano wa jicho la mutu ndani ya mbingu ambae hutazama ku dunia .
3. Roho akaniambia ,akisema:furahi sana,Kalonda,maana umepata kuona siri ya ufalme wa mbingu .
4. Na tazama nikajikuta ndani ya Muskiti mkubwa sana ,ambae ndani yake mulikua sehemu tatu;sehemu mbili ku wanaume na moja kuwanawake.

56

5. Humo ndani mulikua watu wengi,ma rangi pia ma Kabila ya dunia yote.Mulikua watu walio vaa makanzu na viremba ,na mwengine walikua na ndevu ndefu.
6. Baada ya sala ,roho akanichugua,tukatoka ili turejee nyumbani;tulipo toka njee nikajikuta mbele ya muskiti wetu wa benye kadingila .

7. Nikastaajabu sana ,nikamuuliza roho aliye nipeleka,nikisema:ni namna gani hivi?tulikua katika muskiti mkubwa ,wenyi majengo mapya ya kudumu ,kutoka inje tunakua mbele ya muskiti wetu wenyi majengo ya kiasili na nyasi juu.
8. Roho akaniambia ,akisema:muskiti huu ndio uleule tulio kuwamo.
9. Hakika nimekuambia ,Muskiti huu ni utakatifu .

10. Ni lazima ujengewe kadiri ulivyo uona,kuunenepesha mpaka ngambo ya njia. 11. Heri Mutu atakaye jumuika katika sala ndani ya muskiti huu.


44. M'BORA WA VIONGOZI

1. Utukufu ni wake Mwenyenzi Mungu,m'bora wa viongozi .
2. Anaye helekeza fikara ya musilimu kwenyi haki na kweli,na kumpitisha katika njia iliyo nyooka hadi mbinguni. 3. Amemzindua aliye jingikiwa na kumsimamisha aliye anguka katika imani .
4. Mutu anaweza kuzania kufanya haki kumbi sivyo.Lakini mwenyenzi humuhelekeza kulingana na zamiri yake. 

5. Ni lazima kuomba kwa Mungu mwongozo wa zamiri yako,na akuhepushe na vishawishi.
6. Mungu ni msamehevu na mrehemevu ,mjuzi anaye sikia manongonezo ya moyoni mwa kila Mutu.
7. Ogopeni Mungu kwa siri na kwa wazi,hakika mamlaka yake ni kubwa ajabu,hakuna kwa kumfichamia .


45. MTUNZAJI

1. Utakatifu ni wake mwenyenzi Mungu,mtunzaji,anaye ponya walio rogwa na kuwapanguza machozi wanao lia .
2. Mola wa miujiza mwenyi mamlaka ya ajabu,anaye ondoa uchawi kwa kauli yake tukufu.
3. Anapo taka jambo husema: liwe na linakuwa .
4 . Hakuna ligumu kwake yeye mufalme, hakika vyote ni chini ya uwezo wake.
5. Muweza yote anaye pana nguvu ya ushindi kwa waja wake,kama alivyo mupa Kalonda nguvu ya kumshinda Waileshi.
6. Mtukufu anaye jengea vipenzi vyake ngao ili mizinga ya maadui isiwapate.
7. Mungu hawaachake waaminifu ajili ya kudondoka,lakini huwarudilia baada ya toba yao kwa huruma wake ,hakika Mungu ni msamehevu na mrehemevu.


46. MUAMUZI

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, mutukufu anaye tawala ulimwenguni bila mipaka..
2. Mola wa jumla ya viumbe aliye na milki kamilifu ,atendaye kwa idhini bila kazi.
3. Mutu hazae wala hafiwe ispokua kwa mapenzi yake ,bingwa aliye na kasi la uwezo wa kutenda. 4. Mungu ndio anaye bariki waaminifu na ndiye anaye laani makafiri.
5. Hazulumu yeyote miongoni mwa viumbe vyake,m'bora wa kukadiria.
6. Muumba wa vyote aliye fanya roho kadiri ya utimilifu na akafanya muzimu kadiri ya uharibifu.

 7. Muamuzi anaye jua yote bila kuambiwa na yeyote,kiongozi pekee wa jumla ya viumbe.


47. MWANZO WA VYOTE

1. Ukamilifu ni wake Mwenyenzi Mungu anaye enea ulimwenguni.
2. Mwanzo wa vyote anaye tangulia kwa mamlaka yake mwenyewe bila msaada wa yeyote.
3. Amepatikana na ujuzi wa vyote pia na uwezo wa vyote sababu ni mwenyi kukamilika.
4. Hali yake ni uzima, utukufu wa ajabu usio kua na mfano, m'bora wa kuumba.
5. Angeli kua na mfano wake kama hasingeli kua na ukamilifu,na kama angeli kosa ukamilifu bila shaka angeli kua mpungufu. 6. Upungufu hutokana na umbiko, uzaifu unao dai msaada kwa kujumuika na kwa kutenda ulimwenguni.
7. Mwenyi Enzi ndio bwana wa ulimwengu, mshindi aliye na milki kamilifu.


48. ENZI

1. Utangulizi wa Mungu ni muujiza mkubwa sana,namna ya kuenea bila mwanzo wala mwisho.
2. Ni mamlaka ya ajabu kadiri ya uwezo wa vyote, ambae humkamilisha bila upungufu wowote.
3. Uwezo wa vyote ndio milki kamilifu, ambae haishindwake na chochote.
4. Milki hiyo ndio inayo itwa:Enzi ,jambo la upekee pasipo mfano wake ulimwenguni.
5. Enzi ndio hutokeza ulimwengu na walimwengu maana hujua yote na huweza yote.
6. Hakuna kinacho patikana bila ya idhni yake,mutukufu aliye na mamlaka ya kutokeza toka sifuru.
7. Yeyote aliye na upungufu hana uwezo wa kutangulia wala uwezo wa kutokeza toka sifuru ajili ya uzaifu.


49. AHMADI

1. Sema:Ahmadi ni mkweli,alitumwa na Mungu.
2. Na wewe ni shahidi wa Mungu Mwenyenzi.
3. Na maneno unayo andika ni ukweli, na kitabu hiki ni kitukufu.
4. Kwa nini umesoma maneno ya wengine katika sala na ilihali umekwisha funuliwa maneno ma takatifu zaidi ? 

5. Ushuuda unao toa juu ya uzima wa Mungu ndio wa kweli kabisa.

  1. Basi shaidilia, Mungu mwenyenzi yu pamoja nawe ,pia na wote wanao kubali ushuuda wako.

  2. Hakika mwenyenzi Mungu amewapenda sana wanao toa shaada, ambae huamini ujumbe wake.


50. UTAZAMAJI

  1. Mola wa ulimwengu amestawi juu ya maala pa juu arshini.

  2. .Amepatikana mbali sana na dunia maana yeye ni tafauti kabisa na mwili, mwenyi kuhepukana na upungufu wote.

  3. Mungu haiko mashariki wala mangaribi,haiko kaskazini wala kusini,Bali mutukufu amestawi juu sana kupita mbingu.

  4. Kumuhelekea ni kumtumainia ,kumpenda kwa moyo wako wote ,yakini kwamba ndiye mwenyi mamlaka ya vyote.

  5. Ukamtazama kimwili hauweze kuzingatia, ni kawaida kumtazama kiroho ili upate kuzingatia uzima wake.

  6. Akili yako ikazingatia utendaji wake ni kwamba umemuona.

  7. Mungu ni mwenyi kuwako bila kukosekana wakati wowote wala kushindwa na chochote , m'bora wa kuenea.

51. MAJI YA. UHAI

  1. Mwenyenzi Mungu ni nuru ya anga na ukiwa, busara kamilifu ambae hujua yote.

  2. Neno lake huangazia akili urakibuni,kadiri ya upodozi wa nafsi.

  3. Enyi walio silimu, jisafisheni na neno la Mungu ,hakika kauli tukufu ni mfano wa maji ambae husafisha roho.

  4. Huondoa takataka yote ya moyo na kugeuza pumzi ya mutu hali ya kua roho takatifu.

  5. Yesu Masiya ni Nabii na mitume mkubwa aliye jazwa kauli tukufu na kulingana nayo kihakika zaidi ya wenzake.

  6. Na ndio maana yeye ni mfano wa neno la Mungu.

  7. Kauli tukufu ni mfano wa maji ya uhai,ambae hutakasa moyo wa mutu,kutumia neno la Mungu ndio kuamini unabii wake.

57

52. WEMA

  1. Amejaa utukufu wa ajabu Mwenyenzi aliye juu, mkuu anaye wezesha na anaye zaufisha.

  2. Kila tendo lake linao mradi wake na maana yake,sababu hufanyika na busara kamilifu.

3. Ulemavu na utimilifu watokea kwake, wala hana hatia yoyote katika kuumba kwake.
4. Kama watu wangeli fahamu sababu ya kutokeza kwake umbo fulani na upungufu fulani, bila shaka wangeli shangilia ujuzi wake.
5. Heri mutu anaye saidia maskini bila kumshimangi wala kurombokeza ,maana yeye pia atalipwa makubwa na Mola wake.
6. Tendeni wema ili Mungu akulipe mema zaidi ,wala usitende wema ili watu wakulipe ao wakusifu.
7. Dunia haina wema,atakaye tumaini malipo ku dunia atavuna sifuru.


53. MASINGIZIO

  1. Enyi walio silimu ! Jiepusheni na zana pia na masingizio ku watu wenzenu.

  2. Atakaye mzingizia muaminifu ili kutaka kumzalalisha,ataingizwa hadezeni atakapo ihama dunia.

  3. Ogopeni Mungu ukweli wa kuogopa ,hakika hukumu ya Mola wenu haina maondoleo.

4. Katika uwezo wake wa ajabu hakuna wa kupimana naye ulimwenguni.
5. Mwenyenzi ni bingwa anaye zidia wote katika yote,vyote hupatikana kadiri ya idhni yake wala hakuna kilicho njee ya hukumu yake.
6. Hapana kumushambulia muaminifu bure musije mukaanguka pembeni yake mfano wa makapi,msije mukachomwa motoni.
7. Kila mutu atavuna Yale aliyo ya panda,maana Mola wenu ni hakimu mkamilifu

54. VIFAA

  1. Uzima ni wake Mwenyenzi Mungu,mwalimu wa wanahewa wote.

  2. Yeye ndio anaye angazia fikara ya watu ili wagundue vifaa mbali mbali.

  3. Matumizi ya vifaa katika shida mbali mbali sio mubaya,Mola wenu amewatakieni usalama.

  4. Ni makosa kutumia chombo ajili ya kuangamiza watu bure bila ya haki.

5. Kama musilimu anagonjwa,ni bora aanze na maombi na kiisha atibiwe bila kumshirikisha Mola wake na chochote.
6. Mutu anaye kataa kutunzwa ni sawa na majununi anaye kataa kuoga na hali mwili wake umechafuka,na ndio mfano wa muovu anaye kataa kutubu.
7. Usimjaribu Mola wako kamwe ,wala usilazimishe Mungu akufanyie jambo ambae amekwisha kupa ginsi ya kujifanyia mwenyewe.


55. TAJI LA UTUKUFU.

1. Ewe muaminifu ,acheni watu wa dunia wakuzarau ajili ya imani yako,hakika heshima yako ni kubwa sana mbinguni.
2. Mola wako atakuvika taji la utukufu, na furaha kwako haitakua na ukomo.
3. Zaidi umeshambuliwa duniani ,zaidi umeneemeshwa mbinguni.
4. Usivunjike moyo sababu ya kutohukumiwa duniani waovu wanao kubuguzi,kuna wakati ulio wekwa ,ambae haki itainuliwa juu,ndio kilio chao kitaanza bila ukomo.
5. Maisha ya dunia ili wadanganya ,walizani ujanja kumbi upumbafu .
6. Muovu asiye azibiwa na watu duniani,azabu yake ni kubwa zaidi siku ya mwisho.
7. Ole kwao wanao tenda zambi kwa ufic
WAho,wamezani kunusurika kumbi kuhatarika zaidi hiyo siku ya hukumu.


57.  MIUJIZA

1. Mwenyenzi Mungu ndio mwanzo wa vyote ulimwenguni, chemchem ya upatikanaji na maisha.
2.Ujuzi wake ndio ulio kutwa kabla ya ulimwengu na walimwengu,kadiri ya ukamilifu pasipo kabla yake wala baada yake. 3. Mwenyi uzima, mtukufu aliye na uwezo wa vyote, anaye simamia viumbe kwa usawa.
4. Vitu vyote njee ya dhati yake ni miongoni mwa viumbe alivyo viumba.
5. Mungu hafanane na yeyote wala hachangie fasi na yeyote, wala hana shauri na yeyote kwani ni wa pekee.
6. Bingwa aliye tokeza vitu vyote bila kutokezwa na yeyote, mkamilifu.
7. Mufalme wa ajabu anaye stahili kuabudiwa peke yake, wa miujiza aliye huru kuliko wote.
 


56.KADI


1. Roho alinikurubia,akaniita akasema: Kalonda ! twendeni pamoja nikuoneshe.

2. Nikaenda naye,tukafika katika uwanja (ambae) nikaona  humo mutu mmoja alikua amekaa chini juu ya udongo.

3. Mutu yule alikua mwenyi kuzoroteka kiafya,akivaa suruhali ya rangi mweusi yenyi vumbi,na shati mweupe yenyi kufifia na uchafu.

4. Roho akaniambia,akisema: mutu uyu anaye kaa katika mavumbi ya ardhi ndio Kadiri, yaani Kadima.

5. Mutu uyu amejidai unabii na utume na ilihali Mungu hakumtuma.

6. Roho akaniambia ,akisema:tazama kilicho mbele yake.

7.  Nikatazama mbele yake ,nikaona kumewekwa marimbarimba ,juu yake mafulushi na mapiki makundi.

8. Punde kidogo nikaona chombo kile kikaanza kutingizika na nguvu sana.
9. Roho akaniambia, akisema : kitu hiki ndio uchawi wake, kama kinafanya hivi,ishara hufanyika.
10. Hakika mutu uyu ni nabii wa uwongo tena muchawi,miujiza yake sio ila urozi mtupu.
11. Angalisho na walimu wa mafumbo,maana ndio wajumbe wa masih dajali.
12. Zama hizi watu wengi wamejidai utume na ilihali hawakutumwa na Mungu.


58. LENGO

1. Mungu amempenda sana aliye nuruni kuliko aliye gizani.
2. Aliye nuruni hutumia vyote kiroho matendo ya mwili wake huangaziwa na roho yake.
3. Hutumia mwili sababu ndio unao fanya adhihirike duniani,lakini mradi wake ni kiroho.
4. Umungu hauzingatiwe ispokua kiroho ,yaani kwa njia ya roho.
5. Utazamaji kimwili hauzingatie ispokua miili peke yake.
6. Anaye sumbukia dunia hutumikia tu maisha ya dunia ,wala hakumbuke maisha ya mbinguni. 

7. Mutu wa namna hii ndio mwenyi hasara kubwa ya kukosa maisha ya milele.

59. ASIYE ONEKANA

58

1. Enyi wanaadamu ! Aminini Mungu kama vile mungeli kua na muona na macho yenu,wala musiwe na shaka ajili ya kuto onekana kimwili.
2. Watu wengi hawana imani sababu ya kuto muona na macho yao kimwili, wamezani wamefanana naye.
3. Hapana kulazimisha kumuona kimwili yeye ambae hana mwili, tena aliye mbali sana na dunia.

4. Kiungo cha mwili kiitwacho jicho hakizingatiake kisicho kua na mwili, wala kilicho njee ya dunia.
5. Mwili ni umbo zaifu sana ambae hujaana na ujinga,ndio maana fikara inayo changana na ujinga ndani ya mutu ni zaifu,yenyi kufubala.
6. Hali yake Mungu ni tukufu ajabu,tafauti kabisa na umbo zote,maana yeye ni katika ukamilifu na viumbe ni katika upungufu. 7. Kama unapenda kuona utukufu wa Mungu ,basi amini kikweli utaona bayana utukufu wake na hâta kumsikia sauti yake.

60. MWAMBA USIO VUNJIKA

1. Mwenyenzi Mungu ndio mwokozi,ni lazima kuhitaji msaada kwake,mkubwa aliye na uwezo wa vyote.
2. Atakaye tegemea viumbe katika shida yake yote ndio pumbafu atakaye shindwa.
3. Tumaini ya Mungu moyoni ndio husadikisha imani ndani ya mutu.
4. Baada ya dhikri urakibuni ni faraja,hapana kukata tamaa, maana uwezo wa Mola wenu ni tayari kila fasi na kila muda. 

5. Kama unajitupa kwa Mola wako na moyo wako wote hauta pata haya lakini ushindi na heshima.
6. Mwenyenzi ndio mwamba usio vunjika ,shikeni kwa bidii mwamba huu ili mapate kufuzu.
7. Hakika Mwenyenzi Mungu ametosheleza kua mlinzi.Hakuna mwengine kama yeye.

61. USAFI WA MOYO

1. Safisheni moyo wako,ewe mwanaadamu, wala usilinde kamwe wazo mbaya ndani mwako.
2. Hauwezi kulipwa malipo ya mtenda mema na ilihali wewe ni mtenda zambi.,Mola wako ni m'bora wa mahakimu.

 3. Usiunge urafiki na shetani na hali wewe umekwisha silimu.
4. Hakika unafiki ni mila mbaya ambae humfanya mutu anyimwe fazila zote.
5. Ondoa upuuzi na uvivu katika utumishi wako ,bila shaka ujasiri wako humaanisha ukubwa wa imani yako.
6. Na usifanye ibada kama anaye mjaribu Mola wa walimwengu.

7. Mola wako huchunguza zaidi sana yaliyo moyoni, wala hapitiwe na lolote. 


62. UMUTU 

1.Mutu asiye tumia neno la Mungu pumzi yake sio urakibuni lakini uatiduni,,ndio maana nafsi yake sio asili ya roho lakini asili ya muzimu.

2. Matunda yake ni mabaya ajili ya kupatikana gizani ametumia wazo lisilo faa na kisa kisicho faa.
3. Na fikara yake hukomea katika mambo ya kidunia peke yake ,na ilihali dunia ni ya muda mfupi.

4. Na yule anaye tumia wazo inayo stahili na kisa kinacho stahili, ndio pumzi urakibuni, asili ya roho takatifu. 5. Kuona kama yeye ni nuruni, ndio maana huwanukulu wakaaji wa mbinguni,utimilifu wa umutu.
6. Yule asiye amini Mungu ndio mwenyi kukosa akili , amewanukulu wakaaji wa hadezeni,uaribifu wa umutu. 

7. Mutu asiye kua na utaalamu kifikara ni sawa na mnyama, kukosa imani ndio kukosa akili.

63. MLIMA KAROMBWE

1. Niliona, katika ndoto, mlima mrefu ambae juu yake kulisimama mutu mrefu,akivaa koti na suruhali na mtama.

 2. Mutu yule alikua na teremuka kuhelekea upande wetu mpaka mbele yangu,kicheko midomoni.
3. Roho akaniambia, akisema : mutu uyu unaye muona ndio Nabii Saleh .
4. Nilipo mtazama ,moyoni mwangu mulijaa furaha.

59

5. Roho aliye ni peleka, akaniambia, akisema : furahi sana ewe mpenzi wa Mungu, hakika kuonana na nabii uyu ni neema kubwa.
6. Roho akaniambia, akisema : karombwe ni mlima mtakatifu,lakini haija funuliwa kwa yeyote, kama ilivyo kwenyi muji Seule. 7. Mlima huu na muskiti wa benye kadingila ni maala pa takatifu .

64. ONDOA SHAKA

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu ,mwalimu mkamilifu, anaye funulia watu siri ya mbinguni.
2. Dunia isingeli ongoka pasipo ujumbe wake, amelea viumbe na hekima ya ajabu.
3. Kupokea kauli yake ndio kusalamisha nafsi yako, namna ya kustiri maisha yako.
4. Mungu anaendelea kuongoza watu ili wasipotee,wenyewe wasingeli faulu ajili ya uzaifu kibusara. 5. Lakini ijapokua msaada wake, mashaka haimalizike katika nyoyo zao.
6. Huwapinga wajumbe wa Mola wao na kulazimisha Mwenyenzi apate kuishi kama wanavyo ishi.

 7. Ni ujinga sana kulazimisha utendaji wa Mungu ulingane na utendaji wa kibinaadamu.

65. ANAYE STAAJABISHA

1. Mwenyenzi ni mwenyi uzima, mtukufu anaye kamilika peke yake ulimwenguni.
2. Nafsi yenu na maisha yenu ni tafauti kabisa na dhati yake uzimani.
3. Matendo yote ya viumbe ni upungufu,tafauti kabisa na matendo yake ya ukamilifu.
4. Ni vema kufikiri mbele kama yale unayotaka Mungu ayatende humustahili ao hapana, maana yeye ni mkamilifu. 

5. Uzaifu wa kuishi mfano wa viumbe haumkurubie kamwe.
6. Utendaji wake ni wa pekee kadiri alivyo wa pekee bila mfano wake.
7. Mufalme anaye staajabisha ulimwenguni.

66. CHEMCHEM YA FAHAMU

1. Ametakasika Mwenyenzi Mungu, mufalme anaye stahili kuhimidiwa usiku na mchana.
2. Amepatikanisha kila kitu kwa ujuzi wake na uwezo wake, m'bora wa kuumba.
3. Akapenda kugeuza umbiko, anaweza kufuta upatikanaji huu na kutokeza umbiko lipya la aina ingine.
4. Busara yake ni kamilifu,chemchem ya fahamu yote ulimwenguni.
5. Hakuna asilo lijua,mtukufu aliye tayari muda wote kutokeza mapya bila kuiga wala kujifunza.
6. Anafahamu mambo yote inayo fanyika na kila viumbe muda wote pahali pote.
7. Tajiri wa habari yote ulimwenguni, mzima asiye sinzia wala kulala,mfinyanzi wa umbo za walimwengu.

67. BARAZA

1. Ujuzi ni wake Mwenyenzi, wa pekee anaye endelesha maisha ya pumzi ya wanahewa_haramu.
2. Miili yao huaribika duniani, lakini pumzi yao hujumuika barazani.
3. Viumbe vikali katika baraza la hadeze,na viumbe vipole katika baraza la mbingu.
4. Baraza la hadeze hufikiwa na chembe ya utesi wa shetani,.
5. Na baraza la mbingu hufikiwa na chembe ya ulinzi wa malaika.
6. Kifo cha duniani ndio mwanzo wa starehe kwa waaminifu, na pia ndio mwanzo wa mateso kwa makafiri. 

7. Hakika Mwenyenzi ndio m'bora wa mahakimu,humlipa kila mumoja wenu sawa na matendo yake.

68. KABURI

1. Sema:kaburi ni kambi la kimwili udongoni ambae hulinda mauti ya mutu.
2. Humo ndani ya kaburi hamuna maisha ingine Bali mwili huaribika kwa haraka na kugeuka udongo. 

3. Umbo la mutu linayo sehemu mbili : mwili na pumzi.

4. Baada ya kifo,mwili ndio huingizwa na watu kaburini ,na pumzi ndio huingizwa na Mungu barazani.
5. Pumzi huzidi kuishi barazani hadi kiyama,na mwili ndio huoza namna ya kufutika kaburini
6. Sehemu ya baraza inayo gusana na mbingu ndio baraza la mbingu, na sehemu ya baraza inayo gusana na hadeze ndio baraza la hadeze.
7. Kama kweli kaburi ingeli kua na Linda pumzi, ingelikuaje kwa yule ambae mauti yake haikuzikwa kaburini ? 

69. MAPAMBAZUKO

1. Nuru ndio kifaa ambae huondoa giza,kadiri fahamu inavyo ondoa ujinga.
2. Ni utukufu utokao ndani mwake kadiri ya uvuli wake ambae huleta mapambazuko.
3. Kinacho pambanua fikara ya mutu ili maisha yake itimilike sawasawa ni neno la Mungu.
4. Kauli tukufu ni nuru ya busara kamilifu inayo tua mbinguni na kuzagaa angani pote na ukiwani.
5. Malaika na roho wanapo pokea neno la Mungu ndio kuzagaa kwa nuru mbinguni.
6. Na ma nabii na mitume wanapo pokea ujumbe ndio kuzagaa kwa nuru duniani.
7. Asiye tumia neno la mola wake hupatikana gizani maisha yake yote, atajumuika hadezeni mikononi mwa falme za giza.


70. KIMBILIO

1. Utakatifu ni wake Mwenyenzi Mungu, m'bora wa kuumba.
2. Mola wa miujiza aliye na mamlaka ya ajabu
3. Mtukufu apangaye na apanguaye majira ya ulimwengu.
4. Vilivyomo angani na vilivyomo ukiwani hutarajia msaada wake.
5. Mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu, anaye fariji maisha ya kila mutu.
6. Baba wa salama aliye salama ,helekeo na kimbilio la wasilimu.
7. Hakuna Mola mwengine apasaye kuabudiwa kwa haki ispokua Mungu Mwenyenzi peke yake.


Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Kitabu cha ukweli - Mlango wa saba : "KAULI TUKUFU"

Kitabu cha ukweli - Mlango Wa pili "ENZI TUKUFU"

MWANDISHI WA KITABU: